God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Sasa nielezee vipi wakati kila siku nakukosoa, wewe hilo kwangu rahisi na picha uliyo itoa iko wazi na inaonyesha udhaifu mkubwa sana katika namna ya kuhoji, kwanza mtiririko huo na namna alivyofikia hitimisho ameacha mambo mengi sana kuhusu Mola muumba, yaani alikuwa hamjui.

Ndiyo maana Imam Ibn Taymiya katika kitabu chake "Radd 'ala Mantiqiyiin" akasema Wanafalsa walikuwa wanafikiria juu ya maswali sahihi lakini walikosa njia za kuyapata majibu sahihi.

Mfano swali la pili, kwamba je Mola anajua kuhusu maovu au uovu wote ? Jibu ni "NDIYO" anajua tena anajua in "general" na anajua "in details", akajibu "NO" sasa nakuuliza wewe swali, ambaye unaona hii hoja, kwanini amesema "NO" ? Na kwanini hajaweka "YES" ?

Sasa wewe katika bado mdogo sana, nakupa dodoso tu, hapa nataka ujibu maswali yote ninayo kuuliza.
Wewe nimekwambia tatizo lako hujui Kiingereza.

Ndiyo maana umeshindwa kuelewa nilichopost hapa.

Na kwa sababu hii hatuwezi kuelewana.
 
Wewe nimekwambia tatizo lako hujui Kiingereza.

Ndiyo maana umeshindwa kuelewa nilichopost hapa.

Na kwa sababu hii hatuwezi kuelewana.
Hahaha, sasa kama una uwezo si ukosoe kijana. Shida iko wapi ?

Kingine maswali niliyo kuuliza bado hujajibu hata moja.
 
Mambo haya ya Imani yanachanganya sana. Utakuta kuna Malaika walikuja kutembea duniani wakakutana na wanawake warembo wakaamua kulala nao na hawakuweza kurudi tena mbinguni.
Ukisoma kitabu cha Ayubu nacho, shetani aliulizwa na Mungu umetoka wapi wewe, akajibu nimetoka kutembea huku na huko. Shetani akamwomba Mungu amjaribu Ayubu ili aone kamA anamtii Mungu au la.
Mungu alimruhusu shetani amdhuru Ayubu lakini sio kumwondolea uhai.
Mungu alijua fika Ayubu atashikiria msimamo wake wa kumtii. Je' Ayubu angemuasi Mungu baada ya shetani kuruhusiwa kumjaribu, kosa lingekua ni la nani?
Kisa hicho cha Ayubu kinafanana na Yuda alie msaliti Yesu. Kama maandiko mengi yalitabiri kusalitiwa kwa Yesu na mateso yake. Kwanini kutimia kwa maandiko hayo moja kwa moja yanamuweka Yuda kwamba ni muovu?
Ukitazama kwa undani utaona sisi binadamu tumekua kama uwanja wa mapambano kati ya Mungu na Shetani lakini mwisho wa yote sisi ndio tunabeba mzigo huo moja kwa moja
 
But i am not a debator [emoji4]
Ngoja tukuchokoze; a debate has three or four members/participants..... proposers, opposers and members of the floor plus mwenyekiti na katibu na mgeni rasmi na jaji. Even members of the floor are participants in some parts, so: they are debators in more than one way😏😏
 
Ngoja tukuchokoze; a debate has three or four members/participants..... proposers, opposers and members of the floor plus mwenyekiti na katibu na mgeni rasmi na jaji. Even members of the floor are participants in some parts, so: they are debators in more than one way[emoji57][emoji57]
[emoji23]

Chill Bruh!

But i am not a debater [emoji4]
 
You have foreknowledge!!! [emoji33]..... so do you know like if somebody will not change their idea or not. If you would debate?
Whoa! Easy Bro!

I never said 'meant' that

But i am not a debater [emoji17]
 
MADA: Je Mungu anajua hatma ya wanadamu?

Foreknowledge & Free will
 
Hello y’all..

NB
: Naomba moderator mada hii msiihamishie jukwaa la dini maana huko itakosa wachangiaji na lengo langu la kutaka kujuzwa jambo hili halitatimia and that will leave me frustrated and bums me out, Natuamaini mtatii takwa langu hili. Ahsanteni.

Binafsi kiimani ni muumini wa kanisa Katoliki kwa kuzaliwa na kubatizwa, pia ninaamini na kuisadiki kanuni ya imani yangu katoliki isemayo “Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi muumba mbingu na dunia na kwa Yesu Kristu Bwana wetuu….” Self-schemas: katika sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.

Self-Concept ni i hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future self (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo). Toka nilipoanza kutambua Self Concept yangu Nimekua na swali ambalo kwakweli pamoja na kuisadiki imani yangu hii na kupokea ya Sakrament takatifu ya Communion swali hilo limekua mwiba mchungu na kikwazo kikubwa katika imani yangu hii na Mungu kwa ujumla.

Toka nilipoanza kujitambua nimejaribu kuwashirikisha watu wenye uelewa jambo hili ila bado sijapewa majibu thabiti….natumaini hapa JF nitapewa maelekezo vyema , mnivumilie kama maelezo yatakua marefu maana hua siwezi kuelezea kwa ufupi but it worth your time.

The One above all, In-Betweener and The One bellow all.

Monotheism
ni imani ya kua kuna Mungu mmoja pekee ambae aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo. Watu wanao amini katika imani hii ni wafuasi wa dini zilizotokana na Ibrahim ambae anachukuliwa kama baba wa imani ambazo ni Judaism, Ukristo,uislam, mandaeism ,Rastafarian na Bahai. Mungu wa imani hii ndio huyu tunayemfahamu mimi na wewe ambae ana sifa kuu tatu ambazo ni yupo kila mahali, anajua kila kitu, na anaweza kila kitu. Omni ni neno la kilatini lenye maana ya yote au kila kitu na Sciens ni neno la kilatini likimaanisha kujua(conscious)……. Moja kati ya sifa kuu tatu za Mungu nilizotaja hapo juu ni Omniscience ikimaanisha kwamba Mungu anajua yote yaliyopita,yaliyopo na yajayo.

The Great Chain of Being ni mchoro au nadharia ambayo inaonyesha kwamba maisha ya mwanadamu yapo kwenye ngazi /mtiririko Fulani ambapo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,mimea halafu chini kabisa yupo shetani. Mungu ni the one above all, mwanadamu ni aliyekati /in-betweener na shetani ni the one below all. Unajua mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote walioumbwa na mungu kuzidi hata malaika ndio maana kuna malaika wanafanya kazi kwa wanadamu ya kutulind, Moja kati ya utajiri na kitu kikubwa alichonacho mwanadamu hakuna kiumbe kingine anacho ni uwezo wa kuchagua na kuamua Kuishi vile atakavyo yeye yaani Free Will….Katika Great chain of being mwanadamu amewekwa katikati (In-Betweener) maana yeye ameumbwa na roho isiyokufa (immortal) na mwili ambao unaokufa (mortal) hivyo inamuwezesha yeye kuishi duniani au mbinguni . Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi Uungu kwa kutenda mema maishani mwake au ushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Kwakua mwanadamu ana free will uamuzi ni wake ni kuchagua kwenda kwa The One above all au kwa the one bellow all.

Free Will is illusion (?)

Kuna mada Fulani niliwahi kusema kwamba tukio la kuumbwa Adam na eva hadi kufukuzwa eden linapinga uwepo wa Mungu kwa kupinga sifa tatu alizonazo Mungu kwamba anaweza yote,anajua kila kitu na yupo kila mahali… ndio maana mimi hua nalichukulia kama lugha ya picha tu na sio tukio halisi na kama kweli ni kweli lilitokea kama lilivyoelezewa kwenye kitabu cha mwanzo basi linaonyesha Mungu hafai kupokea sifa tunazompa. Kama anajua kila kitu je wakati anamuumba adamu bila Eva hakujua kwamba adamu hatapata uhitaji wa kua na mwenza? Yupo kila mahali jewakati adam na eva wamekula tunda hakuwepo pale walipojificha hadi aanze kuuliza wako wapi? Alikua hajajua juu ya tukio la adam kula tunda maana lilimuudhi kwelikweli like he didn’t know a thing from a first place.

Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni? Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo. Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?


Kuna phrase protestant wanapenda kusema kwamba sisi wakatoliki hatujui kusoma na kuielewa biblia, naamini name ni mmoja wapo nisiojua kusoma biblia. Hivyo basi napenda kuwaalika wale wote wenye uelewa juu ya jambo hili. Naombeni mnijuze kama Mungu anajua hatima yangu na hukumu yangu siki ya mwisho na kama anajua je naweza kubadirisha? Kama mchezo kautengeneza yeye na sharia za mchezo kazitengeneza yeye je wachezaji wanawezaje kua huru?

Vinjii…
Kwa kukusaidia kujibu swali lako, ni kwamba unafanyia kazi nadharia Ilizopitwa na wakati.
Kwa nini Mungu aliwapa mitihani mpaka Manabii/Mitume wake...!

Mtume aliye Tumwa kuja kukamilisha wito wa Mungu juu ya Mwanadamu ni Muhammad (s.a.w)
Na kitabu alicho pewa (Quran) ameambiwa lengo la kuumbwa kwenu sisi wanaadamu (Umma wa Muhammad) ni Kumuabudu /Kumcha Mungu.
Kama utakuwa na malengo yako Mengine wewe ni wa Motoni (wa Shetani) tu.
Usimzungumzie Mungu wa Enzi za Ibrahim, Musa, Yakubu, Issa n.k...
 
Kwa kukusaidia kujibu swali lako, ni kwamba unafanyia kazi nadharia Ilizopitwa na wakati.
Kwa nini Mungu aliwapa mitihani mpaka Manabii/Mitume wake...!

Mtume aliye Tumwa kuja kukamilisha wito wa Mungu juu ya Mwanadamu ni Muhammad (s.a.w)
Na kitabu alicho pewa (Quran) ameambiwa lengo la kuumbwa kwenu sisi wanaadamu (Umma wa Muhammad) ni Kumuabudu /Kumcha Mungu.
Kama utakuwa na malengo yako Mengine wewe ni wa Motoni (wa Shetani) tu.
Usimzungumzie Mungu wa Enzi za Ibrahim, Musa, Yakubu, Issa n.k...
Tatizo lengo la madaa hii sio kuzungumzia existence purposes bali Conscience na Freewill
 
Wacha niharibu conclusion nzuri ya uzi uliishia na neno hitimishi kiutamu sana 'POA' nukta........ mtanisamehe

Nimekuja huku nikidhani ndiko Mokiti anakoendelea kupambana na Kisai kumbe sio huku! sijui wako wapi hawa jamaa.
 
Wacha niharibu conclusion nzuri ya uzi uliishia na neno hitimishi kiutamu sana 'POA' nukta........ mtanisamehe

Nimekuja huku nikidhani ndiko Mokiti anakoendelea kupambana na Kisai kumbe sio huku! sijui wako wapi hawa jamaa.
Wee jamaa kwa kuandika magazeti nakupa hongera. Kuna vitu napika nitakualika vikiiva😅
 
Back
Top Bottom