God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Unanambia jenga hoja kwani hapa mi nafanya nini?

Mi najenga hoja kukuambia madai yako ya kuhusisha hoja yako na self evident truth ni ya uwongo kwasababu yana logical fallacy

Na siku zote umekuwa ukisema hutaki logic halafu leo hii tena unatumia logic hiyo hiyo kutetea hoja zako...tukuelewaje?
Hakuna sehemu yoyote niliyo tumia logic. Mosi.

Pili, hujajenga hoja bila kunakishi hoja, huwezi kusema mimi ni muongo kwa kusema nikichokiandika kina "Logical Fallacy" hapa unayakiwa uonyeshe hilo. Hili najua huwezi ndiyo maana tangu mchana unaruka ruka tu.
 
Ulivyomuonesha kuwa ule ni uthibitisho amekubaliana na wewe kuwa ni uthibitisho?

Nilivyokuambia ni logical fallacy of appealing to self evident truth hukunielewa?
Nilimuonyesha hilo na ule ni uthibitisho ni juu yake kukubali au kutokubali, kutokuendelea kwake kujadili lile jambo ni ishara ya kuwa nilichokiweka ni ushahidi na ni uhalisia, ndiyo maana hakuweza kupinga kwa vyovyote.

Bila kuonyesha, huo ni mdumange na kukimbia hoja. Hivi ndivyo mlivyo, mwenzako kidogo alijaribu kutoa ufafanuzi baada ya kuwa nambana, sababu tabia yenu huwa mnakimbia hoja. Sasa wewe onyesha ya kuwa kuwepo kwa ulimwengu siyo "Self evident truth".
 
Unauliza swali ambalo nimeshakujibu tayari.

Hakuna mtu aliye vumbua kwamba moja jumlisha moja ni mbili au mbili toa moja ni tatu au machunga mawili machungwa matatu, hili ni jambo la kimaumbile lipo tangu Mola alipoumba mbingu na Ardhi.

Ndiyo maan leo hii hatusemi fulani kavumbua hesabu, kisha tukakomea hapo. Tunasema fulani alivumbua hesabu za Aljebra, mwingine Culculus na mfano wa hayo.

Jbo la kujua kumi, kujua mbili kujua ngai, ni la azalia mitume wote walikuwa wanajua haya mambo.
Umeandika hivi, halafu huoni kwamba kuandika Aristotle alianzisha logic ni contradiction.
 
Hakuna sehemu yoyote niliyo tumia logic. Mosi.

Pili, hujajenga hoja bila kunakishi hoja, huwezi kusema mimi ni muongo kwa kusema nikichokiandika kina "Logical Fallacy" hapa unayakiwa uonyeshe hilo. Hili najua huwezi ndiyo maana tangu mchana unaruka ruka tu.
Ukitumia lugha tu kuandika, umeshatumia logic.

Inaelekea hujui hata logic ni nini.
 
Umeandika hivi, halafu huoni kwamba kuandika Aristotle alianzisha logic ni contradiction.
Ndiyo maana nikasema umechanganya au hukunielewa, hapa tunaongelea suala la hesabu na huko juu tuliongelea suala la logic. Huwezi kulinganisha umbile mama la hesabu na umbile la logic. Kama ulikuwa makini kuna swali la muhimu nilikuwa nakuuliza kati ya lugha na logic kipi kikitangulia ? Jibu lugha bali watu walikuwa wanajenga hoja pasi na kutumia kanuni za logic, na wakapatia kama ilivyo kwa falsafa.

Tukaja kuongelea suala la hesabu yaani kujua idadi ya jambo fulani. Umbile mama la hesabu lipo, hapa hesabu inachukua nafasi ya lugha sasa, kisha mengine yanafata. Huwezi kufananisha hesabu na logic, mfano wa hesabu nafasi yake ni nafasi ya lugha katika logic.

Yaani, huwezi kusema leo hii mtu fulani amevumbua lugha mzee wangu. Lugha ni jambo la kimaumbile ambalo Allah ameliumba kwa waja wake. Sasa unatakiwa usome hoja za mtu kisha uzielewe.
 
Ukitumia lugha tu kuandika, umeshatumia logic.

Inaelekea hujui hata logic ni nini.
Una kichwa kigumu sana. Nakuuliza swali, nakutumia logic gani na logic hapo imesimama kama fani au kama nini ?

Logic mimi sasa nikufundishe wewe.
 
Nikija kwenye ishu ya freewill yenyewe hapa napo kuna mambo mengi ya kuzungumza.

Kama ulivyosema kuwa hujapata majibu ya kuridhisha, naweza nikasema imekuwa inatokea hivyo kwasababu watu waliokuwa wanajaribu kukupa majibu walilenga zaidi kuifanya freewill ionekane ni halisia

Kama freewill ni uhuru wa kuchagua wema na ubaya ipo basi hatupaswi kuingiliwa kimaamuzi ili kuonesha tupo free

Uhuru wa kuchagua haupaswi kuambatana na mipaka, kusema hiki sawa na hiki sio sawa ukifanya nakuadhibu, huo sio uhuru hiyo ni amri.

Sasa Mungu kasema amekup uhuru wa kuchagua kumuabudu yeye au shetani halafu ukichagua kumuabudu shetani Mungu huyu anakupa adhabu kali sana ya kuchomwa moto. Je huo ni uhuru kweli?

Katika jamii ikitokea tu kuna mtu kamwambia mke wake nimekuoa uhuru wa kuchagua kufanya chochote utakacho ila ikitokea umechagua kuniacha nitakumwaga ubongo kwa maumivu makali.

Mtu huyo akisikika na watu, watu watamuita mkatili asiye na ubinadamu, ataitwa mnyama asiye na huruma, ataitwa mzushi kwa kutoa ahadi ya uwongo

Lakini kitu kama hicho hicho akikifanya Mungu anaitwa mwenye upendo wote, mjuzi wa vingi na mwenye rehema

Kwanini?
Tofautisha adhabu na taratibu.

Ukiwa na familia yako kisha ukawaeleza ikifika saa 12 jioni muwe mpo ndani ya nyumba na atayekosekana ataadhibiwa huo ni utaratibu wala si adhabu.

Na hata hiyo free will ina mipaka katika kufanya chochote sababu ya utaratibu wa matokeo mazuri, maana ulimwengu ni muunganiko wa viumbe vyote hai na visivyo hai, vinavyoonekana na visivyoonekana tena kwa kutegemeana kimaisha.
 
Mungu anajua jambo gani litamfika mwanadamu na mwanadamu anajua pia.
We ukiona mtu analewa chakari kila siku,miaka mitano mfululizo,huwezi kutabiri jambo gani litamfika huyo mtu?
Ni kama pale mtu anapoleta uzi,"Anayejua Mama Samia anatupeleka wapi atueleze; mimi naona tunapotea."
Ni swala la reasoning tu,na Mungu ni Bingwa wa Reasoning.
 
Nimeshawahi kusema kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu unaowezekana kuwa na mabaya ni sawa na pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika plane Euclidean geometry.

An impossibility due to inherent conceptual contradiction.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, ulimwengu huu unaoruhusu mabaya usingeweza kuwepo kama Mungu huyo angekuwepo.
Kuna mifano ya baba na mtoto nimeitumia sana kwa Scars hadi anamaindi na siachi.

Kiuelewa sisi akili zetu zina mwisho halafu Mungu hana kikomo cha ufikiri. Sisi ni wana yeye ndo Baba lao. Kuna vitu huvielewi sasa ila ukikua kiroho utazidi kuvielewa.

Watoto wa familia moja [famili A-Godly love]wanaweza kuargue kwamba ni kwa nini sisi tupigwe viboko kama kweli baba yetu ana upendo wote, na kwa nini tusinunuliwe pipi na kila wanachokitaka kila siku kama kweli baba anao uwezo mkubwa [kama ambavyo familia ya jirani wao kila siku pipi na chokoleti na hawapigwi, in fact wanakingiwa kifua na baba yao hata kwa mambo waliyostahili yawafunze (helicopter parent) B-Satanic love]. Wasiopigwa wanaona wanafaidi [kutokana na utoto wao kifikra] japo kwa baadae kila mtu atasema baba A alilea wanae vizuri na Baba B aliwaharibu. Nakuhakikishia kisaikolojia hata kama baadae watoto wote wakafikia kiwango sawa cha uhuru na maendeleo; kwa ujumla watoto wa A watafaidi zaidi kuliko watoto wa B.

Euclidian geometry inazo limit zake, tofauti na a living God asiye na ukomo wake. Tukubali tu kuwa sisi ni wadogo na tutaendelea kuuelewa mpango wake kadri tunavyokua.
 
Imani ingekuwa njia ya ya kweli ya kujua jambo kwa hakika basi leo tungekuwa na imani moja na dini moja

Au kila imani kuhusu chochote ingekuwa kweli

Since tuna imani nyingi tena zinazopingana hiyo inaonesha tu jinsi gani imani sio njia ya kuaminika katika kufikia ukweli.

Na pia zipo record za kihistoria za watu walioamini mambo ya uwongo (na mifano ipo) wakidhani ni kweli lakini imani hiyo haikubadilisha chochote kufanya imani yao juu ya jambo hilo liwe hivyo hivyo kihalisia kama walivyo amini.
Historia pia inaonesha imani zilizokuwa ni kweli all along. Nyingine zinaweza zisiwe kweli kamilifu lakini ile kiujumla ni za kweli au zikawa zina ukweli mwingi tu.

Kazi ni kwetu kuzichunguza na kujichunguza kadri tunavyoendelea kuishi nazo.

Ndio maana mi huwa nasema tuanze na kuamini kuwa Mungu yupo, halafu ndio tubaki tunabishana kuwa yupojepoje. In fact sitegemei mijadala ya yupojepoje kuisha leo au kesho! Hii ni kazi tutakayoendelea nayo mpaka mbele sana katika safari yetu ya milele!!
 
Ndiyo maana nikasema umechanganya au hukunielewa, hapa tunaongelea suala la hesabu na huko juu tuliongelea suala la logic. Huwezi kulinganisha umbile mama la hesabu na umbile la logic. Kama ulikuwa makini kuna swali la muhimu nilikuwa nakuuliza kati ya lugha na logic kipi kikitangulia ? Jibu lugha bali watu walikuwa wanajenga hoja pasi na kutumia kanuni za logic, na wakapatia kama ilivyo kwa falsafa.

Tukaja kuongelea suala la hesabu yaani kujua idadi ya jambo fulani. Umbile mama la hesabu lipo, hapa hesabu inachukua nafasi ya lugha sasa, kisha mengine yanafata. Huwezi kufananisha hesabu na logic, mfano wa hesabu nafasi yake ni nafasi ya lugha katika logic.

Yaani, huwezi kusema leo hii mtu fulani amevumbua lugha mzee wangu. Lugha ni jambo la kimaumbile ambalo Allah ameliumba kwa waja wake. Sasa unatakiwa usome hoja za mtu kisha uzielewe.
Wewe ngumbaru hujui kwamba huwezi kuwa na hesabu bila logic.

Hujui kamba addition ina apply logic ya AND.

Hujui hata logic ni nini.
 
Una kichwa kigumu sana. Nakuuliza swali, nakutumia logic gani na logic hapo imesimama kama fani au kama nini ?

Logic mimi sasa nikufundishe wewe.
Nimekujibu logic as a concept.

Kwamba ukijua tofauti ya chungwa moja na mawili, umeweza kutumia concept ya logic kujua kwamba machunga mawili ni chungwa moja AND chungwa moja lingine.

Hiyo AND ni logic.

Sasa unataka kusema watu hawakutumia logic ya AND kabla ya Aristotle?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Huu ni ujinga wa kawaida tu au unafanya extra effort kuwa mjinga hivi?
 
Wewe ngumbaru hujui kwamba huwezi kuwa na hesabu bila logic.

Hujui kamba addition ina apply logic ya AND.

Hujui hata logic ni nini.
Nacheka sana. Tulia kijana usirauke haya mambo yana yenyewe.

Nilikuonyesha huko mwanzo huwezi kuongelea logic nje ya fani ikaleta maana, na ukashindwa kupinga hilo.

Kujumlisha inatumia logic gani ? Hutakiwi kusema tu au kuandika tu bila kunyesha hilo. Kujumlisha na kutoa ni jambo ambalo lipo tangu na tangu, na ndiyo msingi, ndiyo maana kila hesabu zinakuja kuwekwa au kuanzishwa na waja huwa zinamili katika namna ya kujumlisha, kutoa, kugawanya na kuzidisha.

Akili umepewa bure fikiria kiundani.

Logic nakufundisha mimi, sababu wewe unaonekana umeikariri, mimi nimeisoma nikaielewa.
 
Nimekujibu logic as a concept.
Nilikwambia nini baada ya wewe kujibu hivyo ? Na ukaonyesha nini kwenye ile maana uliyo itoa ? Nakusaidia sababu kichwa changu kina tunza kumbumbu vizuri, hilo wazo ulilo litoa mwisho likaangukia kwenye fani.

Lakini, kadhalika hukielezea kiundani logic kama wazo, sababu mimi nafahamu logc, na ile link uliyo nipa nikakwambia nitakuja tujadili ishu ya "Concepts" na "definitions" humu nako kuna makosa mengi sana yaliyo fanywa na Wanafalsafa na Watu wa Mantiki.
Kwamba ukijua tofauti ya chungwa moja na mawili, umeweza kutumia concept ya logic kujua kwamba machunga mawili ni chungwa moja AND chungwa moja lingine.
Hii siyo kweli, sababu hivi vitu vipo tangu logic kama wazo halijaundwa. Kijana huelewi wapi ? Ndiyo maana nikasema hivi huwezi kuongelea logic nje ya fani, sababu tamko "AND" halina maana tu ya kumjulisha au ziada.
Hiyo AND ni logic.
Hii imetokea katika kiasili, na nilikwambia huko kwanzo logic inatumia sehemu ndogo sana ya lugha kung'amua mambo yake ndiyo maana hata Aristoto alipoanza kuweka misingi alianza kujishughulisha na lugha hasa kwenye Kiima (Subject) na kiarifu (Predicate). Sasa ukirudi katika tamko "AND" haliishii kwenye maana ya logic kama fani sasa. Kwahiyo walipo weka sheria za fani ya logic wakaamua kutumia baadhi ya maneno na viunganishi kuwakilisha jambo fulani.
Sasa unataka kusema watu hawakutumia logic ya AND kabla ya Aristotle?
Sasa hii ni lugha ndiyo maana tunasema haya mambo yapo kabla ya logic kuwepo, na wala watu hawakuhitaji mambo hayo. Nilikuonyesha huko nyuma huwezi kuongelea tamko logic nje ya fani, ndiyo maana mpaka muda huu unaduru katika fani, tamko "AND" limechukuliwa kwenye lugha na kupewa sifa moja tu ila kwenye asili tamko "AND" lina sifa zaidi ya moja. Kuna "AND" ya pamoja, kuna "AND" ya jumla na "AND" nyingine. Sasa ili ujue ya kuwa logic ni fani imetanguliwa na lugha na sarufi zake na hesabu zilikuwepo kwanini haijabeba maana zote za "AND" ?
Unajua kusoma kwa ufahamu?
Hili nikuulize wewe sababu, nachokiandika na unacho nijibu au kunikuu ni vitu viwili tofauti.

Tena niko makini sana katika kusoma na kuelewa.
Huu ni ujinga wa kawaida tu au unafanya extra effort kuwa mjinga hivi?
Ndiyo uonyeshe ujinga wangu uko wapi. Jifunze kunakishi hoja na kuzivunja vunja hoja za aliye dhidi yako, hili naona hamliwezi kabisa, najua sababu mnafikiri kitoto sana.
 
Nilikwambia nini baada ya wewe kujibu hivyo ? Na ukaonyesha nini kwenye ile maana uliyo itoa ? Nakusaidia sababu kichwa changu kina tunza kumbumbu vizuri, hilo wazo ulilo litoa mwisho likaangukia kwenye fani.

Lakini, kadhalika hukielezea kiundani logic kama wazo, sababu mimi nafahamu logc, na ile link uliyo nipa nikakwambia nitakuja tujadili ishu ya "Concepts" na "definitions" humu nako kuna makosa mengi sana yaliyo fanywa na Wanafalsafa na Watu wa Mantiki.

Hii siyo kweli, sababu hivi vitu vipo tangu logic kama wazo halijaundwa. Kijana huelewi wapi ? Ndiyo maana nikasema hivi huwezi kuongelea logic nje ya fani, sababu tamko "AND" halina maana tu ya kumjulisha au ziada.

Hii imetokea katika kiasili, na nilikwambia huko kwanzo logic inatumia sehemu ndogo sana ya lugha kung'amua mambo yake ndiyo maana hata Aristoto alipoanza kuweka misingi alianza kujishughulisha na lugha hasa kwenye Kiima (Subject) na kiarifu (Predicate). Sasa ukirudi katika tamko "AND" haliishii kwenye maana ya logic kama fani sasa. Kwahiyo walipo weka sheria za fani ya logic wakaamua kutumia baadhi ya maneno na viunganishi kuwakilisha jambo fulani.

Sasa hii ni lugha ndiyo maana tunasema haya mambo yapo kabla ya logic kuwepo, na wala watu hawakuhitaji mambo hayo. Nilikuonyesha huko nyuma huwezi kuongelea tamko logic nje ya fani, ndiyo maana mpaka muda huu unaduru katika fani, tamko "AND" limechukuliwa kwenye lugha na kupewa sifa moja tu ila kwenye asili tamko "AND" lina sifa zaidi ya moja. Kuna "AND" ya pamoja, kuna "AND" ya jumla na "AND" nyingine. Sasa ili ujue ya kuwa logic ni fani imetanguliwa na lugha na sarufi zake na hesabu zilikuwepo kwanini haijabeba maana zote za "AND" ?

Hili nikuulize wewe sababu, nachokiandika na unacho nijibu au kunikuu ni vitu viwili tofauti.

Tena niko makini sana katika kusoma na kuelewa.

Ndiyo uonyeshe ujinga wangu uko wapi. Jifunze kunakishi hoja na kuzivunja vunja hoja za aliye dhidi yako, hili naona hamliwezi kabisa, najua sababu mnafikiri kitoto sana.

Wewe hata unaelewa kwamba AND ni zaidi ya lugha?
Unaelewa kwamba AND ya lugha ina represent concept?

Unaipomda logic.

Naomba ujibu hii post bila kutumia logic kabisaaa tuone.
 
Kisai naona umekutana na wabishi wenzio 🤣
Watu mnamoyo wa kubishana jamani.. Scars Kiranga Uhakika Bro hadi saa 11 alafajiri mnaporomosha magazeti asee. Hii mada haitakua na mshindi asee..
Kakosekana tu @lovelifelivelife safuher na FaizaFoxy

Btw nawasubiri mmalize kubishana niwaletee Muendelezo wa topic hii ambao utaServe as a Counterpart-Sequel
 
Hao wote wawili (Kisai na Kiranga) wapo kiubishi zaidi, siyo kutafuta ilm.

Ukiwauliza swali hawajibu hata kidogo, ni majuha wasio na kazi za maana za kufanya. Kuna wakati huhisi kuwa ni mtu mmoja tu, anaandika na kujijibu mwenyewe.
 
Lile swali langu nililo kuuliza bado hujalijibu.

Nilikwambia mpaka unaingia kaburini hutaweza, huu mwaka wa tatu unaenda.

Kubishana nilikuwa nabishana zamani nilipokuwa sijui wapi pakuchukua elimu. Ila baada ya kujua namshukuru Mola wangu mlezi, nakitoa kile kidogo alichoniruzuku katika elimi. Sibishani na mtu ila watu wanafanya hivyo.

Kama kutakuwa na maana nyingine ya tamko hili, lihudhurishe tu.
 
Hakuna sehemu yoyote niliyo tumia logic. Mosi.

Pili, hujajenga hoja bila kunakishi hoja, huwezi kusema mimi ni muongo kwa kusema nikichokiandika kina "Logical Fallacy" hapa unayakiwa uonyeshe hilo. Hili najua huwezi ndiyo maana tangu mchana unaruka ruka tu.
KNimebaini kumbe swala lako la kupinga logic linasababishwa na wewe kutokujua logic ni nini

Nimekujibu hiyo ni logical fallacy ya appeal to self evident truth, kulingana na wewe ulivyoweka madai kuwa jambo fulani linapaswa kukubaliwa bila uthibitisho kwasababu i self evident truth. Na sio mara ya kwanza nakuambia

Hiyo ni reason ya kishamba, kinachoonekana kwako ni self evident truth sio necessary kuwa kionekane ni self evident kwa mtu mwingine na ndio hapo unapo hitajika ku reason zaidi.

Usichanganye mawazo yako au mtazamo wako binafsi na interpretation ya self evident truth
 
Kisai naona umekutana na wabishi wenzio 🤣
Watu mnamoyo wa kubishana jamani.. Scars Kiranga Uhakika Bro hadi saa 11 alafajiri mnaporomosha magazeti asee. Hii mada haitakua na mshindi asee..
Kakosekana tu @lovelifelivelife safuher na FaizaFoxy

Btw nawasubiri mmalize kubishana niwaletee Muendelezo wa topic hii ambao utaServe as a Counterpart-Sequel
Tunapeana faida watu tumetofautiana ufahamu na maarifa.
 
Back
Top Bottom