Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Waandishi wa habari undercover wanajifanya kuwa majambazi wenye dola bilioni moja za pesa chafu zinazohitaji kusafishwa. Wanapata upenyo kwa wanachama wa Afrika wa Gold Mafia na kurekodi mikutano ya siri na viongozi wa uhalifu.

Balozi Mkubwa wa Afrika anatoa huduma ya kutakatisha pesa chafu zenye thamani ya dola milioni 1.2 kwa kutumia kofia yake ya Udiplomasia.

Wenyewe wanakwambia kwa Afrika ilimradi unatotoa chochote kitu basi mambo yako yanaenda bila shida yoyote. Gold Mafia imesambaa, hakuna mamlaka au serikali yoyote Afrika inayojaribu kusogeza pua yake.

Wahalifu hutoa donge nono kutakatisha zaidi ya dola milioni 100 kupitia miradi ya serikali ya usafirishaji wa dhahabu. Kitovu cha shughuli zao ni kituo kikubwa cha kutakatisha pesa kusini mwa Afrika, Benki Kuu ya Zimbabwe.

Gold Maafia, ni mfululizo wa sehemu nne wa kitengo cha uchunguzi cha Al Jazeera, unaoangalia jinsi tamaa ya jamii kumiliki dhahabu wanavyoendeleza na kuunga mkono uchumi haramu ulimwenguni. Timu ya siri inafanikiwa kuingia kwenye makundi hasimu ambayo hubadilisha pesa chafu kuwa dhahabu, ambayo baadae inauzwa ulimwenguni kote.

Kupitia maelfu ya nyaraka za siri na mahojiano ya moja kwa moja na whistleblowers kutoka ndani ya makundi vya uhalifu, wachunguzi wanapata muundo wa operesheni za utakatishaji wa pesa zenye thamani ya mabilioni ya pesa ambazo huudumia viongozi wa kisiasa, uchunguzi huo unatupeleka kwenye ofisi za juu Kusini mwa Afrika.

Unadhani viongozi gani wanajihusisha na biashara hii haramu Afrika Kusini, vipi nchi nyingine, je, na Tanzania kuna viongozi wanaojihusisha na biashara hiyo?

Itaendelea...

Kuanza nayo soma Episode 1 - Sehemu ya 1
ZIMBWABWE South Africa Dubai nikiona kwenye aljezira Witness Kuna yule pastor, halafu mnangwagwa halafu Kuna mhindi mmoja pale SA halafu kuna Gupta brothers aise kama movie
 
Episode 2 - Sehemu ya 3

Poleni kwa kuchelewa kuleta muendelezo…. Sasa tuendelee tulipoishia…

Documents na picha alizokuwa anachambua bwana Khan zinatupeleka kwa mwanaume mmoja na kampuni yake inayoitwa PSKA. Pesa kutoka kwenye mauzo ya biashara ya magendo ya sigara ya bwana Rudland zinaingizwa kwenye kampuni hiyo ya PSKA, halafu pesa hizo chafu zinatumwa Dubai kwenye kampuni ya Bwana Rudland Aulion Global Trading. Vitabu vinaonesha kampuni ya PSKA imefanya miamala mara nyingi kwenye kampuni ya Rudland, pesa ambazo zinafikia Dola za Kimarekani milioni 98,615,334.

pesa zilizotumwa Aulion.png


Nakala ya benki inaonesha pesa ni kwaajili ya kufadhili kampuni ya Aulion ili kupata dhahabu. Aulion inasafirisha dhahabu kutoka Benki Kuu ya Zimbabwe na kila mzigo unakuwa na thamani ya Dola za Kimarekani milioni 2.6 na Aulion inatuma bili kwa PSKA ikionesha malipo ye pesa hiyo dola milioni 2.6 yamefanyika

Form inayoonesha thamani ya kila mzigo to Aulion.png


Muamala huo ukikamilika PKSA anatuma tena pesa nyingine kwa Aulion ‘kufadhili’ ununuzi mwingine wa dhahabu. Kwaiyo pesa chafu ya Rudland inabadilishwa kuwa dhahabu Dubai ambako anauza dhahabu hiyo na pesa zinakuwa zimetakaswa.

Ili kukwepa kusababisha mashaka kutoka kwenye benki, pesa zinazotumwa na kampuni ya PSKA zinawasilishwa kama mkopo ambao kampuni ya Aulion inatakiwa kurudisha. Bwana Khan anatuambia hiyo ni geresha tu, Aulion harudishi hela kwa PSKA kama kulipa ‘mkopo’ aliopewa, badala yake wanafoji kwenye vitabu kuonesha kwamba ‘mikopo’ hiyo imelipwa kwenye akaunti ya PKSA kwenye benki ya Absa. Lakini bwana Khan anatuonesha moja ya fomu za malipo zilizofanywa kupitia benki ya Absa, ambapo kwa makusudi kabisa jina la benki linakosewa na kusomeka ‘Aba’, na kama ikitokea hivi fomu hiyo inakuwa imeharibika kwahiyo hakuna malipo yanayofanyika, mchezo wa kuzuga umechezwa vizuri! Mkurugenzi wa PSKA ndio mwamba aliyekuwa anaonekana kwenye picha, jamaa huyu anaitwa Mohamed Khan.

Screenshot 2023-08-09 203025.png
Screenshot 2023-08-09 211828.png

Mohamed Khan

Mohamed Khan ni mtu ambae kwenye mishe zake kamwe hatumii jina lake. Mshirika wa zamani wa Mohamed Khan, Al-Jazeera inamuita ‘Jimmy’, anamuelezea Mohamed Khan kuwa jamaa anajulikana kufanya biashara haramu ya utakatishaji fedha, ukitaka kutoa pesa nje ya Afrika Kusini yeye ndio mwamba wa kushughulikia ishu yako, anatakasa pesa zako, anatoa hela nje ya nchi kwenda kwenye akaunti ya kigeni na mchezo umeisha. Mohamed Khan anasifika kwa kuwa mtaalamu ama tuseme steling wa kutakatisha pesa za vigogo Afrika Kusini, ambako anajulikana kwa A.K.A ya Mo Dollars. Mo Dollars anajulikana kama jamaa mwenye pesa chafu, anatumia pesa kama anapumua vile, jamaa anatakatisha pesa kama hana akili nzuri, ni sawa na kusema yeye ndio boss linapokuja suala la utakatishaji pesa Afrika Kusini😀😀😀! Udhaifu wake mkubwa ni wanawake na magari yenye mwendo kasi, kama Ferrari, Lamborghini nk.

Makala inatukutanisha na mtu mwingine, mwanamama anayeitwa Warda Latif.

Screenshot 2023-08-09 213710.png


Warda Latif alikuwa ameolewa na Mo Dollars na kudumu nae kwa miaka 19. Warda anasema siku amemuacha Mo Dollars, nyumbani kulikuwa na pesa taslimu za Rand kwenye mabegi (pesa inayotumika Afrika Kusini ) milioni 15 ambazo ni sawa na bilioni 1 na ushee za Kitanzania. Kwa Mohamed kujihisi ana nguvu na mamlaka kwa kila mtu ndio mambo muhimu kuliko yote kwake.

Makala inatutambulisha mtu mwingine, Daudi Khan, mdogo wa Mo Dollars! Daudi Khan huyu huyu aliyeamua kushirikiana na Al-Jazeera kueleza uozo unaofanyika kwenye biashara hizi haramu za utakatishaji pesa na biashara za dhahabu kwa magendo!

Screenshot 2023-08-09 215005.png

Daudi Khan

Daudi anasema yeye na kaka yake Mo Dollars wamepitia katika maisha magumu sana, akisema mara zote walikuwa wanadharauliwa kwa jinsi walivyokuwa wanavaa au kwa kutokuwa na chakula, yaani ilikuwa ni mwendo kwa kupigania nafasi ya kuishi. Mo Dollars akapata njia ya kutengeza pesa.

Mamlaka za kubadilishana fedha za Afrika Kusini huweka ukomo wa kiasi gani cha pesa kinachoweza kutumwa nje ya nchi. Daudi anasema kipindi hicho kulikuwa na miundombinu ya hovyo na ufisadi uliotukuka karibu kila sehemu, kila mwenye pesa alikuwa anajaribu kuondoka, na kila mwenye fedha anahamisha pesa zake kwenye akaunti za nje ya nchi kwa mamilioni. Kwahiyo Mo Dollar akaona fursa hapo, kazi yake ikawa ni kutafuta wateja wanaotaka kuhamisha pesa zao kwenye benki za nje ya nchi, ambapo mteja alikuwa anaenda kuacha pesa anazotaka kutuma katika moja ya duka katika kituo cha manunuzi/sehemu ya biashara (tunaweza kusema plaza) Johannesburg. Plaza hiyo ina gorofa 2, sehemu ya chini walikuwa wanauza bidhaa kama masweta, mifagio, madekio na juu ilikuwa sehemu ya benki kufanya biashara kuhesabu pesa, ukifika unatoa hela zako wanahesabu na kuziingiza kwenye akaunt na wewe unapewa fomu ya uthibitisho kuwa pesa imeingia kama vile benki halali, lakini hazikuwa benki halali!

Screenshot 2023-08-09 221807.png

Plaza walipoluwa wanatumia kuhamisha pesa

Mzee wetu wa mishe Mo Dollars akawa anagawanya pesa katika vifungu vidogo vidogo, akawa anaweka kwenye account tofauti tofauti za makumpuni mapya yalikuwa yamefunguliwa. Kampuni hizi vivuli/feki zilikuwa zinatengenezwa kutokana na utabulisho wa watu uliyoibiwa, Jimmy na Mo Dollars walikuwa pia wananunua utambulisho huo. Wanatoka mtaani kutafuta watu wenye njaa waliopigika na maisha usiku wanamwambia tutakupa kiasi fulani cha pesa na wewe cha kufanya ni kutusaidia kufungua akaunti kutumia taarifa zako. Wanampa simu ambako benki inatoa akaunti ya mtandaoni, baada ya kumaliza mchakato huo Mo Dollars anachukua simu biashara imeisha, sasa anakuwa anamiliki account hiyo na hapo anakuwa anaweza kutuma pesa nje ya nchi.

Kampuni za Mo Dollars, PKSA, na Salt Asset Management zinaonekana kufanya malipo ya fedha za kigeni kwa niaba ya kampuni za Afrika Kusini kwa msambazaji nje ya nchi. Kwenye Benki Kuu ya Afrika Kusini, fedha hizo zinakuwa zimeelezwa/zimeandikishwa kama malipo ya awali kwa bidhaa zitakazoagizwa. Hii ni kwasababu ilikuwa ni lazima kutoa taarifa kwenye Benki Kuu kila unapohitaji kufanya muamala unaohusisha kuhamisha fedha nje ya nchi kwa kuwapa sababu ya wewe kuhamisha fedha hizo.

Wakuu naomba tuendelee wakati mwingine.

Muendelez soma
- Episode ya 2 - Sehemu ya 4
 
Episode 2 - Sehemu ya 4

Daudi Khan anaendelea kueleza jinsi kaka yake anavyotakatisha fedha, kuna duka linalouza bidhaa za kidini ambalo ni moja ya kampuni ya Mo Dollars Johannesburg, ambayo inatumika katika kuonesha malipo ya awali yamefanyika. Kampuni hiyo inajulikana vizuri tu katika jiji hilo, inaendeshwa na baba pamoja na mtoto wake.

Invoice ya dola 167700 inaonyesha malipo ya awali yamefanyika katika kampuni ya china Changshu City China kwaajili ya kununua mavazi ya kiislamu, bidhaa ambazo zitapelekwa kwa tarehe ya mbele iliyopangwa, lakini hakuna pesa imetumwa kwenye kampuni hiyo. Malipo haya yanayofanyika yanakuwa makubwa sana kwa kununua mzigo, yaani kwa pesa hiyo unapata nguo nyingi mno kiasi utakosa pa kuziweka na hutakuwa na watu wa kutosha kuwauzia nguo hizo, hiki ni moja ya kiashiria kinachoonesha invoice hiyo ni fake (mkikutana na malipo kama haya sehemu mtaweza kutambua hapa kuna shida pahala😃).

Picha ya invoice

Screenshot 2023-09-17 040912.png

Invoice ikionesha malipo ya awali kufanyika kwaajili ya mavazi ya kiislamu

Invoice inayotumwa na msambazaji ili Mo Dollars alipie bidhaa kwa pesa zake chafu nayo ni feki, account zote mbili zinazotuma pesa pamoja na kupokea (duka la kuuza bidhaa za kiislamu na msambazaji) ni za Mo Dollars! Hakuna bidhaa zinazotoka China kwenda Johannesburg lakini pesa chafu za Mo Dollars zinakuwa zimesafishwa kupitia account hiyo ya nje. Huku kwenye benk kuu kila kitu kinaonekana kipo shwari, muamala halali umepita, hakuna magendo yoyote yanafanyika.

Kutuma pesa kama malipo ya awali ni mbinu inayotumiwa sana na watakatishaji pesa, hii ni kwasababu unaweza kuhamisha pesa kirahisi nje bila kupokea mzigo kama malipo ya awalai na unakuwa na muda wa kutengeza documents za muamala huo kufanyika baadae.


Katika mazunguzo (kutoka kwenye kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao) yaliyorekodiwa, Mo Dollars alisikika akimtahadharisha mshirika mwenzake asifanye biashara na hasimu wao katika utakatishaji pesa, akielezea mbinu yake ya utakatishaji pesa kama biashara, na inatakiwa kuendelea kujulikana hivyo, akisema kwamba uliahidi kufanya biashara hii na sisi tu, ukianza kufanya 'biashara' hiyo na watu wengine wawili, watatu inatoa ishara mbaya.


Daud Khan ndio alikuwa mwandishi wa invoice feki, akielezea ofisini kwao kuna 'strong room', chumba kinachotimiwa kuhifadhia vitu vyenye thamani, na chumba hiko kinakuwa na ulinzi mkubwa. Daud anaelezea kwenye chumba hiko walikuwa na maboksi mengi sana yaliyojaa stempu za benki, passport pamoja na nyaraka za vitambulisho. Daudi pia ndio alikuwa anatengeneza logo, kuweka kiasi cha pesa na kila kitu kwenye invoice hizo, ambapo kwa kukadiria 90% ya rekodi kwenye kitabu cha kampuni ya Salt Management hazikuwa za kweli (halisi).

Makala inaturudisha kwa bwana Pattni, ambaye nae anaujua mchezo huu vizuri. Pattni anasema; huwezi ukaweka mayai yako yote sehemu moja, inabidi utawanyishe kwenye mafungu madogo madogo, na yeye hutawanyisha kwenye makundi madogo madogo kama 20 hivi. Wakati akiwa anaendelea kuongea na bwana Stanley, Pattni anasema yuko na network kubwa. Kwa upande wa UK ana duka la kuiza vito, group ya hotel, kampuni za bidhaa mbalimbali, kwahivyo wana uthibitisho wa sababu pindi wakituma pesa chafu nje ya nchi kama malipo ya bidhaa.

Hela zinatumwa kutoka kwenye kampuni zake za Dubai kwenda kwenye biashara zake za London na wana vitabu vyote vya rekodi hizo, hivyo ni rahisi kuthibitisha sababu ya kufanya malipo kwenye account ya nje katika mchakato wa kutakatisha pesa.


Si unakumbuka bwana Pattni ana utambulisho mwingine kama mtu wa dini anaependa kusaidia masikini, ambapo kwenye upande huu anajulikana kama brother Paul? Timu ya Al-Jazeera inafanikiwa kumpata mhasibu wa zamani wa brother Paul, Bwana Raj. Raj anasema wakati anajiunga na bwana Pattni (brother Paul) alikuwa anamuona kama mtu mwema sana, anaefanya kazi ya Mungu, lakini kituo cha msaada cha Bwana Pattni kinachoitwa Land of Hope ndio kimekuwa kikitumika kama sehemu muhimu ya kutakatishia pesa.

Raj anasema Pattini akaanza kutoa misaada na kwa watu rasmi, akificha rushwa kwenye jina la msaada, Raj ana kitabu kinachoonesha rushwa zilizofanywa na Pattini, kinaonesha malipo ya ada kwenye chuo kwaajili ya watoto wa mtu muhimu kutoka katika tawi la Benki Kuu ya Zimbabwe. Baba mwenye Watoto hao anaitwa David Chirozvi.

Screenshot 2023-09-17 220336.png

David Chirozvi

David anafanya kazi kwenye duka la vito la Aurex Jewellery, ambako wanatengeneza vito, lakini pia duka hilo ni sehemu ya Benki Kuu, David hapo ni Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu. Kampuni ya Pattini ya Suzan ina leseni iliyotoka Aurex, ambayo inawapa kibali cha kusafirisha vito vya dhahabu na almasi, ambapo pia kibali hicho kinajumuisha malipo ya ziada ya 18% ya mauzo kwa kampuni Suzan kutoka serikalini (si unakumbuka kuhusu malipo ya serikali kwa akina Pattini kwa kuwasaidia upatikanaji wa dola na kuruka/kukwepa vikwazo walivyowekewa na mataifa ya nje?). Kampuni ya Pattini ina leseni pia inayowawezesha kununua dhahabu kutoka wachimbaji kwa niaba ya Fidelity Printers. Mhasibu Raj anasema, kila siku Pattni anaingiza 80kg – 100kg za dhahabu.

Screenshot 2023-09-17 220807.png
Screenshot 2023-09-17 221112.png


Lengo la Leseni hizo kutolewa kwa bwana Pattni ni kwaajili ya kuhakikisha uzalishaji na mauzo ya dhahabu yanaongezeka Zimbabwe, lakini uhalisia ni kwamba wananufaika akina Pattni na maafisa waliohusika kuthibitisha mauzo ya dhahabu hizo. Jamaa ambae anasimamia kitengo cha mauzo ya dhahabu, bwana Dube, anapokea kiasi cha Dola za Kimarekani 3000 kwa mwezi kutoka kwa Pattni. Mehluleli Dube alikuwa Mkuu wa Kitego kwenye masuala ya dhahabu kutoka Fidelity Printers, na yeye ndio alikuwa na mamlaka ya kusaini ili kupata leseni kwaajili ya kuuza na kununua dhahabu.

Screenshot 2023-09-17 224307.png

Mehluleli Dube

Jina jingine katika kitabu cha mahesabu alichonacho Raj kinaonesha nguvu ya Bwana Pattni dhidi ya Fidelity Printers, F.Kun. Bwana huyu anapokea Dola za Kimarekani 30,000 kila mwezi kutoka kwa Pattni.

F.Kun ni nani? Tukutane katika muendelezo

Muendelezo soma - Episode 2 - Sehemu ya 5
 
Back
Top Bottom