Godbless Lema: Mungu hawezi kupuuza machozi ya waja wake. Atalipa kwa wakati wake, haki itatimia

Godbless Lema: Mungu hawezi kupuuza machozi ya waja wake. Atalipa kwa wakati wake, haki itatimia

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Godbless Lema anaandika kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X,

Mlisali, mkafunga na mkamwomba Mungu kwa dua na machozi. Maombi yenu yamefika mbinguni. Mnafikiri haya mauaji na mateso ya watoto wenu ndiyo majibu kutoka kwa Mungu? Hapana. Msihofu. Mungu yupo, na bado anafanya kazi yake kwa njia zake.

Kila tone la damu lililomwagika lina thamani mbele zake. Kila kilio, kila pumzi ya mwisho, ni ushahidi wa mateso yasiyo na hatia. Mungu hawezi kupuuza machozi ya waja wake. Atalipa, na kwa wakati wake, haki itatimia.

Msiache kuamini. Jipeni moyo, maana imani ndiyo tumaini letu pekee. Wengi wamekufa, wengi wamepotea, lakini hakuna kinachopotea bure machoni pa Mungu. Siku moja, mtaona kuwa maumivu haya yote hayakuwa ya bure. Siku moja, machozi yatafutwa, na moyo uliojeruhiwa utapata amani. Na hapo mtasema kwa machozi ya furaha “Asante Mungu, kwa sababu ulikuwa nasi hata katika giza.”
 
Mwenyezi Mungu awape pumziko la amani wale wananchi ambao hawakushiriki haya maandamano ya wahalifu ila risasi zikawafikia na kupoteza maisha, na akiangamize kile kizazi cha vibaka kilichokufa kutokana na kuleta machafuko katika ardhi na kuharibu mali za watu.
 
Dick Cheney muuaji wa zaidi ya watu 200,000 huko Iraq, who invented a war out of thin air, died peacefully in his sleep at 84 years of age yesterday.

"Earthly" justice is not guaranteed in the bible

We can only pray for the souls lost
 
Back
Top Bottom