Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Ondoa mfano wa US hapa. Kwa anayesoma habari za huko ataona undani wa hizo kesi za mauaji zinazochukua miaka mingi ya upelelezi na ugumu wake ukihusisha juhudi za dhati za uchunguzi zinazofanywa na vyombo husika. Hata motives za hayo mauaji zinajadiliwa. Details za kutosha zinatolewa.Giza la kiuchumi, ni vigumu kwa Rais kushughulika na kila kitu kwa wakati mmoja.
Madaraka yake ni makubwa na nilimuelewa Mbowe alipotaka apunguziwe ukubwa wa majukumu yake.
Wakati wa JPM maiti zilikuwa zikiokotwa Coco Beach kila siku, tukasema Yeye Rais ni muuaji leo hii mauaji yanaendelea kama kawaida.
Ujambazi, uuaji, utekaji na unyama wa kila aina ni hulka za binadamu.
Kule USA kuna kesi hazijaweza kutolewa hukumu zina miaka 30 mpaka 40, upelelezi unaendelea mwaka baada ya mwaka.
Tatizo letu labda ni uoga wa kibinadamu, kutozoea kuona unyama ukiwa ni sehemu ya kawaida ya maisha yetu ya kila siku.
Hapa kwetu ni mauaji ya kisiasa yanayohusisha vyombo vya dola na wahusika serikalini huchagua kuwa kimya au kuzungusha hizo propaganda za “ kifo ni kifo” tu; ni kitu cha kawaida! Hii kutaka wananchi “wazoee mauaji ya kinyama” yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati ni mtazamo wa ovyo sana. Hauwezi kuhalalishwa kijinga hivyo.