God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema?

Kosa kubwa linalofanywa na wengi wanapomjadili Mungu ni kwamba kufikiri anawaza kama mawazo yetu. Kama apo Vinci unafikiri mungu anajua jema na baya, kitu ambacho sio kweli, kwake yeye yupo beyond good and evil. Good and evil are product of human effort to make sense of this world, ndio maana unakuta jamii nyingi tunatofautiana juu ya kipi ni chema n kipi ni kibaya, mfano kuna jamii kula nguruwe ni soo, pia kuna jamii kaka kumowa ndugue ni sawa kabisa, au kijana wa kiume aliyebalehe kumchukua dogo wa kiume na kuishi nae kama mkewe ni sawa tu.

Cha kujua sir God katuweka tuexpress our truest self, na pia kushangaa na kutukuza utukufu wake anaonyesha kila sehemu ukiangazia macho. siku atakapokuja kuvuna mbegu zakee kuna watu kwa kushangaa taya zao zitagusa chini.
 
Freewill ni illusion tu wala haipo in reality

Nataka nianze na Mfano wako wa kusema malaika hawana freewill na kwamba wamekuwa programmed kutii kile ambacho Mungu anawaagiza

Kumbuka freewill ni dhana yenye kuambatana na selection ya mambo mawili "ubaya na uzuri"

Sasa kama malaika hawana freewill na kwamba hawawezi kufanya ubaya, unaelezeaje ishu ya malaika muovu lucifer ambaye alifanya ubaya kwa kumsaliti Mungu?

Alitumia njia gani kufanya ubaya huo bila kuhusisha freewill?

Vipi kuhusu robo tatu ya malaika walioshawishiwa na shetani na kuungana naye katika mkakati wa kumsaliti Mungu na kupelekea vita huko mbinguni?

Hayo yote yaliwezekanaje kufanyika kama malaika wako programmed na hawana freewill ya kuwawezesha kuchagua kufanya ubaya?

Mnaofikiria kwamba mateso na migogoro ipo duniani na kwmaba mbinguni ni raha tu, mnabidi mkumbuke kuwa vita ya kwanza ilianzia huko huko

Mpaka hapo tushajua mbinguni sio sehemu salama na kwamba kuepuka kwako vikwazo huku duniani unakumbushwa kuwa na mwendelezo huo huo wa kinidhamu hata ukiwa huko.
Kuna hoja moja huwa inahoji ... Unafikiri maisha ya huko mbinguni yatakuwa tofauti na ya hapa duniani. Mostly yatakuwa kama haya haya cuz endapo muumba atawaedit sana alio wachagua basi watakuwa sio binadamu tena
 
Labda tukiiweka kihesabu tuseme ukiwa upo katika pointi fulani A/B/au Z. Mungu anafahamu mwisho wa wewe ukiamua kujongea katika uelekeo wowote hadi mwisho wako, infinity circle of directions.

Hata ukiamua kurudi nyuma au kwenda mbele kidogo halafu ukasimama. Mungu anajua machaguo yote ya maamuzi yako na matokeo ya mchanganyiko wa maamuzi hayo yote mpaka mwisho.

Mfano ukiwa upo DSM, Mungu anajua mikoa yote utakaweza kuamua kwenda na matokeo ya kila kachaguo utakakochagua. Mfano ukachagua kwenda arusha badala ya Mwanza, hapo Mungu atakuwa anajua hadi jina la mjukuu wako kuitwa Manka na wewe kufariki kwa kudondokewa na mgomba uzeeni kwako!
Lakini pia hapohapo anafahamu mtiririko wa machaguo yako ya kwenda Mwanza hadi kumiliki boti za uvuvi na kuwa mbunge wa Misungwi. So ukiamua kwenda Mwanza hautampoteza maboya maana anajua kabisa matokeo yote ya chaguo hilo hadi na wewe kujenga wilaya ya Misungwi na kuwa mvuvi. Na mjukuu wako kuitwa Masanja

Nahisi kila pointi unayoigusa unazidi kujiwekea mazingira ya kuchagua kinamna fulani kutoka katika infinity alternatives ambazo zzooooooote Mungu anazijua matokeo yake. Hakulazimishi kuchagua njia yoyote, tena hata hafuatilii unachaguachaguaje. In fact ukitaka uweze samtaimu jichukulie wewe mwenyewe ni sehemu ya Mungu na mnafanya maamuzi pamoja ya maisha yenu muyaendesheje kwa kushirikiana.
 
binadamu ni roho, baada ya roho kuacha mwili mwili huoza, hivyo roho ndio hubaki sehemu mabayo itasubiri kusomewa hukumu yake. Mungu atahukumu roho, ili uweze kuishi milele mwanadamu lazima uwe katikati mfumo wa roho.

Sasa shida inakuja hapa!

-Je siku ya kuhukumiwa mimi nitakua najifahamu kua ndio mimi? (Kumbuka roho ndio inabeba taarifa zako zote/kwenye roho ndio kuna mind ambayo inahusika nawe kujitambua)

-Kama nitajitambua nitawezaje kuishi heaven kwa raha huku wazazi na ndugu zangu wapendwa nimewashuhudia wakienda kuchomwa moto?

-Labda siku hiyo tutakua hatutambuani, kama hatutambuani it means hata mimi sitajitambua. Sasa kama mimi sitajitambua nitajuaje kama ni mimi ndio niko peponi au motoni? (Kumbuka kama nikijitambua sitafurahia kwenda heaven wakati my wife and any of my kids they're suffering in hell)

-Sawa nitajitambua, nitakubali na matokeo ndigu zangu wateseke motoni. Je wale wanawake 70 bikra nitawafaidi vipi wakati mimi nitakua katika mfumo wa roho, roho haiwezi kufanya mapenzi and lastly huko Mungu hawezi kuparuhusu tupafanye danguro. (Kumbuka Mbinguni tutakua kwa mfumo wa roho, sio mwili maana mwili huharibika. Kama tukiwa nao basi hatutoishi huko milele, mwili ni compatible kwa maisha ya Duniani tu)
 
Nikija kwenye ishu ya freewill yenyewe hapa napo kuna mambo mengi ya kuzungumza.

Kama ulivyosema kuwa hujapata majibu ya kuridhisha, naweza nikasema imekuwa inatokea hivyo kwasababu watu waliokuwa wanajaribu kukupa majibu walilenga zaidi kuifanya freewill ionekane ni halisia

Kama freewill ni uhuru wa kuchagua wema na ubaya ipo basi hatupaswi kuingiliwa kimaamuzi ili kuonesha tupo free

Uhuru wa kuchagua haupaswi kuambatana na mipaka, kusema hiki sawa na hiki sio sawa ukifanya nakuadhibu, huo sio uhuru hiyo ni amri.

Sasa Mungu kasema amekup uhuru wa kuchagua kumuabudu yeye au shetani halafu ukichagua kumuabudu shetani Mungu huyu anakupa adhabu kali sana ya kuchomwa moto. Je huo ni uhuru kweli?

Katika jamii ikitokea tu kuna mtu kamwambia mke wake nimekuoa uhuru wa kuchagua kufanya chochote utakacho ila ikitokea umechagua kuniacha nitakumwaga ubongo kwa maumivu makali.

Mtu huyo akisikika na watu, watu watamuita mkatili asiye na ubinadamu, ataitwa mnyama asiye na huruma, ataitwa mzushi kwa kutoa ahadi ya uwongo

Lakini kitu kama hicho hicho akikifanya Mungu anaitwa mwenye upendo wote, mjuzi wa vingi na mwenye rehema

Kwanini?
Did you use your freewill to write this comment, or you were programmed to write it?
 
Labda tukiiweka kihesabu tuseme ukiwa upo katika pointi fulani A/B/au Z. Mungu anafahamu mwisho wa wewe ukiamua kujongea katika uelekeo wowote hadi mwisho wako, infinity circle of directions.

Hata ukiamua kurudi nyuma au kwenda mbele kidogo halafu ukasimama. Mungu anajua machaguo yote ya maamuzi yako na matokeo ya mchanganyiko wa maamuzi hayo yote mpaka mwisho.

Mfano ukiwa upo DSM, Mungu anajua mikoa yote utakaweza kuamua kwenda na matokeo ya kila kachaguo utakakochagua. Mfano ukachagua kwenda arusha badala ya Mwanza, hapo Mungu atakuwa anajua hadi jina la mjukuu wako kuitwa Manka na wewe kufariki kwa kudondokewa na mgomba uzeeni kwako!
Lakini pia hapohapo anafahamu mtiririko wa machaguo yako ya kwenda Mwanza hadi kumiliki boti za uvuvi na kuwa mbunge wa Misungwi. So ukiamua kwenda Mwanza hautampoteza maboya maana anajua kabisa matokeo yote ya chaguo hilo hadi na wewe kujenga wilaya ya Misungwi na kuwa mvuvi. Na mjukuu wako kuitwa Masanja

Nahisi kila pointi unayoigusa unazidi kujiwekea mazingira ya kuchagua kinamna fulani kutoka katika infinity alternatives ambazo zzooooooote Mungu anazijua matokeo yake. Hakulazimishi kuchagua njia yoyote, tena hata hafuatilii unachaguachaguaje. In fact ukitaka uweze samtaimu jichukulie wewe mwenyewe ni sehemu ya Mungu na mnafanya maamuzi pamoja ya maisha yenu muyaendesheje kwa kushirikiana.
I find it funny
Hahaaaaa
 
Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni? Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo. Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?
Ndiyo, ni kweli Mungu anajua kila kitu kilichopita, kilichopo na kijacho.

Anajua kama wewe ni mwema au utakuwa mwema, na kinyume chake. Anajua kabisa kama utaenda mbinguni ama motoni.

Hii ni moja ya sifa (attribute) ya Mungu kujua yote (all-knowing - omniscient).

Ni kweli kabisa unao uwezo wa kubadili hatma (fate) yako. Mwenyezi Mungu amekupa uwezo, nguvu na mamlaka ya kufanya uamuzi uwe mwema ama muovu kupitia freewill.

Uchaguzi wako huru ndio unaoamua hatma yako, siyo ujuzi wa Mungu.

Ipo hivi; Mungu alipotuumba alipenda sana tuwe wema kama alivyo. Moja ya sifa aliyonayo ni uhuru, akaamua kutushirikisha uhuru huo kwa kutupa hiyo freewill.

Hata hivyo, kwa kuwa anapenda sana tuwe wema "kama" yeye, akatuongezea akili, utashi na dhamiri.

Akili itusaidie kutambua mema na maovu na utashi utusaidie kuchagua kuwa wema. Akatuwekea dhamiri ambayo daima "hutuzawadia" tukiamua kuwa wema na "hutuadhibu" tunapoamua kuwa waovu.

Kumbe akili, utashi na dhamiri hutupa tahadhari kabla ya kufanya uamuzi wetu, hutu-influence kufanya uamuzi mwema na hutuhukumu kwa haki kadiri ya uchaguzi wetu.

Ujuzi wa Mungu juu ya tunakoelekea hauingilii maamuzi yetu wala siyo uthibitisho wa yeye kutupangia maamuzi yetu, bali ni uthibitisho wa uhuru wa kweli tuliopewa na Mungu.

Uhuru ambao tunaweza kuamua kutofautiana naye na bado asiingilie uamuzi wetu. Kuna uhuru zaidi ya huo?

Jitahidi kusoma concept ya Predestination, utaelewa zaidi.
 
Freewill ni illusion tu wala haipo in reality

Nataka nianze na Mfano wako wa kusema malaika hawana freewill na kwamba wamekuwa programmed kutii kile ambacho Mungu anawaagiza

Kumbuka freewill ni dhana yenye kuambatana na selection ya mambo mawili "ubaya na uzuri"

Sasa kama malaika hawana freewill na kwamba hawawezi kufanya ubaya, unaelezeaje ishu ya malaika muovu lucifer ambaye alifanya ubaya kwa kumsaliti Mungu?

Alitumia njia gani kufanya ubaya huo bila kuhusisha freewill?

Vipi kuhusu robo tatu ya malaika walioshawishiwa na shetani na kuungana naye katika mkakati wa kumsaliti Mungu na kupelekea vita huko mbinguni?

Hayo yote yaliwezekanaje kufanyika kama malaika wako programmed na hawana freewill ya kuwawezesha kuchagua kufanya ubaya?

Mnaofikiria kwamba mateso na migogoro ipo duniani na kwmaba mbinguni ni raha tu, mnabidi mkumbuke kuwa vita ya kwanza ilianzia huko huko

Mpaka hapo tushajua mbinguni sio sehemu salama na kwamba kuepuka kwako vikwazo huku duniani unakumbushwa kuwa na mwendelezo huo huo wa kinidhamu hata ukiwa huko.
Uamuzi huu wa malaika unathibitisha dhana ya freewill.

Kwamba; malaika wote walikuwa na uhuru wa ama kuchagua kuwa wema kama Mungu alivyo ama kuchagua kuwa waovu.

Theluthi mbili walichagua kwa uhuru na utashi wao kuwa wema kama alivyo Mungu, na theluthi moja iliyobaki nao kwa uhuru na utashi wao wakachagua kuwa waovu.

Hakuna aliyewapangia wawe waovu, ila wao ndio walichagua kuwa waovu na Mungu akaheshimu uamuzi wao.

Hiyo ndio freewill yenyewe sasa.
 
Nikija kwenye ishu ya freewill yenyewe hapa napo kuna mambo mengi ya kuzungumza.

Kama ulivyosema kuwa hujapata majibu ya kuridhisha, naweza nikasema imekuwa inatokea hivyo kwasababu watu waliokuwa wanajaribu kukupa majibu walilenga zaidi kuifanya freewill ionekane ni halisia

Kama freewill ni uhuru wa kuchagua wema na ubaya ipo basi hatupaswi kuingiliwa kimaamuzi ili kuonesha tupo free

Uhuru wa kuchagua haupaswi kuambatana na mipaka, kusema hiki sawa na hiki sio sawa ukifanya nakuadhibu, huo sio uhuru hiyo ni amri.

Sasa Mungu kasema amekup uhuru wa kuchagua kumuabudu yeye au shetani halafu ukichagua kumuabudu shetani Mungu huyu anakupa adhabu kali sana ya kuchomwa moto. Je huo ni uhuru kweli?

Katika jamii ikitokea tu kuna mtu kamwambia mke wake nimekuoa uhuru wa kuchagua kufanya chochote utakacho ila ikitokea umechagua kuniacha nitakumwaga ubongo kwa maumivu makali.

Mtu huyo akisikika na watu, watu watamuita mkatili asiye na ubinadamu, ataitwa mnyama asiye na huruma, ataitwa mzushi kwa kutoa ahadi ya uwongo

Lakini kitu kama hicho hicho akikifanya Mungu anaitwa mwenye upendo wote, mjuzi wa vingi na mwenye rehema

Kwanini?
Kila uamuzi unaofanyika huambatana na matokeo yake.

Kwa mfano; ukiamua kusoma kwa bidii kuna matokeo yake kama ambavyo ungeamua kutokusoma.

Kinachotokea baada ya wewe kuchagua kuwa mwema ama muovu ni matokeo ya uamuzi na uchaguzi wako.

Na kwa kuwa Mungu anatupenda sana, akatupa akili, utashi na dhamiri ili zitusaidie kufanya informed decisions.

Mungu anatupenda sana aisee.
 
Freewill ni uhuru wa kuchagua mema na mabaya

Na wanasema kwamba bila freewill watu watakuwa kama marobot

At least mushukuru shetani basi

Yes naswma shetani kwakua yeye ndio aliowapa hiyo knowledge ambayo Mungu hakutaka watu wawe nayo

Katika bustani ya eden kina adam na eve walikuwa hawana utambuzi wa kujua lipi jema lipi baya, mpaka pale shetani alipowashawishi walw tunda la utambuzi wa mema na mabaya

Tunda ambalo Mungu hakutaka watu hao wale, kwa tafsiri fupi ni kuwa Mungu hakutaka watu wawe na utashi huru alitaka kuwatenganisha na ukweli.

Na ndio maana kwa miaka mingi walikuwa uchi ila hawakuwahi kustuka ila walipopata maarifa kupitia lile tunda ndio wakagundua kuwa wako uchi.

Lakini pamoja na hayo yote bado watu wanamchukia shetani, lakini ukianza ku count mabaya ya shetani au ukatiri wa shetani sidhani kama utaishia kumuona shetani kafanya ukatiri kumzidi Mungu.
Si kweli kwamba shetani ndio alitupa uelewa wa mema na maovu. Mungu alipotuumba kwa "sura" na "mfano" wake alitupa akili na utashi.

Kazi ya akili ni kupata maarifa na utambuzi wa wema na uovu wakati utashi ukiwa na mamlaka ya daima kufanya maamuzi mema.

Kumbe from the very moment tumeumbwa tulikuwa na uwezo wa kutambua wema na ubaya.

"Tunda" ambalo Mungu hakutaka tulile ni kukosa utii (disobedience).

Kwahiyo wazazi wetu wa kwanza walipokosa utii wa Mungu walijitenga naye (wakajiona wapo uchi), wakawa waovu.

Mavazi waliyotengenezewa na Mungu ni jitihada mbalimbali tunazopewa na Mungu kama second chance ya kurekebisha maamuzi maovu.

Tunda ni figurative language imetumika, na ndio maana halijatajwa kama ni embe, chungwa au tunda la aina gani.
 
Niliwahi kusema hili katika uzi wangu fulani hivi, na leo nakazia, ni hivi: fikra zangu zinanituma kuwa dhana ya free will na Mungu muweza wa yote ni kama pande mbili za sarafu moja. Ili upande mmoja uonekane ni lazima upande mwingine usionekane.

Ili binadamu awe na free will basi inabidi Mungu asiwe muwezz wa yote, kwa maana ya kwamba kuna vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wa Mungu.

Na kama Mungu ni muweza wa yote basi binadamu hawezi kuwa na free will.

Hii ya kusema kwamba Mungu ni muweza wa yote lakini pia ametupa free will kuchagua mema na mabaya ni haiwezekani. Huwezi kuweka sarafu ya shilingi 100 mezani na ukaona Nyerere na swala kwa wakati mmoja. Hell no.
Hapana, dhana ya freewill ni uthibitisho wa uwezo wa Mungu (omnipotence); kwamba ana nguvu na mamlaka yote ya kufanya chochote, hata kutupa uhuru kamili wa kujiamulia hatma zetu.
 
Freewill haipo kwasababu Mungu ndiye anayetengeneza fate

Refer kwa kisa cha yuda kumsaliti yesu, Yuda hata kabla hajazaliwa alikuwa amekwisha andaliwa kutimiza mpango wa Mungu

Kwa maana ya kwamba hakuwa na freewill yeyote ya kuweza kuepuka usaliti

Mungu alimuumba Yuda akiwa tayari msaliti angali yupo tumboni, hakuwa na option ya kuepuka na kwamba usaliti ule aufanye zakayo au mtu mwingine yeyote.

Sasa kama mtu hufanya kile ambacho ameumbiwa aje afanye utasemaje kuwa ni freewill?

Mbali zaidi kwanini mtu ambaye anafanya kile alichoumbiwa aje afanye, aje kuadhibiwa tena?
Yuda hakuwa amepangiwa kumsaliti Yesu. Kulikuwa na mitume 12 na wafuasi wengine wa Yesu wasiohesabika.

Pia; wenye mamlaka na serikali za Wayahudi zingeweza kutumia njia yoyote kumkamata bila hata ya Yuda kama walivyomtengenezea mashitaka ya uongo.

Hata baada ya kumsaliti bado alikuwa na nafasi ya kutubu. Ni yeye aliamua kutumia uhuru wake kufanya alichofanya.

Uamuzi wake ndio uliamua hatma yake.
 
Ngoja nikupe mfano

Mimi ni mfanya biashara ninaye endesha maduka mawili katika eneo moja hapa mjini. Duka langu moja linajihusisha na uuzaji wa silaha na lingine linajihusisha na maswala ya kimichezo

Kwa bahati nikatembelewa na mtu wangu naye mjua anaitwa Calvin, Calvin akataka kununua silaha nzito ila akanieleza kuwa anachukizwa na hao mabinti waliopo kwenye duka langu la michezo na kwa hivyo basi anaenda kuwafundisha adabu

Calvin akaniomba nimuuzie package ya risasi kwa ajili ya silaha, nikamuuzia

Calvin akasema anaenda kuua watu wote waliopo katika eneo hilo, nikamuambia usifanye hivyo. Nikamuambia ni jambo baya sana hutakiwi kufanya

Calvin akaniambia nimfundishe namna ya ku shoot silaha, nikamfundisha

Nikamuonya tena kuwa hupaswi kwenda kutumia hii silaha ku shoot watu

Calvin akatoka na silaha na kwenda kuua kila mtu aliyekuwepo kwenye lile duka linalo jihusisha na michezo

Polisi walivyokuwa wakinihoji nikawasimulia stori nzima ilivyokuwa na nikiwaambia kuwa sio kosa langu ila ni Calvin alikuwa na freewill na nilimuonya asifanye hivyo.

Watu wengi wangeniwajibisha kwa ku-base tu kwenye yale yaliyokuwa sawa kufikiri kwamba Calvin angefanya kutokana na yale ambayo Calvin aliyosema kabla ya kuondoka kwenye duka langu.

Kama nawajibika kwenye sehemu ya mauaji, vipi kuhusiana na Mungu ambaye alimpa Calvin maisha akijua kwa hakika nini Calvin ataenda kufanya kwenye hayo maisha?

Mimi nilijua kidogo tu nini Calvin angeenda kufanya kupitia silaha niliyomuuzia. Lakini nimewajibika

Mungu alijua kwa hakika na anaweza kuzuia chochote. Au vinginevyo Mungu hakujua, au Mungu hana uwezo wote
Kwanza, Mungu ni mwema na daima haungi mkono uovu. Mungu hatufundishi kuwa waovu na hashiriki kwa namna yoyote ile katika uovu wetu.

In fact ametupa kila kitu tunachokihitaji ili kuwa wema - akili, utashi na dhamiri. Kwahiyo tunachokiamua kinatuwia kukiwajibikia.

Kuhusu mfano wako; utawajibika kwa kuwa umeshiriki kutenda uovu kwa kumfundisha na kumrahisishia kutenda huo uovu. Haujamshawishi vizuri aachane na uovu wake.

Mwisho; kama amedhamiria kwelikweli, huwezi kumzuia wala kuingilia wala kubadilisha uamuzi wake wa kuua.

Ndio maana utawajibika kwa ushiriki wako, if any, na siyo kwa uamuzi wake.
 
Ili ulimwengu uwe balanced ilibidi MUNGU amuumbe shetani
Mungu hakumuumba shetani, alimuumba malaika mwema anayeitwa Lucifer. In fact Mungu hajawahi kuumba uovu wala waovu. Alichokiumba Mungu na aliowaumba Mungu wote ni wema (Mwanzo 1:31). Shetani ni matokeo ya Lucifer kuchagua uovu.
 
Ndio mkuu upo sahihi Mungu hatuamulii wapi pa kwenda ila swaki la Muhimu ni je Mungu anajua mimi nitachagua Uzuri au ubaya??
Anajua na anakusaidia (kupitia akili na utashi aliokupa) ujue unachoenda kukichagua kabla haujakichagua, ila kamwe haingilii uamuzi wako.
 
Kosa kubwa linalofanywa na wengi wanapomjadili Mungu ni kwamba kufikiri anawaza kama mawazo yetu. Kama apo Vinci unafikiri mungu anajua jema na baya, kitu ambacho sio kweli, kwake yeye yupo beyond good and evil. Good and evil are product of human effort to make sense of this world, ndio maana unakuta jamii nyingi tunatofautiana juu ya kipi ni chema n kipi ni kibaya, mfano kuna jamii kula nguruwe ni soo, pia kuna jamii kaka kumowa ndugue ni sawa kabisa, au kijana wa kiume aliyebalehe kumchukua dogo wa kiume na kuishi nae kama mkewe ni sawa tu.

Cha kujua sir God katuweka tuexpress our truest self, na pia kushangaa na kutukuza utukufu wake anaonyesha kila sehemu ukiangazia macho. siku atakapokuja kuvuna mbegu zakee kuna watu kwa kushangaa taya zao zitagusa chini.
Umeanza vizuri ila umeendelea na kumalizia vibaya, in my humble opinion.

Things/people are not good or evil because of the society, but with reference to their obedience to God.

Society ina-determine tu usahihi (rightness) au ukosefu (wrongness) ya mtu au kitu husika...

Tunayaita maadili (ethics).
 
Labda tukiiweka kihesabu tuseme ukiwa upo katika pointi fulani A/B/au Z. Mungu anafahamu mwisho wa wewe ukiamua kujongea katika uelekeo wowote hadi mwisho wako, infinity circle of directions.

Hata ukiamua kurudi nyuma au kwenda mbele kidogo halafu ukasimama. Mungu anajua machaguo yote ya maamuzi yako na matokeo ya mchanganyiko wa maamuzi hayo yote mpaka mwisho.

Mfano ukiwa upo DSM, Mungu anajua mikoa yote utakaweza kuamua kwenda na matokeo ya kila kachaguo utakakochagua. Mfano ukachagua kwenda arusha badala ya Mwanza, hapo Mungu atakuwa anajua hadi jina la mjukuu wako kuitwa Manka na wewe kufariki kwa kudondokewa na mgomba uzeeni kwako!
Lakini pia hapohapo anafahamu mtiririko wa machaguo yako ya kwenda Mwanza hadi kumiliki boti za uvuvi na kuwa mbunge wa Misungwi. So ukiamua kwenda Mwanza hautampoteza maboya maana anajua kabisa matokeo yote ya chaguo hilo hadi na wewe kujenga wilaya ya Misungwi na kuwa mvuvi. Na mjukuu wako kuitwa Masanja

Nahisi kila pointi unayoigusa unazidi kujiwekea mazingira ya kuchagua kinamna fulani kutoka katika infinity alternatives ambazo zzooooooote Mungu anazijua matokeo yake. Hakulazimishi kuchagua njia yoyote, tena hata hafuatilii unachaguachaguaje. In fact ukitaka uweze samtaimu jichukulie wewe mwenyewe ni sehemu ya Mungu na mnafanya maamuzi pamoja ya maisha yenu muyaendesheje kwa kushirikiana.
Ila pamoja na kujua yote hayo; anakuchia uhuru wa kuamua uende wapi.
 
Ngoja nikupe mfano

Mimi ni mfanya biashara ninaye endesha maduka mawili katika eneo moja hapa mjini. Duka langu moja linajihusisha na uuzaji wa silaha na lingine linajihusisha na maswala ya kimichezo

Kwa bahati nikatembelewa na mtu wangu naye mjua anaitwa Calvin, Calvin akataka kununua silaha nzito ila akanieleza kuwa anachukizwa na hao mabinti waliopo kwenye duka langu la michezo na kwa hivyo basi anaenda kuwafundisha adabu

Calvin akaniomba nimuuzie package ya risasi kwa ajili ya silaha, nikamuuzia

Calvin akasema anaenda kuua watu wote waliopo katika eneo hilo, nikamuambia usifanye hivyo. Nikamuambia ni jambo baya sana hutakiwi kufanya

Calvin akaniambia nimfundishe namna ya ku shoot silaha, nikamfundisha

Nikamuonya tena kuwa hupaswi kwenda kutumia hii silaha ku shoot watu

Calvin akatoka na silaha na kwenda kuua kila mtu aliyekuwepo kwenye lile duka linalo jihusisha na michezo

Polisi walivyokuwa wakinihoji nikawasimulia stori nzima ilivyokuwa na nikiwaambia kuwa sio kosa langu ila ni Calvin alikuwa na freewill na nilimuonya asifanye hivyo.

Watu wengi wangeniwajibisha kwa ku-base tu kwenye yale yaliyokuwa sawa kufikiri kwamba Calvin angefanya kutokana na yale ambayo Calvin aliyosema kabla ya kuondoka kwenye duka langu.

Kama nawajibika kwenye sehemu ya mauaji, vipi kuhusiana na Mungu ambaye alimpa Calvin maisha akijua kwa hakika nini Calvin ataenda kufanya kwenye hayo maisha?

Mimi nilijua kidogo tu nini Calvin angeenda kufanya kupitia silaha niliyomuuzia. Lakini nimewajibika

Mungu alijua kwa hakika na anaweza kuzuia chochote. Au vinginevyo Mungu hakujua, au Mungu hana uwezo wote
Japo mfano wako hauna uhalisia wowote, na hili nilishawahi kukukosoa katika uzi fulani, maana uliutoa mfano huu huu.

Allah anajua kila kitu "indetails" na "in general". Hili kwanza liweke akilini. Wewe na huyo muhusika nyote mlikuwa na "free will" ndiyo maana hukumuunga mkono kwa kile alichokifanya. Sasa Mola wetu hayo yote aliyajua na akaruhusu yakatokea, na angetaka yasitokee pia yasinge tokea.

Kujua kwa Mola mambo hayo yote hakukuzuii wewe kufanya unalo taka, mola alvyo tuumba akatupa uhuru wa kuchagua, hakuishia hapo akatupa akili za kujua zuri na baya, lenye hasara na manufaa. Wewe unapofanya ovu ujue muda huo hup ulikuwa na uwezo wa kufanya jema. Nikakutolea mfano mwepesi sana, leo hii wewe kwa kumjua vizuri mtu fulani, mfano akipata hela mtu fulani lazima atakunywa pombe, na kweli akipata hela anakunywa. Tofauti ya Mola wetu yeye anajua kabisa "indetails"

Sasa swali linakuja, kwa kile unachokihoji wewe na kutaka kiwe hivyo, kinaondoa kabisa suala la "free will". Ndiyo maana Mola wetu katika Qur'aan akasema ya wazi ya kuwa akatupa uwezo wa kusikia na kuona, kisha akatuacha tukipenda tutashukuru na tusipopenda tutakufuru, ila kila kitu amekuwekea wazi.

Lakini katika huko kukuwekea wazi, akakwambia hili baya usifanye na lile zuri fanya. Yaani sawa na kupewa mtihani wenye majibu tayari.
 
Back
Top Bottom