Tusaidiane labda mi sijui.
Kwani wewe katika ulimwengu unaoishi kila kitu unachoamini kipo ni kile tu umethibitishiwa na watu kuwa kipo.
Tena hata ukiacha kuthibitishiwa, je wewe mwenyewe umeshajithibitishia kila kitu unachoamini kipo.
Unatumiaga neno kujua, je una uthibitisho wa kila unachokijua binafsi kuwa kipo?
Tukirudi kwenye analojia mimi nipo na nina ujuzi mkubwa, na upendo wote na uwezo karibu wote kwa viungo vya mwili wangu. Viseli vyangu vikinitazama vinaniona kuwa ninaishi muda wote [vyenyewe vinakufakufaga sana] mimi ni wa mwanzo na wa mwisho kwavyo. Wakati mimi naweza fika popote vyenyewe vimebaki mwilini tu. Vivyo hivyo na sisi[analogical to cells] na Mungu wetu ---ANALOGICALLY ndivyo ilivyo
Kutokana na we kuwa muumini wa logic, na kuikataa non sequitor nijibu maswali ya post no 373 nifunge mdomo for good. Can I ever use analogy without commiting a fallacy. Does analogy make sense to you in any way? Je unaruhusu matumizi ya analojia? Nipe mfano wa analojia moja unayoweza kuikubali. Mfano ulio free from non sequ... utapendeza zaidi.
Siongelei kila kitu, naongelea uwepo wa Mungu.
Hivyo vingine, kama naamini vipo, kwa makosa au sawa, hakutusaidii kujua kama Mungu yupo au hayupo.
Naweza kuamini mimi ni Katibu Mkuu wa UN, kwa makosa, lakini, kama Mungu hayupo, makosa yangu hayafanyi Mungu awepo.
Ukifikiri vinginevyo, unafanya logical non sequitur. Unaunganisha mambo mawili ambayo hayana muungano wa moja kwa moja.
Analogy yako na cell ni logical non sequitur. Kwa sababu inawezekana vi cell vyako vikakuona hivyo unavyosema, halafu Mungu asiwepo.
Analogy mbona hata mimi natumia?
Nimeshawahi kusema kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu unaowezekana kuwa na mabaya ni sawa na pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika plane Euclidean geometry.
An impossibility due to inherent conceptual contradiction.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, ulimwengu huu unaoruhusu mabaya usingeweza kuwepo kama Mungu huyo angekuwepo.
Ulimwengu huu na Mungu huyo ni mambo mawili yaliyo mutually exclusive.
Ama ulimwengu huu upo, ama Mungu yupo.
Viwili vyote haviwezi kuwa pamoja
Ulimwengu huu upo.
Hivyo, Mungu huyo hayupo.