Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana

Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana

Habari :
Kumekuwa na taharuki tangu jana, baada ya kutoka kwa taarifa ya kuvamiwa kwa mwenyekiti wa UTG, na kada wa chadema, kamanda Malisa GJ. Taarifa hizo ni za kweli, na polisi walifika usiku wa Saa 9 kutoa msaada. Leo asubuhi tumewasiliana na RPC na ametoa maelezo nini kifanyike. Hivyo hadi muda huu Malisa yupo salama na anashughulika na utaratibu wa kipolisi.

Imetolewa na :-
Noel Shao
N/Katibu Mkuu UTG.
 
Mtu unavamiwaje unaanza kupost insta,facebook,JF na whatsapp??
Ulitaka taarifa zitolewe wapi. Bashite mkubwa ziro wewe mlitaka kumsanane sema dili imebuma kisha police ccm wakajigeuza kuwa wamekuja kutoa usalama baada ya dili yao ya kuteka imebuma

Swissme
 
Pole sana MALISA GJ . Tunaomba taarifa ikamilike.
Namna ilivyo happen
Jinsi alivyo escape
Mini madai ya wavamizi
 
Uvccm wajichunge sana na hii tabia walioanzisha ya kuteka watanzania na kuwauwa

Swissme
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mtu unavamiwaje unaanza kupost insta,facebook,JF na whatsapp??
Kusambaza taarifa haraka inaweza kumsaidia mhusika. Msaada unaweza kupatikana toka kona mbalimbali baada ya watu wengi kupata taarifa maana inawezekana aliyepokea ujumbe au kushuhudia tukio likianza akashindwa kufika mahali sahihi pa msaada kwa wakati. Pia inaweza kutokea hata wavamizi kuingiwa hofu pale ambapo watagundua uvamizi wao tayari unasambaa mtandaoni hata kabla hawajafanikiwa kuingia ndani.

Ila taarifa iliyotolewa ni nusu maana hata hatujaambiwa kama polisi walipofika:
1. Walikuta wavamizi wameshaingia ndani?
2. Walikuta wameshaondoka?
3. Kuna madhara yoyote (maisha na mali) yaliyotokana na uvamizi huo?
 
Pole sana Kaka Malisa. Mungu azidi kukulinda.
 
Watu wasiojulikana kama kawaida yao
Malisa awe makini sana kipindi hiki
 
Mtu unavamiwaje unaanza kupost insta,facebook,JF na whatsapp??
Mkuu kwa nyakati hizi za sasa, hizo njia ndio safe zaidi kuliko hapo polisi maana nao hawaaminiki siku hizi.
 
Weka picha yake tumuone.

Siku hizi kila mtu anatafutwa na usalama.

BREAKING NEWS

NYUMBA YA MALISSA GJ IMEVAMIWA MUDA HUU NA WATU WASIOJULIKANA.

Wako hapo mpk muda huu wakilazimisha milango ifunguliwe hili waingie ndani

Msaada tafadhali
______________________________________________

Updates

Habari makamanda...

Malisa yupo salama..

tuliwasiliana nae mpk mida ya saa kumi alfajiri na kutokana na uchunguzi wa swali iligundulika kua ni majambazi, anapoishi pembeni yake kuna godown na mida hiyo kuna gari ilikuja kupakia mizgo, sasa inasemekana jamaa walikua wanafuatilia hilo gari, bado hatujajua dhamira yao mpaka kwenda kwa Malisa.

Mwenyekiti wetu mkoa wa Tabora aliwasiliana na RPC mkoa na akaagiza OCD vijana wake waende kwa Malisa, kama mjuavyo kua watu wa usalama wanamtafuta kwa muda mrefu, hivyo tukakubaliana kua asikubali kutoka na ikiwezekana azime simu zake zote halafu asubuhi hii tutajua nini la kufanya tukiwa wote.

Nadhan kwa ufupi nimewaondo hofu ya swali.
 
Habari :
Kumekuwa na taharuki tangu jana, baada ya kutoka kwa taarifa ya kuvamiwa kwa mwenyekiti wa UTG, na kada wa chadema, kamanda Malisa GJ. Taarifa hizo ni za kweli, na polisi walifika usiku wa Saa 9 kutoa msaada. Leo asubuhi tumewasiliana na RPC na ametoa maelezo nini kifanyike. Hivyo hadi muda huu Malisa yupo salama na anashughulika na utaratibu wa kipolisi.

Imetolewa na :-
Noel Shao
N/Katibu Mkuu UTG.
akina nai walioenda wakamata, walikimbia?
 
Back
Top Bottom