Giza lipi umeliondoa Rais ikiwa wasiojulikana walimtia pingu mtu hadharani Kisha kumuua na kumtupa vichakani?

Giza la kiuchumi, ni vigumu kwa Rais kushughulika na kila kitu kwa wakati mmoja.

Madaraka yake ni makubwa na nilimuelewa Mbowe alipotaka apunguziwe ukubwa wa majukumu yake.

Wakati wa JPM maiti zilikuwa zikiokotwa Coco Beach kila siku, tukasema Yeye Rais ni muuaji leo hii mauaji yanaendelea kama kawaida.

Ujambazi, uuaji, utekaji na unyama wa kila aina ni hulka za binadamu.

Kule USA kuna kesi hazijaweza kutolewa hukumu zina miaka 30 mpaka 40, upelelezi unaendelea mwaka baada ya mwaka.

Tatizo letu labda ni uoga wa kibinadamu, kutozoea kuona unyama ukiwa ni sehemu ya kawaida ya maisha yetu ya kila siku.
Ondoa mfano wa US hapa. Kwa anayesoma habari za huko ataona undani wa hizo kesi za mauaji zinazochukua miaka mingi ya upelelezi na ugumu wake ukihusisha juhudi za dhati za uchunguzi zinazofanywa na vyombo husika. Hata motives za hayo mauaji zinajadiliwa. Details za kutosha zinatolewa.

Hapa kwetu ni mauaji ya kisiasa yanayohusisha vyombo vya dola na wahusika serikalini huchagua kuwa kimya au kuzungusha hizo propaganda za “ kifo ni kifo” tu; ni kitu cha kawaida! Hii kutaka wananchi “wazoee mauaji ya kinyama” yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati ni mtazamo wa ovyo sana. Hauwezi kuhalalishwa kijinga hivyo.
 
Salaam, Shalom!

Nchini petu tangu lini imewahi kutokea mtu akakamatwa hadharani kwenye halaiki na watu waliokuwa na pingu kisha kumfunga mtu na kuondoka naye kisha kwenda kumuua na kumtupa vichakani?

Tangu lini kikundi cha watu kimeruhusiwa kumuua mtu bila kumfikisha mahakamani?

Pia soma: Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya

Giza lipi Hilo uliloliondoa kiongozi wetu?

Basi sawa, tusubiri karma!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni🙏
Inashangaza hakika
 
Nasikia hao wasiojulilana wameruhusiwa kuteka, kutesa na kuua sisimizi!

Kwingineko tunaambiwa kifo ni kifo. Zoeeni tu!
 
Ondoa mfano wa US hapa. Kwa anayesoma habari za huko ataona undani wa hizo kesi za mauaji zinazochukua miaka mingi ya upelelezi na ugumu wake ukihusisha juhudi za dhati za uchunguzi zinazofanywa na vyombo husika. Hata motives za hayo mauaji zinajadiliwa. Details za kutosha zinatolewa.

Hapa kwetu ni mauaji ya kisiasa yanayohusisha vyombo vya dola na wahusika serikalini huchagua kuwa kimya au kuzungusha hizo propaganda za “ kifo ni kifo” tu; ni kitu cha kawaida! Hii kutaka wananchi “wazoee mauaji ya kinyama” yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati ni mtazamo wa ovyo sana. Hauwezi kuhalalishwa kijinga hivyo.
Ushahidi ni mgumu sana. Wameuawa watu wengi na miili yao imeokotwa pale Coco Beach enzi ya JPM kiasi ambacho tukajua mhusika ni serikali yake. Leo hii unyama unaendelea kama kawaida.

Naamini zipo sababu nyinginezo za kibinadamu tofauti na hizi hisia zetu kwamba mhusika mkuu ni kiongozi namba moja wa Tanzania.
 
Yuko kwenye mgandamizo mkali sana, vipindi vya kutojua ushike wapi na ufanye nini uwa vipi....tumuombee.
Hizi kauli za kumuombea mtumishi wa Serikali tuliyemuweka madarakani wenyewe ndio mwanzo wa kuzalisha kundi la " Machawa'' wanaojigalagaza mavumbini kama wehu.

Tunatakiwa kuanza upya kwa kuweka misingi mipya na mfumo mpya wa utawala.

Badala ya kwenda kwenye uchaguzi mwaka huu na ujao, tuandike Katiba, tufanye referendum juu ya muundo wa Muungano na tuweke mfumo mpya wa kupata viongozi.
 
Salaam, Shalom!

Nchini petu tangu lini imewahi kutokea mtu akakamatwa hadharani kwenye halaiki na watu waliokuwa na pingu kisha kumfunga mtu na kuondoka naye kisha kwenda kumuua na kumtupa vichakani?

Tangu lini kikundi cha watu kimeruhusiwa kumuua mtu bila kumfikisha mahakamani?

Pia soma: Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya

Giza lipi Hilo uliloliondoa kiongozi wetu?

Basi sawa, tusubiri karma!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni🙏
Ndgu yangu kuna watu ukiwasikiliza unapata mashaka sana na afya yao ya akili....
 
Body language inaonesha yuko kwenye pressure kubwa asiyoweza kuhimili

Vyombo vya intelejensia nchini Israeli zinaendelea kuwasaka magaidi kwa mafanikio makubwa na kutoa mrejesho.

Lini vyombo vyetu Tanzania vitatoa mrejesho wangapi wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa vitendo vya kigaidi kuteka, kupoteza raia na huku wengine wakitekwa mbele ya macho mawiki ya watu zaidi ya 45 katika badi la abiria lakini hadi leo wanatuma Umoja wa Wanawake Tanzania UWT ijibu suala hili la mauaji kisiasa.

Mary Chatanda kiongozi wa UWT aliyepewa jukwaa kuwasaka watekaji na wauaji

View: https://m.youtube.com/watch?v=TT9DuTsshBc
 
Jamani nyumbu wako tabuni aisee!! Wanahaha si mchezo. Ni mwendo wa kujishikiza kwenye Kila kijijambo anachotamka mama
 
Ushahidi ni mgumu sana. Wameuawa watu wengi na miili yao imeokotwa pale Coco Beach enzi ya JPM kiasi ambacho tukajua mhusika ni serikali yake. Leo hii unyama unaendelea kama kawaida.

Naamini zipo sababu nyinginezo za kibinadamu tofauti na hizi hisia zetu kwamba mhusika mkuu ni kiongozi namba moja wa Tanzania.
Mkuu wewe unaamini kuwa mauaji yanayofanyika kwa kiwango kile cha maiti za coco beach, mauaji ya Ali Kibao, jaribio la kumuua Tundu Lissu n.k. pamoja na ujasiri na jeuri iliyotumika, serikali inaweza kuwa gizani kabisa!?

Halafu serikali isiwe na haraka ya kuchukua hatua kwa vile ushahidi ni mgumu sana kupatikana? Na hayo ni matukio ya kawaida tu. Na kwamba kuituhumu serikali na viongozi hizo ni hisia zetu tu?

Bila shaka umesikia majibu na kauli za mara kwa mara za viongozi na wasemaji wake kuhusu hayo matukio. Hadi hapo kama bado unaamini tuhuma za wananchi kuhusu uhusika wa serikali na viongozi ni hisia zao tu, basi hakuna tena cha ziada cha kujadili.
 
Wale walevi watakuja waseme huyo mama yao anakosolewa sababu ni mwanamke na pili ni mwislamu.

Ulevi sio wa vinywaji hata dini.

Huyo mama hatoshi kwa nafasi ya urais hata umakamu tu sijui alifikaje pale.
 
Aulizwe mstaafu.
 
Mbaya zaidi walikuja kama watu wa Amani wakamfunga pingu, watu wakajua anapelekwa mahakamani,

Sasa kitu kama hiki kiongozi ukikinyamazia, mawe yatainuka kupaza sauti.
Ni kama kulikua na ujumbe
'Tunaweza kukuua tutakavyo, na hamna wa kutufanya chochote!'
 
Salaam, Shalom!

Nchini petu tangu lini imewahi kutokea mtu akakamatwa live kwenye halaiki na watu walio na pingu kisha kumfunga mtu na kuondoka naye kisha kwenda kumuua na kumtupa vichakani?

Tangu lini kikundi cha watu kimeruhusiwa kumuua mtu bila kumfikisha mahakamani?

Pia soma: Rais Samia: Sijawahi kuua mtu labda sisimizi, jibuni hoja zao msikae kimya

Giza lipi Hilo uliloliondoa kiongozi wetu?

Basi sawa, tusubiri karma!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni🙏

Ameongeza giza maradufu kila mahali na kila sehemu kama uwajibikaji, usalama, rushwa, gharama za maisha, ajali kila kukicha barabarani, ufisadi, uonevu kama watu kunyanganywa ardhi, mashamba yao na vitendo vya ubakaji, ulawiti kushamiri.
 
HAKIKA.
 
Back
Top Bottom