Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Episode 1 - Sehemu ya 6

SimonRudland.jpg

Simon Rudland

Simon anaendesha genge lake la uhalifu kupitia kampuni yake ya Gold Leaf Tobacco, na anajulikana kama "The Boss." Rudland anauza dhahabu zaidi kuliko MacMillan na Patni na ana dili jingine tofauti na serikali, ana connection na viongozi wa utawala wa Zimbabwe. Washirika wake wa biashara ni pamoja na Jenerali Mstaafu Stanford Madala Khumalo, aliyekuwa Waziri wa Nishati aliyewekewa vikwazo Michael Reuben Nyambuya, na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Sibusiso Moyo. Waziri wa zamani wa Madini, Obert Mpofu, alinunua kampuni kutoka kwa Rudland kwa zaidi ya dola laki nane.

Screenshot 2023-07-02 021926.png

Nyaraka zikionesha mauziano ya kampuni yaliyofanywa na Obert Mpofu na Rudland

Watu wa undercover wa Aljazeera wanakutana na Moses Nango, mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Harare anayetoa ushirikiano wa kuwasiadia kusafirisha dhahabu kwa siri akiwa hajui kwamba hao wapo kazini kufichua dili zao chafu zinazowaweka mjini.

Screenshot 2023-07-02 010218.png

Moses Nango

Bwana Moses akaanza kwa kujitapa kwanza, bwana Simon Rudland yule namjua kwa 100% yeye na dili zake, na aliondoka juzi tu hapa kwa ndege binafsi. Moses amekuwa akifanya kazi katika uwanja wa ndege kwa miaka 23 na amekuwa akisaidia watu kuhamisha dhahabu, pesa, na almasi kwa magendo. Moses anatoa mchongo wote jinsi Rudland na genge lake la kampuni ya Gold Leaf wanavyoshinda vikwazo walivyowekewe Zimbambwe kwa niaba ya Benki Kuu.

Rudland ana mkataba na Fedility wa kuhamisha au kusafirisha dhahabu kutoka Zimbabwe mpaka Dubai. Anapopewa dhahabu anakuwa na watu wake maalumu wa kusafirisha dhahabu hiyo kutoka Zimbambwe mpaka Dubai, watu hawa ambao wote ni wazungu wanaweza kuwa 3 au 5 kutokana na ukubwa wa mzigo wenyewe kwa wakati huo, na inapotokea dhahabu zinazotakiwa kusafirishwa ni nyingi, kwa wakati mmoja kwenye ndege wanaweza kuwa hata wasafirishaji 3. Wakiwa tayari kwa safari wanapata ulinzi mpaka uwanja wa ndege.

Wanapofika kwenye sehemu ya ukaguzi, mizigo yao haikaguliwi. Ndege wanayotumia ni ya Emirates EK714 kutoka Zimbabwe na ndio ndege hii hii wanarudi nayo wakishakabidhi dhahabu. Hawa jamaa wanakula bata, madaraja wanayosafiria ni yale ya juu tu, ni business au first class. Biashara hii kwa Rudland ni kama chai tu sababu tayari ana wateja wa nguvu Dubai, yaani biashara yake iko vyede.

Wasafirishaji hawa wakifika Dubai, tayari kunakuwa na mtu anayewasubiria na pesa, kwahiyo wenyewe wakitoa dhahabu wanapewa pesa na kugeuza na ndege ile ile waliyokuja nayo ya EK713 kurudi Zimbabwe. Al-Jazeera inawapata watu hawa wanaosafirisha dhababu uwanja wa ndege. Hapo chini utaona picha zao na idadi ya safari walizofanya kwa kipindi cha miezi 2.

1. Patrick Keith
Screenshot 2023-07-02 012439.png

Screenshot 2023-07-02 012615.png

Rekodi za safari zinaonyesha Patrick Keith amesafiri mara 13 katika kipindi cha miezi 2.

2. Talmage George Alexander
Screenshot 2023-07-02 012807.png

Screenshot 2023-07-02 030214.png

Talmage George Alexander anaonekana kwenye camera pia akiwa na shati la safiii la drafti, yeye rekodi zinaonesha amesafiri mara 7 kwenda Dubai katika kipindi hicho hicho.

3. Terrance Ian Keith
Screenshot 2023-07-02 013458.png

Screenshot 2023-07-02 013720.png

Terrance Ian Keith nae jina lake linaonekana kwenye orodha, ikionesha amesafiri mara 9 katika kipindi hicho cha miezi 2.

4. Johannes Swan Sr na mwanae Johannes Swan Jr
Screenshot 2023-07-02 014035.png
Screenshot 2023-07-02 014211.png

Screenshot 2023-07-02 014234.png

Maafisa wa uwanja wa ndege Harare, wanamkaribisha Bwana Johannes Swan Sr na mwanae Johannes Swan Jr, wanaonekana wakiwasili kwenye uwanga wa ndege Harare kutokea Dubai, hawa rekodi zinaonesha wamesafiri mara 10

5. Peter Bowen
Screenshot 2023-07-02 014651.png

Screenshot 2023-07-02 014748.png

Pia kuna Peter Bowen, huyu jamaa anasafiri mara 10 katika kipindi kilekile cha miezi 2. Al- Jazeera inapata hati kutoka Benki Kuu iliyomruhusu Peter Bowen kusafirisha zaidi ya Kg 66 za dhahabu kutoka Zimbabwe kwenda Dubai.

Screenshot 2023-07-02 014831.png

Hati kutoka Benki Kuu iliyomruhusu Peter Bowen kusafirisha ya Kg 66.817 za dhahabu​

Bowen anapiga zake misele akiwa hajui kama anafatiliwa. Jamaa anawasili Dubai saa 6:40 asubuhi, anakabidhi dhahabu na kusubiri katika sehemu ya mapumziko ya uwanja wa ndege. Masaa machache baada ya kuwasili, tayari amerudi kwenye ndege! Yaani ni bandika bandua. Wasafirisha dhahabu hawa wanapofika Harare, wanatoka nje kupitia mlango wa watu wanaowasili, wanakabidhi pesa, wanachukua mzigo mwingine wa dhahabu na kupanda tena kwenye ndege ileile kwenda Dubai tena, mzunguko unakuwa huo huo mpaka wamalize kazi kwa siku husika.

Screenshot 2023-07-02 015301.png

Bowen akiwa katika sehemu ya mapumziko ya uwanja wa ndege akisubiri kupanda ndege kurudi Zimbabwe baada ya kukabidhi dhahabu

Wabeba dhahabu wa Rudland wanapata pesa kwaajili ya viongozi wa Zimbabwe zinazowasadia kuruka vikwazo walivyowekewa na nchi za Magharibi, dhahabu inayotolewa Fideliity inaenda kuuzwa kwa kampuni ya Dubai inayoitwa Aulion Global Trading.

Screenshot 2023-07-02 015818.png

Kampuni ya Aulion Global Trading ambako dhahabu zinaenda kuuzwa

Aulion pia ni sehemu ya himaya ya biashara za Rudland, inapokea mamilioni ya dola kutoka akaunti za kampuni ya Rudland, Gold Leaf Tobacco.

Screenshot 2023-07-02 020140.png

Nyaraka ya benki inayoonesha kampuni ya Aulion ikipokea hela kutoka Gold Leaf Tobacco

Kutokana na kuwa serikali ya Zimbabwe imefilisika na hawana fedha za kununulia dhahabu, Rudland anapata upenyo wa kusogeza pua yake, anatoa mkopo kwa serikali unaouwezesha serikali kununua dhahabu. Dhahabu ambayo ni huyu huyu Rudland ndio anakuwa boss ama kinara wa kwenda kuiuza Dubai! Kila mara Rudland anakuwa anawapa serikali mkopo wa dola milioni 200 mpaka 250 za kununulia dhahabu.

Screenshot 2023-07-02 020412.png

Advance/mkopo wanaopewa serikali kwaajili ya kununulia dhahabu
Kutokana na biashara hii ya kuza dhahabu kwa magendo, Zimbabwe inakadiriwa kupoteza takribani dola bilioni 7, huku bwana Rudland akiwa ni kitovu cha upotevu huo.

Wakuu, tukutane wakati mwingine kwaajili ya muendelezo.

Muendelezo soma - Episode 1 - Sehemu ya 7 (Mwisho wa Episode ya 1)
 
Episode 1 - Sehemu ya 6

View attachment 2675506
Simon Rudland

Simon anaendesha genge lake la uhalifu kupitia kampuni yake ya Gold Leaf Tobacco, na anajulikana kama "The Boss." Rudland anauza dhahabu zaidi kuliko MacMillan na Patni na ana dili jingine tofauti na serikali, ana connection na viongozi wa utawala wa Zimbabwe. Washirika wake wa biashara ni pamoja na Jenerali Mstaafu Stanford Madala Khumalo, aliyekuwa Waziri wa Nishati aliyewekewa vikwazo Michael Reuben Nyambuya, na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Sibusiso Moyo. Waziri wa zamani wa Madini, Obert Mpofu, alinunua kampuni kutoka kwa Rudland kwa zaidi ya dola laki nane.

View attachment 2675565
Nyaraka zikionesha mauziano ya kampuni yaliyofanywa na Obert Mpofu na Rudland

Watu wa undercover wa Aljazeera wanakutana na Moses Nango, mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Harare anayetoa ushirikiano wa kuwasiadia kusafirisha dhahabu kwa siri akiwa hajui kwamba hao wapo kazini kufichua dili zao chafu zinazowaweka mjini.

Bwana Moses akaanza kwa kujitapa kwanza, bwana Simon Rudland yule namjua kwa 100% yeye na dili zake, na aliondoka juzi tu hapa kwa ndege binafsi. Moses amekuwa akifanya kazi katika uwanja wa ndege kwa miaka 23 na amekuwa akisaidia watu kuhamisha dhahabu, pesa, na almasi kwa magendo. Moses anatoa mchongo wote jinsi Rudland na genge lake la kampuni ya Gold Leaf wanavyoshinda vikwazo walivyowekewe Zimbambwe kwa niaba ya Benki Kuu.

Rudland ana mkataba na Fedility wa kuhamisha au kusafirisha dhahabu kutoka Zimbabwe mpaka Dubai. Anapopewa dhahabu anakuwa na watu wake maalumu wa kusafirisha dhahabu hiyo kutoka Zimbambwe mpaka Dubai, watu hawa ambao wote ni wazungu wanaweza kuwa 3 au 5 kutokana na ukubwa wa mzigo wenyewe kwa wakati huo, na inapotokea dhahabu zinazotakiwa kusafirishwa ni nyingi, kwa wakati mmoja kwenye ndege wanaweza kuwa hata wasafirishaji 3. Wakiwa tayari kwa safari wanapata ulinzi mpaka uwanja wa ndege.

Wanapofika kwenye sehemu ya ukaguzi, mizigo yao haikaguliwi. Ndege wanayotumia ni ya Emirates EK714 kutoka Zimbabwe na ndio ndege hii hii wanarudi nayo wakishakabidhi dhahabu. Hawa jamaa wanakula bata, madaraja wanayosafiria ni yale ya juu tu, ni business au first class. Biashara hii kwa Rudland ni kama chai tu sababu tayari ana wateja wa nguvu Dubai, yaani biashara yake iko vyede.

Wasafirishaji hawa wakifika Dubai, tayari kunakuwa na mtu anayewasubiria na pesa, kwahiyo wenyewe wakitoa dhahabu wanapewa pesa na kugeuza na ndege ile ile waliyokuja nayo ya EK713 kurudi Zimbabwe. Al-Jazeera inawapata watu hawa wanaosafirisha dhababu uwanja wa ndege. Hapo chini utaona picha zao na idadi ya safari walizofanya kwa kipindi cha miezi 2.

1. Patrick Keith
View attachment 2675568

View attachment 2675569
Rekodi za safari zinaonyesha Patrick Keith amesafiri mara 13 katika kipindi cha miezi 2.

2. Talmage George Alexander
View attachment 2675570

View attachment 2675571
Talmage George Alexander anaonekana kwenye camera pia akiwa na shati la safiii la drafti, yeye rekodi zinaonesha amesafiri mara 7 kwenda Dubai katika kipindi hicho hicho.

3. Terrance Ian Keith
View attachment 2675572

View attachment 2675573
Terrance Ian Keith nae jina lake linaonekana kwenye orodha, ikionesha amesafiri mara 9 katika kipindi hicho cha miezi 2.

4. Johannes Swan Sr na mwanae Johannes Swan Jr
View attachment 2675574View attachment 2675576

View attachment 2675578

Maafisa wa uwanja wa ndege Harare, wanamkaribisha Bwana Johannes Swan Sr na mwanae Johannes Swan Jr, wanaonekana wakiwasili kwenye uwanga wa ndege Harare kutokea Dubai, hawa rekodi zinaonesha wamesafiri mara 10

5. Peter Bowen
View attachment 2675580
View attachment 2675581

Pia kuna Peter Bowen, huyu jamaa anasafiri mara 10 katika kipindi kilekile cha miezi 2. Al- Jazeera inapata hati kutoka Benki Kuu iliyomruhusu Peter Bowen kusafirisha zaidi ya Kg 66 za dhahabu kutoka Zimbabwe kwenda Dubai.

View attachment 2675582
Hati kutoka Benki Kuu iliyomruhusu Peter Bowen kusafirisha ya Kg 66.817 za dhahabu​

Bowen anapiga zake misele akiwa hajui kama anafatiliwa. Jamaa anawasili Dubai saa 6:40 asubuhi, anakabidhi dhahabu na kusubiri katika sehemu ya mapumziko ya uwanja wa ndege. Masaa machache baada ya kuwasili, tayari amerudi kwenye ndege! Yaani ni bandika bandua. Wasafirisha dhahabu hawa wanapofika Harare, wanatoka nje kupitia mlango wa watu wanaowasili, wanakabidhi pesa, wanachukua mzigo mwingine wa dhahabu na kupanda tena kwenye ndege ileile kwenda Dubai tena, mzunguko unakuwa huo huo mpaka wamalize kazi kwa siku husika.

View attachment 2675583
Bowen akiwa katika sehemu ya mapumziko ya uwanja wa ndege akisubiri kupanda ndege kurudi Zimbabwe baada ya kukabidhi dhahabu

Wabeba dhahabu wa Rudland wanapata pesa kwaajili ya viongozi wa Zimbabwe zinazowasadia kuruka vikwazo walivyowekewa na nchi za Magharibi, dhahabu inayotolewa Fideliity inaenda kuuzwa kwa kampuni ya Dubai inayoitwa Aulion Global Trading.

View attachment 2675591
Kampuni ya Aulion Global Trading ambako dhahabu zinaenda kuuzwa

Aulion pia ni sehemu ya himaya ya biashara za Rudland, inapokea mamilioni ya dola kutoka akaunti za kampuni ya Rudland, Gold Leaf Tobacco.

View attachment 2675595
Nyaraka ya benki inayoonesha kampuni ya Aulion ikipokea hela kutoka Gold Leaf Tobacco

Kutokana na kuwa serikali ya Zimbabwe imefilisika na hawana fedha za kununulia dhahabu, Rudland anapata upenyo wa kusogeza pua yake, anatoa mkopo kwa serikali unaouwezesha serikali kununua dhahabu. Dhahabu ambayo ni huyu huyu Rudland ndio anakuwa boss ama kinara wa kwenda kuiuza Dubai! Kila mara Rudland anakuwa anawapa serikali mkopo wa dola milioni 200 mpaka 250 za kununulia dhahabu.

View attachment 2675601
Advance/mkopo wanaopewa serikali kwaajili ya kununulia dhahabu
Kutokana na biashara hii ya kuza dhahabu kwa magendo, Zimbabwe inakadiriwa kupoteza takribani dola bilioni 7, huku bwana Rudland akiwa ni kitovu cha upotevu huo.

Wakuu, tukutane wakati mwingine kwaajili ya muendelezo.
Kutokana na biashara hii ya kuza dhahabu kwa magendo, Zimbabwe inakadiriwa kupoteza takribani dola bilioni 7, huku bwana Rudland akiwa ni kitovu cha upotevu huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waandishi wa habari undercover wanajifanya kuwa majambazi wenye dola bilioni moja za pesa chafu zinazohitaji kusafishwa. Wanapata upenyo kwa wanachama wa Afrika wa Gold Mafia na kurekodi mikutano ya siri na viongozi wa uhalifu.

Balozi Mkubwa wa Afrika anatoa huduma ya kutakatisha pesa chafu zenye thamani ya dola milioni 1.2 kwa kutumia kofia yake ya Udiplomasia.

Wenyewe wanakwambia kwa Afrika ilimradi unatotoa chochote kitu basi mambo yako yanaenda bila shida yoyote. Gold Mafia imesambaa, hakuna mamlaka au serikali yoyote Afrika inayojaribu kusogeza pua yake.

Wahalifu hutoa donge nono kutakatisha zaidi ya dola milioni 100 kupitia miradi ya serikali ya usafirishaji wa dhahabu. Kitovu cha shughuli zao ni kituo kikubwa cha kutakatisha pesa kusini mwa Afrika, Benki Kuu ya Zimbabwe.

Gold Maafia, ni mfululizo wa sehemu nne wa kitengo cha uchunguzi cha Al Jazeera, unaoangalia jinsi tamaa ya jamii kumiliki dhahabu wanavyoendeleza na kuunga mkono uchumi haramu ulimwenguni. Timu ya siri inafanikiwa kuingia kwenye makundi hasimu ambayo hubadilisha pesa chafu kuwa dhahabu, ambayo baadae inauzwa ulimwenguni kote.

Kupitia maelfu ya nyaraka za siri na mahojiano ya moja kwa moja na whistleblowers kutoka ndani ya makundi vya uhalifu, wachunguzi wanapata muundo wa operesheni za utakatishaji wa pesa zenye thamani ya mabilioni ya pesa ambazo huudumia viongozi wa kisiasa, uchunguzi huo unatupeleka kwenye ofisi za juu Kusini mwa Afrika.

Unadhani viongozi gani wanajihusisha na biashara hii haramu Afrika Kusini, vipi nchi nyingine, je, na Tanzania kuna viongozi wanaojihusisha na biashara hiyo?

Itaendelea...

Kuanza nayo soma Episode 1 - Sehemu ya 1
Duuh noma
 
Mleta mada kwenye hiyo.documentaey sijaona Mwizi au aliyeibiwa hata mmoja kama yupo tuambie wewe Kamwibia nani kwenye hicho kinaitwa Gold Mafia? Rudia tena kuiangalia mimi binafsi sijaona aliyeibiwa hapo nani Tusaidie wewe kwenye hiyo Gold Mafia Documentary nani kaibiwa chochote kwa wahusika wote Sababu hakuna Mlalamikaji kwenye hiyo Documentary sio serikali ya Dubai wala ya Zimbabwe wala wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa dhahabu.Kila mmoja kalipwa chake kwenye chain .

Aljazeera hopeless kabisa.Kwa hiyo Aljazeera ndie Mlalamikaji au?
 
Punguza jazba mkuu!!
Mimi na baadhi hatujaona hiyo documentary...
 
Mleta mada kwenye hiyo.documentaey sijaona Mwizi au aliyeibiwa hata mmoja kama yupo tuambie wewe Kamwibia nani kwenye hicho kinaitwa Gold Mafia? Rudia tena kuiangalia mimi binafsi sijaona aliyeibiwa hapo nani Tusaidie wewe kwenye hiyo Gold Mafia Documentary nani kaibiwa chochote kwa wahusika wote Sababu hakuna Mlalamikaji kwenye hiyo Documentary sio serikali ya Dubai wala ya Zimbabwe wala wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa dhahabu.Kila mmoja kalipwa chake kwenye chain .

Aljazeera hopeless kabisa.Kwa hiyo Aljazeera ndie Mlalamikaji au?
Ipi definition yako ya 'kuibiwa' tuanzie hapo....

Anaetumia mali ya umma kwa manufaa yake ni mwizi usifukie mashimo... Na mifano kwa waliolalamika...part ya Kenya umepitia? Hujaona chochote kuhusu hilo? Waziri wa Fedha Zimbabwe kuongelea magendo yanayofanywa kutorosha dhahabu hiyo ambayo ingetumiwa accordingly kwa manufaa ya nchi ingewasogeza pakubwa...unaona ninsawa kwakuwa kila mtu "Anapewa chake"?
 
Back
Top Bottom