GE2025 Godbless Lema aomba kuwekwa mahabusu kwa hiari mpaka kipindi cha uchaguzi kiishe akihofia maisha yake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Anaandika Godbless Lema kwenye mtandao wa Instagram hivi leo

Mheshimiwa Rais,
Maisha yangu yako katika hatari kubwa. Tafadhali, naomba kwa unyenyekevu mkubwa unisikilize. Ningependa kuishi ili niweze kuwaona watoto wangu wakikua, kuoa na kuolewa mbele ya macho yangu, na ikiwezekana, niweze kufurahia wajukuu wangu ikiwa Mungu atanijalia maisha marefu. Kila mtu anatamani kuishi maisha marefu yenye amani na uzee mwema. Kwa sasa, kuna watu ambao wananifuatilia kwa karibu sana. Hata jioni ya leo, wameonekana maeneo ya nyumbani kwangu, na nina hofu kwamba wangeweza hata kumdhuru mtu yeyote ambaye si mimi. Kwa hali hii, naona ni bora nijiweke mikononi mwa mamlaka kwa hiari yangu kuliko kuendelea kuishi kwa hofu kila siku.Niko tayari kuwekwa mahabusu kwa hiari yangu hadi kipindi cha uchaguzi kipite, kwa sababu naamini kufanya hivyo kutaleta utulivu kwa wazazi wangu, mke wangu Neema, na watoto wangu. Najua watahisi angalau faraja kwamba niko salama.

Ninaomba kwa moyo mkunjufu ulinzi na msaada wako, Mheshimiwa Rais.

For English Language: "My life is in great danger” - Lema fears for his life, requests custody for safety until elections end

Screenshot_20251016_200458_Instagram.jpg
 
Tulipofika kwa nchi yetu mambo yamekuwa hatari sana.

Si salama tena kwa yeyote, Lema amesema jambo ambalo yeyote mwenye akili hawezi kupingana naye.

Bila kurudisha utawala wa sheria kila mtu anakuwa hatarini kupotezwa
 
"kutaleta utulivu kwa wazazi wangu, mke wangu Neema, na watoto wangu. Najua watahisi angalau faraja kwamba niko salama".

Hakuna sehemu LEMA kasema anapambania nyumbu za CHADEMA kama wenyewe wanavyodhani anawapigania. Ni wazazi wake na familia yake kwa maana ya mke na watoto wake. Mnaotaka kufanya maandamano haramu mjue mko wenyewe... hakuna Lema, Mange wala Maria. Wao na familia zao wako salama.
 
Si huyu huyu aliyekuwa anahubiri kwa makamanda "Komaa kamanda dhambi kubwa kuliko zote ni uoga"Hasa uoga wenyewe ukiwa ni paranoia tu.
 
Anaandika Godbless Lema kwenye mtandao wa Instagram hivi leo

Mheshimiwa Rais,
Maisha yangu yako katika hatari kubwa. Tafadhali, naomba kwa unyenyekevu mkubwa unisikilize. Ningependa kuishi ili niweze kuwaona watoto wangu wakikua, kuoa na kuolewa mbele ya macho yangu, na ikiwezekana, niweze kufurahia wajukuu wangu ikiwa Mungu atanijalia maisha marefu. Kila mtu anatamani kuishi maisha marefu yenye amani na uzee mwema. Kwa sasa, kuna watu ambao wananifuatilia kwa karibu sana. Hata jioni ya leo, wameonekana maeneo ya nyumbani kwangu, na nina hofu kwamba wangeweza hata kumdhuru mtu yeyote ambaye si mimi. Kwa hali hii, naona ni bora nijiweke mikononi mwa mamlaka kwa hiari yangu kuliko kuendelea kuishi kwa hofu kila siku.Niko tayari kuwekwa mahabusu kwa hiari yangu hadi kipindi cha uchaguzi kipite, kwa sababu naamini kufanya hivyo kutaleta utulivu kwa wazazi wangu, mke wangu Neema, na watoto wangu. Najua watahisi angalau faraja kwamba niko salama.

Ninaomba kwa moyo mkunjufu ulinzi na msaada wako, Mheshimiwa Rais.

View attachment 3489578
Hawa ndio watu wanaojitambua!.
Tukiwaambia watu humu, October 29 hakuna maandamano yoyote, hamuamini, sasa kamanda huyu anajikabidhi mwenyewe kwa Samia, bado kuna mtu anayeamini kuna maandamano yoyote October 29th?.
P
 
Back
Top Bottom