Mkuu nimekupa like maana wewe ni mpenzi wa chama na mlengo fulani.
Kuna watu hapa nchini hawana vyama na wanatoboa tu bila hata kupepesa macho.
Na kuna akina na nyie mnaoyatazama maisha hapa nchini na miwani ya vyama.
Mnateseka bure!
Sjaona mhindi akishabikia maisha ya siasa, lakini wahindi ndio kundi pekee lenye kuendesha magari ya nguvu, yakiwemo VX.
Na kwa taarifa yako, mimi ni mswahili nashabikia siasa kwa unazi tu, lakini ng'o hutaniona nimeingia siasa kichwa kichwa , biashara yangu hairuhusu.
Tatizo letu sisi waafrika ni kufikiri kutoboa ni kwenda nje na kwamba kule ni maisha kama paradiso, kula nakunywa na barabara zimetandikwa dhahabu!
Hamuelewi kuwa paradiso ni hapa hapa Tanzania.
Mimi nimeishi Ulya!
Najua maisha ya kule.
Kama huna noti wewe sawa sawa na takataka tu.
Sasa mheshimiwa Lema ukimbizi una mwisho, Mgeni siku ya kwanza, siku ya pili atapewa jembe akalime!
Simwonei wivu, namhurumia tu maana nayajua maisha ya huko.
Mkuu 'Jidu', mbona unaturudisha tulikokwishatoka wewe na mimi siku nyingi humu JF. Tulishaelezana kwa uwazi kabisa kila mmoja wetu anakosimamia, halafu leo unanigeuza tena na kuniita "mpenzi wa chama na mlengo fulani"?
Ngoja nirudie kwa kifupi ili kukukumbusha: ushabiki wangu ni Tanzania pekee. Niliwahi kuwa shabiki wa CCM kilipokuwa chama cha wakulima na wafanya kazi na sio kile kilichowahi kuwepo kikiwa "Chama cha Huyu Mwenzetu" na wala siyo hiki "Chama Kilichobinafsishwa kwa mtu mmoja." Mbali na hivyo, sijawahi kuwa shabiki wa chama chochote kati ya hivi vipya. Unapoona tunafanya utetezi juu yao, sio kwa sababu ni 'wapenzi' au 'wanazi'; bali tunasikitishwa na maonezi wanayofanyiwa wao wakiwa ni waTanzania wenzetu. Hili ndilo linalotuumiza.
Wewe ni msahaulifu kiasi hiki kweli, kwamba unasahau yote na leo unanipakazia, ati "wew ni mpenzi wa chama na mlengo fulani"? na wakati huo huo unasahau uliyoungama mbele yangu wakati ule; na huku leo unageuka jiwe la chumvi, eti "nashabikia siasa kwa unazi tu", hata sijui huko ndio kufanya nini?
Michango yako humu JF inajieleza yenyewe; na ya kwangu inajulikana bila kificho; halafu leo unageuka na kunipaka matope?
Hayo ya ulaya, sio peke yako umeishi huko, kama kweli umewahi kuishi huko. Kuishi ulaya sio hoja, unaweza ukaishi huko na ukawa 'miserable' kama unaamua kujiweka jela mwenyewe. Kama hayo ndiyo maisha uliyoishi, usidhani kila mtu anayekwenda huko anayaishi kama wewe ulivyoyaishi.
Huko kutokuwa na 'noti' sio huko tu, hata hapa kama huna noti maisha yatakufanya uonekane kama "takataka" kama ulivyoandika mwenyewe. Kuwa "takataka" kunatokea mahali popote, iwe ulaya au hapahapa. Na mbaya zaidi ni kuwa "takataka" huku ukiwa mateka!
Tatizo letu sisi waafrika ni kufikiri kutoboa ni kwenda nje na kwamba kule ni maisha kama paradiso, kula nakunywa na barabara zimetandikwa dhahabu!
Hamuelewi kuwa paradiso ni hapa hapa Tanzania.
"Paradiso" ya kuwekwa 'mateka'. Hiyo paradiso yako ni ya ajabu. Tanzania ingekuwa 'paradiso' sana, licha ya umaskini unaowakabili wananchi wetu, kama kusingekuwepo na haya ya kufanywa mateka ndani ya nchi yetu wenyewe.