Siyo suala la kumkubali Magufuli, ni suala la ukweli.
Kama kiongozi anayekuwepo madarakani, mambo yakienda vibaya anaanza kujitetea kwa kuonesha watangulizi wake ndiyo wanaosababisha, sasa wewe upo kwenye hiyo nafasi kufanya nini?
Kiongozi unapochukua nafasi ya uongozi, unakubali hali iliyopo, unafanya kazi kuanzia hapo kuleta ufanisi. Hiyo haijalishi kama waliotangulia walikosea au la! Kila awamu watafanya makosa na mazuri, chukua mazuri, mabaya yarekebishe. Haiingii akilini, unashindwa kurekebisha, unabakia kusema aliyetangulia ndiye aliyesababisha.
Ujumbe muhimu ni kwamba, wananchi tunataka umeme wa uhakika, upungufu wa mvua siyo sababu ya kukosa umeme, kuna nchi kama Chile mvua zilinyesha mara ya mwisho mwaka 1954, lakini miji yao kila mahali green, zabibu zinastawi kwa namna ya ajabu, umeme na maji kukatika ni mwiko.
Kudai kuna upungufu wa mvua siyo sababu, kwani huko serikalini hawajui kuwa kuna uwezekano wa kukosa mvua? Wamekuwa na mipango gani ya kupambana na tatizo hili ambalo linafahamika Duniani kote? Au uwezo wa kufikiri na kuoanga, huko serikalini unaishia mita 2?