Japo mfano wako hauna uhalisia wowote, na hili nilishawahi kukukosoa katika uzi fulani, maana uliutoa mfano huu huu.
Allah anajua kila kitu "indetails" na "in general". Hili kwanza liweke akilini. Wewe na huyo muhusika nyote mlikuwa na "free will" ndiyo maana hukumuunga mkono kwa kile alichokifanya. Sasa Mola wetu hayo yote aliyajua na akaruhusu yakatokea, na angetaka yasitokee pia yasinge tokea.
Kujua kwa Mola mambo hayo yote hakukuzuii wewe kufanya unalo taka, mola alvyo tuumba akatupa uhuru wa kuchagua, hakuishia hapo akatupa akili za kujua zuri na baya, lenye hasara na manufaa. Wewe unapofanya ovu ujue muda huo hup ulikuwa na uwezo wa kufanya jema. Nikakutolea mfano mwepesi sana, leo hii wewe kwa kumjua vizuri mtu fulani, mfano akipata hela mtu fulani lazima atakunywa pombe, na kweli akipata hela anakunywa. Tofauti ya Mola wetu yeye anajua kabisa "indetails"
Sasa swali linakuja, kwa kile unachokihoji wewe na kutaka kiwe hivyo, kinaondoa kabisa suala la "free will". Ndiyo maana Mola wetu katika Qur'aan akasema ya wazi ya kuwa akatupa uwezo wa kusikia na kuona, kisha akatuacha tukipenda tutashukuru na tusipopenda tutakufuru, ila kila kitu amekuwekea wazi.
Lakini katika huko kukuwekea wazi, akakwambia hili baya usifanye na lile zuri fanya. Yaani sawa na kupewa mtihani wenye majibu tayari.