Goli la Mama: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Goli la Mama: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Rais wa Tanzania amesema atatoa Tsh 5mil kwa kila goli litalofungwa na hizo timu tajwa, mwishoni mwa wiki hii, watakapokuwa wakicheza michezo yao ya Kimataifa.

1676376882547.png

Hayo yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali;

*******

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kununua kila goli kwa Sh5 milioni litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa mwishoni mwa wiki hii. Ametibitisha Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Simba itakuwa mwenyeji wa Raja Casablanca Februari 18 mwaka huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikiwaalika TP Mazembe Februari 19, 2023, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.


******

MADA NYINGINE ZENYE AHADI YA FEDHA KWA SIMBA NA YANGA
  1. Rais Samia aongeza dau, kutoa Tsh. Milioni 10 kwa kila Goli kwa Yanga na Simba (CAFF na CAFCL)
  2. Rais Samia kulipa Tsh. Milioni 10 kwa kila Goli la CAF
  3. Rias Samia kununua kila goli la Yanga kwa Tsh. Milioni 20
RAIS SAMIA AAHIDI KUTOA NDEGE KWA TIMU YA YANGA
  1. Suala la Rais Samia kutoa pesa na ndege kwa timu kusafiria ni kwa gharama ya nani?
MABANGO YA RAIS SAMIA KUBEBWA NA MASHABIKI WA MPIRA
MALALAMIKO YA MASHABIKI WA SIMBA KWA SERIKALI KUPENDELEA TIMU YA YANGA
  1. Serikali yaonesha ushabiki wa wazi kwa Yanga kupeleka mashabiki South Africa
  2. Ahmed Ally: Si jambo jema hata kidogo Serikali kutoa Posho ya 1.2M pamoja na Usafiri kwa Mashabiki wa Yanga, Mpira ni Starehe
  3. Hili halikubaliki ni kama ubaguzi kwenye timu kama Simba
  4. Serikali iwe makini, itaigawa Nchi
  5. Msigwa: Ufafanuzi wa suala la Simba
 
Rais Samia Suluhu ametangaza kununua kwa Sh 5 milioni kila bao litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa ya mwisho wa wiki hii.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema hayo leo Februari 14, 2023 huku timu hizo zikiwa na kibarua kwa mechi ya pili hatua ya makundi baada za kwanza kufungwa ugenini.

Simba itacheza Jumamosi dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika saa 1:00 usiku uwanja wa Mkapa na Yanga itaikaribisha TP Mazembe Jumapili saa 1:00 usiku katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Hizo pesa Rais angetafuta vituo vya watoto yatima akawapatie walezi zao, hao Simba na Yanga wanajua ushindi ni jukumu lao, na mbele ya safari kuna pesa nyingi watapata wakijitahidi kufika..

Labda kwa timu ya taifa ndio angefanya hivyo.
 
Raisi Samia Suluhu Hassan amesema michezo ya marudio itakayochezwa weekend hii kwa timu ya simba na yanga yeye kila goli litakalo fungwa atatoa milioni tano

Anachezea pesa zetu tu huyu hao wachezaji wanamishahara mikubwa sana huku mtaani wafu hata pesa ya mlo mmoja hawana

Haya ni matumizi ya hovyo ya pesa za walalahoi hizo timu zote pesa wanazo hii ni anasa,je atatumia mshahara wake nani ana hakiki hilo.

Kuna wachezaji pale wanalamba hadi milioni 25 kwa mwezi zaidi ya mishahara ya mawaziri kuna watu hata pesa ya kupanda madaraja hajalipa kuna wazee pensheni hadi leo hakuna kuna hospitali hazina dawa juzi kuna watoto tumeona wanakaa chini shuleni ni matusi na makodi na misururu ya magari kwenye misafara na kutia saini ni malipo ya kila anayehudhuria ,

USSR
FB_IMG_1676365710800.jpg
 
Anachezea pesa zetu tu huyu hao wachezaji wanamishahara mikubwa sana huku mtaani wafu hata pesa ya mlo mmoja hawana

USSR View attachment 2517115
Safi mhe. Raisi
Michezo ni sanaa
Mpira ni burudani

Bora nguvu kubwa ya uwekezaji hii nchi tungeweka kwenye michezo yra ingekuwa inavuna trillion tsh za kodi.
Kongole sana mhe. Rais.
 
Anachezea pesa zetu tu huyu hao wachezaji wanamishahara mikubwa sana huku mtaani wafu hata pesa ya mlo mmoja hawana

USSR View attachment 2517115
That's motivation brother.. Don't be so negative.. Milion 5 ni kitu gani kwa rais? Kumbuka ana mfuko wa entertainment kisheria na hili ni kwa maslahi ya nchi
 
Back
Top Bottom