God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Kama kawaida, nadhani umeendelea kushikilia kwa kiburi kwamba 'unafahamu kila kitu na haya mambo ya kupeana mafundisho na muda hayana maana'

Nahisi kama kungekuwa hakunanuovu wowote wa kuuana wala nini mngetaka watu wawe wanatokea watu wazima tu, kwa nini wajihangaishe kukua? [kukua ingesomeka ni uovu]

Baadaye mngetaka watu wasipate njaa, kwa nini wajihangaishe kukula? [njaa ingekuwa uovu wenu mpya]

Baadaye mngetaka watu wasiongee wawe tu walishaelewana bila kujihangaisha kuzungumza, watokee tu bila kuhitaji elimu yoyote

Na mngemchallenge Mungu afanye vivyo hivyo maana yeye si amejinasibu ni muweza yote. Basi awafanyie yote sasa.

Kimsingi you are against life as we experience it and know it you want a static existance kitu ambacho hata Mungu aliona si vema akatuumba sisi kazi ziendelee.

Kama kweli unaona dunia hiyo isiyo na shida yoyote ya kuiishi wala njia yoyote ya kuipita basi ndiyo utapokea sambamba na matakwa yako. Wacha tuliopenda kuwa watoto wa kukua na kujifunza kuhusu sisi na kuhusu Mungu zaidi, wasafiri wa kupita njiani na kuishi kwa kupambana na changamoto ndogondogo tuendelee kufanya hivyo milele.
Kwa hiyo Mungu aliumba ulimwengu unao ruhusu mabaya ili kukwepa lawama kuwa hata angeumba ulimwengu usio ruhusu mabaya aliogopa tunge hoji?

Sasa mbona lawama ziko pale pale?

Mungu muweza wa yote alikosa namna ya kuumba ulimwengu katika namna isiyopingana na sifa zake na kuzuia mianya ya maswali kama haya?
 
Maswali yote nayajibu ila hayamake sense kabisa kwako, huyaoni in plane sight.

Sasa unadhani tutaishije kama mimi ninakueleza uhalisia wangu unaukataa, na wewe unanieleza uhalisia wako ninaukataa. Dunia haiwezi kubaki moja basi bora tuivunje tu tugawane dunia.

Kila mtu abaki na yake na kama kuna atakayependa anaweza kuhamia ya mwenzake au tkabaki kutembeleana kwa nadra, ikishindikana ndio tunapigiana simu kama tunavyofanya hivi sasa [tunachati kutokea kwenye dunia zetu]
Unavyotaka kunieleza uhalisia wako si namimi lazima ni hoji ili nijue napewa majibu ya kweli

Na ndio maana nimehoji Unajuaje hicho unachokisema kipo katika dunia yako sio imaginations?
 
Mara ngapi nimesema kuwa hakuna anayemuadhibu mtu, ni kwamba mwishoni mtu anapokea sambamba na kile alichoona yeye mwenyewe kuwa ni chema na ndio uhalisia wake?
Kwa maana hiyo hakuna moto kwa waliofanya maovu?
 
Dhambi inakuja pale atakapofanya kitu ambacho ni kosa huku akitambua hilo.

Tofauti na hivyo yanaweza kuwa ni makosa tu hayajafikia kuwa dhambi

Makosa yote mtu anapaswa kuyafanyia kazi na kurekebisha kadri ya anavyoweza.

Mfano aache kufuatilia ugomvi na matusi etc...........hatuiti dhambi hata kama ni kosa maana freewill haijahusika kenye hilo tukio moja kwa moja. Arekebishe vingine mwenye control navyo
Simply ni kwamba kuna tofauti ya vitendo vya hiari na visivyo vya hiari

Vitendo vya hiari vinaegemezwa kwa mja "free will"

Vitendo visivyokuwa vya hiari vinaegemezwa kwa Mungu

Hukumu yake:

* Vitendo vya hiari vya mja vitahukumiwa

* Vitendo visivyo vya hiari havihukumiwi, amejiegemezea Mungu mwenyewe

#Vinafahamika pia kama vitendo vya kutaka vs Vitendo vya kutokutaka

Nimedokeza hivyo kidogo kwa sababu nimeona kuna kundi moja humu kati ya mawili halitofautishi baina ya hivyo viwili kiasi cha kuuliza maswali yaliyo nje ya matakwa ya mwanadamu wakiamini wanapinga kwa hoja kumbe ni kutokufahamu tu, kwa mfano wanauliza:

1. Kwa nini sikuchagua kuzaliwa mzungu au mwarabu? [emoji3]

2. Kwa nini nimezaliwa mfupi? [emoji3]

3. Kwa nini nimezaliwa Afrika? [emoji3]

4. Kwa nini nikila chakula kinameng'enywa? [emoji3]

5. Kwa nini mimi ni kiazi? [emoji3]

Ni nani atakayehukumiwa kwa sababu alizaliwa mfupi?

C'mon!
 
Kwanini umesema uongo ? Wewe na mwenzako kwa kujua logic hakuna anaenifikia, nimeikosoa zaidi ya moja humu ndani.

Nikatoa maana zaidi ya moja kuhusu logic, hamkuweza kuzigusa maana hizo, sababu uwezo wa kukosoa nilichokiandika hamna na hamna kweli.
Wewe hata logic huelewi ni nini

Unapinga pinga tu kila kitu kwasababu tu una bando la kubishia

Ume present hoja yako hapo ambayo ni self evident truth, hiyo ni logic argument sasa ulivyo mweupe hujui hata ulicho kiandika halafu unataka kubishana kujaza server tu
 
Wewe hata logic huelewi ni nini

Unapinga pinga tu kila kitu kwasababu tu una bando la kubishia

Ume present hoja yako hapo ambayo ni self evident truth, hiyo ni logic argument sasa ulivyo mweupe hujui hata ulicho kiandika halafu unataka kubishana kujaza server tu
Nimecheka sana. Umethibitisha ya kuwa self evident truth huijui kwa maandishi yako mwenyewe, mwisho wa siku maswali mnayakimbia.

Kingine ulitakiwa ukosoe nilichokiandika kuhusu logic, lakini hili huwezi na najua huwezi.

Yaani logic nikufundishe mimi, yaani nimekuja kuona wewe umekariri msamiati ndiyo maana unachokiandika umashindwa kukitetea na kukijengea hoja.
 
Wewe hata logic huelewi ni nini

Unapinga pinga tu kila kitu kwasababu tu una bando la kubishia

Ume present hoja yako hapo ambayo ni self evident truth, hiyo ni logic argument sasa ulivyo mweupe hujui hata ulicho kiandika halafu unataka kubishana kujaza server tu
Huyo anejiita Kisai mpaka anajibishia yeye mwenyewe.
 
Jifunze kijana.

Wewe unaibishia mpaka Qur'an. Unaona kuna binadam mwenye kuelewa zaidi ya Allah. Unasikitisha sana.
Swali la pili nililo kuuliza ni kutokana na ulichonishutumu kwamba kuna vitu nabishia humu ndani hasa katika mada hii, vimewekwa wazi ndani ya Qur'aan, hujaniambia ni vitu gani hivyo ? Hili kadhalika unatakiwa ulijibu.

Yaani wapi nimeibishia Qur'aan ? Lile swali hujibu mpaka una kufa halafu ni swali rahisi sana.
 
Swali la pili nililo kuuliza ni kutokana na ulichonishutumu kwamba kuna vitu nabishia humu ndani hasa katika mada hii, vimewekwa wazi ndani ya Qur'aan, hujaniambia ni vitu gani hivyo ? Hili kadhalika unatakiwa ulijibu.

Yaani wapi nimeibishia Qur'aan ? Lile swali hujibu mpaka una kufa halafu ni swali rahisi sana.
Uliza nini unataka kuelewa kutoka ndani ya Qur'an, usisite na kuanza kubadilisha maneno na kujibishia mwenyewe.
 
Kwa hiyo Mungu aliumba ulimwengu unao ruhusu mabaya ili kukwepa lawama kuwa hata angeumba ulimwengu usio ruhusu mabaya aliogopa tunge hoji?

Sasa mbona lawama ziko pale pale?

Mungu muweza wa yote alikosa namna ya kuumba ulimwengu katika namna isiyopingana na sifa zake na kuzuia mianya ya maswali kama haya?
Hapana sio Yeye kukwepa kitu.

Bali hoja ni kwamba chochote kile ambacho kingekuwepo katika mchakato wa maisha mtu mwenye kulaumu anaweza kukitumia kulaumu kuwa kwa nini kimeletwa kiovu, kwa nini ataabike wakati Mungu wake yupo.

Ukiweza kuuona muda/time kwa undani zaidi ndio utagundua kuwa bila muda hakuna uwepo kwa vitu material. Na muda si lolote bali ni muendelezo wa matukio ndani ya maisha. Kitu kikiweza kukaa katika mazingira ambapo hakuna mabadiliko kati ya hatua/state A kwenda B tunasema hakiwezi kuuexperience Muda. Mabadiliko yana maana tunapotoka hali ya chini kwenda ya juu, tukakua kuelekea hali nzuri zaidi bora zaidi. I trust the process. And I love life, living. And I am willing to keep on doing that forever.
 
... atapata tabu hadi agundue ngazi

[emoji23]

[emoji119]
Yaas labda Mungu kwa kutupenda wote kiujmla akawaweka wafupi ili watusaidiage kugundua ngazi

Mwanangu naomba ukipata muda uicheki blogu/link niliyoweka halafu unipe feedback/challenge. Nahitaji challenge za wanabaiolojia ili kujicheck and balance.
 
Yaas labda Mungu kwa kutupenda wote kiujmla akawaweka wafupi ili watusaidiage kugundua ngazi

Mwanangu naomba ukipata muda uicheki blogu/link niliyoweka halafu unipe feedback/challenge. Nahitaji challenge za wanabaiolojia ili kujicheck and balance.
Labda ... kwenye kila jambo kuna hekima na kusudi nyuma yake

Poa, nitapitia
 
Nikiangalia mpambano kati ya bwana Kisai na madam FaizaFoxy naona kabisa umuhimu wa kukubaliana na vya msingi tu generally na kuziacha zile specifics kila mtu ajiumbie dunia yake aah!

Inafika muda mmoja anahisi mwenzake ni mbishi kiasi cha uwezekano wa kiwa Kisai na Kiranga ni ID mbili za mtu mmoja! Hiyo ni next level, level 9999%

Hata hivyo angalizo madamu kadiri ya unavyomuona mwenzako ni mbishi huyo unayebishana naye, tambua wazi kwamba na wewe ni mbishi kwa kiwango kilekile ulichompimia. Na akiamua kukurudishia wewe basi wewe utakuwa ni mbishi wa kiwango hicho kilichozidishwa zaidi, kusukwasukwa na hata kumwagikaa....😏.

Nashauri watu wa dini tuanze kukubaliana na statement kama vile 'Mungu hana upendeleo' 'Mungu anatupenda' etc. halafu kila neno lipimwe kwa hiyo fact na kukubaliwa regardless the source, au kukataliwa regardless the source. Hata hivyo dunia tofauti hazitaepukika maana kila mmoja atakuja na tafsiri yake ya upendeleo na upendo na kuyavuruga matokeo.
 
Hello y’all..

NB
: Naomba moderator mada hii msiihamishie jukwaa la dini maana huko itakosa wachangiaji na lengo langu la kutaka kujuzwa jambo hili halitatimia and that will leave me frustrated and bums me out, Natuamaini mtatii takwa langu hili. Ahsanteni.

Binafsi kiimani ni muumini wa kanisa Katoliki kwa kuzaliwa na kubatizwa, pia ninaamini na kuisadiki kanuni ya imani yangu katoliki isemayo “Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi muumba mbingu na dunia na kwa Yesu Kristu Bwana wetuu….” Self-schemas: katika sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.

Self-Concept ni i hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future self (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo). Toka nilipoanza kutambua Self Concept yangu Nimekua na swali ambalo kwakweli pamoja na kuisadiki imani yangu hii na kupokea ya Sakrament takatifu ya Communion swali hilo limekua mwiba mchungu na kikwazo kikubwa katika imani yangu hii na Mungu kwa ujumla.

Toka nilipoanza kujitambua nimejaribu kuwashirikisha watu wenye uelewa jambo hili ila bado sijapewa majibu thabiti….natumaini hapa JF nitapewa maelekezo vyema , mnivumilie kama maelezo yatakua marefu maana hua siwezi kuelezea kwa ufupi but it worth your time.

The One above all, In-Betweener and The One bellow all.

Monotheism
ni imani ya kua kuna Mungu mmoja pekee ambae aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo. Watu wanao amini katika imani hii ni wafuasi wa dini zilizotokana na Ibrahim ambae anachukuliwa kama baba wa imani ambazo ni Judaism, Ukristo,uislam, mandaeism ,Rastafarian na Bahai. Mungu wa imani hii ndio huyu tunayemfahamu mimi na wewe ambae ana sifa kuu tatu ambazo ni yupo kila mahali, anajua kila kitu, na anaweza kila kitu. Omni ni neno la kilatini lenye maana ya yote au kila kitu na Sciens ni neno la kilatini likimaanisha kujua(conscious)……. Moja kati ya sifa kuu tatu za Mungu nilizotaja hapo juu ni Omniscience ikimaanisha kwamba Mungu anajua yote yaliyopita,yaliyopo na yajayo.

The Great Chain of Being ni mchoro au nadharia ambayo inaonyesha kwamba maisha ya mwanadamu yapo kwenye ngazi /mtiririko Fulani ambapo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,mimea halafu chini kabisa yupo shetani. Mungu ni the one above all, mwanadamu ni aliyekati /in-betweener na shetani ni the one below all. Unajua mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote walioumbwa na mungu kuzidi hata malaika ndio maana kuna malaika wanafanya kazi kwa wanadamu ya kutulind, Moja kati ya utajiri na kitu kikubwa alichonacho mwanadamu hakuna kiumbe kingine anacho ni uwezo wa kuchagua na kuamua Kuishi vile atakavyo yeye yaani Free Will….Katika Great chain of being mwanadamu amewekwa katikati (In-Betweener) maana yeye ameumbwa na roho isiyokufa (immortal) na mwili ambao unaokufa (mortal) hivyo inamuwezesha yeye kuishi duniani au mbinguni . Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi Uungu kwa kutenda mema maishani mwake au ushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Kwakua mwanadamu ana free will uamuzi ni wake ni kuchagua kwenda kwa The One above all au kwa the one bellow all.

Free Will is illusion (?)

Kuna mada Fulani niliwahi kusema kwamba tukio la kuumbwa Adam na eva hadi kufukuzwa eden linapinga uwepo wa Mungu kwa kupinga sifa tatu alizonazo Mungu kwamba anaweza yote,anajua kila kitu na yupo kila mahali… ndio maana mimi hua nalichukulia kama lugha ya picha tu na sio tukio halisi na kama kweli ni kweli lilitokea kama lilivyoelezewa kwenye kitabu cha mwanzo basi linaonyesha Mungu hafai kupokea sifa tunazompa. Kama anajua kila kitu je wakati anamuumba adamu bila Eva hakujua kwamba adamu hatapata uhitaji wa kua na mwenza? Yupo kila mahali jewakati adam na eva wamekula tunda hakuwepo pale walipojificha hadi aanze kuuliza wako wapi? Alikua hajajua juu ya tukio la adam kula tunda maana lilimuudhi kwelikweli like he didn’t know a thing from a first place.

Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni? Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo. Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?


Kuna phrase protestant wanapenda kusema kwamba sisi wakatoliki hatujui kusoma na kuielewa biblia, naamini name ni mmoja wapo nisiojua kusoma biblia. Hivyo basi napenda kuwaalika wale wote wenye uelewa juu ya jambo hili. Naombeni mnijuze kama Mungu anajua hatima yangu na hukumu yangu siki ya mwisho na kama anajua je naweza kubadirisha? Kama mchezo kautengeneza yeye na sharia za mchezo kazitengeneza yeye je wachezaji wanawezaje kua huru?

Vinjii…
Hapa ndipo huwa nasema kila mtu au mwanadamu alie zaliwa na mwanamke, akili yake inaukomo. Hata kama uelewa wako ni wa juu kiasi gani. Ndio utatambua kuwa wewe ni binadamu tu.

Nakupa mfano mdogo Yohana mbatizaji alikua anajua kila kitu kuhusu Yesu, lakini siku ilipo fika mambo yamemwiya vibaya, alitatizika na akawatuma wanafunzi wake
Waende wakamuulize Yesu. Kama wewe ndie yule au tumtazamie mwingine?

Ni swali anamuuliza Yesu kupitia wanafunzi wake.

Kumbuka huyuhuyu aliwahi kushuhudia miaka miwili na zaidi kabla ya hapo akisema :Mathayo 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹ Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
¹² Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.Mathayo 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?
¹⁵ Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.

Kwaio hapo utaona namna ambavyo binadamu kuna wakati tunafikia pamoja na uelewa wetu mkubwa bado tu dhaifu.

Kwanini nimesema ni kwasababu nimeona unauelewa wajuu sana kuhusu Mungu lakini unajitahidi tena kutaka kupotea
 
Nikiangalia mpambano kati ya bwana Kisai na madam FaizaFoxy naona kabisa umuhimu wa kukubaliana na vya msingi tu generally na kuziacha zile specifics kila mtu ajiumbie dunia yake aah!

Inafika muda mmoja anahisi mwenzake ni mbishi kiasi cha uwezekano wa kiwa Kisai na Kiranga ni ID mbili za mtu mmoja! Hiyo ni next level, level 9999%

Hata hivyo angalizo madamu kadiri ya unavyomuona mwenzako ni mbishi huyo unayebishana naye, tambua wazi kwamba na wewe ni mbishi kwa kiwango kilekile ulichompimia. Na akiamua kukurudishia wewe basi wewe utakuwa ni mbishi wa kiwango hicho kilichozidishwa zaidi, kusukwasukwa na hata kumwagikaa....😏.

Nashauri watu wa dini tuanze kukubaliana na statement kama vile 'Mungu hana upendeleo' 'Mungu anatupenda' etc. halafu kila neno lipimwe kwa hiyo fact na kukubaliwa regardless the source, au kukataliwa regardless the source. Hata hivyo dunia tofauti hazitaepukika maana kila mmoja atakuja na tafsiri yake ya upendeleo na upendo na kuyavuruga matokeo.
Nimekuelewa, kuna ubishi na kuna kukosoa.

Ninachokifanya mimi ni kukosoa chanya" (positive criticism" iliwatu watumie bongo zao kufikiri na kukosoana kwa kuleta hoja zenye manufaa kwa wanaosoma. Maswali yangi yote yamelenga mawili tu, au kufunidisha au kujifunza. Nisome vizuri utalielewa hilo.

Nafahamu sana kuwa Kisai na Kiranga ni watu tpofauti na wenye uelewa tofauti lakini jinsi wanavyobishana wanajiweka "level" moja, ya ubishi hasi tu, wa "nani zaidi".
 
Back
Top Bottom