Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
PUMBAVU
Ili uwe Katibu Mkuu sio!
Wewe ni mkimbizi- Canada( Katibu Mkuu)
TAL ni Mkimbizi - Belgium ( Mwenyekiti)
Heche ni Mjaluo wa Kenya ( Makamu Mwenyekiti)
Ndio utakuwa muundo mpya wa chadema🥺😳😳😳😳😳🥺
 
Asante sana Lema kwa maono mazuri ya kujenga taasisi imara.
Wakuu,

Siku ya jana aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini kupitia akaunti yake ya X aliahidi kwamba siku ya leo Tarehe 14 January 2024 atakuwa anazungumza na wanahabari.

Wengi wameshuku kuwa huenda Lema atazungumzia kuhusu Uchaguzi wa CHADEMA na kuainisha ni mgombea gani ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu anamuunga mkono.

Kaa karibu na Jamii Forums kupata updates zote

======================================================

  • Godbless Lema amesema kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti CHADEMA na amemuomba Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe apumzike
"Mimi Mbowe ni kaka yangu, tunajuana. Yeye ni Mchaga na mmachame kama mimi, na familia zetu zinafahamiana, ila kwa uchaguzi ujao wa Mwenyekiti namuomba amuachie Tundu Lissu.

Lissu amekuwa Makamu Mwenyekiti, mnadhimu wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, wanaosema hawezi kuwa Mwenyekiti wanataka nani awe?

Kuna watu wanasema Lissu asiwe Mwenyekiti kwasababu hana pesa, sasa niwaambie katika wakati ambao chama kinapaswa kupata kiongozi asiye na hela ni sasa ili wajumbe wajue kuwa chama hakipaswi kuendeshwa kwa pesa za mtu mmoja bali mobilization kutoka kwa watu. CHADEMA inabidi kitafute namba ya ku-rise fund. Kuna watu waliingia kwenye uongozi bila kuwa na pesa"


  • Aidha Godbless Lema amesema kuwa hatogombea Ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi wa mwaka 2025



View: https://www.youtube.com/live/n4jGmCXtOsc?si=QELvyU3Ewhqvx9gA



 
Mimi hicho ndio sielewi. Kwa vile wameona hastahili kuendelea kuwa Mwenyekiti wafanye kampeni ili wapiga kura wasimchague. Haya ya kumtaka apumzike, oh ni ndugu yangu, oh kabila yangu n.k. halina nafasi hapa. Lema hakuwa na haja ya kuweka press conference kutoa taarifa ya kitu ambacho wote tunakijua. Au anaogopa kuwa Mbowe nae atasema " et tu Lema?"

Mimi ningewashauri kuwa pamoja na kumshauri apumzike wangemwambia pia kuwa apumzike katika kuchangia chama kifedha kupita kiasi. Wanachama watakibeba chama chao.

Amandla...
Ni hiari yake kama shida ni pesa zake sisi kama CHADEMA tunataka timu imara ambayo kila mtu anashiriki kuchangia.
 
Ndivyo inavyopaswa kuwa. Sasa mtathibitisha kuwa mnaweza kukibeba chama chenu. Kama ambavyo mmeweza kumnunulia Lissu gari la kifahari.

Amandla...
Mambo ya gari yametoka wapi wakati mada kuu ni uchaguzi wa mwenyekiti wa CHADEMA?
 
Mbowe ni kiongozi makini hivyo hawataki aaibike bali abaki na heshima aliyojijengea ndani ya chama
Atabaki na heshima baada ya kukachq ushindani? Heri apate kura moja kuliko hiyo heshima ya kinafik. Akijitoe hamtaacha kumsimanga kuwa amewaogopa. Kamtoeni kwenye ballot box na atabaki na heshima ya kuwa ameiishi demokrasia anayoitangaza.

Amandla..
 
Uwezo wa kukiendesha chama kwa michango yenu ni hoja kuu katika huu uchaguzi.

Amandla...
Sisi wanachama wa CHADEMA tumeona hivyo kuliko kuendelea kuikumbatia CCM ambayo haitupendi hata tone bora tuwe na mfumo wetu ambao utaamua mipango ya chi yetu pamoja na mustakabali wa nchi yetu bila kumkumbatia mtu mwenye uwezo wa kifedha hata kama anatupeleka shimoni.
 
Uko sahihi,mimi nilikuwa namwona Paschal Mayala ni mpotoshaji hasa pale alipokuwa anahamasisha Wabunge 19 wa viti maalum bungeni wakubaliwe na Chadema kumbe kuna mambo mengi ya siri siri alikuwa anayajua,Mungu ambariki sana.
Kama Wanataka Upinzani ulio na Walao Nguvu hata kwa 45% Wamchague Lisu
Sio kwamba Lisu Mzuri ila ni Bora ×10 zaidi ya Mbowe!
Kama Majani watapata Kiwewe Ni kuchaguliwa kwa Lisu kuwa Mwenyekiti
 
Me sio mtu wa vyama vyama na siasa ila swali langu ni kwanini CCM ndio wanaumia sana wakisikia lissu anashinda, au kuona watu wanamsapoti Lissu ? Si ni hawa hawa ccm walisema mbowe kakaa muda mrefu ampishe mwingine ?...Baada ya kuona mwingine ni TAL na ni Moto wakuotea mbali wanamtaka tena mbowe ashinde, hahahaha nchi ina matahira wengi sana hii
Hapo sasa.Akina Chiembe,Tlaahtlaah,MamaSmiah2025,ChoiceVariable,Lucas Mwashambwa,Mtoto wa Shule,Makupa nk.
 
Tatizo la Lisu kichwa chake hakijatulia.

Mbowe naye kachoka kwakweli sina tatizo naye apumzike tu.

Chadema inahitaji damu mpya ila wahusika walikosea kutoandaa warithi mapema.

Viongozi wetu wapunguze ubinafsi, nchi ni yetu sote.

Mtu huwezi kaa sehemu moja milele, kupeana nafasi iwe utamaduni wetu wa kudumu.

Hakuna mtu anaweza jimilikishia kitu milele.

Lissu anafaa kwa miaka mitano ijao aisaidie nchi ipate katiba mpya, tume huru. Hapo atakuwa ameliachia Taifa urithi mzuri.

Mbowe hiyo sio agenda yake kabisa kwa sasa yeye sera yake ni kuendelea na maridhiano.
 
Back
Top Bottom