Episode 2 - Sehemu ya 5
Fradreck Kunaka (FKUN) alikuwa Meneja Mkuu kwenye kampuni ya Fidelity, yeye alikuwa analipwa kiasi cha dola za kimarekani 30,000 kwa mwezi. Pattni anaendesha biashara zake katika sehemu ya mji wanaoishi wadosi ambapo kuna mjengo wa maana uliozungushiwa uzio, sehemu hiyo inaitwa Borodare, Harare-Zimbabwe.
FKUN alikuwa anaonekena kwenye ofisini hiyo ya bwana Pattni mara nyingi tu, na saini yake inaonekana kwenye leseni zote za Pattni zinazohusu biashara ya dhahabu. FKUN ndio alikuwa muhusika mkuu wa kutoa leseni za kuuza na kununua dhahabu pamoja na leseni zote zinazohusisha Fidelity Refiner. Kwa hivyo Mr Dube alikuwa analamba dola elf 3 na FKUN alikuwa akilamba dola elfu 30 kila mwezi kutokana na huduma waliyokuwa wanatoa kufanikisha bishara haramu zinaenda bila shida.
Ili kutakatisha pesa za bwana Stanley, Pattni anachaji dola milioni 10 ambazo pia zinahusisha pesa ya kutoa rushwa ili kufanikisha kazi hiyo, ukishatoa kiasi hicho cha pesa wewe unastarehe tu kusubiri kazi yako ifanikishwe, kila kitu wanakuwa wakishughulikia.
*****
Kazi za Mo Dollars Afrika Kusini kama ilivyokuwa kwa Pattni pia zinafanikishwa kwa kutumia rushwa, yeye anawalenga wafanyakazi wa Benki ya Sasfin, benki nchini Afrika Kusini inayowahudumia wafanyabiashara wadogo. Baada ya kutengeneza konekshen na watu hawa wa benk, akina Mo Dollars alikuwa anakutana nao ili kuwajua vizuri ni watu wa aina gani, wana tabia gani, kama wana famila, mke na watoto ambao ukiangalia mishahara wanayopokea haiwatoshi kabisa kuinjoy maisha, nk.
Baada ya kupata taarifa zote wanaambiwa sasa sikia, wewe unakuwa mtu wetu kuhakikisha dili zetu zinaenda vizuri unapitisha malipo yetu yote bila kuuliza uliza maswali utakapoona tu jina la kampuni yetu na sisi tutahakikisha mnakula bata vilivyo, mnaishi kama wadosi. Yaani walikuwa wanachunguza maisha yao vizuri mpaka wahakikishe wanapata kitu cha kuweza kutumia dhidi yao ili wafanikishe dili zao.
Mo Dollars anamwagiza Daud kutoa ombi la malipo kufanyika endapo tu mfanyakazi fulani akiwa ofisini, ambako kwenye ujumbe jamaa huyo anatajwa kama “H”. H inasimama badala ya Hussein Shanara, yeye alikuwa anahusika na kitengo cha kubalisha fedha katika benki ya Safsin.
Hussein na kina Daud Khan na kaka yeake Mo Dollars walikuwa na uhusiano mzuri wa kibiashara, jamaa alikuwa anahakikisha kazi aliyopewa anaifanya vizuri, anahakikisha wafanyakazi wenzake wanapiga mzigo bila kuuliza swali lolote, kwahivyo alikuwa mtu muhimu sana kwao katika kuhakikisha utakatishaji fedha unakamilika vizuri kila mara.
Hussein anatuma ujumbe kwa bosi wake akitoa hitaji la mtu mwingine kuajiriwa, Mo Dollars watakuwa wanamcontrol mtu huyo kwa 100%. Japokuwa alikuwa hana vigezo vyovyote kufanya kazi kwenye benki, jamaa huyo anapata kazi katika benki ya Safsin.
View attachment 2804067
Ili kuhakikisha miamala ya akina Mo Dollars haipati kashkash yoyote, Hussein Shanara alikuwa akilipwa kiasi cha kama dola 1600 kila mwezi. Pia walikuwa wanalipa kiasi cha kama dola 2000 kwa mtu mwingine kwenye benki ya Safsini, Hussein alikuwa ametambulishwa kupitia mtu mwingine aliyekuwa anaitwa Brandon Marshall.
Brandon, alikuwa kwenye biashara mpya ya kuleta wateja mpya, kulikuwa na mtu mwingine pia ambaye aliwasumbua mwanzoni ila alikuja kulainika baadae, huyu alikuwa anaitwa Sheral yeye alikuwa compliance manager (mtu anayehakikisha kanuni na sheria zinafatwa kazini), yeye alikuwa anapokea dola 800 kwa mwezi.
Pesa ilikuwa inaongea kufanya kila kitu, walikuwa wameikamata benki kiganjani, ni kama vile Mo Dollars alikuwa CEO wa benki hiyo bila ya wao kujua. Vitabu vya mahesabu vya Mo Dollars vinaonesha malipo ya rushwa kwa wafanyakazi wa benki nyingine pia, walikuwa na jamaa anaitwa Videsh Seeripat kutoka benki ya Absa, yeye alikuwa anafungua account za benki hewa.
Videsh alikuwa anasimamaia kitengo ya Uhusiano kwenye benki ya Absa, huyu naye alikuwa akilipwa kiasi cha dola 800 kwa mwezi. Watu wote hawa walikuwa wanahakikisha nyaraka zote zote muhimu zinapitishwa bila kukutwa na makosa au mapungufu yoyote ya sheria, na kuweka chochote wanachoambiwa kuweka kwenye nyaraka hizo bila kuuliza maswali. Mbali na watumishi hao, akina Mo Dollars wana watu wengine kwenye orodha yao ya malipo kutoka Benki ya Standard; Viviyan ambaye nae anapokea kiasi cha dola 800
Viviyan alikuwa Msimamizi Mkuu wa idara ya inayosimamia mambo sheria na taratibu za ya Benki ya Standard pamoja na miamala inayohusha nchi za nje na yeye ni mtu muhimu linapokuja suala la kufanya mawasiliano na benki kuu ya Afrika Kusini. Viviyan akitumia jina la uongo kama Vic Grimes, anahakikisha kampuni ya Mo Dollars inasajiliwa na inapata idhini kutoka benki ya Standard. Mo Dollars anampatia nyaraka muhimu zinazohitajika, halafu yeye anakamilisha sehemu iliyobaki kwa kujaza fomu zote zinazohitaka, halafu anapeleka Benki Kuu na kupata kibali kitakachowawezesha akina Mo Dollars kufanya malipo bila ukaguzi wowote kupitia benki yoyote.
*****
Tukirudi kwa Mtume Angel, yeye anamwambia Mr. Stanley pesa yake inaweza kufanya makubwa zaidi ya kununua tu dhahabu, anamwambia ukijenga hoteli utamfurahisha Rais Mnangagwa, akimaanisha kwamba amtengezee Rais kumbukumbu ya kukumbukwa na watu wake kuwa alifanikisha huduma fulani kupatikana Zimbabwe, amtengenezee historia/ legacy, kwa kufanya hivyo mambo yake takuwa yanaenda vizuri zaidi bila usumbufu wowote. Mtume Angel yuko tayari kabisa na eneo la kufanikisha hilo, mji wa maporoko ya Victoria, kwamba akikamilisha hilo watakuwa na moja ya maajabu ya dunia na wageni watafurika kama nyuki kwenda kuangalia.
Mtume Angel anamwambia kinachohitajika hapo ni eneo tu la kujenga, na hilo tukikutana na Mnangagwa unapata dk sifuri tu. Anamwambi hili ni jambo rahisi sana, tulishawahi kuuza ardhi kwa wawekezaji wa kigeni, hii sio mara ya kwanza hivyo usiwe na wasiwasi. Akisema alishafanya dili na familia ya kifalme ya Sharjah, wao walikuwa wanahitaji heka 30,000. Anasema alipomwambia Rais alisema waambie waje chap, ardhi yao ipo tayari.
Msaidizi wa Stanley akataka wapate wasaa wa kuonana na Rais Mnangagwa, Rikki, mshirika wa Mtume Angle, akamwambia kwa sasa Rais yuko bize sana, ila usijali hilo linaweza kupangwa, kwakuwa muda wa Rais una thamani sana, mtatakiwa kulipa pesa ya kufanya mkutano huo kufanikiwa, gharama yake ni dola 200,000.
Itaendelea…