GE2025 Godbless Lema aomba kuwekwa mahabusu kwa hiari mpaka kipindi cha uchaguzi kiishe akihofia maisha yake

GE2025 Godbless Lema aomba kuwekwa mahabusu kwa hiari mpaka kipindi cha uchaguzi kiishe akihofia maisha yake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Anaandika Godbless Lema kwenye mtandao wa Instagram hivi leo

Mheshimiwa Rais,
Maisha yangu yako katika hatari kubwa. Tafadhali, naomba kwa unyenyekevu mkubwa unisikilize. Ningependa kuishi ili niweze kuwaona watoto wangu wakikua, kuoa na kuolewa mbele ya macho yangu, na ikiwezekana, niweze kufurahia wajukuu wangu ikiwa Mungu atanijalia maisha marefu. Kila mtu anatamani kuishi maisha marefu yenye amani na uzee mwema. Kwa sasa, kuna watu ambao wananifuatilia kwa karibu sana. Hata jioni ya leo, wameonekana maeneo ya nyumbani kwangu, na nina hofu kwamba wangeweza hata kumdhuru mtu yeyote ambaye si mimi. Kwa hali hii, naona ni bora nijiweke mikononi mwa mamlaka kwa hiari yangu kuliko kuendelea kuishi kwa hofu kila siku.Niko tayari kuwekwa mahabusu kwa hiari yangu hadi kipindi cha uchaguzi kipite, kwa sababu naamini kufanya hivyo kutaleta utulivu kwa wazazi wangu, mke wangu Neema, na watoto wangu. Najua watahisi angalau faraja kwamba niko salama.

Ninaomba kwa moyo mkunjufu ulinzi na msaada wako, Mheshimiwa Rais.

View attachment 3489578
Duuh hii hatari sasa.
 
Si huyu huyu aliyekuwa anahubiri kwa makamanda "Komaa kamanda dhambi kubwa kuliko zote ni uoga"Hasa uoga wenyewe ukiwa ni paranoia tu.
Tatizo nyinyi ccm hamfanyi siasa bali uuaji. Hebu kama mna siasa za hoja fanyeni hayo kuliko kuteka watu na kuwaua kisa utofauti wa kimawazo. Mmeamua kuongoza bila ya ushindani kwanini wasiokuwepo mchezoni mnawatafuta na kuwapoteza?
 
Mmoja wa watu mnaowategemea wawe mbele ya maandamano ndo huyu anajisalimisha 😂

Hii nchi haihitaji Maandamano kujikomboa, hii nchi inahitaji watu wa kujitoa mhanga kwa kujilipua huku umemkumbatia adui wako, hakuna lingine zaidi ya hilo.
Ni wapi chadema imesema inaandamana?

Kwahiyo kuteka na kupoteza watu ndio kukubalika kwa Samia?
 
natamani niseme anatafuta kiki ila Kwa Tanzania ya Sasa Si ya kufanya masihara na uhai wa mtu.

Unaweza ukambeza wakapita nae kweli pole sana
Yupo mtu humu kamtabiria yeye na familia yake watakufa kwa ajali ya kuchomwa moto
 
Hivi Lema hana glock?asitembee kipimbi kama Polepole.
 
Too Bad.

Ujumbe unaeleweka; lakini kuna wapumbavu wengi watautumia kutisha waTanzania.

Wengine watakwambia si ni heri uwe chawa, ili uepushe maisha yako?

Sasa nami nakushauri; badala ya kuweka taarifa humu ambayo itatumiwa na hawa waovu kwa manufaa yako; kwa usalama wa maisha yako; nakuomba ufungashe mahitaji muhimu; na nenda moja kwa moja kituo cha polisi kajikabidhi hapo mwenyewe; usisubiri kuja kuchukuliwa kuwekwa ndani. Nenda mwenyewe, na waandishi wa habari na ndugu zako muhimu wakusindikize na kushuhudia ukijikabidhi kwa polisi hapo kituoni. Kaa hapo muda wote hadi hapo hali itakapokuwa ni salama kwako kurudi nyumbani.

Sote tunajuwa hali ngumu sana inayo wahusu viongozi wa CHADEMA wakati huu.

Lakini ifahamike, Oktoba 29, uwepo wao mitaani hautahitajika. Hii kazi ilisha kamilika, kilichobaki ni kwa waTanzania kuihitimisha tarehe hiyo.
 
"kutaleta utulivu kwa wazazi wangu, mke wangu Neema, na watoto wangu. Najua watahisi angalau faraja kwamba niko salama".

Hakuna sehemu LEMA kasema anapambania nyumbu za CHADEMA kama wenyewe wanavyodhani anawapigania. Ni wazazi wake na familia yake kwa maana ya mke na watoto wake. Mnaotaka kufanya maandamano haramu mjue mko wenyewe... hakuna Lema, Mange wala Maria. Wao na familia zao wako salama.
Hivi Samia anakupambania wewe; hadi ukaamua kuchukuwa jina lake?
Mtu kama wewe utadiriki vipi kuwaita waTanzania nyumbu, huku wewe ukiwa nguruwe anayefugwa na kulishwa makombo na Samia?
 
Unataka kauli rasmi kutoka chadema kuwa wanaunga mkono maandamano?
Kauli rasmi ndio muhimu ili tujue kama wamepanga maandamano. Ukichukulia hivyo hata ccm wako wanaopenda hayo maandamano.

Kwanza kuteka ni ushamba na kutokujiamini na kile unachokitaka, tumia hoja na maendeleo. Leo hii mnafurahia watu kutekwa na kupotezwa kisa mnanufaika na mfumo wa kutokujushughulisha na uchafu unao endelea nchini. Hebu ni hatua gani ccm na serikali yake imechukua kutokana na watu kupotea? Mwisho wa maji ni tope.
 
alaf cc tuandamane sio, we ukiwa mahala salama sio? hua siwaelwag wanasiasa wa tz


fullstop, kwishaaaa
Hakuna mTanzania atakaye andamana kumfurahisha Lema au kiongozi yeyote wa siasa.; wataandamana kwa sababu wanayakataa maovu na kulinda HAKI zao wenyewe, siyo za Lema na wenzake.
 
Back
Top Bottom