Jamaa muungwana sana wewe, ujasiri wako wa kukiri makosa ni wa kipekee. Kila siku najifunza Jambo jipya kutika kwako
Hahaa dah! Shukran jazilan Bw. BJ.
Walau wewe una akili ya kuona na kutambua kuwa huwa ninakiri ninapokosea, nakosoa ninapoona si sawa, napongeza kama naona ni sawa, na kadhalika.
Ila kuna watu sijui ni akili finyu au sijui ni nini tu. Jitu lipo miaka yote humu halafu linaibuka tu na kudai mimi kila siku, kila mara, huwa ni kumpongeza Magufuli tu.
Kuna mdada mmoja jana kaibuka naye out of nowhere, anadai eti mimi huwa nawashambulia wote wanaomkosoa Trump.
Nilipoangalia mabandiko yangu kadhaa ya miezi michache ilopita, nikakutana na mada zangu kadhaa zinazomkosoa huyo huyo Trump ambaye nimeambiwa huwa ninawashambulia wote wanaomkosoa.
Sasa, kwa kutumia mantiki yake, ina maana hata mimi mwenyewe huwa najishambulia, siyo?
Hahahahaaa nachoka kabisa.
Watu wengine hawa sijui huko shuleni walikuwa wanapata maksi gani tu!!!