'...nilifurahi mno siku alipoapishwa Samia kuwa Rais na niliamini Nchi ilipata mwarobaini wa yote mabaya yaliyo pata kufanywa na mtangulizi wake. Na hali ile ilifanya nimpigie simu Mstaafu mmoja na kumweleza ninataka kurudi nyumbani.'
'....lakini kwa yanaoyoendelea sasa ndani ya Utawala wa Samia ni ya hovyo kuzidi hata ya Magufuli na hiyo inaleta maana ya Utawala wa Magufuli ni bora kuliko wa Samia jambo ambalo halikutarajiwa kabisa!'
Godbless Lema.
NoTofauti za kauli za Kipindi cha Magufuli na kauli za Kipindi cha Mama Samia.
Kauli za kipindi cha uongozi wa Dr Magufuli.
1. Tunakushukuru Mheshimiwa Rais, kwa mara ya kwanza nchi yetu imepata barabara za juu (fly over). Ni kwa sababu ya usimamizi wako mathubuti tumeona matokeo ya fedha ulizozielekeza kwenye huu mradi mkubwa.
2. Mheshimiwa Rais, tunakushukuru sana kwa kuliona hili, ilikuwa ni aibu kwa taifa lenye umri wa miaka 60 halina ndege bali shirika la ndege lisilokuwa hata na ndege ya mfano tu, sasa umenunua ndege 11 na 8 tayari zipo hapa mbele yako mheshimiwa Rais.
3. Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutuletea huu mradi wa mradi wa nyumba za askari magereza, askari hawa walikuwa wanaishi katika nyumba za kupanga huko mtaani, sasa umewajengea maghorofa hapa Ukonga na juzi ulikuwa pale Magomeni kota ukikagua ujenzi wa ule mradi wa nyumba za wakazi wa eneo hilo. Tunakushuru sana.
4. Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuliona hili la umeme, umeanzisha ujenzi wa wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, na mimi kama Waziri wa Nishati nakuhakikishia ifikapo June 21, 2022 nakukabidhi bwawa hili, Mwenyezi Mungu anisaidie uhai tu. Mwezi November 2021 tunajaza maji katika bwawa hili. Mradi huu umefikia pazuri kiasi ambacho tunaweza kukabidhiwa hata kabla ya tarehe ya mwisho ya makabidhiano.
5. Mheshimiwa Rais, wananchi wanakushukuru sana, sana sana, mwaka wa 5 sasa hawajaonja mgao wa umeme wala maji mijini. Wewe ni shahidi wa hili na wananchi ni mashahidi kwenye hili. Umeme wa uhakika zaidi na wa bei nafuu tunaungoja kutoka bwawa la Mwalimu Nyerere.
6. Mheshimiwa Rais, mradi wa ujenzi wa madaraja ya Busisi, Tanzanite (salenda), terminal III, Masoko katika miji mikubwa na stendi zake za mabasi ni kielelezo kwamba kazi zako zinaonekana. Tafsiri ya "hapa kazi tu" inaonekana kwa vitendo.
7. Mheshimiwa Rais, tunakushukuru kwa hili la mikataba ya madini kusainiwa upya na taufa letu kupata mgawanyo wa asilimia tajwa hapo ambazo hatukuwahi kuzipata tangu taifa hili lianzishwe. Hivi sasa na taifa letu linahisa katika kampuni hii ya TWIGA CORPORATION ambapo tutaluwa ni sehemu ya wamiliki wa kampuni hii ya uchimbaji madini.
8. Mheshimiwa Rais, tunashukuru katika kipindi chako hiki, shule zote zina madawati, madarasa na zaidi umepeleka na vifaa vya maabara za watoto wetu kwa msaada wa usafirishaji wa Jeshi letu la wananchi wa Tanzania. Tunakushukuru sana.
9. Mwaka huu kwa mara ya kwanza mbuzi wa Mtwara wamenyweshwa soda. Inamaana kwamba Mheshimiwa Rais fedha zimewafikia wananchi wa mtwara kwa kuuza dhahabu nyeupe (korosho).
10. Mheshimiwa Rais, kweli hii kauli ya "Hapa kazi tu" inaonekana kwa vitendo, kila sehemu ukipita vumbi limetimuka, kila sehemu ardhi inafukuliwa, barabara zinajengwa, lami inamwagwa, mabwawa yanachimbwa na kujengwa, Mheshimiwa Rais wananchi wanakupenda na huu umati unaouona hapa umesema unahitaji kukusikiliza.
11. Mheshimiwa Rais kwa mara ya kwanza katika Ardhi yetu, tunaijenga reli ya kiwango cha juu, reli ya kiwango cha kimataifa, SGR katika ardhi yetu. Mheshimiwa Rais reli tuliyonayo tulijengewa na wakoloni, na hii nyingine tulijengewa kwa ufadhili (msaada) lakini leo tunajenga kwa fedha zetu wenyewe. Jambo la kujivunia sana hili.
12. Mheshimiwa Rais, vituo vya afya, hospitali kila Wilaya, ni matokeo ya usimamizi wako wa fedha kwa umakini. Tunayaona matunda ya kazi zako, niseme tu kwamba itatuchukua miaka mingi kumpata tena mtu wa aina yako kwani hawazaliwi kila siku.
13. Mheshimiwa Rais, wazo la serikali kuhamia makao makuu Dodoma yalikuwa ya Baba wa Taifa, leo hii tunavyoongea hapa, umehamishia serikali yako hapa, Ikulu imefikia asilimia 90, miezi mitano ijayo tutakuwa tunaizindua ikulu hapa na mafundi na wahandisi ni WAZAWA. Mheshimiwa Rais wewe ni wa kutumainiwa na kuigwa na vizazi vijavyo.
14. Mheshimiwa Rais, nchi hii kweli imekuwa yetu, wamachinga, wachuuzi wadogowadogo, mama ntilie, sasa hivi wanafanya biashara zao kila sehemu na uhuru huo wanao na uhalifu umepungua kama sio kuisha kabisa. Hatuna panda Road tena mtaani. Nchi hii imepiga hatua na uchumi wa kati tumeingia kabla ya wakati.
Kauli za Kipindi cha Mama Samia.
1. Mama unaupiga mwingi, umeimarisha mahusiano ya kimataifa, tunaona sasa ndege za watalii zinaingia kwa wingi.
2. Mheshimiwa Rais, wewe ni kielelezo cha upendo, umeponya wengi majeraha. Umetuponya Mama, Mungu akuweke sana.
3. Mheshimiwa Rais, ule mkopo wako uliotuombea huko Duniani kimataifa tumeupata na fedha zingine tayari zimeanza katika ujenzi wa madarass na vyoo vya shule mbalimbali. Na mimi ni mnufaika katika jimbo langu. Tunakushukuru sana.
4. Mheshimiwa Rais, wewe safiri tu, safiri sana mheshimiwa Rais, acha waseme, wewe safiri tu mheshimiwa Rais. "RC Mkoa wa Dar, Amos Makalla"
5. Mheshimiwa Rais, umefanya mengi sana na makubwa kuliko watangulizi wako, umeupiga mwingi na hatujawahi kuwa na kiongozi kama wewe, tumeyaona, ujenzi wa hili daraja la tanzanite bila nguvu yako tusingekuwa hapa kuzindua hili daraja--- Uzinduzi wa Daraja la Tanzanite 😂😂😂
6. Mheshimiwa Rais, umeupiga mwingi, bila fedha zako ulizozitoa kwa wakati, Ikulu hii mpya hapa Dodoma tusingekuwa hapa; Mheshimiwa rais maamuzi yako ya serikali kuhamia hapa Dodoma yametekelezwa. Tunakushukuru sana.
7. Mheshimiwa Rais, hili la mgao wa umeme ni kutokana na miundombinu kuchakaa kwa muda mrefu bila matengenezo ama ukarabati, umetoa fedha na kazi inaendelea. Tunakupongeza sana.
8. Mheshimiwa Rais, huko nyuma tulidanganywa kuwa mambo yetu yanaweza kwenda bila kusaidiwa na mtu yeyote, kumbe bado nchi yetu hii ni masikini na tunahitaji misaada na mikopo, tunashukuru leo umetuletea mkopo wa mashariti nafuu. Na ule msaada ulioupata kutoka kwenye lile shirika tumeupokea tutaulekeza kwenye ujenzi wa madarasa na vituo vya afya.
9. Mheshimiwa Rais, tunaweza kujiendesha, hili la TOZO tumelipitisha na wananchi walilikubali na ambao hawalikubali wahamie hata Burundi. Tutakulinda na kukutetea na 2025 utashinda kwa kishindo.
10. Mheshimiwa Rais, tumeona matunda ya Royal Tour, watalii wanamiminika. Sasa hivi fedha zipo mitaani. Wanapiga tu kelele ila uhalisia maisha ni rahisi huko mtaani.
11. Umeongeza mishahara kwa wafanyakazi na watumishi wa umma. Umewaponya wengi.
NB: Kuna watu wameniambia niandike mazuri ya awamu ya sita, nimejitahidi sana kuyaandika, hizi 11 za mwisho ni za awamu tuliyonayo. Unaweza kuongeza na zako pia.
Abdoulquarim Malisa
21112022
Kilimanjaro