Godbless Lema: Rais Samia na Makamba wanatafuta mbinu za kumbebesha lawama hayati Magufuli

Godbless Lema: Rais Samia na Makamba wanatafuta mbinu za kumbebesha lawama hayati Magufuli

Hakika. Huu mshikamano uongezwe hata kwa mambo mengine ya msingi kama, Katiba mpya na Bora, Tume huru ya uchaguzi. Hivi vyote ni kwa faida ya watanzania. Hawa wanasiasa wanatudanganya kwa maneno yao kwa faida yao, kwa sababu wameshika "keki" mkononi, lakini sisi tuweke kwanza Taifa letu mbele.

KATIBA Bora na Tume huru ya uchaguzi ni kwa watanzania. Hali tuliyopita nayo kwenye uchaguzi wa 2020 kila mmoja wetu anaiona kwamba haina afya kwa Taifa.

Cc YEHODAYA johnthebaptist
Shida inayokabili wananchi Kwa Sasa Ni umeme na maji sio katiba mpya au tume huru watu wanataka umeme na maji usitutoe kwenye reli.Umeme na maji unahitajika na wenye vyama na wasio na vyama ndio maana Kuna mshikamano sababu Ni common problem yenye athari kwa wore.Lema kaliona na nimpongeze .Kaibua tatizo common linaloweza pata support toka kwa kila mtanzania bila kujali chama alichopo Cha siasa au Hana chama au hataki siasa kabisa iwe ya katiba mpya au tume huru
 
Mnaabudu maiti, LAANAKUM
Unanichokoza Mimi? Utaniweza ? Wewe mwenyewe mwabudu maiti Mohamed kutwa kumtaja na kumwombea .LaanKum wewe Mohamed Yuko hai?

Mohamed maiti na Magufuli maiti lakini kutwa ukienda swala mdomoni huachi kuongelea Marehemu Mohamed Laana Kum wewe
 
Unanichokoza Mimi? Utaniweza ? Wewe mwenyewe mwabudu maiti Mohamed kutwa kumtaja na kumwombea .LaanKum wewe Mohamed Yuko hai?

Mohamed maiti na Magufuli maiti
Uwezi fanananisha mitume na Magufuli mnakosea sana.
 
Unanichokoza Mimi? Utaniweza ? Wewe mwenyewe mwabudu maiti Mohamed kutwa kumtaja na kumwombea .LaanKum wewe Mohamed Yuko hai?

Mohamed maiti na Magufuli maiti
Huyo mvaa madera na mwabudu majini mwache akuchokoze sisi tunamwabudu aliyeshinda kifo pale msalabani anatuletea ngojera za kuabudu mtu aliyekufa na hasikii! Wao kazi yao wanamshabikia kwa sababu ni Rais Mwislam sijui wakikosa maji au umeme huwa ankuja kuwasaidia!
 
Wakati Magufuli Yuko hai ulisema unampinga Magu kwa Mambo yake yote,Leo unaonekana kumtetea 🤣🤣,UPINZANI WA TANZANIA HAUNA MWELEKEO
 
Nikajua kaja hata na hiyo mbinu kumbe Domo Domo tuu kama kawaida.

Magu hawezi kukwepa lawama kwa namna yeyote,miaka 6 hajajenga mtambo wa umeme wa gas in case kuna dharura kama hizi wakati anajua kwamba Bwawa lake haijulikani lini litakamilika na hata likikamilika ,je litakuwa immune na ukame?

Sio mara ya kwanza Tzn kubwa na ukame lakini hakufanya lolote la kukabili dharura.

Mwisho serikali haijakaa kimya imetoa mbinu hizo ikiwa ni kuwekeza kwenye gas na kuwasha mitambo ya mafuta kwa ajili ya dharura.Unaleta mchezo na mgwt 300 kuondoka kwenye grid?
Team Maushungi, Team Urojo... [emoji2781]
 
LEEMA anaona watanzania wengi wanamkubali Magu naye kaona afuate upepo ulipo
Siyo suala la kumkubali Magufuli, ni suala la ukweli.

Kama kiongozi anayekuwepo madarakani, mambo yakienda vibaya anaanza kujitetea kwa kuonesha watangulizi wake ndiyo wanaosababisha, sasa wewe upo kwenye hiyo nafasi kufanya nini?

Kiongozi unapochukua nafasi ya uongozi, unakubali hali iliyopo, unafanya kazi kuanzia hapo kuleta ufanisi. Hiyo haijalishi kama waliotangulia walikosea au la! Kila awamu watafanya makosa na mazuri, chukua mazuri, mabaya yarekebishe. Haiingii akilini, unashindwa kurekebisha, unabakia kusema aliyetangulia ndiye aliyesababisha.

Ujumbe muhimu ni kwamba, wananchi tunataka umeme wa uhakika, upungufu wa mvua siyo sababu ya kukosa umeme, kuna nchi kama Chile mvua zilinyesha mara ya mwisho mwaka 1954, lakini miji yao kila mahali green, zabibu zinastawi kwa namna ya ajabu, umeme na maji kukatika ni mwiko.

Kudai kuna upungufu wa mvua siyo sababu, kwani huko serikalini hawajui kuwa kuna uwezekano wa kukosa mvua? Wamekuwa na mipango gani ya kupambana na tatizo hili ambalo linafahamika Duniani kote? Au uwezo wa kufikiri na kuoanga, huko serikalini unaishia mita 2?
 
Team Maushungi, Team Urojo... [emoji2781]
Ulitaka niwe timu Mbowe mkishilikiana na timu 👇

2952061_JamiiForums569115795.jpg
 
Sasa Lema pilipili ya shamba ya kuwashia nini? Wewe jadidili mambo ya Ontario huko.

Lakini si wewe ulimtabiria kifo Mzee wetu? Ulimuona hafai? Je, upendo wako kwake umeanza lini?
 
Kwa hili mimi nakubaliana na God bless Lema.
Kuna mkakati wa kuihujumu TANESCO ili msoga team ikamilishe hujuma zao za tangia awali.
Msishangae kusikia TANESCO ikiuzwa katika serikali awamu ya sita.
Ndio maana Makamba ameivunja Bodi ya TANESCO na kuondoa wajumbe waadilifu na kuwaleta kina Maajar na Mchechu,wapigaji tupu.
Anamtoa Mwinuka Proffesional na kutuletea mswahili Chande Maharage.
 
Wakimbizi wa kisiasa huwa wanajipa kazi moja siku zote, ya kuwa wachonganishi.
Team mwendazake hapa umepiga bonge la U_turn. Hata hili jina unalotumia hapa ni wazi unalitumia kwa malengo rasmi. Endelea kupasha, huenda ukakumbukwa.
 
Sasa Lema pilipili ya shamba ya kuwashia nini? Wewe jadidili mambo ya Ontario huko.

Lakini si wewe ulimtabiria kifo Mzee wetu? Ulimuona hafai? Je, upendo wako kwake umeanza lini?
Unabii ni maono, hayana uhusiano na kumpenda au kumchukia mtu. Unabii unalenga kutoa onyo. Onyo utaisikia na kulifuata, ni suala jingine. Ni watawala wachache sana, katika historia, waliwahi kuzingatia maonyo ya kinabii.
 
Sasa asipige yowe za umeme sijui marehemu anasingiziwa, ajikite na kutabiri.
Nadhani ujumbe wa Lema upo wazi - watawala wa sasa wafanye kazi, na siyo kukimbia udhaifu wao kwa kumtupia lawama marehemu. Marehemu awe alitenda vema au vibaya, haituhusu, wao wanatakiwa watimize wajibu wao, au waseme tu kuwa wameshindwa. Ukiwa dhaifu, huwezi kuondokana na udhaifu kwa kuonesha madhaifu ya mwingine.
 
Back
Top Bottom