God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Kwa hiyo Mungu aliumba ulimwengu unao ruhusu mabaya ili kukwepa lawama kuwa hata angeumba ulimwengu usio ruhusu mabaya aliogopa tunge hoji?

Sasa mbona lawama ziko pale pale?

Mungu muweza wa yote alikosa namna ya kuumba ulimwengu katika namna isiyopingana na sifa zake na kuzuia mianya ya maswali kama haya?
 
Unavyotaka kunieleza uhalisia wako si namimi lazima ni hoji ili nijue napewa majibu ya kweli

Na ndio maana nimehoji Unajuaje hicho unachokisema kipo katika dunia yako sio imaginations?
 
Mara ngapi nimesema kuwa hakuna anayemuadhibu mtu, ni kwamba mwishoni mtu anapokea sambamba na kile alichoona yeye mwenyewe kuwa ni chema na ndio uhalisia wake?
Kwa maana hiyo hakuna moto kwa waliofanya maovu?
 
Simply ni kwamba kuna tofauti ya vitendo vya hiari na visivyo vya hiari

Vitendo vya hiari vinaegemezwa kwa mja "free will"

Vitendo visivyokuwa vya hiari vinaegemezwa kwa Mungu

Hukumu yake:

* Vitendo vya hiari vya mja vitahukumiwa

* Vitendo visivyo vya hiari havihukumiwi, amejiegemezea Mungu mwenyewe

#Vinafahamika pia kama vitendo vya kutaka vs Vitendo vya kutokutaka

Nimedokeza hivyo kidogo kwa sababu nimeona kuna kundi moja humu kati ya mawili halitofautishi baina ya hivyo viwili kiasi cha kuuliza maswali yaliyo nje ya matakwa ya mwanadamu wakiamini wanapinga kwa hoja kumbe ni kutokufahamu tu, kwa mfano wanauliza:

1. Kwa nini sikuchagua kuzaliwa mzungu au mwarabu? [emoji3]

2. Kwa nini nimezaliwa mfupi? [emoji3]

3. Kwa nini nimezaliwa Afrika? [emoji3]

4. Kwa nini nikila chakula kinameng'enywa? [emoji3]

5. Kwa nini mimi ni kiazi? [emoji3]

Ni nani atakayehukumiwa kwa sababu alizaliwa mfupi?

C'mon!
 
Kwanini umesema uongo ? Wewe na mwenzako kwa kujua logic hakuna anaenifikia, nimeikosoa zaidi ya moja humu ndani.

Nikatoa maana zaidi ya moja kuhusu logic, hamkuweza kuzigusa maana hizo, sababu uwezo wa kukosoa nilichokiandika hamna na hamna kweli.
Wewe hata logic huelewi ni nini

Unapinga pinga tu kila kitu kwasababu tu una bando la kubishia

Ume present hoja yako hapo ambayo ni self evident truth, hiyo ni logic argument sasa ulivyo mweupe hujui hata ulicho kiandika halafu unataka kubishana kujaza server tu
 
Nimecheka sana. Umethibitisha ya kuwa self evident truth huijui kwa maandishi yako mwenyewe, mwisho wa siku maswali mnayakimbia.

Kingine ulitakiwa ukosoe nilichokiandika kuhusu logic, lakini hili huwezi na najua huwezi.

Yaani logic nikufundishe mimi, yaani nimekuja kuona wewe umekariri msamiati ndiyo maana unachokiandika umashindwa kukitetea na kukijengea hoja.
 
Huyo anejiita Kisai mpaka anajibishia yeye mwenyewe.
 
Jifunze kijana.

Wewe unaibishia mpaka Qur'an. Unaona kuna binadam mwenye kuelewa zaidi ya Allah. Unasikitisha sana.
Swali la pili nililo kuuliza ni kutokana na ulichonishutumu kwamba kuna vitu nabishia humu ndani hasa katika mada hii, vimewekwa wazi ndani ya Qur'aan, hujaniambia ni vitu gani hivyo ? Hili kadhalika unatakiwa ulijibu.

Yaani wapi nimeibishia Qur'aan ? Lile swali hujibu mpaka una kufa halafu ni swali rahisi sana.
 
Uliza nini unataka kuelewa kutoka ndani ya Qur'an, usisite na kuanza kubadilisha maneno na kujibishia mwenyewe.
 
Hapana sio Yeye kukwepa kitu.

Bali hoja ni kwamba chochote kile ambacho kingekuwepo katika mchakato wa maisha mtu mwenye kulaumu anaweza kukitumia kulaumu kuwa kwa nini kimeletwa kiovu, kwa nini ataabike wakati Mungu wake yupo.

Ukiweza kuuona muda/time kwa undani zaidi ndio utagundua kuwa bila muda hakuna uwepo kwa vitu material. Na muda si lolote bali ni muendelezo wa matukio ndani ya maisha. Kitu kikiweza kukaa katika mazingira ambapo hakuna mabadiliko kati ya hatua/state A kwenda B tunasema hakiwezi kuuexperience Muda. Mabadiliko yana maana tunapotoka hali ya chini kwenda ya juu, tukakua kuelekea hali nzuri zaidi bora zaidi. I trust the process. And I love life, living. And I am willing to keep on doing that forever.
 
... atapata tabu hadi agundue ngazi

[emoji23]

[emoji119]
Yaas labda Mungu kwa kutupenda wote kiujmla akawaweka wafupi ili watusaidiage kugundua ngazi

Mwanangu naomba ukipata muda uicheki blogu/link niliyoweka halafu unipe feedback/challenge. Nahitaji challenge za wanabaiolojia ili kujicheck and balance.
 
Yaas labda Mungu kwa kutupenda wote kiujmla akawaweka wafupi ili watusaidiage kugundua ngazi

Mwanangu naomba ukipata muda uicheki blogu/link niliyoweka halafu unipe feedback/challenge. Nahitaji challenge za wanabaiolojia ili kujicheck and balance.
Labda ... kwenye kila jambo kuna hekima na kusudi nyuma yake

Poa, nitapitia
 
Nikiangalia mpambano kati ya bwana Kisai na madam FaizaFoxy naona kabisa umuhimu wa kukubaliana na vya msingi tu generally na kuziacha zile specifics kila mtu ajiumbie dunia yake aah!

Inafika muda mmoja anahisi mwenzake ni mbishi kiasi cha uwezekano wa kiwa Kisai na Kiranga ni ID mbili za mtu mmoja! Hiyo ni next level, level 9999%

Hata hivyo angalizo madamu kadiri ya unavyomuona mwenzako ni mbishi huyo unayebishana naye, tambua wazi kwamba na wewe ni mbishi kwa kiwango kilekile ulichompimia. Na akiamua kukurudishia wewe basi wewe utakuwa ni mbishi wa kiwango hicho kilichozidishwa zaidi, kusukwasukwa na hata kumwagikaa....😏.

Nashauri watu wa dini tuanze kukubaliana na statement kama vile 'Mungu hana upendeleo' 'Mungu anatupenda' etc. halafu kila neno lipimwe kwa hiyo fact na kukubaliwa regardless the source, au kukataliwa regardless the source. Hata hivyo dunia tofauti hazitaepukika maana kila mmoja atakuja na tafsiri yake ya upendeleo na upendo na kuyavuruga matokeo.
 
Hapa ndipo huwa nasema kila mtu au mwanadamu alie zaliwa na mwanamke, akili yake inaukomo. Hata kama uelewa wako ni wa juu kiasi gani. Ndio utatambua kuwa wewe ni binadamu tu.

Nakupa mfano mdogo Yohana mbatizaji alikua anajua kila kitu kuhusu Yesu, lakini siku ilipo fika mambo yamemwiya vibaya, alitatizika na akawatuma wanafunzi wake
Waende wakamuulize Yesu. Kama wewe ndie yule au tumtazamie mwingine?

Ni swali anamuuliza Yesu kupitia wanafunzi wake.

Kumbuka huyuhuyu aliwahi kushuhudia miaka miwili na zaidi kabla ya hapo akisema :Mathayo 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹ Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
¹² Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.Mathayo 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?
¹⁵ Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.

Kwaio hapo utaona namna ambavyo binadamu kuna wakati tunafikia pamoja na uelewa wetu mkubwa bado tu dhaifu.

Kwanini nimesema ni kwasababu nimeona unauelewa wajuu sana kuhusu Mungu lakini unajitahidi tena kutaka kupotea
 
Nimekuelewa, kuna ubishi na kuna kukosoa.

Ninachokifanya mimi ni kukosoa chanya" (positive criticism" iliwatu watumie bongo zao kufikiri na kukosoana kwa kuleta hoja zenye manufaa kwa wanaosoma. Maswali yangi yote yamelenga mawili tu, au kufunidisha au kujifunza. Nisome vizuri utalielewa hilo.

Nafahamu sana kuwa Kisai na Kiranga ni watu tpofauti na wenye uelewa tofauti lakini jinsi wanavyobishana wanajiweka "level" moja, ya ubishi hasi tu, wa "nani zaidi".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…