Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Waandishi wa habari undercover wanajifanya kuwa majambazi wenye dola bilioni moja za pesa chafu zinazohitaji kusafishwa. Wanapata upenyo kwa wanachama wa Afrika wa Gold Mafia na kurekodi mikutano ya siri na viongozi wa uhalifu.

Balozi Mkubwa wa Afrika anatoa huduma ya kutakatisha pesa chafu zenye thamani ya dola milioni 1.2 kwa kutumia kofia yake ya Udiplomasia.

Wenyewe wanakwambia kwa Afrika ilimradi unatotoa chochote kitu basi mambo yako yanaenda bila shida yoyote. Gold Mafia imesambaa, hakuna mamlaka au serikali yoyote Afrika inayojaribu kusogeza pua yake.

Wahalifu hutoa donge nono kutakatisha zaidi ya dola milioni 100 kupitia miradi ya serikali ya usafirishaji wa dhahabu. Kitovu cha shughuli zao ni kituo kikubwa cha kutakatisha pesa kusini mwa Afrika, Benki Kuu ya Zimbabwe.

Gold Maafia, ni mfululizo wa sehemu nne wa kitengo cha uchunguzi cha Al Jazeera, unaoangalia jinsi tamaa ya jamii kumiliki dhahabu wanavyoendeleza na kuunga mkono uchumi haramu ulimwenguni. Timu ya siri inafanikiwa kuingia kwenye makundi hasimu ambayo hubadilisha pesa chafu kuwa dhahabu, ambayo baadae inauzwa ulimwenguni kote.

Kupitia maelfu ya nyaraka za siri na mahojiano ya moja kwa moja na whistleblowers kutoka ndani ya makundi vya uhalifu, wachunguzi wanapata muundo wa operesheni za utakatishaji wa pesa zenye thamani ya mabilioni ya pesa ambazo huudumia viongozi wa kisiasa, uchunguzi huo unatupeleka kwenye ofisi za juu Kusini mwa Afrika.

Unadhani viongozi gani wanajihusisha na biashara hii haramu Afrika Kusini, vipi nchi nyingine, je, na Tanzania kuna viongozi wanaojihusisha na biashara hiyo?

Itaendelea...

Kuanza nayo soma Episode 1 - Sehemu ya 1
 
Aya ya nne ya huu Uzi na comment namba 11 ya chotera ndio maisha halisi ya mafia a.k.a mafioso. Ukibahatika kusoma riwaya ya Mario puzo ya the godfather utagundua kwamba mafia Wana play role kubwa katika ku support project kadhaa za serikali na pia kupenyeza rupia Ili mambo Yao na biashara zao Haramu ziende. Na amini usiamini hata bills zinazokuwa proposed bungeni haswa mabunge yetu haya ya kiafrika muda mwingine zinakuwa ni kwa ajili ya kuwa favor Hawa THE MEN OF HONOR au mafia. Hawa mafia ndio hutoa chochote kitu ku fund kampeni za wanasiasa Ili kulainisha mambo Yao na wapo kila sekta kila idara za serikali na pia ni miongoni mwa DEEPSTATE.
 
Aya ya nne ya huu Uzi na comment namba 11 ya chotera ndio maisha halisi ya mafia a.k.a mafioso. Ukibahatika kusoma riwaya ya Mario puzo ya the godfather utagundua kwamba mafia Wana play role kubwa katika ku support project kadhaa za serikali na pia kupenyeza rupia Ili mambo Yao na biashara zao Haramu ziende. Na amini usiamini hata bills zinazokuwa proposed bungeni haswa mabunge yetu haya ya kiafrika muda mwingine zinakuwa ni kwa ajili ya kuwa favor Hawa THE MEN OF HONOR au mafia. Hawa mafia ndio hutoa chochote kitu ku fund kampeni za wanasiasa Ili kulainisha mambo Yao na wapo kila sekta kila idara za serikali na pia ni miongoni mwa DEEPSTATE.

Huo ndio ukweli maana kihalali utapata pesa za kula tu, angalia kwa mfano kipindi JK anaelezwa akamate wauza madawa ya kulevya alisema nchi itatikisika kwani wako wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa dini, hao barrick wenyewe kwenye migodi ya africa na duniani kote wanacheza dili feki za kukwepa kodi kuliko kawaida, biashara ya usafirishaji anzia mabasi hadi meli na ndege kuna siri kubwa ya usafirishaji wa magendo mbalimbali ya kila aina duniani kote, anagalia kwenye hata biashara za mazao mnunuzi wa mwisho anakuja na bei nzuri mwanzo halafu baadae anashusha bei ili apate faida zaidi, anagalia biashara kama pamba, kahawa, korosho mnabaki mnapiga kelele mara soko la dunia mara blah blah kumbe wenzenu mafia gangs washafanya yao, yaani mwaka huu wanawapa bei nzuri sana ili mwakani kila mmoja alime hilo zao, wakishaona lipo kwa wingi hawanunui mapema wanawaacha kwanza baadae wakija wanatoa pesa kidogo tayari hamna pa kupeleka na mnakua mshapigwa tayari, ndio maana hata issue ya bandari tunasema hakuna huruma utayopata kutoka kwa unayemwita mwekezaji hivo lazima uwe macho kuokoa chochote
 
Episode 1 - Sehemu ya 1

Sehemu ya kwanza inatukutanisha kwanza na bwana Kamlesh Pattni (ama Brother Paul kama mwenyewe anavyopenda kujiita baada ya kuanzisha kanisa lake), moja ya wafanyabiashara maarufu wa dhahabu Afrika.

kamlesh.jpg

Huku timu ya Al-Jeezera ikiwatoa;

1. Bwana Stanley kama kiongozi wa timu ya undercover. Stanley anaenda kama mhalifu wa genge (gangster) ambaye anataka kutakatisha fedha zake kutoka China.

Stanley.jpg


2. Dada Sin, undercover reporter ambaye alisimama kama mshauri wa Stanley kwenye masuala ya uchumi.

3. Bwana Jonny (reporter wa undercover) ambaye anaenda kama mfanyabiashara wa black market, bwana Hawala (mtu ambaye anahamisha pesa kutoka mpaka mmoja mwingine bila kupitia benki).

Screenshot 2023-06-22 205404.png


NB: Watu wengine watafahamika mbeleni kadri wanavyojitokeza ili kuhakikisha biashara zinafanyika.

Mchongo unaanza....

Gangster wetu Stanley anaenda kumuona bwana Patni ili amsaidie kutakatisha hela zake kutoka China. Patni anaona mchongo huu hapa, na kuwaambia hilo sio tatizo kabisa kwani viongozi wa Afrika wanamuamini sana, imani yao kwake iko mawinguni. Patni anaanza kutamba kuonesha uthibitisho wa picha mbalimbali alizopiga na viongozi wa Afrika kuthibitisha alichosema kuwa yeye ni mtu muhimu kwao na akitaka jambo basi litafanyika kwa uzuri kabisa. Patni akaanza kutiririka, picha yake na Hayati Robert Mugabe ikifungua dimba;

Screenshot 2023-06-22 210121.png


Picha iliyofuata akaonesha jinsi alivyopata tuzo Kenya - Lifetime Africa Achievement Award, Bwana Patni pia alifanywa kuwa Balozi wa Amani na Baraza la Wazee wa Kenya

Screenshot 2023-06-22 210500.png


Akaonesha pia picha akiwa na Mwai Kibaki

Screenshot 2023-06-22 211036.png


Hapa Patni akiwa na Rais Museven wa Uganda

Screenshot 2023-06-22 210545.png


Screenshot 2023-06-22 210734.png


Huku Patni akiwa na mfalme Chevy Zeh Jean Gervais wa Ivory Coast
Screenshot 2023-06-22 211201.png


Hapa akiwa na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma
Screenshot 2023-06-22 211355.png


Hapa Patni akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati ule, Muamar Gaddafi, ambapo alimsimika Gaddafi kwa kumvisha taji kama Mfalme wa Wafalme wa Afrika.

Screenshot 2023-06-22 211510.png


Na Gaddafi alipofariki Mchungaji Patni alimbariki cheo hicho cha Ufalme wa Wafalme Hayati Robert Mugabe.

Kama unakumbuka mwaka 2017 Mugabe aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi, na liyefata baada yake ni Rais Emmerson Mnangagwa. Rais Mnangagwa anatumia Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuvutia uwekezaji kutoka nje, Mwakilishi wa Rais pia alihudhuria mkutano huo, Muwalishi wa Rais ambaye alikubali kukutana Stanley (undercover) akisema kuwa ana mamlaka ya Rais yanayomuwezesha kupiga nao dili bila tatizo lolote!

Muwakilishi huyo wa serikali alijitapa kuwa na mamlaka kamili ya kusaini mikataba kwa niaba ya serikali bila Rais kuhusika na mkataba huo kutambulika kisheria! Muwakilishi akaendelea kutamba kuwa, cheo chake kama balozi kinagusa nchi 85, lakini kwenye ujumbe maalum wa Rais yeye ni Muwakilishi wa Rais, na ni namba mbili kimamlaka, akimaanisha baada ya Rais anafuata yeye. Akiendelea kusema hakujawahi kuwepo nafasi hiyo nchini, imetokea moja tu na yeye ndio aliteuliwa kiuibeba!

Huyo ni Balozi Uebert Angel
AngelUebert.jpg

Uebert ni Balozi wa Zimbabwe kwa Marekani na Ulaya, yeye kwenye mchezo huu mchafu ni sehemu ya kile kilichotajwa kama Mafia wa Kidiplomasia, Angel pia ni Nabii (aliyejiba unabii)! Naamini wengi hapa mnafahamu Angel ama kwa kufatilia mafundisho yake kama kiongozi wa dini au kwa kumuona tu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na sifa zake kuvuma kutoka kwa wafuasi wake.

Angle anaendesha kanisa linaloitwa Good News, ambalo lina matawi 15 katika nchi mbalimbali duniani. Nabii Angel anafanya uponaji/miujiza kwa wagonjwa, kutaja matokea ya mechi za mpira kabla haujachezwa na ikawa hivyo (mfano alisema mechi ya West Ham na Leicester City watatoka sare ya magoli 2 na ikawa hovyo) na kadhalika.

Rais Mangagwa alimteua Angle katika moja ya nafasi kubwa kwenye uongozi serikalini, Ubalozi ambao alikuwa na kazi ya kuitangaza Zimbabwe ili kuvutia wawekezeji.

Angel pia anadai anaweza kuona hatma ya viongozi wa Afrika. Siku nne kabla ya uchaguzi mkuu wa Ghana, Nabii Angel alitoa Unabii wake kuwa Addo Nana ataendelea kuwa madarakani, lakini pia akatabiri ushindi wa kiongozi wa upinzani kwenye kiti cha Urais Zimbabwe, dili la kutakatisha pesa za bwana Stanley liko salama! Angle aliwahakikishia wasiwe na wasiwasi biashara yao itaenda salama, kwani Mnangagwa atakuwa Rais wa maisha!

Ilikuwaje bwana Kamlesh Pattni akafika Afrika na kuwa na ushawishi kiasi hicho? Vipi kuhusu biashara na reporter undecover bwana Stanley, mambo yataenda vizuri kama Nabii Angel alivyoahidi au kutakuwa na mizengwe?

Tukutane kesho Wakuu....

Muendelezo soma - Episode 1 - Sehemu ya 2
 

Attachments

  • Screenshot 2023-06-22 220311.png
    Screenshot 2023-06-22 220311.png
    88.8 KB · Views: 43
Kuna mwaka nilikamatwa huko kanda ya kaskanzini nikalala sero siku tatu siku nikaamishiwa gerezani c nikakuta kuna mgeni wa nje ya Tz tukaanza kula story yule ndugu akaniambia Kuna ela ipo online nitafute kituo Cha watot yatima ndo tupigie dili la kuingiza hizo fedha nchini Sasa tatizo likaja huku cjaweka mchongo wangu vizuri ndugu zangu wakawa washamaliza kesi huko nje nashangaa nakuja itwa nisepe hm niliona wamenipotezea utajiri
 
Huo ndio ukweli maana kihalali utapata pesa za kula tu, angalia kwa mfano kipindi JK anaelezwa akamate wauza madawa ya kulevya alisema nchi itatikisika kwani wako wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa dini, hao barrick wenyewe kwenye migodi ya africa na duniani kote wanacheza dili feki za kukwepa kodi kuliko kawaida, biashara ya usafirishaji anzia mabasi hadi meli na ndege kuna siri kubwa ya usafirishaji wa magendo mbalimbali ya kila aina duniani kote, anagalia kwenye hata biashara za mazao mnunuzi wa mwisho anakuja na bei nzuri mwanzo halafu baadae anashusha bei ili apate faida zaidi, anagalia biashara kama pamba, kahawa, korosho mnabaki mnapiga kelele mara soko la dunia mara blah blah kumbe wenzenu mafia gangs washafanya yao, yaani mwaka huu wanawapa bei nzuri sana ili mwakani kila mmoja alime hilo zao, wakishaona lipo kwa wingi hawanunui mapema wanawaacha kwanza baadae wakija wanatoa pesa kidogo tayari hamna pa kupeleka na mnakua mshapigwa tayari, ndio maana hata issue ya bandari tunasema hakuna huruma utayopata kutoka kwa unayemwita mwekezaji hivo lazima uwe macho kuokoa chochote
Na Hawa mafia wanakuwa favorerd na akili tia maji tia maji za Hawa viongozi ambao hawajui hata ku reason kwenye mambo nyeti ya nchi . Na ndio maana Hawa don jamii ya Asians Hawa ......[emoji119][emoji119] Ngoja niuambie mdomo koma[emoji850]
 
Hapa nimeona mchoro wa dogo mmoja aliyeibuka majuzi kwa hekima na kuhubiri akiingia kwenye mfumo!

They are smart enough to pick their allies. Huyu nabii yupo Bongo toka jana.
Na Patni ameshiriki sana kwenye deals Kenya akiwa ni raia wa Nchi hiyo. Mwaka 1994 yeye na washiriki wengine wakiwamo viongozi Serikalini waliingia kwenye scandal ya Goldenberg na kuitia Kenya hasara ya zaidi ya Dola milioni 200. Kumbuka Mwaka 1994 bajeti ya Tanzania ilikuwa ni around 1 billion usd!

Tokea wakati huo uchumi wa Kenya uliyumba sana. Huyo ndiye Kamlesh Pattni. Hapigi deal peke yake, lazima viongozi wawemo
 
Episode 1 - Sehemu ya 2

Kutokana na maelezo ya bwana Patni yeye alizaliwa Kenya, na ametembelea sehemu nyingi Afrika, anaijua vilivyo. Harakati za Patni kuwa 'mtatuzi wa mambo' au tuseme 'mmaliza matatizo' ya viongozi wa Afrika zilianzia mahali alipozaliwa, Kenya. Akisema kipindi hiko wakati wa uongozi wa Arap Moi kulikuwa na udikteka, serikali ilikuwa haitaki mfumo wa vyama vyangi na kufanya shughuli zake chini ya mfumo wa chama kimoja. Patni aliandika mpaka vitabu kuhusu hilo, taratiibu akawa anaingiza mizizi yake kimkakati. Akiwa na miaka 24 siku moja ameenda kununua suti kwenye moja ya maduka Nairobi, Patni anakutana na Mkurugenzi wa kitengo cha Ujasusi (Usalama wa Taifa) Kenya kwa bahati tu, wakapiga stori mbili tatu na kuongelea kuhusu dhahabu. Jamaa hakupoteza muda, akatumia mwanya huo kupenyeza jambo lake.

Patni akamwambia Mkurugenzi unajua kuna dhahabu nyingi inayopita Kenya, lakini Kenya haifaidiki kwa chochote, inaishia tu kupitishwa kimagendo kwenda chini nyingine. Patni anamwambia Mkurugenzi kuwa ana suluhisho la tatizo hilo, yeye anaweza kuzalisha dola milioni 500 kila mwaka ikiwa watafuata utaratibu sahihi wa kupata leseni ya dhahabu hiyo. Mkurugenzi akaona ulaji huu hapa, akamchukua bwana Patni haraka na kumpeleka kwa Rais Moi ili akaeleze ule mchongo vizuri. Rais Moi akamuelewa sana bwana Patni mpaka akamfanya kuwa mshauri wake! Kiurahisi, kampuni ya Patni inayoitwa Goldenberg International ikapata shavu la kuwa kampuni pekee itakayokuwa inajihusisha na kusafirisha dhahabu ya Kenya (exclusive licence).

Screenshot 2023-06-24 011233.png

Patni akiwa amekutana na Moi

Kwahiyo kampuni hiyo ikawa kama geresha tu kuwa mambo yanafanyika kwa uhalali, ila huku chini dhahabu kutoka inayojulikana sasa kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaingizwa kimagendo Kenya na kwenda kuuzwa ughaibuni ambapo Patni anapata 35%. Kwa jumla Patni akawa anaingiza milioni 600, ambapo yeye alikuwa anapata mgao wake, mgao wa Rais Moi na Maafisa wote wa serikali waliompa leseni.

Patni, sasa akiwa pia ni Mshauri wa Rais Moi kipindi hicho Moi anapata upinzani mkubwa kwa kukataa mfumo wa vyama vingi, akampa ushauri kabambe Moi, akamwambia sikia Mzee baba, we kubali tu mfumo wa vyama vingi, wao wataona wameshinda ila ukweli tunajua sisi. Si umeona pesa kwangu sio tatizo, zitasaidia kununua watu wakuunge mkono tusambaratishe wapinzani. Pesa ziko na wewe, utashinda usiwe na wasiwasi. Basi bwana Patni ndio akawa kama oxgyen ya kumuwezesha Moi kubaki madarakani. Moi akastaafu baada ya miaka 24 kama Rais, upinzani wakaingia madarakani, wakamfahamu Patni, mambo yote yakawa hadharani, Patni akashtakiwa kwa udanganyifu, kesi zikaanza!

Screenshot 2023-06-24 015202.png

Patni akiwa akionekana mgonjwa Mahakamani katika moja ya session ya kesi yake

Kesi ilirindima Kenya na kuchukua karibia miaka 13, lakini mwishowe kesi ikafa, ikazimwa hivyo yaani shwaa na Patni hakuwahi kuhukumiwa, akawa mtu huru. Wakenya wakaripuka kwa hasira, wakamkalia kooni Patni, piga kelele weee za kumuita mwizi ila mambo ndio yakawa yameisha hivyo, zikabaki kuwa kelele tu ambazo hazimzuii tembo kunywa maji.

Baada ya hapo Patni akafunga virago vyake Kenya na kuhamia Zimbambwe, huko Patni akazaliwa upywa, sio kwa tabia, bali utambulisho mwingine tofauti na wa Kenya, akaanzisha dini mpya pamoja na kanisa lake, akiitwa Pastor Paul.

Mwaka 2008 Zimbabwe ilikuwa na mfumuko wa bei wakutisha uliozorotesha uchumi vibaya sana, thamani ya hela ya Zimbabwe ikaporomoka, pia kulikuwa na machafuko ya kisaisa wakati huo na viongozi wa upinzani wakafungwa jela sababu ya udanganyifu kwenye Uchaguzi Mkuu. Marekani na Ulaya ikaingilia kati na kuwawekea Zimbabwe vikwazo, ikiwataka walete demokrasia nchini lakini pia ikawekea vikwazo vya kiuchumi ikiamini Zimbabwe haitakiwi kuingia kwenye mfumo wa kimataifa wa uchumi, kwa maana hii Zimbabwe haiwezi kufanya shughuli zake kwa kutumia dola ya Kimarekani bali itumie pesa yake. Zimbabwe inabidi watafute njia nyingine ya kupandisha thamani ya pesa yao, na moja ya njia hiyo ni kubadili sarafu yao kuwa dhahabu, sababu kwa kufanya hivyo ni rahisi kuvuka mipaka na kufanya biashara na nchi nyingingine lakini pia haitaathiri mfumo wa uchumi kimataifa. Hii ikawa mwiba zaidi kwa Zimbabwe, bwana Patni akapata upenyo wa kuweka mizizi yake Zimbabwe vizuri.

Patni anafanya makubaliano na viongozi wa Zimbabwe waliowekewa vikwazo vya kiuchumi. Patni anajisifia kuiokoa Zimbabwe kutokana na anguko la uchumi, kwani bila jitihada zake na wenzake hela ya Zimbabwe ingekuwa haina thamani kabisa, uzuri ni kwamba Rais anawasikiliza hata kama kuna nguvu kidogo ya mataifa ya nje ila hilo sio tatizo kubwa kwao!

Nini kitaendelea Zimbabwe na bwana Patni? Tukutane jioni kwa muendelezo.

Muendelezo soma - Episode 1 - Sehemu ya 3
 
Back
Top Bottom