Goli la Mama: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Goli la Mama: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Hizo pesa Rais angetafuta vituo vya watoto yatima akawapatie walezi zao, hao Simba na Yanga wanajua ushindi ni jukumu lao, na mbele ya safari kuna pesa nyingi watapata wakijitahidi kufika..

Labda kwa timu ya taifa ndio angefanya hivyo.
Acha kupangia watu namna ya kutumia pesa zao......tafuta za kwako zipangie matumizi.
 
Rais kafanya jambo zuri sana.
Ila angetofautisha thamani ya magoli tu.
Huwezi kulinganisha thamani ya goli la mashindano ya Ligi ya Mabingwa Africa na ile ya Ligi ya Shirikisho.

Ingekuwa vyema kabisa goli la Shirikisho lingekuwa japo 1m. na la club bingwa ndio iwe 5m, yaani angalau ratio iwe 1:5
 
Kwa nini wamechagua mechi za wekend ijayo?

Mama Samia mjanja anajua pesa yake haitapotea

Maana hakuna ujanja wa Simba kumfunga Raja Casablanca saa moja usiku Dar

Na wala hakuna ujanja wa yanga kumfunga Tp Mazembe
Sijakuelewa mkuu, inamaana za weekend hii hazihusiki?
 
Yani hapo ndo sijui..inamaana kikubwa wafunge hata kama watafungwa...
Yeye ananunua kila goli litakalofungwa na simba ama Yanga.
Hata wafungwe 10 ila ikitokea wamefunga hata 1 atalinunua.
 
Hizo pesa Rais angetafuta vituo vya watoto yatima akawapatie walezi zao, hao Simba na Yanga wanajua ushindi ni jukumu lao, na mbele ya safari kuna pesa nyingi watapata wakijitahidi kufika..

Labda kwa timu ya taifa ndio angefanya hivyo.
Hi ndio comment ya msingi Sana niishie hapotu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wewe hupendi hamasa ?...acha vijana wakapambane wapate pesa za kuongeza mlo.
Hizo hamasa ndizo zinazosababisha timu kucheza kwa presha. Hamasa kama hizo zingefanyika ndani ya klabu kati ya wachezaji/benchi la ufundi na viongozi/wadhamini wao.

Serikali kama inapenda kuona mafanikio ya timu zetu, basi ingekuwa inazisaidia kifedha timu zote zinazofuzu kucheza mashindano ya Kimataifa; kwa ajili ya kuweka kambi, kulipa wachezaji posho, kusafiri nje ya nchi, nk.
 
Rais wa Tanzania amesema atatoa Tsh 5mil kwa kila goli litalofungwa na hizo timu tajwa, mwishoni mwa wiki hii, watakapokuwa wakicheza michezo yao ya Kimataifa.

Hayo yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali;

=====

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kununua kila goli kwa Sh5 milioni litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa mwishoni mwa wiki hii. Ametibitisha Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Simba itakuwa mwenyeji wa Raja Casablanca Februari 18 mwaka huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikiwaalika TP Mazembe Februari 19, 2023, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: Mwananchi
 
TPM apewe kabisa Mil 15 zake...
 
Tunahitaji kuona uwezo wa timu hizi Mbili Simba na yanga kwenye mechi za kimataifa.Mi siangaliagi haya mamechi yao ya Vodacom sijui ya nbc ligi ambayo ni ya upande mmoja.Kwa hiyo wanasiasa ni muhimu tuziache hizi timu tuone uwezo wao halisi.
 
Back
Top Bottom