Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera

Waandishi wa habari undercover wanajifanya kuwa majambazi wenye dola bilioni moja za pesa chafu zinazohitaji kusafishwa. Wanapata upenyo kwa wanachama wa Afrika wa Gold Mafia na kurekodi mikutano ya siri na viongozi wa uhalifu.

Balozi Mkubwa wa Afrika anatoa huduma ya kutakatisha pesa chafu zenye thamani ya dola milioni 1.2 kwa kutumia kofia yake ya Udiplomasia.

Wenyewe wanakwambia kwa Afrika ilimradi unatotoa chochote kitu basi mambo yako yanaenda bila shida yoyote. Gold Mafia imesambaa, hakuna mamlaka au serikali yoyote Afrika inayojaribu kusogeza pua yake.

Wahalifu hutoa donge nono kutakatisha zaidi ya dola milioni 100 kupitia miradi ya serikali ya usafirishaji wa dhahabu. Kitovu cha shughuli zao ni kituo kikubwa cha kutakatisha pesa kusini mwa Afrika, Benki Kuu ya Zimbabwe.

Gold Maafia, ni mfululizo wa sehemu nne wa kitengo cha uchunguzi cha Al Jazeera, unaoangalia jinsi tamaa ya jamii kumiliki dhahabu wanavyoendeleza na kuunga mkono uchumi haramu ulimwenguni. Timu ya siri inafanikiwa kuingia kwenye makundi hasimu ambayo hubadilisha pesa chafu kuwa dhahabu, ambayo baadae inauzwa ulimwenguni kote.

Kupitia maelfu ya nyaraka za siri na mahojiano ya moja kwa moja na whistleblowers kutoka ndani ya makundi vya uhalifu, wachunguzi wanapata muundo wa operesheni za utakatishaji wa pesa zenye thamani ya mabilioni ya pesa ambazo huudumia viongozi wa kisiasa, uchunguzi huo unatupeleka kwenye ofisi za juu Kusini mwa Afrika.

Unadhani viongozi gani wanajihusisha na biashara hii haramu Afrika Kusini, vipi nchi nyingine, je, na Tanzania kuna viongozi wanaojihusisha na biashara hiyo?

Itaendelea...

Kuanza nayo soma Episode 1 - Sehemu ya 1
Naweka kambi
 
Episode 1 - Sehemu ya 5

Tulipoishia Bwana pili Patni naye kwa upande wake alitoa njia nyingine ya kusafirisha pesa chafu za Bwana Stanley kutoka China kwenda Dubai. Njia hizo ni kwa kutumia wakala wa usafirishaji na njia ya pili ni kupitia Hawala.

Tuendelee...

Hawala ni kama neno la kitamaduni linalomaanisha njia isiyo rasmi ya kuhamisha fedha nje ya njia za benki kutoka nchi A kwenda nchi B. Kawaida, hawala hujumuisha watu wenye uhusiano wa karibu unaoweza kuwa wa kindugu (familia) au wanaojuana kwa njia nyingine ambao hubadilishana fedha na kuweka rekodi katika vitabu vya hesabu. Mfano unataka kutuma dola mia katika jambo letu, wakala wa Hawala wa Patni huko Hong Kong angechukua noti ya dola mia chafu kutoka kwa Bwana Stanley, kisha wataandika katika kitabu chao cha hesabu kwamba wamepokea pesa, halafu watatuma ujumbe kwa mshirika wao Dubai ukiwaambia tumepokea pesa kiasi kadhaa, tafadhali mlipeni pesa sawa kama iliyolipwa huku.

Mtu mwingine wa operesheni hii ya hawala anayefanya kazi na Pattni huko Dubai atamlipa Stanley dola mia. Kwa hivyo, dola mia hazitumwi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, ila ni kanjia ka kufanya account zisome bila shida. Mawakala hawa wa Hawala wanahakikisha vitabu vyao viko sawa kwa pande zote mbili kadri wateja wanavotuma pesa. Kwa upande mmoja, njia hii ni halali, mara nyingi ndio njia pekee kwa wahamiaji wa kiuchumi (wahamiaji wanaohama nchi moja moja kwenda nyingine kwaajili ya fursa za kiuchumi) kuhamisha pesa, lakini pia inaweza kutumiwa kama njia ya wahalifu na magenge ya uhalifu kuepuka kugundulika kupitia mfumo wa benki, na akina Pattni na wahalifu wenzake wanaitumia njii hii vizuri kwenye biashara zao za kutakatisha pesa.

***​

Unamkumbuka Nabii Angel? Makala hii inaturudisha kwake kutuonesha jinsi naye alivyoingia mkenge kwa Bwana Stanley akidhani ni mteja kweli anayetaka kutakatishiwa pesa zake. Nabii Angel anamwambia Stanley kama unataka dhahabu hilo halina shida ninaweza kumpigia Rais wa Chama cha Wachimbani wa Madini nchini, ukamsikiliza mwenyewe anavyoelezea mlolongo huu tukafanya biashara.

Screenshot 2023-06-30 004138.png

Nabii Angel akiwa anaongea na Rais wa Chama cha Wachimba Madini akiwa kwenye loud speaker

Rais wa Chama cha Wachimba Madini anavutiwa waya chaap, huyu si mwingine bali ni bibie Henrietta Rushwaya, mpwa wa Rais Manangagwa. Nabii Angel anamuleza dili lililopo mezani na kumwabia bibie Rushwaya kuwa jamaa wanataka kuwekeza pia kununua na kuwekeza kwenye dhahabu, Rushwaya anasema hamna tatizo, hilo jambo dogo sana sana, limeisha.

Rushwaya.jpg

Rais wa Chama cha Wachimba Madini, Henrietta Rushwaya

Rushwaya anaanza kuelezea mchakato wa jinsi wanavyofanya biashara, kwa kila kilo 100 za dhahabu wanapata punguzo la 4% katika bei soko ya dunia, mpango wa Rushawa utakuwa unatakatisha dola milioni 5 kila wiki kwa njia ya mzunguko. Mchakato unaanza na malipo ya fedha chafu kiasi cha dola milioni 10 kwa wenye jukumu la kuchakata dhahabu Zimbabwe, Fidelity Printers. Wakipeleka kiasi cha milioni 10 kwa mfano, milioni 5 zitawekwa Fidelity Printers kwa kipindi cha uhusiano wao na watakuwa wanapata dhahabu yenye thamani ya milioni 5 kila wiki, wakitakata tena huduma hiyo mzunguko unakuwa huohuo wataacha dola milioni 5 na kila wiki watakuwa wanapata dhahabu yenye thamani wa dola milioni 5. Mchakato huu unaendelea mpaka hela zote zisafishwe.

Mfumo wa Rushwaya unaweza kusafisha pesa nyingi zaidi za Bwana Stanley. Ikiwa atapeleka fedha chafu milioni 20, utaratibu ni ule ule nusu ya fedha hizo zitawekwa (zitabaki) Fidelity Printers, dola milioni tano zitasafishwa kila wiki kwa wao kupewa dhahabu zenye thamani sawa na kiasi hicho na dola milioni 5 nyingine zilizoongezeka zitasafishwa kupita moja ya connection za Rushwaya. Hivyo kwa mpango huo bwana Stanley ataweza kusafisha dola milioni 10 kila wiki. Rushwaya anamaliza kutoa maelezo yake na wanaahidiana kutafutana baadae Nabii Angel akishawekana sawa na Stanley. Wakati wanaendelea na mazunguzo, Nabii Angel anamtambulisha mtu anayefanya naye kazi (wa kushoto kwenye picha inayoonekana hapo chini) kwenye kampuni yake inayoitwa Billion Group iliyoko Zimbabwe na inafanya shughuli zake zote Zimbabwe, ambaye anaweza kuwa mshirika wa bwana Stanley kila atakapokuwa anashughuli Zimbabwe, ili awe na mtu anayemfamu akitata kufanya biashara wakati mwingine.

Screenshot 2023-06-30 025443.png

Mshirika wa Nabii Angel kwenye kampuni yake inayoitwa Billion Group

Wakati hayo yanaendelea Nabii Angel yuko Glasgow na Rais Manangagwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa ambako anadai kuwa vikwazo walivyowekewa vinaizuia Zimbabwe kutekeleza ahadi zake kwenye uchumi endelevu. Angel anamwambia Bwana Stanley kwamba anaweza kukutana na Rais.

Screenshot 2023-06-30 013942.png

Rais Manangagwa akihutubia kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali hewa wa UN

Vikwazo vilivyowekwa na mataifa ya nje vinazuia uwezo wa wanasiasa na taasisi za serikali za Zimbabwe kufanya biashara, hivyo wanatumia watu (binafsi) wengine kufanya biashara kwa niaba yao kwakuwa mtu mmoja mmoja haguswi na vikwazo hivyo vilivyoikusudia Zimbabwe kama nchi. MacMilan ana uhusiano wa kifamilia na mfanyabiashara mwingine anayesaidia serikali kukiuka vikwazo ama tuseme kupigana na vikwazo hivyo. MacMillan anamuelezea jamaa huyu kama baba lao, yaani ana pesa za kutosha yeye na Pattni wanakaa, na hela zake ndio zinatumika kufadhili benki zote Zimbabwe. Jamaa anaweza kumpigia simu Gavana wa Benki kuu muda wowote na kupanga mkutano. Yeye ni mmiliki wa kampuni kubwa ya sigara nchini Afrika Kusini, chapa ya bidhaa zake ni jina lake, huyo si mwingine bali ni Bwana Simon Rudland.

Wakuu tukutane siku nyingine kwaajili ya muendelezo na kumfahamu zaidi kubwa lao Bwana Simon Rudland

Muendelezo soma - Episode 1 - Sehemu ya 6
 
Kuna mwaka nilikamatwa huko kanda ya kaskanzini nikalala sero siku tatu siku nikaamishiwa gerezani c nikakuta kuna mgeni wa nje ya Tz tukaanza kula story yule ndugu akaniambia Kuna ela ipo online nitafute kituo Cha watot yatima ndo tupigie dili la kuingiza hizo fedha nchini Sasa tatizo likaja huku cjaweka mchongo wangu vizuri ndugu zangu wakawa washamaliza kesi huko nje nashangaa nakuja itwa nisepe hm niliona wamenipotezea utajiri
Huyo alikuw tapeli tu.

Hakuna mchongo wa hivyo acha tamaa,😅😅
 
Kuna mwaka nilikamatwa huko kanda ya kaskanzini nikalala sero siku tatu siku nikaamishiwa gerezani c nikakuta kuna mgeni wa nje ya Tz tukaanza kula story yule ndugu akaniambia Kuna ela ipo online nitafute kituo Cha watot yatima ndo tupigie dili la kuingiza hizo fedha nchini Sasa tatizo likaja huku cjaweka mchongo wangu vizuri ndugu zangu wakawa washamaliza kesi huko nje nashangaa nakuja itwa nisepe hm niliona wamenipotezea utajiri
Huyo alikuw tapeli tu.

Hakuna mchongo wa hivyo acha tamaa,😅😅
 
Back
Top Bottom