God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Haiwezi kuwa considered kama ni uchaguzi mbaya kwasababu alichokichagua au kuto kichagua hakipo katika orodha ya vitu vibaya

Sasa chukulia kama wewe ndio umempa mtoto uhuru wa kuchagua kati ya kula nyama ya ng'ombe au ya mtu

Halafu mtoto achague kula nyama ya mtu, je kuna namna yeyote unaweza kuwaza kuwa kachagua kisicho chema ila sio kibaya?
Ulioutoa ni mfano wa kisicho chema[kiuhalisia] na kibaya[kiukweli] japo yeye mchaguaji kaona kwake ni chema. Free will yake imempelekea kuwa na maoni mabaya hapo
 
Mtoto anayechagua tikiti ambalo kwake sio interest yake anaweza kupewa adhabu ya kuchomwa motoni?
 
Hapana ila automatically atakosa citrulline ya kumusaidia katika mzunguko wa damu, na lycopene.

Na kwa kuwa amekula bromelain basi itamsaidia katika mmengenyo wa chakula na akizidisha basi atachubuka ulimi. Kumbuka haya yote hayajafanywa na baba yake bali ni matokeo yaliyo sambamba na chaguo la mtoto mwenyewe.

Haihitaji hisia wala muingilio wowote toka kwa mzazi hapo, ni machaguo na matokeo tu kama ambavyo hahitajiki yeyote kuja kutuchoma moto bali matokeo yetu wenyewe.
 
Na ndio freewill hiyo hiyo inapatikana na huko peponi?
Nilishalijibu hili mbona.

Freewill ya peponi inadili zaidi na machaguo mema, mambo ya dhambi kule ni hakuna japo makosa yana uwezekano wa kutokea. Watu walioko kule walishapimwa na wameonekana wanapenda mema japo hayo mema yanatofautiana baina yao, kila mmoja ataendelea kuyapigania mema anayoyaamini na wote tutakuwa tunajenga nyumba moja. Upinzani wa utashi huko utakuwa umejengwa katika upendo na ndiyo didfinition ya mbinguni

Ni kama tu sasa hivi theists walishakubaliana kwamba tumeamini Mungu yupo, ila tukija kwenye yupojeyupoje kila mtu utaona anampinga mwenzie japo wote tunakubaliana kuwa yupo!

Mbona mifano ni mingi tu asee, machaguo ni mengi sana hata katika mema.
 
Weka umakini sio kila jibu linaanza na neno "kwasababu"

Nimekuambia hakuna freewill ya mtu kuchagua anachotaka kwasababu choice iko fixed haina option nyingine

Choice ikiwa fixed unapataje uhuru wa kufanya unacho kitaka?
Sasa unasaje choice ilo fixed bila kuonyesha hilo, huoni hayo ni matatizo ya akili na kufikiri ? Lakini unasemaje choice iko fixed wakati "free will" ipo kabisa ?

Unafikiri kwa kutumia nini ?
 
Mungu akijua utaenda kushoto, hapo una uchaguzi wa kufanya unachotaka ukaenda kulia?
Kijana hili jambo naona limeshakushinda, swali langu mpaka muda huu hujajibu, nimekuuliza hivi onyesha uhusiano wa Mola kujua na wewe kufanya jambo au kutofanya jambo ?

Uchaguzi wa kufanya unachotaka ni huo ambao umechagua kwenda kushoto na hujaenda muda ambao ungetaka kwenda kulia pia ungeenda.

Allah anajua ya kesho, yaliyopo na ambayo hayapo. Anajua kesho yako sababu kujua kwake hakujatanguliwa na kutokujua na wala hakujafungamana na wewe na kuchagua kwako. Mfano wewe leo hii kuna mtu wako unae mjua sanaa, yaani mtu huyo unajua kabisa huyu kwa jinsi anavyo penda pombe, nikimpa tu hela lazima ataenda kunywa pombe na kweli anaenda. Swali, kujua kwako hilo kumetokana na nini ? Jibu ni kwa sababu unamjua vizuri sana, je kujua kwako kumemzuia huyo mtu asifanye anachokitaka ? Saza tofauti yetu na Allah ni kuwa yeye anajua mambo "in general" na "in details".

Kama huna option hiyo utasemaje una uhuru wa kufanya unachotaka wakati choice ilishakuwa fixed kabla hata hujazaliwa?
Huna hiyo options kivipi ?
 
Ni baadhi ya maswali niliowahi kujiuliza miaka michache ilio pita! Na automatic nilijikuta najijibu mwenyewe!

Pia Nilishawahi kujiuliza na mengine kama haya kwanini Mungu kanileta duniani pasi matakwa yangu, sikumoja nikaja kujiuliza vipi kama nikioa halafu nikakosa mtoto kwenye ndoa yangu?(unaweza ukajiuliza tu feeling unayoweza kuipata japo unataka mtoto ambaye hajataka kuja duniani au pengine asingependa azaliwe na wewe) so hiyo ni PRINCIPLE tu Inayo fanya kazi

Binadamu kapewa Ile free will ,anaamua Nini kitokee duniani sio Mungu! Ile free will aliyopewa mwanadamu imefungamanishwa na PRINCIPLE ndani yake, chochote unachofanya uwe na hakika kina matokeo (consequences iwe negative or positive so your free to choose depending on the outcome of your choice)

So hata mivurugano iliopo duniani ni matokeo ya free will! Na Mungu anachohitaji ni ww kufuata misingi na Sheria zake katika kuishi hapa duniani!

Naamini Mungu ni Omnipotent & Omnipresent na Hilo kwangu lipo kiimani tu sio katka logic , I CAN'T PROVE IT BUT BY FAITH I BELIEVE HIM!

Napia naamini Mungu ametuumba na predetermined course na sio predetermined end except Kwa wale wenye kazi maalumu hao Wana predetermined end!
 
Nilishalijibu hili mbona.

Freewill ya peponi inadili zaidi na machaguo mema, mambo ya dhambi kule ni hakuna japo makosa yana uwezekano wa kutokea. Watu walioko kule walishapimwa na wameonekana wanapenda mema japo hayo mema yanatofautiana baina yao, kila mmoja ataendelea kuyapigania mema anayoyaamini na wote tutakuwa tunajenga nyumba moja. Upinzani wa utashi huko utakuwa umejengwa katika upendo na ndiyo didfinition ya mbinguni

Ni kama tu sasa hivi theists walishakubaliana kwamba tumeamini Mungu yupo, ila tukija kwenye yupojeyupoje kila mtu utaona anampinga mwenzie japo wote tunakubaliana kuwa yupo!

Mbona mifano ni mingi tu asee, machaguo ni mengi sana hata katika mema.
Freewill ni uchaguzi kati ya mema na mabaya

Freewill inayochagua mema pekee sio freewill
 
Sasa unasaje choice ilo fixed bila kuonyesha hilo, huoni hayo ni matatizo ya akili na kufikiri ? Lakini unasemaje choice iko fixed wakati "free will" ipo kabisa ?

Unafikiri kwa kutumia nini ?
Choice iko fixed kwakua huwezi kuchagua otherwise ilisahakua predetermined

If the future is already set, free will cannot exist
 
Freewill ni uchaguzi kati ya mema na mabaya

Freewill inayochagua mema pekee sio freewill
Pole sana, hii inamaanisha kuwa kichwani kwako umejiaminisha kuwa mabaya ni kitu muhimu sana ili mwanadamu ajiskie vizuri, ajisikie huru!

Binafsi, na najua wapo na wengine wengi tu tunaamini kuwa tunaweza kuishi kikamilifu kabisa bila kuhitaji ubaya ili kutukamilisha. Na tukabaki na freewill vizuri kabisa.

Ndiyo maana mi nahisi mtu aliyejiamulia kuwa ubaya ndio kitu kizuri, halafu labda Mungu akamlazimisha akaishi mbinguni na watu wanaoamini katika wema. Itakuwa ni kumuonea na wala hatafaidi mbingu. Bora tu aendelee akaishi na mashetani ili hilo 'vaibu' alilotoka nalo duniani akaliendeleze. Ubaya ubaya tu.

Kwa hiyo ndugu zangu waamini msiwatishe wasiotaka kuamini kwamba eti wataumia, sijui moto sijui funza. Walaa. Unachoamini wewe kuwa ndiyo uhalisia mzuri ni tofauti na wanachoamini wao. Inawezekana kumbe kwa relativity jehanamu na wanajehanamu ndiyo best possible universe ya kikwao!! na mbingu na wanambingu ndiyo best possible universe ya kiwaamini!

Oneni huyu jamaa, hataki kabisa kuamini kama freewill inawezekana bila ya mtu kuwa mbaya?
 
Kijana hili jambo naona limeshakushinda, swali langu mpaka muda huu hujajibu, nimekuuliza hivi onyesha uhusiano wa Mola kujua na wewe kufanya jambo au kutofanya jambo ?

Uchaguzi wa kufanya unachotaka ni huo ambao umechagua kwenda kushoto na hujaenda muda ambao ungetaka kwenda kulia pia ungeenda.

Allah anajua ya kesho, yaliyopo na ambayo hayapo. Anajua kesho yako sababu kujua kwake hakujatanguliwa na kutokujua na wala hakujafungamana na wewe na kuchagua kwako. Mfano wewe leo hii kuna mtu wako unae mjua sanaa, yaani mtu huyo unajua kabisa huyu kwa jinsi anavyo penda pombe, nikimpa tu hela lazima ataenda kunywa pombe na kweli anaenda. Swali, kujua kwako hilo kumetokana na nini ? Jibu ni kwa sababu unamjua vizuri sana, je kujua kwako kumemzuia huyo mtu asifanye anachokitaka ? Saza tofauti yetu na Allah ni kuwa yeye anajua mambo "in general" na "in details".

Huna hiyo options kivipi ?
Una tatizo moja la kujitoa ufahamu, haijalishi ni kwa namna gani unajibiwa ila umekuwa ukijipumbaza kimakusudi na kujidai huoni majibu

Hilo unalosema hujajibiwa nimekujibu na hapa tena nakujibu kukuwekea msisitizo, sitarajii tena kuona swali hilo post zijazo.

Kama Mungu anaweza kujua nini kitaenda kutokea mbeleni in 100% accuracy with no margin of errors then kile kinachoenda kutokea ni predetermined na predetermined ina pingana na freewill kwasababu choice ishakuwa fixed na kwamba huwezi kuchagua vinginevyo

Kama huwezi kuchagua vinginevyo huwezi kuwa na freewill

Ingawa unaweza kujiona kama uko free kwenye kile ambacho unaona umekichagua kwa utashi wako lakini uhalisia ni kuwa uchaguzi huo ulishakuwa fixed you couldn't choose otherwise
 
Sasa tujikite katika yale ambayo ukiyachagua yanaweza kukupelekea uende motoni au peponi maana hicho ndio kipimo cha freewill
Hapana. Hiki sio kipimo.

Mzee wangu akinipa uhuru wa kusomea arts au sayansi inaonesha wazi anaheshimu freewill yangu. Hata kama kati ya hivyo hakuna kitakachosababisha anikatae kama mwanae.
 
Pole sana, hii inamaanisha kuwa kichwani kwako umejiaminisha kuwa mabaya ni kitu muhimu sana ili mwanadamu ajiskie vizuri, ajisikie huru!

Binafsi, na najua wapo na wengine wengi tu tunaamini kuwa tunaweza kuishi kikamilifu kabisa bila kuhitaji ubaya ili kutukamilisha. Na tukabaki na freewill vizuri kabisa.

Ndiyo maana mi nahisi mtu aliyejiamulia kuwa ubaya ndio kitu kizuri, halafu labda Mungu akamlazimisha akaishi mbinguni na watu wanaoamini katika wema. Itakuwa ni kumuonea na wala hatafaidi mbingu. Bora tu aendelee akaishi na mashetani ili hilo 'vaibu' alilotoka nalo duniani akaliendeleze. Ubaya ubaya tu.

Kwa hiyo ndugu zangu waamini msiwatishe wasiotaka kuamini kwamba eti wataumia, sijui moto sijui funza. Walaa. Unachoamini wewe kuwa ndiyo uhalisia mzuri ni tofauti na wanachoamini wao. Inawezekana kumbe kwa relativity jehanamu na wanajehanamu ndiyo best possible universe ya kikwao!! na mbingu na wanambingu ndiyo best possible universe ya kiwaamini!

Oneni huyu jamaa, hataki kabisa kuamini kama freewill inawezekana bila ya mtu kuwa mbaya?
Kwanini kuna mabaya?
 
Hapana. Hiki sio kipimo.

Mzee wangu akinipa uhuru wa kusomea arts au sayansi inaonesha wazi anaheshimu freewill yangu. Hata kama kati ya hivyo hakuna kitakachosababisha anikatae kama mwanae.
Unaonekana kuwa na definition yako ya kipekee kuhusu freewill

Niambie kwanini Mungu aliumba limwengu unao ruhusu mabaya kuwepo?
 
Back
Top Bottom