God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Nakukumbusha kuwa Freewill ni uchaguzi wa mema na mabaya
Kumbe na we unajidanganya pia kuwa dunia haiwezekani ikiwa hakuna mabaya?

Freewill ipo hata kama hakuna kibaya kinachofanyika mfano: mimi kuamua kuishi Dar, au Arusha au Mwanza.....hakuna kibaya hapo na bado freewill ipo nachagua pa kwenda kuishi.

Kwa hiyo hata huko hatua za juu za kimbingu watu watatumia freewill zao kubishana kwamba je? Haya masaa mawili tuyatumie kuabudu? au kusifu?...... watatokea na vichwa ngumu kama kina sisi tutaanza kutoa logic kuwa hapa leo hakuna cha kusifu wala kuabudu! bali tujigawe twende tukawahubirie walio duniani huko ndio la msingi. Nadhani wapo watu watakaotuchukulia sisi kama version ya 'viatheist' fulani huko mbinguni. Ubishi utaendelea maana watu watakuwa wapo huru kuamua mambo yao. Mind you ubishi na sio necessarilly uovu.
 
Hajakupangia wala haku control ila anakuona unavyofanya maamuzi yako na unavyovuna matokeo yake.
Lakini utashi una mipaka yake. Mungu haku relinquish sovereignity yake. Bado ana mamlaka ya kuingilia uhuru huo anytime akitaka. Na akiingilia kati hapo sio uhuru wako tena bali ni kile anataka kiwe.

Mfano wakati wa ujenzi wa mnara wa Babeli, Mungu aliingilia kati akawatawanya. Kutawanyika haikuwa matokeo ya wao kutumia utashi wake bali Mungu kutumia Uungu wake!

So Mungu ana reserve rights za ku intervene anytime, but that is another issue!
 
Scars kumbuka mimi tangu mwanzo sikukubaliana na specific difinition yako ya free will ambayo inalazimisha 'mema na mabaya'

Miminnilisema hivii; Ndiyoni freewill ni kuchagua mema na yasiyo mema kwetu, kuchagua kwenda left ama right wewe tu na utaendelea kuyapata matokeo kadri ya unavyochagua...

Na tafsiri ya utashi kutoka wikipedia hailazimishi mema na mabaya ila imeiweka hivi;Utashi ni kipawa cha binadamu kinachomfanya aweze kutaka mwenyewe chochote. Kitu hicho kinaweza kuwa chema na hata kibaya, ingawaakili yake mwenyewe inaona zaidi wema fulani uliomo na ambao unamvuta.

Hakuna ulazima wa uovu ili freewill iwepo bro
 
Niliwahi kusema hili katika uzi wangu fulani hivi, na leo nakazia, ni hivi: fikra zangu zinanituma kuwa dhana ya free will na Mungu muweza wa yote ni kama pande mbili za sarafu moja. Ili upande mmoja uonekane ni lazima upande mwingine usionekane.

Ili binadamu awe na free will basi inabidi Mungu asiwe muwezz wa yote, kwa maana ya kwamba kuna vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wa Mungu.

Na kama Mungu ni muweza wa yote basi binadamu hawezi kuwa na free will.

Hii ya kusema kwamba Mungu ni muweza wa yote lakini pia ametupa free will kuchagua mema na mabaya ni haiwezekani. Huwezi kuweka sarafu ya shilingi 100 mezani na ukaona Nyerere na swala kwa wakati mmoja. Hell no.
Hapa unachokisema ni human sovereignity na sio free will. Hata kama una mambo mawili tu ambayo uko huru kuchagua unalolitaka, free will ipo. So free will & sovereignity of God can exist. But sovereign man and Sovereign God are mutually exclusive.

Mwanadamu hawezi kuwa huru kufanya kila analolitaka. Mungu bado ana haki ya kuingilia uhuru aliompa mwanadamu. So mwanadamu ana utashi na ana mipaka ya kuutumia utashi huo. Mungu ndiye ambaye ana mamlaka na say ya mwisho ya kila kitu!

kama by free will una maana a sovereign human then uko sahihi. Haviwezi kuishi pamoja!
 
Lakini utashi una mipaka yake. Mungu haku relinquish sovereignity yake. Bado ana mamlaka ya kuingilia uhuru huo anytime akitaka. Na akiingilia kati hapo sio uhuru wako tena bali ni kile anataka kiwe.

Mfano wakati wa ujenzi wa mnara wa Babeli, Mungu aliingilia kati akawatawanya. Kutawanyika haikuwa matokeo ya wao kutumia utashi wake bali Mungu kutumia Uungu wake!

So Mungu ana reserve rights za ku intervene anytime, but that is another issue!
Ni kweli mkuu, Mungu hakuachilia ownership ya ulimwengu ila alituachia mamlaka ya kutawala kwa niaba yake. Pale aliingilia kwasababu ilikuwa kinyume na plan yake kwamba watu wazaliane na kuijaza dunia.
 
Kumbe na we unajidanganya pia kuwa dunia haiwezekani ikiwa hakuna mabaya?

Freewill ipo hata kama hakuna kibaya kinachofanyika mfano: mimi kuamua kuishi Dar, au Arusha au Mwanza.....hakuna kibaya hapo na bado freewill ipo nachagua pa kwenda kuishi.

Kwa hiyo hata huko hatua za juu za kimbingu watu watatumia freewill zao kubishana kwamba je? Haya masaa mawili tuyatumie kuabudu? au kusifu?...... watatokea na vichwa ngumu kama kina sisi tutaanza kutoa logic kuwa hapa leo hakuna cha kusifu wala kuabudu! bali tujigawe twende tukawahubirie walio duniani huko ndio la msingi. Nadhani wapo watu watakaotuchukulia sisi kama version ya 'viatheist' fulani huko mbinguni. Ubishi utaendelea maana watu watakuwa wapo huru kuamua mambo yao. Mind you ubishi na sio necessarilly uovu.
Mi na hoji kulingana na namna ambavyo theists mna defend freewill

Theists mnadai kwamba haya mabaya yanatokana na uchaguzi wetu tuliopewa kutokana na freewill

Na kwamba ulimwengu usingekuwa mahala pazuri endapo kungekuwa na mema pekee

Kuwepo na mema bila freewill ni kufanya creatures wakose utashi na hivyo wa behave kama robots

Na kwamba kungekuwepo na mema pekee basi hapo watu wasingekuwa na freewill kwasababu wamenyimwa uhuru wa kuchagua maovu.

Sasa hivyo ndivyo navyoelewa.

Labda uniambie wewe kwanini kuna freewill?

Au kwanini Mungu wako aliweka freewill?
 
Ni kweli mkuu, Mungu hakuachilia ownership ya ulimwengu ila alituachia mamlaka ya kutawala kwa niaba yake. Pale aliingilia kwasababu ilikuwa kinyume na plan yake kwamba watu wazaliane na kuijaza dunia.
Nilitaka kuweka sawa kwamba Mungu hakutupa utashi usio na mipaka. Mnara wa Babeli, Gharika ya Nuhu, Sodoma na Gomora, Kifo cha Herode, Yona na Ninawi ni mifano michache kuwa mwanadamu hakupewa uhuru wa kufanya chochote bali kuna mipaka!
 
Scars kumbuka mimi tangu mwanzo sikukubaliana na specific difinition yako ya free will ambayo inalazimisha 'mema na mabaya'

Miminnilisema hivii; Ndiyoni freewill ni kuchagua mema na yasiyo mema kwetu, kuchagua kwenda left ama right wewe tu na utaendelea kuyapata matokeo kadri ya unavyochagua...

Na tafsiri ya utashi kutoka wikipedia hailazimishi mema na mabaya ila imeiweka hivi;Utashi ni kipawa cha binadamu kinachomfanya aweze kutaka mwenyewe chochote. Kitu hicho kinaweza kuwa chema na hata kibaya, ingawaakili yake mwenyewe inaona zaidi wema fulani uliomo na ambao unamvuta.

Hakuna ulazima wa uovu ili freewill iwepo bro
Sasa hapo kuna utofauti gani na nilichokiandika mimi?

Freewill ni uchaguzi kati ya Mema na yasiyo mema

Kinyume cha mema ni ubaya

Sasa nikisema freewill ni uhuru wa kuchagua kati ya mema na mabaya kuna utofauti gani hapo na mtu aliyesema mema na yasiyo mema?
 
Nilitaka kuweka sawa kwamba Mungu hakutupa utashi usio na mipaka. Mnara wa Babeli, Gharika ya Nuhu, Sodoma na Gomora, Kifo cha Herode, Yona na Ninawi ni mifano michache kuwa mwanadamu hakupewa uhuru wa kufanya chochote bali kuna mipaka!
Na ndio maana tunasema freewill ni scam

Penye uhuru hakuna mipaka
 
Mi na hoji kulingana na namna ambavyo theists mna defend freewill

Theists mnadai kwamba haya mabaya yanatokana na uchaguzi wetu tuliopewa kutokana na freewill

Na kwamba ulimwengu usingekuwa mahala pazuri endapo kungekuwa na mema pekee

Kuwepo na mema bila freewill ni kufanya creatures wakose utashi na hivyo wa behave kama robots

Na kwamba kungekuwepo na mema pekee basi hapo watu wasingekuwa na freewill kwasababu wamenyimwa uhuru wa kuchagua maovu.

Sasa hivyo ndivyo navyoelewa.

Labda uniambie wewe kwanini kuna freewill?

Au kwanini Mungu wako aliweka freewill?
Ntasema, maovu ni matokeo tu ya matumizi yasiyo sawa ya freewill.

Ila nakataa kwamba bila kuwepo maovu basi kusingekuwepo na freewill. Hapana.

Nitasema kuwa kuna freewill kwa sababu ya upendo. Mungu aliweka utashi ili kuwe na uwezekano wa kupenda, kumpenda na kupendana.

Upendo ni pale ambapo mtu mwenye uwezo wa kufanya vyovyote anapoamua kwa hiyari yake kutumia uwezo huo kutimiza matakwa/mapenzi ya huyo anayempenda. Wanazuoni wanasema ni viumbe wenye utashi tu ndio wenye uwezo wa kupenda.

Mungu anao uwezo wote, utashi wote na ujuzi wote. Lakini badala ya kutumia assets zake hizo akaamua kuwapa wanadamu uwezo, na utashi pia na yeye anasikiliza kile wanadamu wanajiamulia wao wenyewe kwa freewill zao.......... huu tunauita ni Upendo mkuu sana.
 
We live in the universe of 'duality'

Good|bad, juu|chini, kulia|kushoto, ukweli|uongo
MUNGU | SHETANI
Katika falsafa ya dualism hakuna Mungu. Kwa hiyo hili swali haliwezi kujibiwa na dualism.

Ili ulimwengu uwe balanced ilibidi MUNGU amuumbe shetani
Dualism ni self defeating. Kama Mungu alimuumba shetani then Mungu vs shetani ni Muumba vs kiumbe na hiyo sio dualism kwa sababu dualism implies equal but opposite objects. Hakuna true dualism in practice.

Kosa kubwa watu hufanya kwenye majadiliano yahusuyo Imani ni kuuliza swali la MUNGU ni Nani badala ya MUNGU ni nini? Na ndicho kinachojadiliwa hapa

Kwanza kabisa tujiulize MUNGU ni nini?
Mungu hawezi kuwa nini. Kwa sababu nini haiwezi kusababisha nani kwa namna yoyote ile. Mungu angekuwa ni kitu asingeweza kuumba watu wenye utashi. Utu hutoka kwa mtu. Mungu lazima awe nani au la na sisi tutakuwa ni vitu. Kama si vitu na tuna mwanzo basi tulitoka/kuumbwa na Mtu, na ndiye Mungu. Na kama sisi ni vitu hatuna tofauti na chupa za kemikali maabara na mjadala mzima unakuwa useless!

Nikupe mfano huu,
MUNGU katika kusudi lake la milele kabla hajamuumba binadamu aliuliza HAKI,KWELI NA HURUMA endapo ni vema wamuumbe binadamu au lah

Haki akajibu "usimuumbe binadamu Kwa kuwa atazivunja Sheria na kanuni zako zote"

Kweli akajibu "usimuumbe Kwa kuwa binadamu atakuwa mbaya na daima atatafuta uwongo na hila( udanganyifu)

Huruma akajibu "ninajua mwanadamu atakuwa mbaya Sana lakini Mimi nitamuhifandhi na kutembea naye katika njia zake za Giza mpaka mwishowe nitamrejesha kwako"
Hii umeipata wapi?

Kuna tofauti Kati ya dhambi na nakosa.Ukifanya dhambi MUNGU hawezi kukuona maana ni mtakatikfu ,
Mungu ambaye kuna mambo haoni inakuwaje awe Mungu? Na utakatifu unamaanisha nini? Nini tafsiri yako juu ya neno utakatifu?

ndy maana Adam alipokula tunda, MUNGU hakumuona Adam ndy maana akauliza "Adam uko wapi"
Mungu hakumuuliza Adamu kwa sababu alikuwa hamuoni.

Mwanzo 3:8 - 13
"Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya?

Hapa ukisoma unaona stori unayoisema haipo. Nikimkuta mwanangu amechukua sukari na nilishamkataza asile, nikamwuliza "unakula nini?" ina maana sijui anachokula? Jibu ni kuwa nafahamu, ila nataka kuona atajibu nini. The same with God.

Unless of course una ka mungu unakokawaza kwenye akili yako!
 
Ntasema, maovu ni matokeo tu ya matumizi yasiyo sawa ya freewill.

Ila nakataa kwamba bila kuwepo maovu basi kusingekuwepo na freewill. Hapana.

Nitasema kuwa kuna freewill kwa sababu ya upendo. Mungu aliweka utashi ili kuwe na uwezekano wa kupenda, kumpenda na kupendana.

Upendo ni pale ambapo mtu mwenye uwezo wa kufanya vyovyote anapoamua kwa hiyari yake kutumia uwezo huo kutimiza matakwa/mapenzi ya huyo anayempenda. Wanazuoni wanasema ni viumbe wenye utashi tu ndio wenye uwezo wa kupenda.

Mungu anao uwezo wote, utashi wote na ujuzi wote. Lakini badala ya kutumia assets zake hizo akaamua kuwapa wanadamu uwezo, na utashi pia na yeye anasikiliza kile wanadamu wanajiamulia wao wenyewe kwa freewill zao.......... huu tunauita ni Upendo mkuu sana.
Kwako wewe na kwa tafsiri yako ni kuwa maovu yanafanyika nje ya dhana ya freewill?
 
Sasa hapo kuna utofauti gani na nilichokiandika mimi?

Freewill ni uchaguzi kati ya Mema na yasiyo mema

Kinyume cha mema ni ubaya

Sasa nikisema freewill ni uhuru wa kuchagua kati ya mema na mabaya kuna utofauti gani hapo na mtu aliyesema mema na yasiyo mema?
Nimesisitiza kuwa ni 'mema na yasiyo mema kwetu/kwako binafsi'.

Ukiwa na watoto wawili na matunda mawili nanasi na tikiti ukawaambia chagueni tunda utakalopenda kula;

Mtoto A akachagua tikiti tutasema tikiti ni kitu chema kwake na hajaona kama nanasi ni jema kwake.
Mtoto B yeye kachagua nanasi ndiyo ameliona jema na sio tikiti. Na wala hatathubutu kusema tikiti ni ovu/baya. Hapana. Hahitajiki kuwa na baya ili achague jema bali anachagua jema analojiskia kutoka katika mema meeeengi. Na hiyo ni freewill

Akikataa vyote na kutaka kula mawe hapo labda ndio tuseme anataka vitu viovu, lakini kama ulivyoona hajahitaji kula mawe ndio tuseme anao uchaguzi. La. Hata kama angekula nanasi bado angekuwa ameonesha freewill bila kuhitaji mabaya yawepo
 
Kwako wewe na kwa tafsiri yako ni kuwa maovu yanafanyika nje ya dhana ya freewill?
Hapana.

Kama nikisummarize ntasema uovu umo ndani ya dhana ya freewill, so freewill ni kitu kikubwa kisichohitaji uovu ili kiwepo, ila uovu unahitaji freewill ili uwezekanike kuwepo.
 
Nimesisitiza kuwa ni 'mema na yasiyo mema kwetu/kwako binafsi'.

Ukiwa na watoto wawili na matunda mawili nanasi na tikiti ukawaambia chagueni tunda utakalopenda kula;

Mtoto A akachagua tikiti tutasema tikiti ni kitu chema kwake na hajaona kama nanasi ni jema kwake.
Mtoto B yeye kachagua nanasi ndiyo ameliona jema na sio tikiti. Na wala hatathubutu kusema tikiti ni ovu/baya. Hapana. Hahitajiki kuwa na baya ili achague jema bali anachagua jema analojiskia kutoka katika mema meeeengi. Na hiyo ni freewill
Bado nakuona una maanisha kile kile nachozungumzia mimi

Wema na ubaya, unaweza ukazi classfiy kwa namna nyingi

Ubaya na uzuri, kinachofaa na kisicho faa

Kupitia mfano wako wewe dhana iliyotumika hapo ni interest yani jambo ambalo ukifanya haliwi dhambi na wala usipolifanya haiwi dhambi

Sasa wewe umetumia hoja ya mtoto kutokuwa interested na tikiti kuonekane kama ni option ya freewill kati ya mema na yasiyo mema. Kitu ambacho sio sahihi

Haiwezi kuwa considered kama ni uchaguzi mbaya kwasababu alichokichagua au kuto kichagua hakipo katika orodha ya vitu vibaya

Sasa chukulia kama wewe ndio umempa mtoto uhuru wa kuchagua kati ya kula nyama ya ng'ombe au ya mtu

Halafu mtoto achague kula nyama ya mtu, je kuna namna yeyote unaweza kuwaza kuwa kachagua kisicho chema ila sio kibaya?
 
Hapana.

Kama nikisummarize ntasema uovu umo ndani ya dhana ya freewill, so freewill ni kitu kikubwa kisichohitaji uovu ili kiwepo, ila uovu unahitaji freewill ili uwezekanike kuwepo.
Na ili iitwe freewill si lazima ihusishe mambo yote mawili uovu na wema?
 
Ntasema, maovu ni matokeo tu ya matumizi yasiyo sawa ya freewill.

Ila nakataa kwamba bila kuwepo maovu basi kusingekuwepo na freewill. Hapana.

Nitasema kuwa kuna freewill kwa sababu ya upendo. Mungu aliweka utashi ili kuwe na uwezekano wa kupenda, kumpenda na kupendana.

Upendo ni pale ambapo mtu mwenye uwezo wa kufanya vyovyote anapoamua kwa hiyari yake kutumia uwezo huo kutimiza matakwa/mapenzi ya huyo anayempenda. Wanazuoni wanasema ni viumbe wenye utashi tu ndio wenye uwezo wa kupenda.

Mungu anao uwezo wote, utashi wote na ujuzi wote. Lakini badala ya kutumia assets zake hizo akaamua kuwapa wanadamu uwezo, na utashi pia na yeye anasikiliza kile wanadamu wanajiamulia wao wenyewe kwa freewill zao.......... huu tunauita ni Upendo mkuu sana.
Katika hii video imeelezewa dhana iliyotypiwa hapa. Challenges are welcome;

Na ili iitwe freewill si lazima ihusishe mambo yote mawili uovu na wema?
Basi labda tuseme uovu na wema kwa kutegemea/relatively to mtu fulani. Yaani huo uovu na wema uwe wa mtu binafsi anavyouona hapo sawa
 
Nazungumzia uovu ambao ni katazo kwa Mungu

Uovu ambao unaweza ukakufanya uende motoni

Uovu huo upo kwenye hiyo freewill?
 
Back
Top Bottom