God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Mi nadhani ungejibu hoja kwasababu nikianza kuangalia hata hoja zako za kusema "thibitisha Mungu hayupo" nami niseme nitumie mfumo wako nitaziona zina utoto na ulichokiandika typically kitakuwa ni ujinga

Hiyo hoja kama umeiona ya kitoto basi ujue hata swali ulilouliza lina utoto pia, so what?
 
Sasa nijibu hoja gani kijana wakati huna hoja ?
 
Habari ya ndoa,wazazi sijui wife hayo ni ya duniani mbinguni hakuna vitu hivyo huko ni wewe tu
 
Umeanza na assumption ya kwamba wewe ni mfugo wa Mungu.

Watu wanafuga mifugo kwa sababu nyingi, kwa kutaka chakula, kwa kutaka kulindwa, kwa kutaka company, etc.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini anahitaji mifugo?
 
Nimecheka sana.

Huna hoja ya kunifanya nikwepe.
Unacheka ujinga wako

Ukiweza kuthibitisha Eric God eater hayupo umethibitisha Mungu wako hayupo

Ukishindwa kuthibitisha Eric God eater hayupo unakuwa umethibitisha Mungu wako hayupo

Thibitisha
 
Unacheka ujinga wako

Ukiweza kuthibitisha Eric God eater hayupo umethibitisha Mungu wako hayupo

Ukishindwa kuthibitisha Eric God eater hayupo unakuwa umethibitisha Mungu wako hayupo

Thibitisha
Sijawahi kushindwa kithibitisha juu ya uwepo wa Allah.

Ndiyo maana nikakwambia unatakiwa uache utoto.
 
Huna uwezo wa kujibu maswali yangu.

Hata nikikupa miaka kumi uonyeshe ujinga wa maswali yangu hutaweza.
Nimekueleza kuhusu "the problem of evil", halafu bado unaniuliza ulimwengu unakanushaje uwepo wa Mungu?

Unajua hata "the problem of evil" ni nini?
 
Hujathibitisha Mungu yupo.
 
K

Kwahiyo una biase kuwa unaamini muhimili upo licha ya kuwa hujauona ila huamini Mungu kama yupo kwasababu hujamuona.

Nimeamini sasa kwanini Mungu kawafananisha wasioamini kuwa ni sawa na wanyama au ni zaidi ya wanyama
Kwani wapi nimesema sikubali Mungu yupo kwa sababu sijamuona?

Unaweza kunionesha sehemu hiyo?

Mbona wewe sikuoni na najibizana nawe hapa kwa kulkubali kwamba upo?
 
Kinachopima uhalali ni kanuni, kanuni zimewekwa na watu kwa uchunguzi na urekebishanaji wa miaka mingi, hata wewe unaweza kupinga hizo kanuni na uki make sense dunia ikakuelewa na kukukubali, unabadilisha.

Logic si ukweli wenyewe, kwa sababu hata uongo una logic, mashaka ya kutojua ukweli ni upi na uongo ni upi yana logic, logic ni nyenzo ya kupata ukweli.

Mihemko si lazima iwe kiini macho, muhemko ni hali ya kupandwa na hasira au hamu kubwa. Inaonekana hili neno hulijui maana yake.
Jaribu kusoma tena maana ya mhemko ni nini, kama unataka kutoa maana nyingine, tumia neno tofauti, naona huelewi maana ya mhemko ni nini.

Kusema binary system ya computer si logic kwa sababu haina ukamilifu ni sawa na kusema mtu mfupi si mtu, kwa sababu si mrefu.

Usahawahi kumsoma Godel? Unafahamu mchango wake katika logic? Unajua "Godel's Incompleteness Theorems" zinasemaje?

Godel's incompleteness theorems zimeonesha kwamba hakuna system ya logic iliyokamilika. Kwa hivyo, hiyo dhana yako ya logic iliyokamilika ni njozi tu.

Again, mhemko rudia kusoma tafsiri yake, hujui maana ya hili neno inaonekana.
 
Sijawahi kusema Mungu hayupo popote, nimesema Mungu ni dhana iliyo mawazoni mwa watu tu.

Kikiwepo kwenye mawazo yako tu kipo angalau kwenye mawazo yako na si sawa kusema hakipo popote.

Pembetatu duara inawezekana kuwepo katika mawazo lakini si kiuhalisia.

Mungu naye ni hivyo hivyo, yupo katika mawazo tu, hayupo kiuhalisia.
 
Kinachopima uhalali ni kanuni, kanuni zimewekwa na watu kwa uchunguzi na urekebishanaji wa miaka mingi, hata wewe unaweza kupinga hizo kanuni na uki make sense dunia ikakuelewa na kukukubali, unabadilisha.
Kutambua na kuishi facts zisizo na Ukamilifu wa 100% kuna tofauti gani na IMANI?
JE, SI SAHIHI KUSEMA NAWE NI WALEWALE WAISHIO KWA IMANI KAMA WATU WA DINI?
Logic si ukweli wenyewe, kwa sababu hata uongo una logic,
Hakuna kitu kinaitwa Uongo. Uongo ni Nothing. Popote uionapo Logic tambua ndio UKweli wenyewe.
Nilitamka hili hapo mwanzo:
Kutokuwa hivi ni Ukamilifu wa kuwa Tofauti.
2+28=1 wakati 1-2=–1. Ukiishia kwenye formula ya kwanza utaishia kwenye kiiini macho, ila ukifika ya pili utaupata UKweli kuwa Hilo Si jibu sahihi. Hili jibu ni Ukweli wa kuwa 1+28 si 1.
mashaka ya kutojua ukweli ni upi na uongo ni upi yana logic, logic ni nyenzo ya kupata ukweli.
Logic ni Ukamilifu.
Mkuu, JE kweli unafikiri ni Nyakati za kujadili tafsiri za Kikamusi? Ingekuwa hivyo sidhani kama kungekuwa na mjadala hapa.
Kusema binary system ya computer si logic kwa sababu haina ukamilifu ni sawa na kusema mtu mfupi si mtu, kwa sababu si mrefu.
Hii ni hoja ya kulazimisha, hujanielewa vizuri nafikiri.
Usahawahi kumsoma Godel? Unafahamu mchango wake katika logic? Unajua "Godel's Incompleteness Theorems" zinasemaje?
Sijawahi, Sijui.
Godel's incompleteness theorems zimeonesha kwamba hakuna system ya logic iliyokamilika. Kwa hivyo, hiyo dhana yako ya logic iliyokamilika ni njozi tu.
Sijasema Logic iliyokamilika, ila LOGIC NI UKAMILIFU. Ukisema ILIYOKAMILIKA inakaribisha Uwepo wa Isiyokamilika, nao ni UWILI tayari.
Again, mhemko rudia kusoma tafsiri yake, hujui maana ya hili neno inaonekana.
Hatujadili maana za Kikamusi bali dhana bebwa na neno husika, tukihusianisha na kila kitu.
 
Sijawahi kusema Mungu hayupo popote, nimesema Mungu ni dhana iliyo mawazoni mwa watu tu.
Nitakuletea ushahidi.
Kikiwepo kwenye mawazo yako tu kipo angalau kwenye mawazo yako na si sawa kusema hakipo popote.
Je mawazo hayana mchango wowote katika Uhalisia?
Je, hujawahi kuona Mawazo ya MTU yakamgharimu?
Pembetatu duara inawezekana kuwepo katika mawazo lakini si kiuhalisia.

Mungu naye ni hivyo hivyo, yupo katika mawazo tu, hayupo kiuhalisia.
UPI ni mpaka uliopo kati ya Mawazo na Uhalisia, ikiwa matendo mengi ya watu huanzia kwenye Mawazo?
 
Sijawahi kusema Mungu hayupo popote, nimesema Mungu ni dhana iliyo mawazoni mwa watu tu.
Nitakuletea ushahidi.
Kikiwepo kwenye mawazo yako tu kipo angalau kwenye mawazo yako na si sawa kusema hakipo popote.
Je mawazo hayana mchango wowote katika Uhalisia?
Je, hujawahi kuona Mawazo ya MTU yakamgharimu?
Pembetatu duara inawezekana kuwepo katika mawazo lakini si kiuhalisia.

Mungu naye ni hivyo hivyo, yupo katika mawazo tu, hayupo kiuhalisia.
UPI ni mpaka uliopo kati ya Mawazo na Uhalisia, ikiwa matendo mengi ya watu huanzia kwenye Mawazo?
 
Nimekueleza kuhusu "the problem of evil", halafu bado unaniuliza ulimwengu unakanushaje uwepo wa Mungu?

Unajua hata "the problem of evil" ni nini?
Jibu maswali maswali niliyo kuuliza. Suala la hili nimeshakujibu zaidi ya mara moja.

Tangu nawajua nyinyi huwa mnakimbia maswali, na kuna muda huwa tunawauliza maswali ili kuonyesha ujinga wenu ulipo.

Kwahiyo usilete kona kona, nimekuuliza maswali jibu maswali.
 
Mara tu utakapoipersonalize hiyo Perfection itavaa UWILI nao hautaweza kuwa nje ya Makosa,Udhaifu, Mapungufu, Uovu, Ujinga, Ulimbukeni, MIHEMKO, Hulka, Chuki, Husda, woga, nk.....

Hakika. Ni Ukamilifu.
Anhaa nimeupata msimamo wako, wa kwamba ukamilifu hauendani na sifa yoyote ni just UKAMILIFU. Nakubaliana nayo kuwa ile highest 'I AM THAT IAM' unaweza kuiacha hivyo. Labda kwa hatua zetu [sisi wadoooogo sana] kumuelewa Mungu kinamna hiyo kunakuwa hakuna kitu practical cha kutenda sasa kutokana na imani ya namna hiyo. Tutaelewa vizuri tukifika level fulani, tukikaa na Yesu na kujifunza/kutawala pamoja naye.

Wakati huo msimamo wangu ni kwamba ni ukamilifu na ni sifa zote za UKAMILIFU huo. Umenijibu mahala kwamba hiyo itaonesha ana hulka mbalimbali na uwili [uko na point], kwangu sioni kama ni hatari sana maana sijamvua personality japo tu sijamuanthropormorphize na hizo hulka ni perfection yazo; upendo, ukweli, uzima, uzuri. Itakuwa taabu sana kuhusiana na jitu lisilo na personality yoyote yaani liwe neutral kama LOGIC?! Ikishindikana kuziweka hizo sifa kwa Mungu basi ninaziweka kwa mwana wa Mungu maana hata hivyo Yeye ndio njia ya kufika hata huko kwa Mungu. I mean kuuishi huo ufalme wa Mungu maana hata sasa upo. Yeye atatusaidia kujua machaguo mazuri ambayo LOGIC yake itaishia kwenye matokeo mazuri kwa muhusika binafsi.

Kwa Yesu personality inakaa bila shida yoyote. Kwa kumtii Mwana anayemtii Baba yake unakuwa umemtii na kumkubali Mungu[Bado nimemuacha Mungu katika hali ambayo anayo Will na ndio WILL yenyewe]. Baba atukuzwe katika Mwana. And that gives us something practical to relate to.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…