Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Free will ni uhuru wa kuchagua mema na mabaya, wote tunakubaliana na tafsiri hiyo.Safi sana, safi sana umereinforce point moja ilikuwa inapelekea watu kumuona Mungu isivyo. Kumuona kama vile yeye ndio anaye'dictate' hali zetu huku duniani. Wakati kumbe ni matokeo ya chaguzi zetu wenyewe ndiyo tunajiumbia dunia zetu.
Mtu akisoma kwa bidii na akaelewa kinamna fulani yeye mwenyewe mwisho wake atapata ufaulu fulani sambamba na alivyofanyafanya. Yaani ni kama automatically hivi.
Pia hata kuishi baadaye katika ufalme wa mbingu au ufalme wa shetani inawezekana hakuna kiumbe kutoka nje kinachokuja kukuambia wewe nenda huku au nenda kule. La!. Itakuwa ni mtu mwenyewe tu mfano akijifanya mbinafsi mwovu mwishoni atachaguachagua hadi kujikuta na washirika wenzie wenye tabia hizo baada ya kufa. Ukizungukwa na watu wabinafsi na waovu mara nyingi inamaanisha 'hell' hata kama upo wapi. Fikiria wewe uwe tajiri sehemu iliyozagaa 'ma-panya road' je utafaidi?
Lakini pia fikiria mfano ukafanya fikira na maamuzi yako ya kijamaa/communal ukapenda ushirikiano na upendo usio wa kibinafsi, upendo wa kimungu. Halafu mwishoni ukajitengenezea uhusiano wa karibu na marafiki wa namna hiyo mkajikuta wote baada ya kufa mpo katika dunia yenye watu wenye utashi huru/freewill lakini wote mna maamuzi ya kiupendo kwa kila mmoja wenu. Ndugu yangu hiyo mojakwa moja ndiyo tafsiri ya kuuishi ufalme wa mbinguni. Fikiria labda mazingira ambapo hata nyumba yako imebomolewa na upepo ukiwa haupo upo safarini, utarudi na utakuta vyombo vyako vi salama [tena hata kukuta wamekurekebishia wanakijiji!] Na siku nyingine ikimtokea mwingine wewe na wanakijiji wenzio mtashirikiana kumjengea 'victim mpya'. So kazi zitaendelea, hakuna kupumzika mbinguni wala jehanamu, lakini kwa mbinguni zitaleta raha mno kuzishiriki maana ni za upendo.
Kwa hiyo hata kama Scars alivyopendekeza kuwa na mbinguni napo tutaendelea na kuhustle kinamna fulani afahamu utofauti mkubwa uliopo kati ya; watu wanaohustle kati ya mijitu mibinafsi, na wanaohustle kati ya watu waupendo kuna utofauti mkubwa sana mfano wa hell and heaven figuratively and literally too! Kila mtu kutokana na namna anyoiona sahihi anajielekeza anakokupenda mwenyewe. Mungu anajua kuwa njia ya upendo ni nzuri, ila mwanadamu akimsisitizia kwamba njia ya ubinafsi ndio yenyewe sasa. Akajitia u-much-know basi Mungu humruhusu aendage huko maana ndiko atakakofaidi kwa mujibu wake yeye mwanadamu. Huo ni upendo mkuu sana!
Upendo ni pale unao uwezo na utashi kufanya lolote, lakini unaamua kutumia uwezo huo kwa uamuzi huru wako kuyafanya matakwa/mapenzi ya yule unayempenda. Mungu anatupenda sana mazee
Na kwamba ubaya unatokea kwasababu kuna freewill na bila freewill kusingekuwa na raha kwasababu watu wangeishi kama robots
Anyway. Peponi kuna freewill au haipo?