Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 9,138
- 22,236
Hauezi ielewa, twende tu tukapiganie Katiba Mpya.Mada ngumu sana hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hauezi ielewa, twende tu tukapiganie Katiba Mpya.Mada ngumu sana hii
Siyo huenda, hiyo ni fact.Huenda mungu hakumuumba shetani
Hatujalazimishwa kutenda au kuchagua kile anachokijua au anachokiwaza Mungu.Mungu akijua utaenda kushoto, hapo una uchaguzi wa kufanya unachotaka ukaenda kulia?
Kama huna option hiyo utasemaje una uhuru wa kufanya unachotaka wakati choice ilishakuwa fixed kabla hata hujazaliwa?
View attachment 2242516
Kama ambavyo hakuna baya linaweza kutokea bila freewill kuhusika.Hakuna jema linaweza tokea bila freewill kuhusika
Hello y’all..
NB: Naomba moderator mada hii msiihamishie jukwaa la dini maana huko itakosa wachangiaji na lengo langu la kutaka kujuzwa jambo hili halitatimia and that will leave me frustrated and bums me out, Natuamaini mtatii takwa langu hili. Ahsanteni.
Binafsi kiimani ni muumini wa kanisa Katoliki kwa kuzaliwa na kubatizwa, pia ninaamini na kuisadiki kanuni ya imani yangu katoliki isemayo “Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi muumba mbingu na dunia na kwa Yesu Kristu Bwana wetuu….” Self-schemas: katika sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.
Self-Concept ni i hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future self (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo). Toka nilipoanza kutambua Self Concept yangu Nimekua na swali ambalo kwakweli pamoja na kuisadiki imani yangu hii na kupokea ya Sakrament takatifu ya Communion swali hilo limekua mwiba mchungu na kikwazo kikubwa katika imani yangu hii na Mungu kwa ujumla.
Toka nilipoanza kujitambua nimejaribu kuwashirikisha watu wenye uelewa jambo hili ila bado sijapewa majibu thabiti….natumaini hapa JF nitapewa maelekezo vyema , mnivumilie kama maelezo yatakua marefu maana hua siwezi kuelezea kwa ufupi but it worth your time.
The One above all, In-Betweener and The One bellow all.
Monotheism ni imani ya kua kuna Mungu mmoja pekee ambae aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo. Watu wanao amini katika imani hii ni wafuasi wa dini zilizotokana na Ibrahim ambae anachukuliwa kama baba wa imani ambazo ni Judaism, Ukristo,uislam, mandaeism ,Rastafarian na Bahai. Mungu wa imani hii ndio huyu tunayemfahamu mimi na wewe ambae ana sifa kuu tatu ambazo ni yupo kila mahali, anajua kila kitu, na anaweza kila kitu. Omni ni neno la kilatini lenye maana ya yote au kila kitu na Sciens ni neno la kilatini likimaanisha kujua(conscious)……. Moja kati ya sifa kuu tatu za Mungu nilizotaja hapo juu ni Omniscience ikimaanisha kwamba Mungu anajua yote yaliyopita,yaliyopo na yajayo.
The Great Chain of Being ni mchoro au nadharia ambayo inaonyesha kwamba maisha ya mwanadamu yapo kwenye ngazi /mtiririko Fulani ambapo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,mimea halafu chini kabisa yupo shetani. Mungu ni the one above all, mwanadamu ni aliyekati /in-betweener na shetani ni the one below all. Unajua mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote walioumbwa na mungu kuzidi hata malaika ndio maana kuna malaika wanafanya kazi kwa wanadamu ya kutulind, Moja kati ya utajiri na kitu kikubwa alichonacho mwanadamu hakuna kiumbe kingine anacho ni uwezo wa kuchagua na kuamua Kuishi vile atakavyo yeye yaani Free Will….Katika Great chain of being mwanadamu amewekwa katikati (In-Betweener) maana yeye ameumbwa na roho isiyokufa (immortal) na mwili ambao unaokufa (mortal) hivyo inamuwezesha yeye kuishi duniani au mbinguni . Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi Uungu kwa kutenda mema maishani mwake au ushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Kwakua mwanadamu ana free will uamuzi ni wake ni kuchagua kwenda kwa The One above all au kwa the one bellow all.
Free Will is illusion (?)
Kuna mada Fulani niliwahi kusema kwamba tukio la kuumbwa Adam na eva hadi kufukuzwa eden linapinga uwepo wa Mungu kwa kupinga sifa tatu alizonazo Mungu kwamba anaweza yote,anajua kila kitu na yupo kila mahali… ndio maana mimi hua nalichukulia kama lugha ya picha tu na sio tukio halisi na kama kweli ni kweli lilitokea kama lilivyoelezewa kwenye kitabu cha mwanzo basi linaonyesha Mungu hafai kupokea sifa tunazompa. Kama anajua kila kitu je wakati anamuumba adamu bila Eva hakujua kwamba adamu hatapata uhitaji wa kua na mwenza? Yupo kila mahali jewakati adam na eva wamekula tunda hakuwepo pale walipojificha hadi aanze kuuliza wako wapi? Alikua hajajua juu ya tukio la adam kula tunda maana lilimuudhi kwelikweli like he didn’t know a thing from a first place.
Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni? Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo. Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?
Kuna phrase protestant wanapenda kusema kwamba sisi wakatoliki hatujui kusoma na kuielewa biblia, naamini name ni mmoja wapo nisiojua kusoma biblia. Hivyo basi napenda kuwaalika wale wote wenye uelewa juu ya jambo hili. Naombeni mnijuze kama Mungu anajua hatima yangu na hukumu yangu siki ya mwisho na kama anajua je naweza kubadirisha? Kama mchezo kautengeneza yeye na sharia za mchezo kazitengeneza yeye je wachezaji wanawezaje kua huru?
Vinjii…
Not really.But sovereign man and Sovereign God are mutually exclusive.
Hakuna mipaka, kuna matokeo ya uamuzi wetu.Nilitaka kuweka sawa kwamba Mungu hakutupa utashi usio na mipaka. Mnara wa Babeli, Gharika ya Nuhu, Sodoma na Gomora, Kifo cha Herode, Yona na Ninawi ni mifano michache kuwa mwanadamu hakupewa uhuru wa kufanya chochote bali kuna mipaka!
Ukishakuwa na hofu juu ya adhabu fulani uliyoahidiwa kupewa endapo hutafanya yale uliyoamrishwa ufanye utasemaje uko huru?Tuna hatua kadhaa za hisia zinazotawala katika kumjua Mungu;
Hatua ya hofu ya Mungu au uoga wa mabaya yanayoweza kukupata kama kifo na jehanamu humsaidia mtu auache ujinga aanze kumtafuta Mungu. [Uoga huwafaa wote wasiotaka kutumia akili vizuri, mfano watoto kwa baba - ila wakikua mbinu hii haifai]
Akishampata anaanza kumjua na kadri anavyomjua hofu inampungua wakati imani 'trust' ikiongezeka.
Trust ikikomaa inazaa hisia za upendo na kujitolea 'dedicated' kwa kutenda kazi za Mungu kunakuwa ni matokeo. [Watu waliokomaa, trust na love na service ndizo zinawashikamanisha]
Watu wengi tu leo tupo hatua ya kumpenda Mungu na kujitolea kwake hata kama labda hakuna mambo ya moto. Hata kama hakuna mambo ya miujiza. Tumemuamini Mungu na tunampenda na tunamtumikia. Binafsi hata kama hakuna maisha baada ya haya nimekubali kuwa katika hayahaya maisha nitajitahidi kuyaishi vizuri uweponi mwake.
In fact tushawahi kukaa na mzee mmoja tukajadili uwezekano wa hiki tulichonacho ndicho chenyewe tukagundua hata zile ahadi za mbingu mpya na nchi mpya zinaweza kutimizwa hapahapa na maisha yakawa ufalme wa Mungu! sio lazima wote tufe;
Mfano 1. kila mmoja akafuata dhamiri na Roho Mtakatifu [sheria ya Mungu iliyoandikwa mioyoni mwetu], 2. akafanya kazi anayoipenda na 3. matunda yake akayafaidi na familia na jamii, 4. jamii zote zikaacha kujifunza vita badala yake nguvu zikaelekezwa kwenye uzalishaji mali matrekta[kufua panga zetu ziwe plau] 5. upendo kiujumla ukatawala. Sifa za ki utawala wa Mungu
Au 1. Kila mmoja akaongozwa na ubinafsi hata kama dhamiri inamsuta, 2. Kila mmoja akafanya kazi kitumwa na bado asilipwe stahiki [tabu tupu] 3. unyonyaji 4. Tukaendelea kuwekeza katika tafiti za silaha kalikali za kinyuklia, silaha etc 5. kiujumla chuki ikatawala. Sifa za ki utawala wa shetani
Kuchagua masomo ya sayansi kwako kunaweza kuonekana kama umefanya uamuzi huo kwa utashi wako lakini kihalisia ulikwisha amuliwa uje uchague sayansi na haukua na uchaguzi mwingineMungu hajampangia yeyote kitu chochote.
Kila kitu kinatokea kwa sababu ya uamuzi ulioufanya ambao utapelekea uamuzi mwingine.
Kwa mfano; Ukiamua kuchukua masomo ya sayansi yatakuja kusababisha uchague course ya aina fulani ambayo nayo itapelekea uishi maisha tofauti kabisa na let's say ungeamua kuchagua masomo ya sayansi.
Lakini sababu zote hizo ni matokeo tu ya uamuzi unaoamua kuufanya. Hakuna anayekupangia.
Hakuna mtu ambaye yuko free kufanya maamuziUngepangiwa usingekuwa na mamlaka ya kufanya uchaguzi. The very moment unakuwa na uwezo wa kufanya uamuzi, hapohapo dhana ya kupangiwa inaondoka.
Mwalimu ambaye anajua majibu utayoenda kuchagua kabla hajakupa mtihani, anasababu yeyote ya kukupa huo mtihani?Unakuwaje na uhuru wa kuchagua kama tayari umeshapangiwa?
Unaambiwa chagua jibu sahihi kati ya yafuatayo;
Rais wa kwanza wa Tanzania ni:
(a) Mwl. Julius Kambarage Nyerere
Hapo unachagua nini sasa?
Kwani ya kingereza imepotosha?Rudia kuisoma, nimekuwekea na kwa Kiswahili.
Nakumbuka uliwahi kunimind kutumia mfano wa baba na mtoto lakini sidhani kama nitaacha. Nitaachaje sasa wakati hata Yesu mwenyewe alipenda kutumia mfanano wa namna iyo hiyo? Mimi kama mfuasi wake nitaendelea kuiga mfano wake.Ukishakuwa na hofu juu ya adhabu fulani uliyoahidiwa kupewa endapo hutafanya yale uliyoamrishwa ufanye utasemaje uko huru?
Kama upendo huja kwa hiari kwanini Mungu hakuweka mfumo huru ambao watu wangemuabudu kwa hiari yao bila kulazimishwa kumpenda kwa kuogopa moto?
Pana free will mpaka hapo?
Mipaka ipo. Ndio maana wote waliovuka mipaka Mungu aliingilia kati. Mfano mmojawapo ni Yona. Hakutaka kwenda kuhubiri Ninawi, kwa utashi wake akaamua kwenda Tarshishi. Mungu angeweza kumwacha afanye kwa utashi wake ili avune matokeo ya ubishi wake. Lakini akaingilia kati akampa kichapo mpaka akakubali kwenda Ninawi kinyume na utashi wake.Hakuna mipaka, kuna matokeo ya uamuzi wetu.
Please explain how a sovereign man can exist with a Sovereign God.Not really.
True but we were not created gods.We were created in the image and likeness of God.
No man is sovereign! If you debate that, I will be waiting for an answer to the first point/Just as how God is sovereign, so we are.
We have free will because God allowed us to choose things.This is the reason for the existence of our free will.
No, we were not! If you debate it, prove it (see point 1)We were created sovereign.
Huyo baba anakuwa na uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kiasi ashindwe namna ya kufanya mwanae aende katika mienendo anayoitaka?Nakumbuka uliwahi kunimind kutumia mfano wa baba na mtoto lakini sidhani kama nitaacha. Nitaachaje sasa wakati hata Yesu mwenyewe alipenda kutumia mfanano wa namna iyo hiyo? Mimi kama mfuasi wake nitaendelea kuiga mfano wake.
Wakati ambapo Baba hajamuamini kikamilifu mwanae anaruhusiwa kutumia vitisho. Kusema hajamuamini nadhani ni makosa, tuseme amemuamini kuwa anaweza kuwa mtu mzuri. Ila kwa wakati huo bado hajaamini uwezo wa akili yake kufanya maamuzi sahihi. Anajua fika kwamba mwanae bado hana ujuzi sahihi tayari bali mtoto ako na ujinga mwingi. Atamtisha, atamchapa atamlazimisha kutii baadhi ya vitu. Na hii ni sehemu ya uzoefu utakaomjenga kuweza kuaminika baadaye kadri elimu/ujuzi/uzoefu wake unavyokua.
Lakini akikua ndio utamuacha ajiamulie. Unaamini sasa anao ujuzi wa kutosha na uzoefu unaofaa anaweza kuamua kufanya vema kwa upendo na kuyafaidi matokeo yake!
Ndiyo Mungu anajua kila kitu, na anajua hadi kwamba hii ndio njia nzuri zaidi ya kupitia sisi wanaye ili tuyafurahie maisha mazuri. Wewe mwenye ujuzi pungufu ndio umeshindwa kun'gamua hilo.
Hata tukirudi kwenye mifano usiyoipenda: Kumpatia mwanao starehe moja kwa moja ni kumuharibu. Hata ukijidanganya kwamba mwanangu hana haja ya kujifunza kushughulika sana kisa mimi babaake tayari nina mali nitamrithisha kampuni, bado humtendei haki. Utashangaa hapati njaa, wala kiu ya pesa ila anapata vigonjwa vya kijinga mara depression. Hafurahii mali yake I mean mali yako vizuri. Lakini kama ungempa mazingira ya kuitafuta mali na kuexperience upatikanaji wake atakuwa na furaha kinyama, maana ameipata mali yake sio kopi ya mali ya baba. Labda na Mungu anatupa nafasi ya kuutafuta utakatifu ili tutakapouexperience tuufaudu kinyama.
Hata ukiitazama biblia kuna evolution ya jinsi watu wanamchukulia Mungu kuanzia kimsingi jitu lenye nguvu la kutisha kwenda li jaji lenye haki kamili hadi hapa mwishoni kuwa baba mwenye upendo na rehema na neema😊
Hata kama angekuwa na huo uwezo wote na ujuzi wote hiyo sio njia ya kuiexpress power/uwezo wake.Huyo baba anakuwa na uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kiasi ashindwe namna ya kufanya mwanae aende katika mienendo anayoitaka?
Baba anakosea, sio mara zote anaweza kuwa sahihiHata kama angekuwa na huo uwezo wote na ujuzi wote hiyo sio njia ya kuiexpress power/uwezo wake.
Mungu anatufundisha kuwa 'power is best expressed through love' otherwise hakuna anayefaidi sana iwe upande wa mtawala au mtawaliwa.
Au ndugu yangu Scars wewe binafsi unapenda sana kuwa karoboti kakuendeshwa. Je hujiamini kuwa unaweza kufanya maamuzi sahihi kwa hiyo unaona ni bora tu kama kuna anayejua zaidi yako akuendeshage tu. Je huupendi ubinadamu wako?
Sifikirii kama kuna mfano mzuri zaidi ya huo.Baba anakosea, sio mara zote anaweza kuwa sahihi
Baba ni kiumbe duni, hana upendo wote kwani ni mara ngapi katika jamii tumeshuhudia ukatiri wa wazazi kwa watoto?
Mfano wako wa baba hauna nguvu katika kutetea hoja kuhusu Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote
Ni kweli hakuna mfano zaidi ya huo kwasababu hakuna namna utaelezea swala la kitu chenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kikasirishwe na matendo yanayofanywa na kiumbe ambacho kipo chini ya uwezo wake bila contradictionSifikirii kama kuna mfano mzuri zaidi ya huo.