Episode 1 Sehemu ya 3
Usafirishaji wa dhahabu wa Zimbabwe una thamani ya hadi dola bilioni mbili kwa mwaka, ni biashara yenye pesa ndefu. Sehemu ya tatu inatukutanisha na mshindani wa bwana Patni, wa pili kwenye biashara hii ya kuuza dhahabu kwa magendo, wa kwanza akiwa kubwa lao Patni, huyu ni bwana Ewan MacMillan.
Mara ya kwanza MacMillan alikuwa akifanya biashara hii mwenyewe na kumiliki kila kitu, baadaye akaanza kushirikiana na wadogo zake wawili. MacMillan alienda jela kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 21 kwa kosa la kumiliki dhahabu yenye kiasi cha kg 1.2 kimagendo, pia alifungwa sana miaka ya 90 kwa makosa yanayohusisha kufanya biashara ya dhahabu kwa magendo.
MacMillan anafanya biashara ya kubadili kilo 200 za dhahabu kuwa pesa kila wiki. MacMillan anakutana pia na undercover, wanampa mchongo wa kutakatisha pesa zao kutoka china, Ewan anaingia kingi, anawaambia mmefika kwa mtu sahihi, hilo limeisha.
Awaambia sikia kama unataka dola za Kimarekani katika akaunti ya benki, basi unatakiwa kuwa na akaunti ya dola kwenye benki ya Dubai. Kule Dubai Ewan ana mshirika, ambaye yeye ndio mtaalamu wa kutakatisha pesa za watu, jamaa huwa anatakatisha mpaka pesa za Warusi. Mtu anayetaka kutakatisha pesa anampatia pesa hizo Ewan, ambapo yeye anazibadilisha kuwa dhahabu anamtumia huyo mshirika wake wa Dubai ambaye naye anafanya manuva ya kubadili dhahabu mpaka kwenye pesa, kutoka hapo unaweza kuipata pesa yako popote ulimwenguni. Mshirika wa Ewan si mwingine, bali ni bwana Alistair Mathias.
Mathias pia ni mfanyabiashara wa dhahabu, yeye ni mtaalamu wa mambo ya fedha, anayepanga mikakati ya kutakatisha fedha za wanasiasa mafisadi, amekuwa kwenye biashara hii kwa takribani miaka 14. Mathias anakubali dili la kutakatisha fedha za bwana Stanley kupitia connections zake alizokuwa nazo kwenye biashara hii Afrika, ambapo kwa mwezi huwa anatakatisha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 70 - 80. Mathias pamoja na watu wengine waliokuwa kwenye biashara hii kama vile bwana Patni wanafanya biashara kwenye nchi nyingi Afrika kama vile Zimbabwe, Ghana, Zambia, Angola, Afrika Kusini, Mozambique, Malawi, DRC Congo, Uganda, Kenya, Tanzania, yaani mtandao ni mkubwa.
Patni pia anafanyakazi kutoka Dubai. Dubai ni kama makao makuu ya biashara na huduma za kifedha kwa Waafrika, hakuna kodi za ajabu ajabu, huna haja ya kuwa na nyaraka zote, ni rahisi kufanya mambo yao. Hawa mabwana huko Dubai wana sehemu yao kwenye uwanja wa ndege wa Dubai ya kuhakikisha leseni zao za kusafirisha dhahabu hazisumbuliwi, wana idhini ya Benki Kuu ya Dubai, wana vyeti vya ukaguzi wa kutakatisha pesa, yaani wamejipanga kwelikweli kuhakikisha biashara zao haramu hazikwami. Ili kukuhakishia mchakato huu uko salama na uelewe zaidi, unapelekwa kabisa katika ofisi zao Dubai uone jinsi mambo yanavyofanyika, ukitoka hapo wewe mwenyewe unakubali hawa watu wamejipanga kwenye hili.
Patni akionesha mchakato wa kubadili dhahabu kwenda kwenye pesa unavyofanyika
Je, ilikuaje mpaka Benki Kuu ya Zimbabwe ikaanza kufanya kazi na akina Patni? Tukutane kwenye muendelezo...
Muendelezo soma -
Episode 1 - Sehemu ya 4