Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Giza la kiuchumi, ni vigumu kwa Rais kushughulika na kila kitu kwa wakati mmoja.Salaam, Shalom!
Nchini petu tangu lini imewahi kutokea mtu akakamatwa na watu waliokuwa na pingu kisha kumfunga mtu na kuondoka naye kisha kwenda kumuua na kumtupa vichakani?
Tangu lini kikundi cha watu kimeruhusiwa kumuua mtu bila kumfikisha mahakamani?
Pia soma: Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya
Giza lipi Hilo uliloliondoa kiongozi wetu?
Basi sawa, tusubiri karma!!
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.
Karibuni🙏
Madaraka yake ni makubwa na nilimuelewa Mbowe alipotaka apunguziwe ukubwa wa majukumu yake.
Wakati wa JPM maiti zilikuwa zikiokotwa Coco Beach kila siku, tukasema Yeye Rais ni muuaji leo hii mauaji yanaendelea kama kawaida.
Ujambazi, uuaji, utekaji na unyama wa kila aina ni hulka za binadamu.
Kule USA kuna kesi hazijaweza kutolewa hukumu zina miaka 30 mpaka 40, upelelezi unaendelea mwaka baada ya mwaka.
Tatizo letu labda ni uoga wa kibinadamu, kutozoea kuona unyama ukiwa ni sehemu ya kawaida ya maisha yetu ya kila siku.