Maswali yako ni boring.
Yamejaa logical non sequitur.
Umeuliza.
1. Je sisi tumejiumba wenyewe au
2. Tumetokana pasi na kitu chochote ?
Hapo hakuna swali ambalo linalazimisha uwepo wa Mungu.
Yani nibsawa na mtu anayesema yeye lazima ni mtoto wa Komredi Kipepe . Kwa sababu hajajiumba mwenyewe na haiwezekani awe hakutokana na chochote.
Kwa vitu ambavyo huwa unaviandika kuna muda huwa naona kabisa najadiliana na mtu fulani asiye jua kitu katika suala la kuhoji na kujenga hoja na kuzing'amua hoja, halafu muda huo huo mnajifaragua na Falsafa na Logic, mimi viwili hivi nilivyosoma kisha nikaviacha sababu niliona vinanifanya niwe mjinga zaidi.
Nakuonyesha utoto wako ulipo katika kuchambua hoja, yaani huwa mnaacha vitu vya msingi na kutoa mifano nako kuna elimu, na nyinyi mmenyimwa elimu hiyo.
Hakuan mtu atakaye sema amezaliwa na Comrade kipepe wakati nasaba inajulikana, sababu vizazi ni vingi. Mfano wako ni mfu, sababu umeruhusu yasiyo husiana na jambo husika kuingia. Suala la kuumba na kuumbwa ni jambo maalumu halitoki nje ya maswali hayo.
Je sisi timejiumba au sisi tumetokana pasi na chochote ? Ili kuonyesha hapo hakuna swali linalo onyesha kuumbwa na Mungu, ukitakiwa kuonyesha uwezekano uliopo wa sisi aidha kujiumba au kutokana pasi na chochote. Kinyume na hapo hoja yangu hujaigusa hata kuisogelea umebaki una ambaa ambaa tu juu. Na haya ndiyo madhara ya Logc, yaani hamgusagi hoja na kilichomo katika hoja.
Kipepe ni mtu au siyo mtu ? Sasa mjifunze kujenga hoja kwa kuzingatia uhalisia vijana.
Sawa, labda hajajiumba mwenyewe, labda haiwezekani awe hakutokana na chochote.
Ondoa tamko labda hapo, hapo ni uhakika hakuna aliye jiumba mwenyewe wala kutokana pasi na chochote. Hilo unayakiwa ukiri,usijipotee muda wa bure.
Lakini, amefikia vipi hitimisho kwamba yeye ni mtoto wa Komredi Kipepe? Anaweza hata kuthibitisha kwamba huyo Komredi Kipepe yupo kweli nje ya hadithi tu?
Huu mfano wako ni batili, sababu nasaba ya huyo kipepe kwa wanao mjua wanaijua yaani chanzo cha huyo kipepe, kuna mawili mtu anayejiita kwa lakabu ya Komredi Kipepe au ni muhusika katika katuni ya Komredi kipepe.
1. Kama tumejiumba wenyewe, au hatujajiumba wenyewe, hilo halilazimishi Mungu awepo.
Sasa ndiyo uonyeshe uwezekano wa kutokuwepo kwa hilo. Yaani usikimbie hoja. Shida yenu huwa hamgusi hoja. Wewe tuambie lililo sahihi ni lipi.
2. Dhana nzima ya "kutoka" ni umasikini wa mawazo tu.
Kivipi ?
Ni hivi, suala zima la kwamba lazima kuna hiki cha kwanza, halafu hiki cha kwanza kinasababisha kingine cha pili (cause and effect) ni ujinga wetu tu. This is not an indispensable fundamental of the universe.
Unachekesha sana, unachotakiwa wewe uonyeshe kutokuwa na ulazima wa kuwepo hicho cha kwanza, hii ndiyo hoja hoja ya msingi. Kisha ujenge hoja kwa uhalisia.
Fundamental ya Universe ikoje ? Yaani hutakiwi kuacha mambo juu juu.
At the quantum level, the effect can happen before the cause
Hiyo Quantum level umeshawahi kuidiriki na nani wa kwanza kuelezea hizi habari ? Isiwe mnapenda tu stori za waja bila kuzinakishi.
Kisha toa mfano ni matokeo gani hutokea bila kisababishi.
Sasa, kama hujui mambo hayo, unaweza kuwa hujui ujinga wako halafu ukanikashifu mimi kuwa sina akili.
Mimi sikufichi mzee wangu na unri wangu huu mdogo ila katika haya mambo wewe hujafikia hata balehe yake na mimi hunigusi hata chembe hata kuvaa viatu vyangu huwezi.
Mimi huwa nasoma elimu kwa lengo la kujua ila nyinyi kwa hoja zenu huwa mnakariri ndiyo maana huwa hamuwezi kutoka nje ya yale waliyo yafikiria kina Aristoto.