Godbless Lema amuandikia Jakaya Kikwete Waraka Mzito

Godbless Lema amuandikia Jakaya Kikwete Waraka Mzito

K
View attachment 3414169




Mh Rais wetu Mstaafu Jakaya Kikwete. Uongozi wa kweli haujengwi juu ya ndoto za kifamilia, bali juu ya msingi wa haki, utu na ujasiri wa kusema ukweli hata pale ambapo ukimya ni salama zaidi.

Leo hii Tanzania inalia. Tundu Lissu, aliyenusurika kuuawa kwa risasi akiwa mpinzani mkuu wa serikali, sasa amefungwa kwa tuhuma za kisiasa. Vyama vya upinzani vinazuiwa, chaguzi zinaibwa mchana kweupe, na watu wanaishi kwa hofu ya kutekwa au kufungwa kwa kusema tu kile wanachoamini. Na wewe Mheshimiwa, unanyamaza.

Unanyamaza kana kwamba haya hayakuhusu. Kama kwamba haki ni jambo la watu wengine si la wale waliowahi kuongoza. Tunajua kuwa huna tena mamlaka ya kisiasa, lakini bado una mamlaka ya kimaadili. Sauti yako inaweza kuamsha dhamira zilizolala. Lakini unapokaa kimya, unaacha hisia kuwa pengine uko tayari kuona taifa likiteketea mradi familia yako ibaki salama pengine na ndoto zako binafsi kama mzazi zisivurugwe.

Hii si hekima. Hii si busara. Hii ni hofu inayojificha ndani ya tabasamu la kisiasa. Na hofu ya mtu mkubwa huzaa mateso kwa watu wadogo.Historia itamkumbuka kila aliyesema hata kama sauti yake itanyamazishwa. Lakini itamhukumu kila aliyenyamaza hasa kama alikuwa na nafasi ya kusema.

Rizwan anaweza kuwa na ndoto ya kuwa Waziri Mkuu. Lakini ni bora awe Waziri Mkuu wa taifa la haki, si la watu walioumizwa kwa ukimya wa baba yake. Uongozi hauwezi kurithiwa kama mali, bali huhesabiwa kwa misingi ya utu na historia ya ujasiri wa familia.

Mh Rais Mstaafu , bado una nafasi ya kuchagua upande wa historia utakaoandika jina lako. Sema. Kemea. Simama upande wa haki. Si kwa ajili ya siasa, bali kwa ajili ya nafsi yako na heshima ya watoto wako mbele ya taifa linaloteseka.Kwa sababu ukimya mwingine ni kosa la maadili ambalo halionekani mara moja lakini halisahauliki.
Ati ya watu waliotembea dunia hii, karibu @ nchi ni huyo bwana. Huko nje huzisifia democracy na uongozi wa huko. Lakini akifika anauleta unafiki wa kiswahili.
 
Mh Rais mstaafu ... wakati wa uongozi wako tuliiona demokrasia huru , mihimili ya serikali ikifanya kwa uhuru mfn Bunge lilikuwa la kuisimamia serikali ipasavyo , madaraja ya mishahara ilipanda na mengine mengi mazuri tu ..... kwa sasa mambo ni tofauti kabisa na wewe huko kimya ... ndiyo maana mtoq mada anauliza ,je haya yanayoendelea sasa huyaoni ? Au unataka huyu Rais wa sasa asiwe na amani kama uliyonayo wewe ? Au unataka baada ya urai huyu mwezio SSH awe na maadui wengi umcheke
 
kikwete historia itamhukumu.mkapa alifanya sehemu yake km mshauri nyerere pia.leo kikwete yuko kimya nchi inaangamia amebaki kupigania familia yake.jamaa ni mbinafsi
 
Huyo chek bob ndo aisaidie nini nchi bwana wee? So far huyo ni kumuachia muumba yeye ndo atamalizana naye na familia yake pia. Mateso yote haya nchi inapitia shida kwani nani kama si mkono wake wa upanga?
 
K

Ati ya watu waliotembea dunia hii, karibu @ nchi ni huyo bwana. Huko nje huzisifia democracy na uongozi wa huko. Lakini akifika anauleta unafiki wa kiswahili.
Bwana hawa kazi yao Mungu aliwaumbia ni kucheza ngoma, mdundiko, kusasambua, etc etc haya mengine ya intelectuality ni kuwabambikia/kuwasumbua tu!
 
Jakaya leo hii amekuwa rais wenu mstaafu?
Mtatapa tapa sana mwaka huu!

NYIE ENDELEENI NA MANOO NOO YENU!
 
Kikwete yupo pale kutetea maslahi ya familia yake hana habari yoyote na taifa hili
 
Back
Top Bottom