God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Mungu anajua hatma kwasababu yupo nje ya time dimension. Hivyo yeye anakuona mwaka 2000, anakuona mwaka 2022 na anakuona mwaka 2040 (mfano tuu).

Hajakupangia wala haku control ila anakuona unavyofanya maamuzi yako na unavyovuna matokeo yake.

Hata hivyo ameweka njia ambayo ukichagua kuifuata unapata matokeo mazuri wakati wote.
Nakubaliana na wewe,
Kabisa
 
Hii kitu nilikuwa natafakari Sana, isome yote,

kama Mungu anajua mwisho wa dunia katika mtiririko wote, ni dhahiri kuwa atakuwa anajua pia mwanzo na mwisho wa kila mwanadamu katika mtiririko wote…

ikiwa na maana kuwa anajua ni yupi ataokolewa na yupi hataokolewa, ni yupi ataingia mbinguni na ni yupi hataingia mbinguni siku ya mwisho…

Na kama anayajua hayo ni dhahiri kuwa ni yeye huyo huyo ndiye anayechagua ni yupi ataokolewa na yupi hataokolewa..Kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema “Hakuna awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenipeleka (Yohana 6:44)”.

Kwahiyo ni Roho Mtakatifu ndiye anayemvuta mtu kwa MUNGU na sio mtu mwenyewe anayejipeleka kwa Mungu.
 
Ngoja nikupe mfano

Mimi ni mfanya biashara ninaye endesha maduka mawili katika eneo moja hapa mjini. Duka langu moja linajihusisha na uuzaji wa silaha na lingine linajihusisha na maswala ya kimichezo

Kwa bahati nikatembelewa na mtu wangu naye mjua anaitwa Calvin, Calvin akataka kununua silaha nzito ila akanieleza kuwa anachukizwa na hao mabinti waliopo kwenye duka langu la michezo na kwa hivyo basi anaenda kuwafundisha adabu

Calvin akaniomba nimuuzie package ya risasi kwa ajili ya silaha, nikamuuzia

Calvin akasema anaenda kuua watu wote waliopo katika eneo hilo, nikamuambia usifanye hivyo. Nikamuambia ni jambo baya sana hutakiwi kufanya

Calvin akaniambia nimfundishe namna ya ku shoot silaha, nikamfundisha

Nikamuonya tena kuwa hupaswi kwenda kutumia hii silaha ku shoot watu

Calvin akatoka na silaha na kwenda kuua kila mtu aliyekuwepo kwenye lile duka linalo jihusisha na michezo

Polisi walivyokuwa wakinihoji nikawasimulia stori nzima ilivyokuwa na nikiwaambia kuwa sio kosa langu ila ni Calvin alikuwa na freewill na nilimuonya asifanye hivyo.

Watu wengi wangeniwajibisha kwa ku-base tu kwenye yale yaliyokuwa sawa kufikiri kwamba Calvin angefanya kutokana na yale ambayo Calvin aliyosema kabla ya kuondoka kwenye duka langu.

Kama nawajibika kwenye sehemu ya mauaji, vipi kuhusiana na Mungu ambaye alimpa Calvin maisha akijua kwa hakika nini Calvin ataenda kufanya kwenye hayo maisha?

Mimi nilijua kidogo tu nini Calvin angeenda kufanya kupitia silaha niliyomuuzia. Lakini nimewajibika

Mungu alijua kwa hakika na anaweza kuzuia chochote. Au vinginevyo Mungu hakujua, au Mungu hana uwezo wote
Hapa nafikiria Kila mwanadamu ana lessons zake lazima apitie .
 
Kwanini Mungu aliumba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya kufanyika?
Kwa sababu ya upendo kaka.

Mungu anatupenda sisi na ndiyo maana ameruhusu tuweze kufanya maamuzi kulingana na mapenzi yetu. Ametuamini tuna uwezo wa kufanua maamuzi mema na anatupenda.

Maamuzi hayo muda mwingine yanakuwa ni yenye makosa [mabaya] na ndiyo maana husamehe na kutupatia muda wa rehema kuyaelewa kupitia matokeo yake na mwishoni kuyatubu[change of mind] hayo makosa.

Ikiwa angeweka kusiwezekane kufanyika kitu kinyume na mapenzi yake basi tungesema anatumia tu uwezo/power yake na sio upendo. Lakini kwa kutusikiliza sisi matakwa yetu anatupa mfano wa matumizi mazuri ya nguvu/uwezo/ujuzi/power.

Power is best expressed through LOVE

Kufanya mtu afe ghafla baada ya kuwaza kutenda dhambi sio upendo ni uwezo/power. Kufanya mtu afanye unachotaka tu hata kama hapendi [yaani hata kama unaamini ni kizuri kwake] bado sio upendo ni uwezo.

Wazazi hutumia uwezo kwa watoto wadogo maana bado hawajauamini utashi wao upo na ujinga mwingi. Ila watoto wakikua upendo ndiyo hutawala maana utashi umeshabalansi.

Mungu ametutrain kupitia mitume na manabii na hadi sasa ameshatuamini. Tusimuangushe
 
Kwahiyo ni Roho Mtakatifu ndiye anayemvuta mtu kwa MUNGU na sio mtu mwenyewe anayejipeleka kwa Mungu.
Sahihi kuwa Roho wa Mungu ndiye anayevuta watu waende kwa Mungu.

Pia ni ukweli kwamba Mungu hana upendeleo

Hivyo Roho wa Mungu anawavuta watu wote wenye akili timamu kwa Mungu.

Wenye kukubali wanaitikia, wenye kukataa wanaitikia.

Mvuto upo kwa kila mtu, baada ya kuja Masihi sheria ya Mungu iliandika katika kila moyo. Inabaki utashi wako tu kukubali au kukataa!
 
Sahihi kuwa Roho wa Mungu ndiye anayevuta watu waende kwa Mungu.

Poa ni ukweli kwamba Mungu hana upendeleo

Hivyo Roho wa Mungu anawavuta watu wote wenye akili timamu kwa Mungu.

Wenye kukubali wanaitikia, wenye kukataa wanaitikia.

Mvuto upo kwa kila mtu, baada ya kuja Masihi sheria ya Mungu iliandika katika kila moyo. Inabaki utashi wako tu kukubali au kukataa!
Safi kabisa ,
 
Una tatizo moja la kujitoa ufahamu, haijalishi ni kwa namna gani unajibiwa ila umekuwa ukijipumbaza kimakusudi na kujidai huoni majibu

Hilo unalosema hujajibiwa nimekujibu na hapa tena nakujibu kukuwekea msisitizo, sitarajii tena kuona swali hilo post zijazo.

Kama Mungu anaweza kujua nini kitaenda kutokea mbeleni in 100% accuracy with no margin of errors then kile kinachoenda kutokea ni predetermined na predetermined ina pingana na freewill kwasababu choice ishakuwa fixed na kwamba huwezi kuchagua vinginevyo

Kama huwezi kuchagua vinginevyo huwezi kuwa na freewill

Ingawa unaweza kujiona kama uko free kwenye kile ambacho unaona umekichagua kwa utashi wako lakini uhalisia ni kuwa uchaguzi huo ulishakuwa fixed you couldn't choose otherwise
Kijana mpaka najiuliza kwanini hujibu swlai langu ? Swali langu linakutaka wewe uonyeshe mafungamano kati ya kupangiwa jambo, Mola kujua na uhuru wako wa kufanya hayo mambo.

Mola amekuoangia jambo fulani, Mola anajua jambo fulani ila hajakushurutisha wewe ufanye jambo hilo, ndiyo maana ukapewa utashi na akili, na uwezo kufanya jambo na kutolifanya.
 
Wewe unapofanya mambo yako kwa uhuru inamaanisha sisi wengine hatupo huru?

Mungu anatumia uhuru wake kufanya mema, sisi nasi tunatumia uhuru wetu kadiri tupendavyo.

Kila mmoja anashinda mechi zake.
Nakufuatalia na nakuelewa mkuu, Kongole sana. Sasa kwanin uwezo wa kuamua kati ya mtu na mtu unatofautiana, yaan utakuta mtu mmoja ana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko mwingine, huon hapa Mungu aliweka bias kweny kufanya maamuzi sahihi na ambayo sio sahihi kwa kutofautisha uwezo wetu wa kufikiri? Huon hawa aliowapa uwezo mkubwa wa kufikiri unawakandamiza walio wa uwezo mdogo wa kufikiri? Kwanin Mungu hakuumba watu wote tuwa na utashi, akili na ufahamu sawa?
 
Unathibitisha ya kuwa mfano wako si halisi. Swali langu la msingi unalotakiwa kujibu ni kuwa kujua kwake kuna kuzuia nini wewe kufanya unalo taka ?

Mola wetu kwa kutuumba sisi na kutujua vizuri nje ndani anajua cha kabla na baadae, mfano mwepesi sana, wewe lro hii kwa kumjua kwako vizuri mtu fulani basi huwa unajua nini atafanya baada ya jambo fulani.

Sasa hapo ndipo ulipo uhuru kamili wa mwanadamu, Allah anajua kila kitu ana uwezo wa kila kitu, lakini anakuacha ufanye unachotaka sababu amekupa uhuru ila angetaka kuzuia angezuia.
Uwezo wa kufanya uovu na ubaya amenipa Mungu, sio? Mimi kufanya uovu ni matokeo ya kushindwa kufanya mema kutokana na vichocheo vya ubaya kuzidi ndani yangu, sasa nani aliniumba hivi? Kwanin aruhusu vichocheo vya ubaya kuzid wema ndani yangu? Utasema mim ndo nimechagua, Kwanin nimechagua ni kwasababu ya udhaifu uliopo ndani yangu ambao Mungu ameniumbia nao, kwanin aniwekee mtego huu?
 
Kwa sababu ya upendo kaka.

Mungu anatupenda sisi na ndiyo maana ameruhusu tuweze kufanya maamuzi kulingana na mapenzi yetu. Ametuamini tuna uwezo wa kufanua maamuzi mema na anatupenda.

Maamuzi hayo muda mwingine yanakuwa ni yenye makosa [mabaya] na ndiyo maana husamehe na kutupatia muda wa rehema kuyaelewa kupitia matokeo yake na mwishoni kuyatubu[change of mind] hayo makosa.

Ikiwa angeweka kusiwezekane kufanyika kitu kinyume na mapenzi yake basi tungesema anatumia tu uwezo/power yake na sio upendo. Lakini kwa kutusikiliza sisi matakwa yetu anatupa mfano wa matumizi mazuri ya nguvu/uwezo/ujuzi/power.

Power is best expressed through LOVE

Kufanya mtu afe ghafla baada ya kuwaza kutenda dhambi sio upendo ni uwezo/power. Kufanya mtu afanye unachotaka tu hata kama hapendi [yaani hata kama unaamini ni kizuri kwake] bado sio upendo ni uwezo.

Wazazi hutumia uwezo kwa watoto wadogo maana bado hawajauamini utashi wao upo na ujinga mwingi. Ila watoto wakikua upendo ndiyo hutawala maana utashi umeshabalansi.

Mungu ametutrain kupitia mitume na manabii na hadi sasa ameshatuamini. Tusimuangushe
You are using evil to produce good huh?

Alishindwa kuwa na upendo ambao ungefanya yafanyike mazuri bila ubaya?

Umejenga hoja ya mabaya kwa kuangalia maamuzi, vipi na yale mabaya ynayofanyika bila maamuzi ya watu kama matetemeko, yanayouwa hadi watoto wadio na hatia?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu usio wezekana hayo yote kutokea?
 
Unachanganya kati ya foreknowledge, kujua kitu kabla hakijatukia na kufanya kitukie.
Ukiwa na utashi maana yake unaamua utafanya nini. Mungu anajua kuwa katika kuutumia utashi utautumiaje.

Mfano, kabla X hajazaliwa, Mungu anajua matendo yake yote atakayoyafanya na kuwa atakufa akiwa anafanya ujambazi na kuwa atahitimisha safari yake motoni. Mungu anajua kwa sababu kila sekunde anajua jamaa atafanya uchaguzi gani. Mungu kujua uchaguzi ambao X ataufanya kwa utashi wake (X) hajahusika kumfanya X afanye ujambazi. Ni uchaguzi binafsi wa X ambao Mungu aliujua kabla hajaumbwa kwa sababu Omniscience inajumlisha na foreknowledge.

Wengi hujichanganya hapo!
Mfano ambao sio mkamilifu ila utafaa kukusaidia kuelewa ni huu.
Fikiria una mtoto wako. For some reason ukajua kuwa kesho ataiba sukari. Je ni wewe ndiye umesababisha aibe kwa sababu unajua kuwa ataiba sukari?

Kuongezea kwenye haya, Mungu hujua tutakachochagua na ndio maana hutuletea watu wa kutuhubiria habari njema ili kutupa nafasi. Na anajua wangapi watazipokea nafasi hizo na wangapi watazikataa. Ili siku ikifika wasiseme haukutupa nafasi!

Hope hizo nafasi utazitumia vyema ikiwemo hii!

Mungu anajua maamuzi yako yote na utakavyoishia. Ni kama uone mkanda wa video mpaka mwisho halafu muwe mnaangalia na wengine. Hakuna kinachobadilika. Sema mfano huu sio mkamilifu kwa sababu Mungu hana mfanowe. lakini utakupa picha!

Kila mwanadamu ametenda dhambi na amehukumiwa kwenda Jehanamu. Yesu ametoa nafasi kwa wanaotaka kulipiwa deni lao kumwamini. Mungu anajua kama utatumia utashi wako kuchagua kumwamini Yesu ama la! Na kwa sababu hiyo anajua kama uchaguzi wako ni wa Jehanamu ama mbinguni. Kumbuka kwenye hili Mungu sio bystander bali ndiye Jaji haswa na sheria anaijua vizuri.

Kwa hiyo huwezi kupewa utashi ukachagua kumkataa Mungu halafu ukienda Jehanamu useme haukuwa na uhuru wa kuchagua. Kama wanadamu tusingekuwa huru hakuna angekwenda Jehanamu. Mungu anataka wote tuione mbingu ila kwa sababu ya utashi wengi wataishia Jehanamu!

Hapa sijui kama umetumia akili sawasawa kuwaza. Kama nikijua leo utaamua kuwa mwizi kesho maana yake hauko huru kwa sababu nimejua? Kwamba nimekupangia kwa kuwa nimejua utakachofanya?

Shida yako unachanganya mambo. Mungu kujua au kutojua utakachofanya kwa uchaguzi wako hakuna madhara kwenye utashi. Mimi nikijua ama nisjue kesho utaiba sukari haibadilishi uhalisia kuwa ulichagua kuba sukari!
Swali, kama Mungu alijua huyu ninayemuumba ataenda moton, na moton ataenda kwa kuchagua yeye mwenyew lakin uchaguzi wake ndo huo aende moton, sasa kwanin aniumbe nikateseke wakat yeye anajua kabisa naenda moton maana anajua mwsho wangu kabla ya mwanzo?
 
Kijana mpaka najiuliza kwanini hujibu swlai langu ? Swali langu linakutaka wewe uonyeshe mafungamano kati ya kupangiwa jambo, Mola kujua na uhuru wako wa kufanya hayo mambo.

Mola amekuoangia jambo fulani, Mola anajua jambo fulani ila hajakushurutisha wewe ufanye jambo hilo, ndiyo maana ukapewa utashi na akili, na uwezo kufanya jambo na kutolifanya.
Nishakujibu

Hakuna cha utashi what seems to be utashi is just an illusion though you may experience a freedom lakini in reality everything has been predetermined and you have no freewill to choose otherwise
 
Alishindwa kuwa na upendo ambao ungefanya yafanyike mazuri bila ubaya?

Umejenga hoja ya mabaya kwa kuangalia maamuzi, vipi na yale mabaya ynayofanyika bila maamuzi ya watu kama matetemeko, yanayouwa hadi watoto wadio na hatia?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu usio wezekana hayo yote kutokea?
Watu waliokwisha amini kuwa kuna mambo ya kiroho hawatishwi na dhoruba za kimwili kwa kiwango unachotishwa wewe nikwambie. Wanayo Imani na amani pia.

Labda wewe utachukulia mtu kufa katika tetemeko ni jambo baya kuliko vyote kwa kuwa umeamini hapa duniani ndiyo kila kitu. Na uhai huu ndio kila kitu. Sio hivyo.

Kwa kuwa Mungu anapenda tuuexperience upendo na utashi kama tu yeye alivyo ndiyo maana katuumbia huu ulimwengu. Na kingine hapangiwi kaamua kaona huu ni mzuri kwetu kwa upendo kabisa
 
The same kwa mtu asiye amini Mungu hawezi tishwa na habari za jehanamu

Ila hapa tunajadili yale ambayo yanaleta madhara kwa watu wote hata wasio amini habari za roho

Mtu asiyeamini na anayeamini wote hawapendi kukutwa na mabaya kama hayo

Ingekuwa mabaya hayo sio tishio basi tusingeona hata wanaoamini katika roho wakifanya jitihada za kuhangaika namna ya kuepuka hayo mabaya kwasababu washajua kua hata wakipatwa na hayo mabaya watakua na extra time huko mbeleni.

Kwa hiyo swali langu bado hujajibu

Ikiwa mabaya yapo kwasababu ya uamuzi wa mtu, ilikuwaje Mungu akashindwa kuumba ulimwengu ambao viumbe wangeweza kuchagua yaliyo mema (kama ufafunuzi wako wa freewill unaohusisha mema pekee)

Kwanini Mungu hakuumba ulimwngu huo?

Na pia sio kweli kuwa kila baya linalifanyika linatokana na maamuzi yetu, mafuriko, natural calamities kwa ujumla wake husababisha maafa makubwa massively

Kivipi mabaya hayo yameweza kutokea licha ya kwamba hayajatokea kupitia maamuzi yetu?
 
Ndio sio kweli kutokana na kwamba tupo wengi na maamuzi yanafanuwa na watu wengi sio wewe binafsi pekee. Kukiwa na upendo na mshikamano hata hayo unayoyaita mabaya ya asili sio ya kusikitikiwa kihivyo. Ndiyo maana nikakuambia ili tupate experience mbalimbali kulingana na maamuzi yetu tujirudi kisha tutubu [tubadili fikra zetu].

Wanajeshi wanaokabiliana na adui huwa na furaha ya ajabu hata kama wenzao wanakufa. Ni feeling fulani nzuri sana kujua kuwa kuishi kwako na kufa kwako na kwa wengine ni katika upendo kwa wote. Hata majanga na kifo yana tafsiri tofauti jamii za kidunia zikiunganishwa na kuongezewa upendo katika kupambana na 'common enemy'

Kufurahi pamoja, kusikitika pamoja ni furaha hata kama sio raha. Endelea kushangaa na kulabel vitu kuwa vibaaaaya. Kama hutaki kuuona uzuri ndiyo. Tunasema kusudi la yote hayo ni jema hata kama wewe kwa wakati huo huelewi.

Mfano huu mfano niliupata kwa concept ya Mcqueenen alisema watu walipogundua moto ndio wakaweza kupika na kusapoti bongo kubwa zaidi kwa kuwa chakula kilichopikwa kinatokeza nishati zaidi.

Sasa ukichukulia labda sehemu kupigwa na baridi kali ni kitu kiovu, sehemu ikapigwa na baridi kali ukasema ni baya limetokea. Kumbe ndani yake kuna kusudi la kuwafundisha watu watafute moto na walishe chakula bora bongo zao. Watakaokataa kutumia akili kutumia moto automatically watakufa watapotea kwa ubishi wao. Ila waliobaki wataishi katika dunia iliyojaa watu wanaopenda kutumia bongo zao zaidi.

Au ukichukulia kuliwa na simba ni kitu kiovu bila maamuzi ya mliwa. Lakini angalia raha atakazozipata mtu atakayeweza kujenga mfumo wa asibugudhiwe na simba tena. Nyumba imara. Matumizi ya moto. Kutokutembea tena maporini na kubugudhi viumbe!

The earth is a training ground. Strengteningnground. Ukibaki na hiyo notion yako ya kutaka Mungu atufanyie kila kitu kisa ana uwezo ukaitafsiri kuwa na wewe uwafanyie kila kitu wanao kisa una uwezo jiandae kupata kizazi cha hovyo. Kuwakinga watoto na dhoruba ndogondogo hata zile za kuwajenga hayo ni mapenzi at best na sio upendo. Na inawatesa baadhi yao hawataweza kuexperience raha jata kama wataishi rahani maana hawaijui shida.

Unajua sifuri ndiyo inaanza na moja ni ya pili? -Songa
 
Sahihi kuwa Roho wa Mungu ndiye anayevuta watu waende kwa Mungu.

Pia ni ukweli kwamba Mungu hana upendeleo

Hivyo Roho wa Mungu anawavuta watu wote wenye akili timamu kwa Mungu.

Wenye kukubali wanaitikia, wenye kukataa wanaitikia.

Mvuto upo kwa kila mtu, baada ya kuja Masihi sheria ya Mungu iliandika katika ki

Kijana mpaka najiuliza kwanini hujibu swlai langu ? Swali langu linakutaka wewe uonyeshe mafungamano kati ya kupangiwa jambo, Mola kujua na uhuru wako wa kufanya hayo mambo.

Mola amekuoangia jambo fulani, Mola anajua jambo fulani ila hajakushurutisha wewe ufanye jambo hilo, ndiyo maana ukapewa utashi na akili, na uwezo kufanya jambo na kutolifanya.
Safi Sana
 
Ndio sio kweli kutokana na kwamba tupo wengi na maamuzi yanafanuwa na watu wengi sio wewe binafsi pekee. Kukiwa na upendo na mshikamano hata hayo unayoyaita mabaya ya asili sio ya kusikitikiwa kihivyo. Ndiyo maana nikakuambia ili tupate experience mbalimbali kulingana na maamuzi yetu tujirudi kisha tutubu [tubadili fikra zetu].

Wanajeshi wanaokabiliana na adui huwa na furaha ya ajabu hata kama wenzao wanakufa. Ni feeling fulani nzuri sana kujua kuwa kuishi kwako na kufa kwako na kwa wengine ni katika upendo kwa wote. Hata majanga na kifo yana tafsiri tofauti jamii za kidunia zikiunganishwa na kuongezewa upendo katika kupambana na 'common enemy'

Kufurahi pamoja, kusikitika pamoja ni furaha hata kama sio raha. Endelea kushangaa na kulabel vitu kuwa vibaaaaya. Kama hutaki kuuona uzuri ndiyo. Tunasema kusudi la yote hayo ni jema hata kama wewe kwa wakati huo huelewi.

Mfano huu mfano niliupata kwa concept ya Mcqueenen alisema watu walipogundua moto ndio wakaweza kupika na kusapoti bongo kubwa zaidi kwa kuwa chakula kilichopikwa kinatokeza nishati zaidi.

Sasa ukichukulia labda sehemu kupigwa na baridi kali ni kitu kiovu, sehemu ikapigwa na baridi kali ukasema ni baya limetokea. Kumbe ndani yake kuna kusudi la kuwafundisha watu watafute moto na walishe chakula bora bongo zao. Watakaokataa kutumia akili kutumia moto automatically watakufa watapotea kwa ubishi wao. Ila waliobaki wataishi katika dunia iliyojaa watu wanaopenda kutumia bongo zao zaidi.

Au ukichukulia kuliwa na simba ni kitu kiovu bila maamuzi ya mliwa. Lakini angalia raha atakazozipata mtu atakayeweza kujenga mfumo wa asibugudhiwe na simba tena. Nyumba imara. Matumizi ya moto. Kutokutembea tena maporini na kubugudhi viumbe!

The earth is a training ground. Strengteningnground. Ukibaki na hiyo notion yako ya kutaka Mungu atufanyie kila kitu kisa ana uwezo ukaitafsiri kuwa na wewe uwafanyie kila kitu wanao kisa una uwezo jiandae kupata kizazi cha hovyo. Kuwakinga watoto na dhoruba ndogondogo hata zile za kuwajenga hayo ni mapenzi at best na sio upendo. Na inawatesa baadhi yao hawataweza kuexperience raha jata kama wataishi rahani maana hawaijui shida.

Unajua sifuri ndiyo inaanza na moja ni ya pili? -Songa
Utetezi wako ume contains logical fallacy kama attempt yaku fabricate hoja ionekane factual

Mabaya yanayotokea bila kuamuliwa na mtu umetumia red herring fallacy kuyafanya yasionekane mabaya na kwamba ni mambo ya kawaida yasiyopaswa kuwa considered kama mabaya

Matetemeko, vimbunga, tsunami, nk. hayo ni mabaya ambayo yanafanyika bila watu kuamua yafanyike

Ikiwa kila baya linalotendeka hutokana na maamuzi ya watu, mfano mtu kamsababishia mwenzake kufa hilo tunaweza kuliweka katika matokeo ya uamuzi wa mtu

Lakini vipi kwa matsunami yanayoua maelfu na kuacha watu wakiwa na majonzi kwa kuondokewa na watu wao wapendwa wakiwemo watoto wasio na hatia?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya kama hayo hayawezi kutokea?
 
Back
Top Bottom