Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Haya yote mnayajua baada ya Lisu kutaka Uenyekiti?

Mlimpa Umakamu akiwa wapi?

Ni hasara sana kwa wazazi waliowazaa na kuwasomesheni.
Kama huyu ndio juha hana hata chembe ya hekima, yaani ukitetewa au kupigiwa debe na huyu jua hauko sawa kichwani kujihusisha nae
 
Kuchangia Chama? Kwani anatoa Pesa zake Mfukoni? Kwanini anafanya Ivo sasa au Chama ni cha familia mpaka anajitoa Kiasi icho?
FAM amehudumu for 21 good years bado ameshindwa Kuweka Mpango mzuri wa fedha kwa taasisi mpaka atoe hela Mfukoni?
Ana mapenzi gani na Chama mpaka atoe hela zake mfukoni au kuna interest nyingine?
Maswali ya msingi haya.
 
Tatizo la Lisu kichwa chake hakijatulia.

Mbowe naye kachoka kwakweli sina tatizo naye apumzike tu.

Chadema inahitaji damu mpya ila wahusika walikosea kutoandaa warithi mapema.

Viongozi wetu wapunguze ubinafsi, nchi ni yetu sote.

Mtu huwezi kaa sehemu moja milele, kupeana nafasi iwe utamaduni wetu wa kudumu.

Hakuna mtu anaweza jimilikishia kitu milele.
Tupe mifano kuonyesha Lissu hajatulia
 
Wakuu,

Siku ya jana aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini kupitia akaunti yake ya X aliahidi kwamba siku ya leo Tarehe 14 January 2024 atakuwa anazungumza na wanahabari.

Wengi wameshuku kuwa huenda Lema atazungumzia kuhusu Uchaguzi wa CHADEMA na kuainisha ni mgombea gani ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu anamuunga mkono.

Kaa karibu na Jamii Forums kupata updates zote

======================================================

  • Godbless Lema amesema kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti CHADEMA na amemuomba Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe apumzike
"Mimi Mbowe ni kaka yangu, tunajuana. Yeye ni Mchaga na mmachame kama mimi, na familia zetu zinafahamiana, ila kwa uchaguzi ujao wa Mwenyekiti namuomba amuachie Tundu Lissu.

Lissu amekuwa Makamu Mwenyekiti, mnadhimu wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, wanaosema hawezi kuwa Mwenyekiti wanataka nani awe?

Kuna watu wanasema Lissu asiwe Mwenyekiti kwasababu hana pesa, sasa niwaambie katika wakati ambao chama kinapaswa kupata kiongozi asiye na hela ni sasa ili wajumbe wajue kuwa chama hakipaswi kuendeshwa kwa pesa za mtu mmoja bali mobilization kutoka kwa watu. CHADEMA inabidi kitafute namba ya ku-rise fund. Kuna watu waliingia kwenye uongozi bila kuwa na pesa"


  • Aidha Godbless Lema amesema kuwa hatogombea Ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi wa mwaka 2025



View: https://www.youtube.com/live/n4jGmCXtOsc?si=QELvyU3Ewhqvx9gA




I salute to Mr Godbless Lema, he has shown leadership and true friendship. A leader is person who is not afraid to speak the truth. And a good friend is a person whose not afraid to tell the truth to anyone and everyone. And if Mbowe is smart he should listen to those who are opposing him. They are his true friends.
 
I salute to Mr Godbless Lema, he has shown leadership and true friendship. A leader is person who is not afraid to speak the truth. And a good friend is a person whose not afraid to tell the truth to anyone and everyone. And if Mbowe is smart he should listen to those who are opposing him. They are his true friends.
Hakika.
 
nabii mnyang'anyi mashuhuri wa malori hana ushawishi wala credibility ya kuskizwa na wanachadema kuelekea uchaguzi wao muhimu wa kitaifa,

nadhani inafaa zaidi aendelee kupuuzwa kama alivyo puuzwa na wana Arusha wa chadema 🐒
Wewe mzee wa hovyo na wewe ni mwanachadema hadi uwasemee?
Aisee hatutaacha kuona vihoja kwa vizee vya CCM
 
Nikweli anamaanisha? Maana nnavyowajua wachagga asilimia kubwa wanabebana
 
Hakuna anayekataa kumpigia kura Mbowe bali ni ushauri tu watu wanatoa,usishangae kwenye sanduku la kura akaibuka kidedea,kinachotusikitisha na kutufikirisha sana ni namna jinsi makada wa ccm wanavyompambania Mbowe ili aendelee tu kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wakati Wanachadema wanashauri Mbowe apumzike na abaki kuwa mshauri mkuu na vile vile mjenzi wa chama .
Hamuwezi kuwa na keki na kuila. Kama kuna kada wa Chadema atakayempigia kura Mbowe kwa sababu anapigiwa debe na CCM basi huyo toka mwanzo hana mapenzi mema na chama chake. Ni wafuasi wa Lissu ndio waliougeuza huu uchaguzi kuwa wa kitaifa na sio wa kichama. Kwa hali hiyo hamuwezi kumzuia mtu yeyote kumpigia debe mtu anayemtaka hata kama lengo lake ni kubomoa chama.
Mimi sielewi hilo la kumtaka Mbowe awe mjenzi wa chama wakati mnasema ama hajafanya lolote wakati wa uongozi wake au amefanya vya kutosha awaachie wengine kazi ya kujenga chama.
FAFO

Amandla...
 
Kuchangia Chama? Kwani anatoa Pesa zake Mfukoni? Kwanini anafanya Ivo sasa au Chama ni cha familia mpaka anajitoa Kiasi icho?
FAM amehudumu for 21 good years bado ameshindwa Kuweka Mpango mzuri wa fedha kwa taasisi mpaka atoe hela Mfukoni?
Ana mapenzi gani na Chama mpaka atoe hela zake mfukoni au kuna interest nyingine?
Kwani unapochangia kanisa au msikiti ni kwa sababu ni vya ndugu zako? Hakuna chama cha siasa katika nchi ya kidemokrasia kinachofanya biashara. Muundo wake hauruhusu hilo. CCM walikuwa na Sukita ikafa. Walirithi viwanja vya michezo kibao ambavyo navyo wameshindwa kuviendeleza.Na hii miradi yao mingine inadumu kwa sababu tu ni chama dola. Kikiachia dola nayo itakufa.
Vyama vya siasa vinategemea michango. Ni hilo tu.

Amandla...
 
Ukiona mpaka watu wako wa karibu wanatoka kukupinga hadharani kwa mambo ambayo wangeweza kukuambia faragha, jitafakari sana.

Lema umeonesha kwa vitendo wewe ni mkweli na muadilifu, pamoja na mafungamano yote na Mwenyekiti ila umesimamia ukweli.
Respect!
 
Huu uchaguzi wao kama ukiisha halafu wakauchukulia kama part tu ya demokrasia bila kutengana ,wataibuka na nguvu kubwa mno.
Sio Rahisi Lisu na team yake wamewachezea sana rafu wenzao na kuchafua sana sifa ya Chadema bila kutoa ushahidi wowote hakikika

Si tu wamemchafua Mbowe bali na Chadema mbele ya macho ya public kukionyesha kama chama cha hovyo kiluchojaa rushwa kuwa vionhozi wake wanahongana na kuhongeka kirahisi

Kwenye scenario kama hiyo sio Rahisi uchaguzi ukipita wakawa wamoja
 
Back
Top Bottom