Hapana kaka hakuna uroboti, ukiwa huko unaweza kuamua kufanya uovu, unaweza kuamua kukaidi na kutokuwa mtii kwa Mungu ukiamua. Ukiweza sijui kinamna gani.
Kila nikiandika hiyo statement sitaacha kuweka msisitizo kuwa pamoja na kuwa unaweza kuamua kwenda kinyume hautakaa uamue hivyo wewe mwenyewe kwa kuwa wewe ni mwema na mtii [yaani muislamu] kwa Mungu. Na tayari unaishi katika utukufu wa Mungu ndani yake, na Mungu anaishi ndani yako sasa hayo mawazo ya kukaidi unayatoa wapi? Ego na pride/kiburi vinaweza kuwa vishawishi kutokea ndani yako lakini nisikatae sana. Ila tambua kuwa mpaka unafika mbinguni hivyo vitu umevimaster ujue. Sijui tu utaanzaje kukaidi ila mfano ukaamua kukaidi utaweza na utakufa nadhani automatically kama wengine waliokufa kabla.