Gilead Teri: Sera za Uchumi za Rais Samia Zavutia Uwekezaji wa Trilioni 20 ($7.7b). Amfananisha na Deng Xiaoping Baba wa Uchumi wa China

Watanzania wachache tunapenda masuala haya, wengi tupo na mada za kina TL na Mbowe pamoja na utekaji unaendelea. Kina Mdude Nyagali wapo midomoni mwa wengi wetu kuliko masuala chanya ya kiuchumi. Tupo kisharishari zaidi.
Nitafurahia sera ya kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja kama itakuwepo
 
Deng xiaoping etiii ? Foolish
 
Mbombo ngafu, Mimi sio mtalaam wa uchumi.
Ila mambo mengine yanahitaji akili ya kawaida na sio Elimu husika, hasa hili la nchi kuwa na uchumi wakueleweka.

Ninachoona ni milango iko wazi wahuni wadunia wanamwagika + wale wa ndani hasa wale ndugu zetu tunaowaita Watanzania wenye asili ya -------
 
Watanzania wachache tunapenda masuala haya, wengi tupo na mada za kina TL na Mbowe pamoja na utekaji unaendelea. Kina Mdude Nyagali wapo midomoni mwa wengi wetu kuliko masuala chanya ya kiuchumi. Tupo kisharishari zaidi.
Huyo Gerald Teri, dish lirakuwa limeyumba:

Yaani unalinganisha uwekezaji wa nje (FDI) wa Tanzania wa dola bilioni 7, na uwekezaji wa makampuni ya kigeni nchini china wa dola bilioni 90 kwa mwaka!! Lazima uwe mgonjwa. Ni sawa na muuzaji wa nyanya, ambaye mwakajana aliuza nyanya akapata shilingi milioni 1, halafu mwaka huu akapata shilingi milioni 3, halafu aseme anafanana na mauzo ya Bakhresa, kwa vile tu mauzo ya Bakhresa mwaka uliopita yalikuwa shilingi bilioni 100, na mwaka huu yamekuwa bilioni 300.
 
Mfanyabiashara maarufu na mwenye uzoefu wa uwekezaji Rostam anasema hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia wawekezaji wa nje. Mtaalamu wa theory za uchumi anaiona Tanzania ikikuwa kwa kutumia wawekezaji wa nje. Hapo sasa!
 
Wewe ndio dishi likeyumba na unahangaishwa na mihemko ya chuki.

Hoja hapa ni ongezeko la miradi zaidi ya mara 3 sawa ilivyowahi kutokea huko China ya Deng.

Hajalinganisha value hapo.
 
Mfanyabiashara maarufu na mwenye uzoefu wa uwekezaji Rostam anasema hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia wawekezaji wa nje. Mtaalamu wa theory za uchumi anaiona Tanzania ikikuwa kwa kutumia wawekezaji wa nje. Hapo sasa!
Uwekezaji mkubwa ni WA ndani na sio hao wa Nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…