Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Episode 1 - Sehemu ya 7 (Mwisho wa Episode ya 1)

Pattni nae ana vijana wake special wanaofanya kazi ya kusafirisha dhahabu kwenda Dubai na kurudi na pesa Zimbabwe. Ripota Undercover anafanikiwa kukutana na mmoja wa vijana hawa. Mwamba huyu anaitwa Dmytro Abakumov.

Screenshot 2023-07-05 220838.png

Dmytro Abakumov

Mbali na Abakumov kufanya kazi hiyo ya kuwa msafirishaji wa Bwana Pattni, Abakumov pia ni Mkurugenzi katika moja ya kampuni za Pattni ambayo ipo Zimbabwe. Kamera ya Al-Jazeera haikumuacha salama, inamdaka jamaa akiwa katika majukumu yake ya magendo Uwanja wa Ndege wa Harare, Zimbabwe.

Screenshot 2023-07-05 221510.png

Abakumov akiwa amenaswa na kamera ya Al-Jazeera uwanja wa ndege wa Harare

Ili waweze kufanya biashara zao bila shida, lazima wawe na nyaraka sahihi kwa ajili ya biahsara hiyo. Bwana Pattni bila kujua kama ananaswa na kamera, anaonyesha barua kutoka Fidelity Printers kwenda Dubai inayotaja majina ya Abakumovu na ndugugu yake Pattni, Mishaal Pattni inayoidhinisha kampuni ya Pattni inayoitwa Susan General Trading kubeba dola za Kimarekani milioni 3 kila wiki kuingia Zimbabwe

Screenshot 2023-07-05 221719.png
Barua kutoka Fidelity Printers kwenda Dubai inayowataja Abakumovu na Mishaal Pattni kuidhinisha kampuni ya Susan General Trading kubeba dola za Kimarekani milioni 3 kila wiki kuingia Zimbabwe

Benki Kuu inatangaza kuwa biashara/kampuni ya Susan's jewelry and gold exports ndio inayoongoza kwa kuingiza dola za Marekani nchini. Kampuni hii ya Susan imejiimarisha na kukuza network yake iliyipa nguvu kifedha na kuzalisha dola za Kimarekanani milioni 168 kwa mwaka 2020. Biashara ya Susan inachukuliwa kuwa ni yenye thamani kubwa katika kuzalisha fedha taslimu kwaajili Zimbabwe, mpaka serikali imeamua kuwalipa bonasi ya thamani ya 18% ya mauzo yake. Lakini nyaraka zilizopatikana kutoka kitengo cha Al-Jazeera zinaonyesha kuwa yote ni sehemu ya himaya ya Pattni kwenye biashara zake chafu za dhahabu.

Screenshot 2023-07-05 224110.png

Benki Kuu inatangaza kampuni ya Susan's jewelry and gold exports kuwa kinara wa kuingiza dola za Marekani nchini

Screenshot 2023-07-05 224517.png

Barua inayoonesha serikali kupitisha bonasi ya thamani ya 18% ya mauzo yake kwa Suzan General Trading

Al-Jazeera walitafuta wahasabu wa zamani wa Pattni kupata taarifa zaidi na kufanikiwa kuwapata baadhi. Muhasibu Sami (utambulisho wake halisi umefichwa), akaeleza jinsi Pattni alivyokuwa akifanya kazi, akisema kuwa Pattni anauza vito na dhahabu nchini Dubai na sehemu nyingine za dunia, ambapo yeye anapaswa kupeleka fedha za kigeni Zimbabwe. Wakati hao wabeba/wasafirisha dhahabu wakifika uwanja wa ndege wa Harare baada ya safari zao za Dubai, walitakiwa kusema pesa walizorejesha Zimbabwe kwa kutumia Fomu 47 ambayo kwa kawaida huitwwa Fomu ya Bluu. Akaendelea kusema kuwa wakati mawakala wao/wasafirisha dhahabu wakitaja kiasi cha fedha walizorejesha huwa hawasemi kweli, wanadanganya! Wakati mwingine hupeleka dola elfu 50 au laki moja lakini kwenye kujaza fomu/kutaja kiasi walichopeleka huandika milioni 1 au 2.

Pattni mwenyewe siku moja anarekodiwa katika Fomu ya Bluu akiwa anarejesha pesa Zimbabwe. Pattni akajaza kuwa amepeleka dola milioni 1.2, pesa zilizopatikana baada ya kuuza vito Dubai. Lakini Patni hakupelea pesa hizo dola milioni 1.2 badala yake alipeleka hela ambayo haifiki hata dola laki moja. Pattni na wenzake wanaweza kufanikisha hilo kwa kuhonga wafanyakazi wa uhamiaji na kuwaambiwa waandike kiasi wanachotaka.

Screenshot 2023-07-05 232529.png

Fomu ya Bluu iliyorekodi pesa alizoingia nazo Pattni Zimbwabwe

Wakati mhasibu anarekodi kwenye vitabu vyake hakuandika dola milioni 1.2 badala yake aliandika pesa halisi bwana Patni aliyokuja nayo ambayo ilikuwa haifiki data dola laki moja.

Screenshot 2023-07-06 001926.png
Screenshot 2023-07-06 002046.png

Kitabu kikionesha kiasi halisi cha pesa alichoingianacho Bwana Patni

Screenshot 2023-07-06 080752.png

Patni akionesha Fomu ya Bluu ambayo wanasema kiasi cha fedha walichoingia nacho Harare kutoka mauzo ya dhahabu Dubai

Patni anaacha sehemu kubwa ya pesa za mauzo ya dhahabu Dubai, kutokana na hili sasa Bwana Pattni anakuwa hana hela za kutosha kununua dhahabu kwaajili ya roundi nyingine (kupeleka dhahabu Dubai kuuza na kurudisha fedha Zimbabwe). Ili kuendelea kuwa na leseni inayomsuhuru kwenda kuuza dhahabu nje ya nchi itabidi sasa anunue dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo, anafidia kiasi cha pesa ambacho hana kutoka kwenye soko la Hawala (si unaikumbuka hii, wale wanafirisha pesa bila pesa yenyewe kutembea?) wa Zimbabwe wanaotaka kutuma pesa Dubai. Kwahiyo hela anayoipata kwa hawa watu ndio anayotumia kununua dhahabu, huku Dubai wateja wake wa Hawala wanalipwa kutokana na mauzo ya dhahabu aliyoinunua Zimbabwe na mzunguko unakuwa huo huo kila wakati huku yeye akiweka mfukoni 18% yake. Pesa inayohitajika kwa udi na uvumba haingii kwenye uchumi wa Zimbabwe haifiki kama inavyotajariwa.

Screenshot 2023-07-06 082757.png

Fomu inayoonesha hela zilizopokelewa na Pattni kutoka soko la Hawala

Kutokana na anachofanya, Pattni anakuwa mafia mara mbili, kwenye hizo dili zake tayari ni mhalifu tayari lakini anaongezea na kuibia na serikali ambayo imemruhusu kufanya uhalifu wake! Anajifanya kuisaidia Zimbabwe kwa kupeleka fedha za kigeni zinazohitajika sana lakini anachopeleka ni kiduchu sana ambacho ni sawa sawa na 0. Hii tunaiitaje, mbwa kala mbwa au mbuzi kafia kwa muuza supu?

Sasa hapa kila mtu amaeshaonesha uwezo wake wa kukamilisha kazi ya Bwana Stanley (kutakatisha pesa zake kutoka china), washajiuza vya kutosha na kutoa ramani yote ya jinsi mchongo unavyofanyika na mambo yatakavyoenda vizuri bila wasiwasi, sasa ni muda wa kutamba kujionesha kwamba wewe ni zaidi ya genge fulani. Nabii Angel anatamba mbele ya ripota wa undercover, anasema bwana we mimi sio mjinga, nina degree mbili za uchumi, kwahiyo ninajua vizuri nini nafanya, anasema jamani mi siongei sana CV yangu inajieleza; mbali na degree zangu mbili niliingia pia kwenye orodha ya matajiri ya Forbes kwa Afrika mwaka 2013, lakini pia ni Waziri wa Injili.

Screenshot 2023-07-07 010233.png

Nabii Angel akitamba kuonesha nguvu alizonazo akiwa na chawa (wasaidizi) wake
Stanley anamwambia Nabii Angel hapa tumesomana vizuri, mimi ntaleta mtaji ambao ni pesa Taslimu, nataka kuwekeza hela zangu hapa, chawa wa Bwana Stanley akaongezea maneno kumuelezea tajiri, akasema anachomaanisha bosi wangu hapa ni kuwa hela zote alizokuwanazo haziwezi kuchukuliwa/kukubaliwa au kutumika huko tulikotoka kwahivyo inabidi mzigo wote uingie kwenye uwekezaji ili tuweze kupata pesa safi na hatutaki tuje tuingie kwenye matatizo yoyote.

Nabii Angel na chawa wake wanajibu, jamani msiwe na shaka, tumeshaongea kuhusu hilo, mmeshuhudia wenyewe simu kadhaa zikipigwa kwa watu wa nguvu, yaani mambo yameshawekwa sawa, tunasubiri nyinyi tu mtie mzigo tufanye biashara, halafu Nabii Angel akauliza, kwani mnataka kuwekeza mpunga kiasi gani?

Bwana Stanley akajibu kwa kuanzia nataka niwekeze kama dola bilioni moja hivi, Nabii akajibu okaaaay (hapo anaona ameulmba), kisha anamjibu Bwana Stanley kuwa, sisi tumewahi kufanya biashara za dola milioni 200 au 300 lakini hatujawahi kufanya kwa kiasi kikubwa hivyo kama bilioni 1.

Angel na msaidizi wake wanamchukua Bwana Stanley pembeni, na kumwambia bwana sikia, mimi ndio mtu wa pili mwenye nguvu kimamlaka Zimbabwe, unajua naweza kumuweka huyu chawa wangu (akionesha upande wa msaidizi wake) kwenye mfuko na hakuna mtu ataruhusiwa kugusa wala kukagua mzigo wangu? Unajua naweza kuweka kwenye mkoba wangu dola bilioni 1.2 kwenye mkoba wangu nikazungushia utepe mwekundu wa kibalozi na kazi imeisha? Nabii Angel anajitamba jinsi anavyoweza kutumia kofia yake ya ubalozi kupiga dili zake chafu bila shida yoyote. Anamwambia Bwana Stanley usiwe na wasiwasi wowote kwani kofia ya ubalozi itaingiza hizo hela Zimbabwe fasta tu, kama nakunywa maji vile, mzigo utafika Zimbabwe hakuna mtu ataugusa mpaka utafika nyumbani kwangu (kwa Nabii Angel).

***​

Uchunguzi kwa Episode ya 1 ukaishia hapa, matokeo ya uchuguzi huu, yaani kila kilichorekodiwa mwanzo mpaka mwisho kilipelekwa/wasilishwa kwa kila aliyohusishwa/aliyeonekana katika Makala hii, na haya ndio yalikuwa majibu yao;

Simon Rudland ~ Alisema tuhuma zote kuhusu yeye ni uongo, ni kampeni zilizofanywa dhidi yake na watu wasiojulikana kumchafua, akajielezea yeye kama mfanyabiashara imara, mwenye nguvu, anaejiweza, anaepambana na watu wenye tamaa na wivu

Gold Leaf Tobbaco ~ Walikanusha kuhusika kwao katika Sakata hili kwa nguvu zote kwenye chochote kilichofanyika kipindi cha nyuma ama sasa kuhusisha shughuli za utakatishaji fedha, biashara ya magendo ya dhahabu ama chochote kinachoendana na hayo.

Fidelity Printers and Refiners ~ Walikanusha kuwa na uhusiano wowote wa kibiashara na Bwana Simon Rudland au kumpa leseni ama kutoa upendeleo au motisha kwa yeyote aliyetajwa kwenye Makala hii. Pia Fidelity ikakanusha kuhusika kwa vyovyote vile kwenye shughuli za utakatishaji pesa, biashara za magendo au majaribio ya kukwepa/kuvunja vikwazo walivyowekewa na chi za Magharibi kupitia mlango wa nyuma.

Benki Kuu ya Zimbabwe ~ Iliwaambia Al-Jazeera kuwa inachukulia vitendo vya utakatishaji pesa na shughuli zote za biashara haramu/magendo kwa uzito mkubwa sana na kwa vyovyote vile iwe moja kwa moja wao au kupitia mtu/taasisi nyingine haiwezi kujihusisha na shughuli hizo.

Alistair Mathias ~ Alikanusha kutengeza mpango wa kutakatisha pesa na kusema hajawahi kutakatisha pesa au kufanya biashara ya dhahabu kwa magendo kwa Warusi ama kwa mtu yoyote yule, na kuongeza kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wowote wa kibiashara na Bwana Ewan MacMillan.

Kamlesh Pattni ~ Amekanusha kufanya uhalifu wowote Kenya na kusisitiza kuwa hajawahi kukutwa na hatia kuhusiana na shughuli alizokuwa anafanya Kenya. Pia alikanusha uhusika wake kwenye utakatishaji pesa wala kuisaidia Zimbabwe kukwepa vikwazo walivyowekewa na chi za magharibi, alikanusha pia kuwahi kuajiri mtu yoyote kuingiza pesa kimagendo au kujitolea kushughulikia pesa ambazo anajua zimetokana na shughuli za uhalifu, na kwamba alipokutana na wachunguzi wa Al-Jazeera alidhani amekutana na mwekezaji aliyetaka kuuza sehemu ya biashara ya hoteli na ambaye alitaka “Kujiondoa katika mfuko wa uwekezaji nchini China ili kuwekeza katika kununua dhahabu na uchimbaji madini nchini Zimbabwe”.

Suzan General Trading ~ Walisema kwamba shughuli zao ni halali na zilizingatia sheria katika kila hali.

Dmytro Abakumov ~ Alikanusha kuajiriwa na Bwana Pattni au kujihusiha na vitendo vyovyote vya kiuhalifu, ama kupitia yeye mwenyewe au kampuni yake ya Skorus Investiments, na kwamba kila kitu yeye na kampuni yake ilifanya ilikuwa katika utekelezaji kamili wa masharti ya leseni yake na sheria zote zinazotumika.

Mishaal Pattni ~ Ndugu wa Bwana Kamlesh Pattni aliyetajwa kwenye barua kutoka Fidelity kwenda Uhamiaji Dubai pia alikanusha kuhusika na chochote na kuwaambia Al-Jazeera kuwa hajasafiri kwenda Zimbabwe toka mwaka 2017.

Aurex Jewellery ~ Walisema hawakuwa na ufahamu juu ya shughuli za utakatishaji fedha za Bwana Kamlesh Pattni wala Ewan MacMillan au kuhusu hatia (vifungo gerezani) za MacMillan kwenye usafirishaji haramu wa dhahabu na kwamba yenyewe inatoa huduma zake za utengenezaji wa mapambo ya vito kwa kampuni mbalimbali zilizosajiliwa kwenye eneo hilo baada ya kufanya uchunguzi na kufuata taratibu zote zinazostahili.

Watu/Pande nyingine zilizohusiswa kwenye Makala hii ~ Hawakujibu chochote.

Pale ambapo mtu anakuonesha vithibitisho vyote lakini unakomaa kuwa sio wewe ila ni mkono wa baunsa😂😂😂.

Katika Episode ya 2 ya Gold Mafia Simon Rudland anatafuta mtakajishaji pesa, na anamapata. Je ni nani huyo? Upande mwingine mkutano wa Bwana Stanley na Rais Manangagwa unakuja na gharama kubwa… Tukutane wakati mwingine wakuu kwa muendelezo wa makala hii.

Muendelezo Soma - Episode 2 - Sehemu ya 1
 
Gold Mafia imenifumbua sana macho nikagundua Kuna mambo mengi sana yanafanywa na hawa wanaojiita viongozi, ila kwasababu waandishi wa habari wa bongo ni ma mbumbumbu wanaoendekeza uchawa hatuwezi kuyajua.
Kumbe hawagusiki ila sasa mie nitawawagusa pamoja na pesa zao , pesa zao hazitauza bandari za Tanganyika kamwe ,

Nimeona mtu mmoja akimtisha mwanasheria wa Mbeya ,mfikishie ujumbe akiendelea atakufa mdomo wazi asema Bwana , na sio maneno yangu na ujumbe ukawafikie wanafiki wote ,na wahusika kwa jambo ili ,watakufa midomo wazi
 
Episode 2 - Sehemu ya 1

Sehemu ya pili inaanza, bwana Stanley akiwa kwenye mazungumzo na mshirika wa Nabii Angel, huyu ni Bwana Rikki Doolan, ambapo kwenye makala hii yeye ni mmoja wa Mafia au tuseme Jambazi wa Kidiplomasia.

Screenshot 2023-07-13 211237.png

Rikki Doolan

Rikki Doolan anajulikana pia kama Mchungaji Rikki. Rikki anahubiri katika kanisa la kiinjili (Evengelical Church) Uingereza

Screenshot 2023-07-13 212107.png

Waumini wakifurahia mahubiri ya Mchungaji Rikki

Kabla hawajaanza kuongea mambo ya biashara Mchungaji Rikki anahakikisha hakuna mtu yoyote anasikiliza mazungumzo yao, anaita kiongozi wa masuala ya ulinzi na kuwaambia Bwana Stanley na wenzake kuwa wanatakiwa kukabidhi simu zao mpaka watakapomaliza mazungumzo yao.

Bwana Stanley kama kawaida anatupia mistari yake, bwana mimi nina mzigo wa kutosha kutoka china, lakini mzigo mchafu na nataka zote ziwe safi. Mchungaji Rikki anasema hamna tatizo, hiyo ni kazi ndogo sana, lakini anawatwanga swali, kwanini wameamua kupeleka pesa zao Afrika? Bwana Stanley anajibu bila kupepesa macho we si unajua hizi biashara zetu, tunaenda sehemu ambazo mamlaka hazitii nguvu sana. Mchungaji Rikki akamwabia kama ni hivyo, basi unahitaji watu hawa muhimu ili mambo yaweze kwenda vizuri. Watu hao ni Rais na Balozi Mkuu.

Mchungaji Rikki akawaambia akina Stanley kwamba tukiwa tunaonea hapa hakuna kutaja majina, tutatumia maneno ya code, neno Mkuu (akimaanisha Balozi Mkuu Nabii Angel) na Namba 1 (ikimaanisha Rais Manangagwa).

Screenshot 2023-07-13 214255.png

Nabii Angel na Mchungaji Rikki wakiwa pamoja kwenye mishe zao za kikanisa

Mchungaji Rikki anamwambia Stanley, nadhani unaijua Afrika vizuri, ukiwa unatoa chochote kitu mambo yanaenda bila shida, na ndio njia hiyo hiyo tutatumia kwa hii miamba miwili Namba 1 na Mkuu kufanya mambo yaende, yaani hawa wawili wakifurahi unafikiri kuna mtu mwingine wa kuuliza swali, Hakuna! Hii ni kwasababu hawa wawili ni kama wanaendesha kila kitu. Mchungaji akaendelea kujimwambafai, yaani mtapitia kwangu kuwafikia hawa, mimi kazi yangu ni kuhakikisha wao wanajua kila kinachoendelea, wenyewe watakuwa wanapitisha tu mambo yaendelee. Yaani mkifika airport mnasindikizwa na msafara, mnaingia nchini kama wawekezaji na kupata ulinzi ule wenyewe kutoka ngazi ya juu kabisa, hamtaingia nchini kama wahalifu wanaojaribu kuingia nchini kama wahalifu.

Mchungaji Rikki akaendelea kujimwaga, kila kitu mtakachofanya Namba 1 lazima aambiwe na kumwambia Bwana Stanley kwamba, kwenye hizi dili lazima kila mmoja afaaidike, na kwamba huo mchongo ni project ya Rushwaya (si unamkumbuka Henrietta Rushwaya, Rais wa Chama cha Wachimbaji na mpwa wa Rais Manangagwa, aliezea jinsi anavyotakatisha pesa chafu), ambapo mpango wa kutakatisha pesa za bwana Stanley itakuwa ni kuwekeza kwenye kununua vifaa kwaajili ya wachambaji wadogo, kurahisha kazi zao na malipo yake yataingia kama dhahabu. Baada ya kupata dhahabu wanaweza kuamua kuiacha Zimbabwe au wakasafirisha kwenda Dubai. Wote wanakubaliana njia hii ya kutakatisha pesa ni nzuri.

***​
Makala inatupeleka sehemu nyingine kwa mtu ambaye anakubali kumsaidia Bwana Stanley kwenye huu mchakato wa kutakatisha pesa, huyu ni Bwana Cleopas Chidodo. Chidodo ni Meneja wa masuala ya Ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Harare Zimbabwe, anafanyia kazi Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Zimbabwe, amekuwa kazini kwa takribani miaka 23 sasa, ampapo amekuwa akipanda cheo kidogo kidogo, mpaka kufikia kuwa Meneja.

Screenshot 2023-07-13 223747.png

Je, Chidodo atamsaidiaje Bwana Stanley? Tukutane wakati mwingine Wakuu.

Muendelezo soma
- Episode 2 - Sehemu ya 2
 
Episode 2 - Sehemu ya 2

Tuendelee tulipoishia kwa mzee wa mishe Chidodo.

Ukiwa na chochote cha magendo unataka kukitoa nje ya nchi kupitia uwanja wa Harare Bwana Chidodo ndio mtu wako, mwenyewe anasema lazima uniambie mimi kwa chochote unachotaka kukitoa nje nchi, hii inasaidia pia kupanga na gharama inayohitajika kukamilisha jambo lako. Kwa mfano ikiwa mtu anataka kuvusha pesa, lazima ajue unataka kutoka na kiasi gani, ambapo kwenye suala la kupitisha pesa unachajiwa 5% ya kile unachotaka kupitisha, lakini kama unavusha madini kama vile dhahabu, almasi bei inakuwa imechangamka.

Screenshot 2023-07-17 201940.png

Bwana Chidodo akiwa anaeleza jinsi anavyofanya biashara

Bwana Stanley anamuleza Chidodo kuwa yeye anataka kusafirisha dhahabu kupitia uwanja wa ndege, dhahabu zilizopatikana baada ya pesa zake chafu kutakatishwa. Bwana Chidodo akasema hamna tatizo, mimi ntadili na yeyote utakaemuajiri kusafirisha dhahabu hizi, kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri. Jamaa anaesafirisha dhahabu akifika uwanja wa ndege atatakiwa kumtafuta bwana Chidodo kumjulisha kuwa amefika kwa kumtumia ujumbe, na wakati mwingine bwana Chidodo anaweza kuwa kwenye chumba cha kamera, atamuuliza jamaa alivyovaa na kupata taarifa zote za mtu yule anavyoonekana, kwahivyo atamuona akiwa anapita kwenda sehemu ya ukaguzi.

Kwenye sehemu ya ukaguzi Chidodo ana mtu wake hapo ambae anamwambia; mtu wangu atapitisha mzigo wake hapa, utapata kiasi fulani, kwaiyo wewe ukiona kitu piga kimya kama vile hujaona chochote. Mzigo ukipita kutoka kwa jamaa wa ukaguzi, mtu wa Chidodo atamjulisha mzigo umepita ikiwa na mizigo mengine, Chidodo atamwambia aupakize kwenye ndege. Mzigo unapakiwa kwenye ndege kiurahisi kabisa, huku alieajiriwa na Bwana Stanley kusafiri na dhahabu anapita tu na kwenda zake kwenye ndege kama abiria wengine bila tatizo lolote.

Msafirishaji huyu anaitwa Aleck Yasini, ndiye anajitolea kufanya kazi ya kusafirisha dhahabu za Bwana Stanley, jamaa huyu anafanya kazi na Chidodo, wanajuana vizuri.

Screenshot 2023-07-17 204328.png

Aleck Yasini, msafirisha dhahabu za Bwana Stanley

Chidodo anasema jamaa yangu hana mbambamba, ukimpa kazi inaenda vizuri bila shida yoyote, ni Mzimbabwe na ana sura ya upole. Yasini nae anatia neno kwa Bwana Stanley, kwamba akifika pale Chidodo anampa ramani yote, na kumwambia muda sahihi wa kupita mpaka akifanikisha kuingia kwenye ndege. Yasini anasema hajawahi kupata matatizo hata siku moja toka aanze kufanya hii kazi miaka 8 iliyopita, yaani inakuwa kama anatembea kwenye bustani vile. Bwana Chidodo anasema Yasini akifika uwanjani ni kama hawajuani, kila mtu anakula 50 zake, kama ni kuongea ni nje ya hapo wakiwa mtaani huko, au wanaweza kupigiana simu wakakutane mtaani huko lakini hawasalimiani au kufanya wanajuana wakiwa uwanja wa ndege.

Chidodo anasema anashughulika pia na mizigo inayobebwa mkononi, tofauti na ile inayopita kwenye mashine na kupelekwa kwenye sehemu ya mizigo moja kwa moja. Msafirishaji akifika kwenye ofisi za uhamiaji anagongewa muhuri kwenye passport yake, akitoka kwa mtu wa uhamiaji anaelekea sehemu ya ukaguzi ambapo atakutana na watu wa Chidodo. Chidodo hapo sasa anakupa maelezo kutokana na jinsi watu wake walivyokaa, unaweza kuwambiwa pita kwenye mashine ya mkono wa kulia, watu wake wakiwa wameshapangwa, sehemu hii ya ukaguzi ndio unatoa mkanda, viatu na kadhalika unaweka kwenye mashine ukaguliwa, ila vitu vya anaesafirisha mzigo kwa maagizo ya Chidodo havikaguliwi sababu tayari mchongo unakuwa umeshapangwa. Akishatoka kwenye sehemu ya ukaguzi, anaenda zake kwenye sehemu ya watu wanaondoka kusubiria ndege akiwa na mzigo wake, kazi imeisha.

****

Makala inaturudisha kwa Bwana Rudland, mwenye kampuni kubwa ya sigara Afrika Kusini. Rudland anapata tumbaku kutoka kwenye mashamba nchini zimbabwe na kampuni yake ya Gold Leaf Tobacco ni moja ya watengenezaji wakubwa wa sigara eneo hilo. Rudland mbali na dili zake chafu nyingine, anapiga pesa ndefu kwenye biashara ya kuuza sigara kwenye soko la magendo Afrika Kusini. Kampuni ya Gold Leaf inatengeza sigara ambazo zinajulikana kama 'cheapies'. Sigara hizi zinakwepa kulipiwa kodi za serikali hivyo zinauzwa kwa bei ya chini ukilinganisha na sigara za kampuni nyingine, ndio jina la 'cheapies' lilipotokea kutokana kuwa na kuuzwa kwa bei chee.

Rudland anatakatisha pesa kupitia mauzo ya sigara kwa magendo kwa kusafirisha dhahabu kutoka Zimbabwe. Dhahabu inayosafirishwa na watu wa Rudland inaenda kuuzwa kwa kampuni ya Aulion Global Trading Dubai, Aulion inaendeshwa na Rudland (naamini unakumbuka sehemu iliyopita ilipoonesha Aulion ni sehemu ya himaya ya Rudland).

Daud Khan alikuwa moja ya mtu mwenye jukumu muhimu kwenye utakatishaji fedha za bwana Rudland, ametoka (ameacha) kwenye biashara hii haramu ya dhahabu na anaisaidia timu ya Al-Jazeera (exclusive) kwenye uchunguzi huu akitokea kwenye nyumba ya uangalizi zinazotumiwa na mashahidi wa jambo fulani walioamua kusema ukweli (safe house).

Screenshot 2023-07-17 215254.png

Daud Khan

Khan anaeleza jinsi bwana Rudland anavyotakatisha pesa, pesa ambazo haziripotiwi katika njia halali na zinahitaji kuhamishwa. Rundo la faili zilizopatikana na kikosi cha Al-Jazeera ikiwemo picha ambazo hazijawahi kuonekana kwa watu zinaoneshwa. Kwenye picha hizo anaonekana mtu mmoja mzito, muhimu sana, mashuhuri, kila mtu anataka kumpata, wengine wanataka kujadiliana naye, wengine kumkamata, wengine kumshtaki na wengine wanataka kumtumia, yaani kila mtu ana jambo lake na bwana huyu. Jamaa huyu anaweza kupata faida ya dola milioni 1 kwa siku, akisafirisha pesa kwenda nchi tofauti, maeneo tofauti, na ana konekshen zote za kufanikisha hayo.

Jamaa huyu ni nani na anafanya nini, ana uhusiano gani na Bwana Rudland? Tukutane wakati mwingine wakuu.

Muendelezo soma - Episode ya 2 - Sehemu ya 3
 
Gold Mafia imenifumbua sana macho nikagundua Kuna mambo mengi sana yanafanywa na hawa wanaojiita viongozi, ila kwasababu waandishi wa habari wa bongo ni ma mbumbumbu wanaoendekeza uchawa hatuwezi kuyajua.
Siku hizi dhahabu hazikamatwi tena au wafanyabiashara wameacha kutorosha ?
 
Back
Top Bottom