God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Baba anakosea, sio mara zote anaweza kuwa sahihi

Baba ni kiumbe duni, hana upendo wote kwani ni mara ngapi katika jamii tumeshuhudia ukatiri wa wazazi kwa watoto?

Mfano wako wa baba hauna nguvu katika kutetea hoja kuhusu Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote
Labda tunatofautiana baba,

Binafsi nililelewa na baba aliyekuwa na upendo wote [kulingana na mimi], alikuwa na ujuzi wote [ukilinganisha na utoto na ujinga wangu] na uwezo wote. So nimekua nikiwa na mfano bora. Hata kama angeweza kuninunulia pipi kila siku hakufanya hivyo na nilimuamini kwamba anajua chema zaidi kwangu.

Kama wewe unayo mifano ya ukatili tu wa wazazi basi usihangaike kubisha hapa watafute wanasaikolojia wakusaidie.
 
Ni kweli hakuna mfano zaidi ya huo kwasababu hakuna namna utaelezea swala la kitu chenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kikasirishwe na matendo yanayofanywa na kiumbe ambacho kipo chini ya uwezo wake bila contradiction
Kukasirishwa. Mungu akasirishwe na sisi!?

Watu waliosoma tu wa hapahapa duniani wakaelewa jamii, uhalisia na saikolojia za watu ni ngumu kukasirishwa na wajingawajinga sasa leo ije kwa Mungu mwenye elimu yote umkasirishe wewe?
 
Labda tunatofautiana baba,

Binafsi nililelewa na baba aliyekuwa na upendo wote [kulingana na mimi], alikuwa na ujuzi wote [ukilinganisha na utoto na ujinga wangu] na uwezo wote. So nimekua nikiwa na mfano bora. Hata kama angeweza kuninunulia pipi kila siku hakufanya hivyo na nilimuamini kwamba anajua chema zaidi kwangu.

Kama wewe unayo mifano ya ukatili tu wa wazazi basi usihangaike kubisha hapa watafute wanasaikolojia wakusaidie.
Kwa sifa hizo unamtofautishaje na Mungu?

Yani umefika point unatumia hadi hoja ambazo zina contradiction ili tu kumfanya Mungu awepo?

Baba yako alikuwa anauwezo wote alishindwa kufanya namna itayokufanya ufanye kile ambacho yeye kinampendeza na wewe vile vile kinakupendeza?
 
Uzi mzuri ngoja niendele kuelimika
Kuna kitu kimoja cha ajabu kwa watu wazima, ukiona unaelimika na kufurahia elimu mpya, ujue hata sio mpya kweli. Ni kitu ulikuwa unachontangu mwanzo sema tu kuna jamaa kaamua kukiweka katika maneno.

So unaresonate nacho. Kwa mantiki hiyo naamini unajua na tunakaribisha maoni yako pia✌
 
Baba yako alikuwa anauwezo wote alishindwa kufanya namna itayokufanya ufanye kile ambacho yeye kinampendeza na wewe vile vile kinakupendeza?
Unaupenda uroboti, na unautetea kwa nguvu zote.

Ukweli ni kwamba hiyo sio njia bora zaidi ya kuyaishi maisha. Uwe na uwezo ama la.

Kama una nguvu sana hebu watie nguvu marafiki zako ili wote muwe na nguvu ndio utaona raha yao na yako maradufu. Kutengeneza chawa na kupenda uchawa vyote ni dalili ya kutojiamini.

Wachina /wajapani/korea na watabe wengine wa sanaa za mapigano wana ka msemo 'It is so lonely at the top'. Ntarudia the best way to express power is through love
 
Kukasirishwa. Mungu akasirishwe na sisi!?

Watu waliosoma tu wa hapahapa duniani wakaelewa jamii, uhalisia na saikolojia za watu ni ngumu kukasirishwa na wajingawajinga sasa leo ije kwa Mungu mwenye elimu yote umkasirishe wewe?
Kumbukumbu la torati 9:8

"Tena mlimkasirisha BWANA katika Horebu, BWANA akakasirika hadi akataka kuwaangamiza"

kutoka 15:7

"Kwa wingi wa ukuu wako wawaangamiza wapinzani wako; wawapulizia ghadhabu yako nayo yawateketeza kama makapi"
 
Yani umefika point unatumia hadi hoja ambazo zina contradiction ili tu kumfanya Mungu awepo?

Baba yako alikuwa anauwezo wote alishindwa kufanya namna itayokufanya ufanye kile ambacho yeye kinampendeza na wewe vile vile kinakupendeza?
Elewa mambo ya relativity utatatua mambo mengi, nilisema alikuwa na uwezo wote na ujuzi wote na uwezo wote kulingana na nafasi yangu ya utoto niliyokuwa nayo.

Maswali yote niliyomuuliza alijibu au angeweza kujibu[mengine hakujibu aliona ni bora niyatafute majibu kadri navyokua]. Alikuwa na uwezo wote wa kuninunulia pipi na vigari vya watoto na hakufanya hivyo etc etc
 
Unaupenda uroboti, na unautetea kwa nguvu zote.

Ukweli ni kwamba hiyo sio njia bora zaidi ya kuyaishi maisha. Uwe na uwezo ama la.

Kama una nguvu sana hebu watie nguvu marafiki zako ili wote muwe na nguvu ndio utaona raha yao na yako maradufu. Kutengeneza chawa na kupenda uchawa vyote ni dalili ya kutojiamini.

Wachina /wajapani/korea na watabe wengine wa sanaa za mapigano wana ka msemo 'It is so lonely at the top'. Ntarudia the best way to express power is through love
Peponi kuna uroboti?
 
Kumbukumbu la torati 9:8

"Tena mlimkasirisha BWANA katika Horebu, BWANA akakasirika hadi akataka kuwaangamiza"

kutoka 15:7

"Kwa wingi wa ukuu wako wawaangamiza wapinzani wako; wawapulizia ghadhabu yako nayo yawateketeza kama makapi"
Tangu mwanzo ninakuambia kuwa picha ya Mungu inabadilika kadri tunavyozidi kumuamini na kumjua.

Mtoto mdogo ana haki ya kusema baba yake ni mkali ana hasira naye.

Ila akikua, au kaka yake anaweza kumuelewesha kwamba baba actually anakupenda, na ule ni upendo sio mahasira.

Mwana wa Mungu [YESU[ alikuja kutuonesha njia bora zaidi ya kumuelewa Mungu, msikilizzage yeye
 
Elewa mambo ya relativity utatatua mambo mengi, nilisema alikuwa na uwezo wote na ujuzi wote na uwezo wote kulingana na nafasi yangu ya utoto niliyokuwa nayo.

Maswali yote niliyomuuliza alijibu au angeweza kujibu[mengine hakujibu aliona ni bora niyatafute majibu kadri navyokua]. Alikuwa na uwezo wote wa kuninunulia pipi na vigari vya watoto na hakufanya hivyo etc etc
Kwa hiyo hapa mfano wako uanzungumzia katika akili ya kitoto kuwa ulikuwa na mawazo hayo?
 
Tangu mwanzo ninakuambia kuwa picha ya Mungu inabadilika kadri tunavyozidi kumuamini na kumjua.

Mtoto mdogo ana haki ya kusema baba yake ni mkali ana hasira naye.

Ila akikua, au kaka yake anaweza kumuelewesha kwamba baba actually anakupenda, na ule ni upendo sio mahasira.

Mwana wa Mungu [YESU[ alikuja kutuonesha njia bora zaidi ya kumuelewa Mungu, msikilizzage yeye
Picha ya Munhu haibadilika unaye badilika ni wewe kwa kujipinga mwenyewe

Kwa hiyo nishike lipi

Nikuamini maneno yako na kuipuuza biblia?
 
Hapana, nafikiri utashi huru unatawala zaidi. Sijui kuhusu kama kuna viumbe hawakupewa utashi nikifika ntajua zaidi🤔
Sijajua kama umenijibu au hujanijibu

Peponi kuna uroboti au haupo?
 
Sijajua kama umenijibu au hujanijibu

Peponi kuna uroboti au haupo?
Peponi bado sijafika lakini nini kinashindikana.

Kama duniani tunao wanetu [freewill] na pia tunazo mashine za atm [roboti]

Basi hata mbinguni kuna vyenye utashi na visivyokuwa nao labda.

Lakini kama unauliza kuhusu sisi wanadamu tutakaoishi huko basi jibu ni hakuna uroboti
 
Chance ya kufanya uovu kupitia free will peponi ipo?
 
Picha ya Munhu haibadilika unaye badilika ni wewe kwa kujipinga mwenyewe

Kwa hiyo nishike lipi

Nikuamini maneno yako na kuipuuza biblia?
Sio mimi bro, historia inaonesha hivyo;

Mungu ni mkubwa na sisi kwa akili zetu tunamuelewa kulingana na uwezo wetu kwa wakati huo. Akili inavyopanuka unamjua Mungu zaidi naamini hivyo. Na ndivyo ilivyo anyways.
 
Chance ya kufanya uovu kupitia free will peponi ipo?
Ndiyo, kinadharia chance ipo kiuhalisia haipo wala. Rejea mfano wangu wa mwanajeshi wa kawaida vs yule mwanajeshi mkubwa na mzalendo damu, ambaye hata identity yake amejipiga chapa ya nchi yake ndani kwa ndani
 
Back
Top Bottom