chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
SERIKALI ya Tanzania, imeshauriwa kurekebisha baadhi ya vifungu vinavyolalamikiwa na wananchi katika mkataba wa ushirikiano wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam, kati yake na Kampuni ya Dubai Port World (DP World).
Ushauri huo umetolewa leo tarehe 19 Juni 2023, katika mjadala wa kulinda na kuendeleza umoja wa kitaifa wakati wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi, uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mjadala ulioandaliwa na Kampuni ya Media Brains, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema, amesema nchi inahitaji uwekezaji lakini Serikali inapaswa irekebishe vifungu hivyo, kisha itoke kwa wananchi kueleza maboresho yaliyofanyika.
“Si dhambi kuleta mwekezaji, katika nchi huwezi kukwepa suala la uwekezaji. Dunia yote inafanya kazi kwa ushirikiano. Nchi inahitaji mwekezaji zaidi ya bandarini, kimsingi uwekezaji hakuna mtu anaukataa na hakuna namna Tanzania inaweza kuishi bila nchi nyingine,” amesema Lema na kuongeza:
“Kwenye ibara ya 4(2) ya makubaliano hayo imeeleza vizuri kwamba Tanzania ikitaka ku-adress jambo lolote la uwekezaji kuhusu bandari hawatamwambia mtu yeyote kwanza isipokuwa Dubai. Sasa mkirekebisha haya mambo halafu mkaja mkawaelewesha watu, mkaondoa vitu vyenye mashaka na watu wa kuwaambia wananchi ni wale wenye uweledi…msitume wale wanaocheza sarakasi bungeni watawaharibia,” amesema.