Hili wazo ni baya na nitatoa sababu mbili tatu.
Kwanza, linaweza kuharibu mipango ya uchezaji wa timu. Siku hizi timu zinacheza kwa mipango siyo tu kufunga magoli. Tumeona juzi Watunisia baada ya kupata goli mbili wakatulia. Ukiahidi pesa ya magoli kuna timu au wachezaji wanaweza kuwaza kufunga badala ya kucheza kimbinu hasa kama timu tayari inaongoza.
Pili, kwa mazingira ya sasa Rais kuahidi tumilioni 5 kwa shughuli pevu kama ya weekend hii ni kushusha umuhimu wa magoli yenyewe.
Tatu, tuache kutafuta njia za mkato za mafanikio. Simba mwaka 1993 waliahidiwa kupewa basi kila mchezaji na bado wakashindwa kutoboa katika mechi moja tu uwanja wa nyumbani. Nchi iwekeze ipasavyo katika michezo na tuache kurukia pale tunapoona kuna upenyo wa kufaidika kisiasa, hizi njia nyingine tumezijaribu sana hazina mafanikio.