ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,869
- 3,852
Je mleta maada, wakati unajiuliza uwezo wa Mungu na Uhuru wa kuchagua. Je umejiuliza maswali haya mawili?. 1. Je ni kweli tuliumbwa na Mungu?. 2. Kama ni kweri kwa Nini alituumba?. Kama hatujaumbwa na Mungu maada hiii Haina maana. Sasa kwa umuhimu wa maada hii ni kwanza lazima tukiri tuliumbwa na Mungu. Sasa kwa Nini alituumba?. Kwa wakatoliki jiubu huwa tumpende, tumujue na tumutumikie ( kwa kifupi Yeye anatafuta recognization only).Mungu anajua hatma kwasababu yupo nje ya time dimension. Hivyo yeye anakuona mwaka 2000, anakuona mwaka 2022 na anakuona mwaka 2040 (mfano tuu).
Hajakupangia wala haku control ila anakuona unavyofanya maamuzi yako na unavyovuna matokeo yake.
Hata hivyo ameweka njia ambayo ukichagua kuifuata unapata matokeo mazuri wakati wote.
Kwa Kuwa binadamu tunamwili na hivyo unatuongonza kwenye matakwa ya mwili ( Tamaa za mwili, Tamaa za Mali na tafasiri zetu binafisi kukwepa uhalisia). Sasa hapa kwa Kuwa lengo lake ni recognization ndiyo maana kaweka kitu kuomba msamaha kwake. Binadamu ni Roho iliyofunikwa na mwili na Roho ndiyo uungu wetu hivyo sisi tunaweza kutumia Roho zetu Kuwa na Mungu au tukazichafua tukawa kwa shetani. Sasa hoja ya uwezo wa uungu ipo ndani yetu na ndiyo inayotunza history ya mema na mabaya yote . Maana ya free will ni kuchagua Kuwa kwa Mungu ama kwa shetani. Ukichagua kwa Mungu maana yake umechagua kutumia nguvu za uungu ulio nao hapo Sasa binadamu wewe unakuwa na nguvu za Mungu na ushetani haukusogelei Tena. Maana yake uwezo wa kujikinga na mabaya utakuwa nazo na Mungu atakuwa ndani yako. Mleta maada God blesses are always there , the issues we opt to use or to damp?. Huenda nimeongea kwa kifupi Sana Hoja nzituo niulize kivingine nikujibu.