Kama upendo huja kwa hiari na sio sheria kali kwanini kuna adhabu ya moto?
Watu wanafanya mema sio kwa kupenda ni kwasababu ya kuogopa moto, sasa hiyo hiari hapo iko wapi?
Tuna hatua kadhaa za hisia zinazotawala katika kumjua Mungu;
Hatua ya hofu ya Mungu au uoga wa mabaya yanayoweza kukupata kama kifo na jehanamu humsaidia mtu auache ujinga aanze kumtafuta Mungu. [Uoga huwafaa wote wasiotaka kutumia akili vizuri, mfano watoto kwa baba - ila wakikua mbinu hii haifai]
Akishampata anaanza kumjua na kadri anavyomjua hofu inampungua wakati imani 'trust' ikiongezeka.
Trust ikikomaa inazaa hisia za upendo na kujitolea 'dedicated' kwa kutenda kazi za Mungu kunakuwa ni matokeo. [Watu waliokomaa, trust na love na service ndizo zinawashikamanisha]
Watu wengi tu leo tupo hatua ya kumpenda Mungu na kujitolea kwake hata kama labda hakuna mambo ya moto. Hata kama hakuna mambo ya miujiza. Tumemuamini Mungu na tunampenda na tunamtumikia. Binafsi hata kama hakuna maisha baada ya haya nimekubali kuwa katika hayahaya maisha nitajitahidi kuyaishi vizuri uweponi mwake.
In fact tushawahi kukaa na mzee mmoja tukajadili uwezekano wa hiki tulichonacho ndicho chenyewe tukagundua hata zile ahadi za mbingu mpya na nchi mpya zinaweza kutimizwa hapahapa na maisha yakawa ufalme wa Mungu! sio lazima wote tufe;
Mfano 1. kila mmoja akafuata dhamiri na Roho Mtakatifu [sheria ya Mungu iliyoandikwa mioyoni mwetu], 2. akafanya kazi anayoipenda na 3. matunda yake akayafaidi na familia na jamii, 4. jamii zote zikaacha kujifunza vita badala yake nguvu zikaelekezwa kwenye uzalishaji mali matrekta[kufua panga zetu ziwe plau] 5. upendo kiujumla ukatawala.
Sifa za ki utawala wa Mungu
Au 1. Kila mmoja akaongozwa na ubinafsi hata kama dhamiri inamsuta, 2. Kila mmoja akafanya kazi kitumwa na bado asilipwe stahiki [tabu tupu] 3. unyonyaji 4. Tukaendelea kuwekeza katika tafiti za silaha kalikali za kinyuklia, silaha etc 5. kiujumla chuki ikatawala.
Sifa za ki utawala wa shetani