Mimi hicho ndio sielewi. Kwa vile wameona hastahili kuendelea kuwa Mwenyekiti wafanye kampeni ili wapiga kura wasimchague. Haya ya kumtaka apumzike, oh ni ndugu yangu, oh kabila yangu n.k. halina nafasi hapa. Lema hakuwa na haja ya kuweka press conference kutoa taarifa ya kitu ambacho wote tunakijua. Au anaogopa kuwa Mbowe nae atasema " et tu Lema?"
Mimi ningewashauri kuwa pamoja na kumshauri apumzike wangemwambia pia kuwa apumzike katika kuchangia chama kifedha kupita kiasi. Wanachama watakibeba chama chao.
Amandla...