God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Umeshawahi kuthibitisha Mungu yupo? Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Thibitisha Mungu yupo.
Hili kila siku nalithibitisha na hapa nathibitisha :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Tur : 35)
 
Unakubali kama logic ni fani kama fani, na muanzilishi wa fani hii ni Aristoto ?

Kati ya logic na lugha kipi kimetangulia ? Usikimbie swali.

Bila shaka kabisa.

Hii siyo kweli.

Kila siku nakujibu swali hili, msingi wa logic ni kutumia akili. Unakubali kama akili ina ukomo ? Kama ina ukomi vipi logic iweze kukidhi mahitaji...?
Logic ni nini?

Daraja lina ukomo? Daraja linakidhi mahitaji ya kuvuka mto?

Yani hapo ulichoandika ni sawa na kusema hutaki kutumia daraja kuvuka mto kwa sababu daraja lina ukomo!

Kufikiri kwamba kitu kikiwa na ukomo hakikidhi mahitaji ni logical non sequitur.
 
Hili kila siku nalithibitisha na hapa nathibitisha :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Tur : 35)
Wewe sio tu huthibitishi, hujui hata kuthibitisha ni nini.

Unachanganya kuhubiri na kuthibitisha.

Hapo umehubiri, hujathibitisha.

Kuhubiri si kuthibitisha.
 
Wewe sio tu huthibitishi, hujui hata kuthibitisha ni nini.

Unachanganya kuhubiri na kuthibitisha.

Hapo umehubiri, hujathibitisha.

Kuhubiri si kuthibitisha.
Nimecheka sana. Sasa unatakiwa ukosoe nilichokiandika usilete dibaji.

Nifundishe kuthibitisha ni nini na kuhubiri ni nini ? Shida yenu huwa mnaishia juu juu.

Aya imekamilika hiyo, ukisoma sababu za kushuka aya hiyo ndipo utakapo jiona wewe ni mjinga na logic ni elimu ya kupigwa vita sababu inawafanya watu kuwa wajinga. Wakana mungu hawajaanza juzi wala jana, bali wale wa kale ni tofauti na nyinyi wale walikuwa wananua kuhoji, wanajua historia na wanajua lugha, nyinyi hamna vyote hivyo.

Kuhubiri ni nini ?
 
Logic ni nini?
Ni fano kupitia fani hiyo humfanya mtu asikosee katika katika kujenga hoja. Zimekuja maana nyingine zikisema logic ni elimu inayo mfunza mtu namna ya kujenga hoja bali zimekuja katika maana za logic (Mantiki) ni elimu ya kutumia akili.
Daraja lina ukomo? Daraja linakidhi mahitaji ya kuvuka mto?
Daraja lina ukomo kwa kile kilichosanifiwa kwacho, maana yake ilikuwa vizuri zaidi kuwa zaidi ya hapo.
Yani hapo ulichoandika ni sawa na kusema hutaki kutumia daraja kuvuka mto kwa sababu daraja lina ukomo!
Hii si maana yangu, naposema akili ina ukomo, ni kwamba ukom wake inakidhi haja na kwa muongozo mzuri wa namna ya kuitumia akili hiyo, lakini kwa ukomo wake pakawa na visaidizi vya kuitoa katika huo ukomo na kwenda mbali zaidi. Hizi ala wanafalsafa wa kale hawakuwa nazo.

Shaykhul Islam Ibn Taymiyah katika kitabu chake "Raddi 'al mantiqiyiin (Ukosoaji kwa watu wa mantiki (logic)) akasema Wanafalsafa walikuwa na maswali sahihi lakini walikosa nyenzo za kufikia majibu sahihi.
Kufikiri kwamba kitu kikiwa na ukomo hakikidhi mahitaji ni logical non sequitur.
Hili kosa lingine.

Kingine uwe unajibu maswali ninayo kuuliza.
 
Nimecheka sana. Sasa unatakiwa ukosoe nilichokiandika usilete dibaji.

Nifundishe kuthibitisha ni nini na kuhubiri ni nini ? Shida yenu huwa mnaishia juu juu.

Aya imekamilika hiyo, ukisoma sababu za kushuka aya hiyo ndipo utakapo jiona wewe ni mjinga na logic ni elimu ya kupigwa vita sababu inawafanya watu kuwa wajinga. Wakana mungu hawajaanza juzi wala jana, bali wale wa kale ni tofauti na nyinyi wale walikuwa wananua kuhoji, wanajua historia na wanajua lugha, nyinyi hamna vyote hivyo.

Kuhubiri ni nini ?
Uthibitisho unatumia ushahidi na hoja kuonesha uhalisia naukweli , evidence na argument to establish fact and truth.

Wewe umehubiri, hujaweka ushahidi wala hoja, hujaweka evidence wala fact.

Kuhubiri ni kama ulivyofanya hapo, unaweka aya halafu unasema aya imeshuka hiyo.

Una uhakika gani imeshuka na haijatungwa na watu hapahapa duniani? Unaweza kuthibitisha aya hiyo imeshuka na haijaandikwa na watu kama hadithi tu?
 
Ni fano kupitia fani hiyo humfanya mtu asikosee katika katika kujenga hoja. Zimekuja maana nyingine zikisema logic ni elimu inayo mfunza mtu namna ya kujenga hoja bali zimekuja katika maana za logic (Mantiki) ni elimu ya kutumia akili.

Daraja lina ukomo kwa kile kilichosanifiwa kwacho, maana yake ilikuwa vizuri zaidi kuwa zaidi ya hapo.

Hii si maana yangu, naposema akili ina ukomo, ni kwamba ukom wake inakidhi haja na kwa muongozo mzuri wa namna ya kuitumia akili hiyo, lakini kwa ukomo wake pakawa na visaidizi vya kuitoa katika huo ukomo na kwenda mbali zaidi. Hizi ala wanafalsafa wa kale hawakuwa nazo.

Shaykhul Islam Ibn Taymiyah katika kitabu chake "Raddi 'al mantiqiyiin (Ukosoaji kwa watu wa mantiki (logic)) akasema Wanafalsafa walikuwa na maswali sahihi lakini walikosa nyenzo za kufikia majibu sahihi.

Hili kosa lingine.

Kingine uwe unajibu maswali ninayo kuuliza.
Umesema logic imeanzishwa na Aristotle.

Mpaka hapo umejionesha ungumbaru wako.
 
Kosa kubwa linalofanywa na wengi wanapomjadili Mungu ni kwamba kufikiri anawaza kama mawazo yetu. Kama apo Vinci unafikiri mungu anajua jema na baya, kitu ambacho sio kweli, kwake yeye yupo beyond good and evil. Good and evil are product of human effort to make sense of this world, ndio maana unakuta jamii nyingi tunatofautiana juu ya kipi ni chema n kipi ni kibaya, mfano kuna jamii kula nguruwe ni soo, pia kuna jamii kaka kumowa ndugue ni sawa kabisa, au kijana wa kiume aliyebalehe kumchukua dogo wa kiume na kuishi nae kama mkewe ni sawa tu.

Cha kujua sir God katuweka tuexpress our truest self, na pia kushangaa na kutukuza utukufu wake anaonyesha kila sehemu ukiangazia macho. siku atakapokuja kuvuna mbegu zakee kuna watu kwa kushangaa taya zao zitagusa chini.
Kama ndivyo kwamba Mungu hawazi kama sisi, basi yote tunayoamini hata yaliyoandikwa kwenye so called "vitabu takatifu" bado ni upuuzi cause nayo pia yaliandikwa na binadamu kama sisi. Na the fact kwamba hakuna aliyemuona Mungu na kupiga naye stori mahali, hata wanaosema wamemuona hatuna uhakika sababu, its not in our experience. Hivyo bottom line ni kwamba we don't know nothing.
 
Umesema logic imeanzishwa na Aristotle.

Mpaka hapo umejionesha ungumbaru wako.
Basi vizuri. Kielimu ulitakwia uonyeshe kama logic kama fani haikuanzishwa na Aristoto. Hivi ndivyo wajuzi wa mambk wanafanya.

Nasuburi uje kuionyesha nani muanzilishi wa fani ya Logic.
 
Uthibitisho unatumia ushahidi na hoja kuonesha uhalisia naukweli , evidence na argument to establish fact and truth.
Safi kabisa huwa napata mashaka sana na ufahamu wako, yaani akili yako ni ndogo sana kiasi kwamba huujui uhalisia na hoja.

Aya niliyo kuwekea ina uhalisia ambao ndiyo fack, tena ile self evident truth.

Ngoja nikuonyeshe hualisia na uthibitisho katika hiyo aya. Hiyo aya imetoa changamoto kwa wale wanao mkana Mola, na kuwauliza maswali mawili :

1. Je sisi tumejiumba wenyewe au
2. Tumetokana pasi na kitu chochote ?

Sasa ili hayo maswali yasiwe hoja wala yasiwe na uhalisia unatakiwa ututhibitishie ya kuwa aidha sisi tumejiumba wenyewe au tumetokana pasi na chochote.

Sasa nasubiri majibu ya maswali hayo.
Wewe umehubiri, hujaweka ushahidi wala hoja, hujaweka evidence wala fact.
Kwanini hujifunzi maana za maneno kabla ya kuyatumia. Hapo nimehubiri nini ? Kwamba dunia imejiumba au nyinyi mmejiumba ?

Hapo hakuna facts ? Huo siyo uhalisia ? Sasa jifunze kuifata hoja na kuikosoa siyo kuikimbia na kulalama. Yaani hujawahi kuifata hoja bali siku zote huwa unaikimbia hoja.
Kuhubiri ni kama ulivyofanya hapo, unaweka aya halafu unasema aya imeshuka hiyo.
Hapo sija hubiri bali nimehoji na kuthibitisha yaani kunukuu yale ambayo wajinga wenzako wa kale walikuwa wakikanusha.
Una uhakika gani imeshuka na haijatungwa na watu hapahapa duniani? Unaweza kuthibitisha aya hiyo imeshuka na haijaandikwa na watu kama hadithi tu?
Hili swali huwa unalikwepa sana, hujawahi kunijibu kwanini unasema ni hadithi ?

Mimi nina uhakika sababu kuna chain ya mapokezi ya hizo habari.
 
Basi vizuri. Kielimu ulitakwia uonyeshe kama logic kama fani haikuanzishwa na Aristoto. Hivi ndivyo wajuzi wa mambk wanafanya.

Nasuburi uje kuionyesha nani muanzilishi wa fani ya Logic.
Aristotle systematized logic, but logic was there before Aristotle.

Plato and Socrates used logic.

The pre-Socratic philosophers used logic.

Anyone who used language in a systematic way used logic.

Surely, you are not saying Aristotle started language, are you?

Hilo nimeliandika mara nyingi, nakubali na ninasisitiza ni kweli taswira inayofanyika akilini mwetu [picha] ya Mungu inabadilika na itaendelea kubadilika milele.

Mimi, hata wewe na yeyote ndio tunaobadilika kila siku kadri tunavyojua mambo mapya. Sisi ni kweli tunabadilika kuendelea kuwa bora, kuwa watakatifu zaidi maana sisi sio wakamilifu tusipokufa tutaendelea kukamilika milele na milele.
Saizi umebadilisha kutoka picha ya Mungu kubadilika mpaka kuongeza taswira akilini mwetu?

Vipi kama kubadilika kwa taswira ya Mungu akilini mwako ni kutokana na kutokuwepo kwake kiasi cha kufanya upate ugumu unapojaribu kumfikiria katika uhalisia?
 
Tilia mkazo maneno yaliyokuwa 'capitalized': JAMANI MBINGUNI NI MAHALA PEMA NA PAMEZUNGUKWA NA 'U'- WEMA.
Je unaweza kutumia uwezo wako wa kujenga taswira halafu ukaona jinsi maswali yako yanavyokuwa yanapotea.?

Binafsi nilipojilazimisha kufikiri namna uovu unaweza kutokea Mbinguni nikapata jibu kwamba ili mtu afanye uovu huko ataanza kwanza kwa kukataa kuwa mtii kwa Mungu ndipo afanye uovu. Sasa ukikataa kuwa mtii automatically unakoma 'cease' kuwa mbinguni na [kuondoka uweponi mwa Mungu]. Kwa hiyo itakapofika steji unafanya uovu ni tayari kama umenusurika kufa basi tayari upo eneo jingine linalosapoti maovu.

Mbinguni sio sehemu unaenda physically ili kwamba kuondoka huko kuhitaji muda mwingi wafanye booking wakukatie tiketi upande ndege ndo uondoke. Mbinguni ni hali zaidi kuliko mahali.

Nitaomba nitumie mbinu ya kushambulia ego yako kiasi bro: Unafahamu kuwa watu wenye IQ ndogo ndio huwa wabishi sana hawawezi kuchukulia vitu vya kufikirika abstract kiumakini 'reluctant to take the hypothetical' seriously? on average iq of mentally retarded!
Hata hivyo nisikutishe sana maana kundi jingine lenye kupitiliza na kuchukulika vitu vya kufikirika kuwa ni halisi na vinashikika wao huitwa 'vichaa' 😂😂. Psychotic.

Wee not so fast! kuna kundi jingine tena hapohapo wenye kuijua asili ya uhalisi wa vya kufikirika na uhalisi wa vitu vingine bila kujichanganya hao wapo gifted/jiniazi. Nakuombea mwishoni usettle hapa. Na ni wengi tu wapo hapa hata hivi sasa.

Kukiwa mahala pema maana yake hakuwezekani kufanyika uovu ambao upo ndani ya free will

Kwa maana hiyo mbinguni kuna uroboti
 
Kama ndivyo kwamba Mungu hawazi kama sisi, basi yote tunayoamini hata yaliyoandikwa kwenye so called "vitabu takatifu" bado ni upuuzi cause nayo pia yaliandikwa na binadamu kama sisi. Na the fact kwamba hakuna aliyemuona Mungu na kupiga naye stori mahali, hata wanaosema wamemuona hatuna uhakika sababu, its not in our experience. Hivyo bottom line ni kwamba we don't know nothing.
Yes, exactly na Mungu will always be mystery. Na atapoteza nguvu zake zote pale mwanadamu atakapomjua complete.
 
Nikija kwenye ishu ya freewill yenyewe hapa napo kuna mambo mengi ya kuzungumza.

Kama ulivyosema kuwa hujapata majibu ya kuridhisha, naweza nikasema imekuwa inatokea hivyo kwasababu watu waliokuwa wanajaribu kukupa majibu walilenga zaidi kuifanya freewill ionekane ni halisia

Kama freewill ni uhuru wa kuchagua wema na ubaya ipo basi hatupaswi kuingiliwa kimaamuzi ili kuonesha tupo free

Uhuru wa kuchagua haupaswi kuambatana na mipaka, kusema hiki sawa na hiki sio sawa ukifanya nakuadhibu, huo sio uhuru hiyo ni amri.

Sasa Mungu kasema amekup uhuru wa kuchagua kumuabudu yeye au shetani halafu ukichagua kumuabudu shetani Mungu huyu anakupa adhabu kali sana ya kuchomwa moto. Je huo ni uhuru kweli?

Katika jamii ikitokea tu kuna mtu kamwambia mke wake nimekuoa uhuru wa kuchagua kufanya chochote utakacho ila ikitokea umechagua kuniacha nitakumwaga ubongo kwa maumivu makali.

Mtu huyo akisikika na watu, watu watamuita mkatili asiye na ubinadamu, ataitwa mnyama asiye na huruma, ataitwa mzushi kwa kutoa ahadi ya uwongo

Lakini kitu kama hicho hicho akikifanya Mungu anaitwa mwenye upendo wote, mjuzi wa vingi na mwenye rehema

Kwanini?
Asee nomaa
 
Freewill ni illusion tu wala haipo in reality

Nataka nianze na Mfano wako wa kusema malaika hawana freewill na kwamba wamekuwa programmed kutii kile ambacho Mungu anawaagiza

Kumbuka freewill ni dhana yenye kuambatana na selection ya mambo mawili "ubaya na uzuri"

Sasa kama malaika hawana freewill na kwamba hawawezi kufanya ubaya, unaelezeaje ishu ya malaika muovu lucifer ambaye alifanya ubaya kwa kumsaliti Mungu?

Alitumia njia gani kufanya ubaya huo bila kuhusisha freewill?

Vipi kuhusu robo tatu ya malaika walioshawishiwa na shetani na kuungana naye katika mkakati wa kumsaliti Mungu na kupelekea vita huko mbinguni?

Hayo yote yaliwezekanaje kufanyika kama malaika wako programmed na hawana freewill ya kuwawezesha kuchagua kufanya ubaya?

Mnaofikiria kwamba mateso na migogoro ipo duniani na kwmaba mbinguni ni raha tu, mnabidi mkumbuke kuwa vita ya kwanza ilianzia huko huko

Mpaka hapo tushajua mbinguni sio sehemu salama na kwamba kuepuka kwako vikwazo huku duniani unakumbushwa kuwa na mwendelezo huo huo wa kinidhamu hata ukiwa huko.
Point
 
Safi kabisa huwa napata mashaka sana na ufahamu wako, yaani akili yako ni ndogo sana kiasi kwamba huujui uhalisia na hoja.

Aya niliyo kuwekea ina uhalisia ambao ndiyo fack, tena ile self evident truth.

Ngoja nikuonyeshe hualisia na uthibitisho katika hiyo aya. Hiyo aya imetoa changamoto kwa wale wanao mkana Mola, na kuwauliza maswali mawili :

1. Je sisi tumejiumba wenyewe au
2. Tumetokana pasi na kitu chochote ?

Sasa ili hayo maswali yasiwe hoja wala yasiwe na uhalisia unatakiwa ututhibitishie ya kuwa aidha sisi tumejiumba wenyewe au tumetokana pasi na chochote.

Sasa nasubiri majibu ya maswali hayo.

Kwanini hujifunzi maana za maneno kabla ya kuyatumia. Hapo nimehubiri nini ? Kwamba dunia imejiumba au nyinyi mmejiumba ?

Hapo hakuna facts ? Huo siyo uhalisia ? Sasa jifunze kuifata hoja na kuikosoa siyo kuikimbia na kulalama. Yaani hujawahi kuifata hoja bali siku zote huwa unaikimbia hoja.

Hapo sija hubiri bali nimehoji na kuthibitisha yaani kunukuu yale ambayo wajinga wenzako wa kale walikuwa wakikanusha.

Hili swali huwa unalikwepa sana, hujawahi kunijibu kwanini unasema ni hadithi ?

Mimi nina uhakika sababu kuna chain ya mapokezi ya hizo habari.

Maswali yako ni boring.

Yamejaa logical non sequitur.

Umeuliza.

1. Je sisi tumejiumba wenyewe au
2. Tumetokana pasi na kitu chochote ?

Hapo hakuna swali ambalo linalazimisha uwepo wa Mungu.

Yani nibsawa na mtu anayesema yeye lazima ni mtoto wa Komredi Kipepe . Kwa sababu hajajiumba mwenyewe na haiwezekani awe hakutokana na chochote.

Sawa, labda hajajiumba mwenyewe, labda haiwezekani awe hakutokana na chochote.

Lakini, amefikia vipi hitimisho kwamba yeye ni mtoto wa Komredi Kipepe? Anaweza hata kuthibitisha kwamba huyo Komredi Kipepe yupo kweli nje ya hadithi tu?

1. Kama tumejiumba wenyewe, au hatujajiumba wenyewe, hilo halilazimishi Mungu awepo.

2. Dhana nzima ya "kutoka" ni umasikini wa mawazo tu.

Ni hivi, suala zima la kwamba lazima kuna hiki cha kwanza, halafu hiki cha kwanza kinasababisha kingine cha pili (cause and effect) ni ujinga wetu tu. This is not an indispensable fundamental of the universe.

At the quantum level, the effect can happen before the cause, and the cause can happen after the effect.

Sasa, kama hujui mambo hayo, unaweza kuwa hujui ujinga wako halafu ukanikashifu mimi kuwa sina akili.
 
Hili kila siku nalithibitisha na hapa nathibitisha :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Tur : 35)
Kwa hiyo hapo ndo unakuwa umethibitisha?
 
Yes, exactly na Mungu will always be mystery. Na atapoteza nguvu zake zote pale mwanadamu atakapomjua complete.
Kwa hiyo maana yake hata watu wa dini nao wanapuyanga tu ingawa wanajifanyaga wao ndo wapo sahihi kweli kweli!?
 
Safi kabisa huwa napata mashaka sana na ufahamu wako, yaani akili yako ni ndogo sana kiasi kwamba huujui uhalisia na hoja.

Aya niliyo kuwekea ina uhalisia ambao ndiyo fack, tena ile self evident truth.

Ngoja nikuonyeshe hualisia na uthibitisho katika hiyo aya. Hiyo aya imetoa changamoto kwa wale wanao mkana Mola, na kuwauliza maswali mawili :

1. Je sisi tumejiumba wenyewe au
2. Tumetokana pasi na kitu chochote ?

Sasa ili hayo maswali yasiwe hoja wala yasiwe na uhalisia unatakiwa ututhibitishie ya kuwa aidha sisi tumejiumba wenyewe au tumetokana pasi na chochote.

Sasa nasubiri majibu ya maswali hayo.

Kwanini hujifunzi maana za maneno kabla ya kuyatumia. Hapo nimehubiri nini ? Kwamba dunia imejiumba au nyinyi mmejiumba ?

Hapo hakuna facts ? Huo siyo uhalisia ? Sasa jifunze kuifata hoja na kuikosoa siyo kuikimbia na kulalama. Yaani hujawahi kuifata hoja bali siku zote huwa unaikimbia hoja.

Hapo sija hubiri bali nimehoji na kuthibitisha yaani kunukuu yale ambayo wajinga wenzako wa kale walikuwa wakikanusha.

Hili swali huwa unalikwepa sana, hujawahi kunijibu kwanini unasema ni hadithi ?

Mimi nina uhakika sababu kuna chain ya mapokezi ya hizo habari.
Self evident truth unaielewa au unaandika tu imradi umejisikia?

Hiyo uliyoandika wewe hapo ni fallacy of appeal to self evident truth
 
Back
Top Bottom