Goli la Mama: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Goli la Mama: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Hili wazo ni baya na nitatoa sababu mbili tatu.

Kwanza, linaweza kuharibu mipango ya uchezaji wa timu. Siku hizi timu zinacheza kwa mipango siyo tu kufunga magoli. Tumeona juzi Watunisia baada ya kupata goli mbili wakatulia. Ukiahidi pesa ya magoli kuna timu au wachezaji wanaweza kuwaza kufunga badala ya kucheza kimbinu hasa kama timu tayari inaongoza.

Pili, kwa mazingira ya sasa Rais kuahidi tumilioni 5 kwa shughuli pevu kama ya weekend hii ni kushusha umuhimu wa magoli yenyewe.

Tatu, tuache kutafuta njia za mkato za mafanikio. Simba mwaka 1993 waliahidiwa kupewa basi kila mchezaji na bado wakashindwa kutoboa katika mechi moja tu uwanja wa nyumbani. Nchi iwekeze ipasavyo katika michezo na tuache kurukia pale tunapoona kuna upenyo wa kufaidika kisiasa, hizi njia nyingine tumezijaribu sana hazina mafanikio.
 
Hizo pesa Rais angetafuta vituo vya watoto yatima akawapatie walezi zao, hao Simba na Yanga wanajua ushindi ni jukumu lao, na mbele ya safari kuna pesa nyingi watapata wakijitahidi kufika..

Labda kwa timu ya taifa ndio angefanya hivyo.
We unadhan yatafungwa magoli mangapi? Hata yakifungwa manne ni milioni 20 tu, shida ipo wapi katika kutoa hamasa?

Inajua impact ya michezo kwenye nchi? Hao watoto yatima wanaisaidiaje nchi ukiwapa hio milioni 20? Kimahesabu ukiwapa watoto yatima bila kufikiria kwa mtazamo wa dini ni sawa na kuwekeza patupu.

Michezo ni ajira, michezo inakuza utalii leo mnalia hakuna ajira lkn unapochochea michezo baadhi ya Raia wataajiriwa kwenye michezo.

Kwa jicho pana hakuna bata katika hilo kwanza anaweza kuwa anatoa pesa kwenye bajeti ya wizara ya michezo fungu la mengineyo. Shida ipo wapi

Ecko madam President
 
Hamasa ni sawa lakini kutangaza sioni sahihi,na hii ina madhara makubwa kwasababu timu pinzani kama binadamu zitafanya juu chini kwa kuona mpaka mkuu wa nchi kaingia,hapa sio sahihi hata kidogo,pili zawadi hii itadumuza jitihada za Kila siku za wachezaji kwani mpira na kushinda ni kazi yao,angetoa zawadi basi,ishu ya kutangaza sio
 
Wanasiasa bana, hiki ni nini sasa amefanya? kawasiliana na viongozi wa timu husika na kuona hio ni njia sahihi ya kutoa hamasa yake?

kwanini wanasiasa wetu hawaheshimu nafasi za watu lakn?
 
Mvo
Hizo pesa Rais angetafuta vituo vya watoto yatima akawapatie walezi zao, hao Simba na Yanga wanajua ushindi ni jukumu lao, na mbele ya safari kuna pesa nyingi watapata wakijitahidi kufika..

Labda kwa timu ya taifa ndio angefanya hivyo.
Mbona kila kitu twakosoa tu? Kuna ubaya gani akichagiza mambo ya soka? Ifike mahali tuelewe kuwa rais naye anahisia za soka, na tusimpangie aziexpress vipi.
 
Ngada FC, Sembe FC, Pusha FC, Punda FC, Bwimbwi FC watajifunga hata 2.
 
Back
Top Bottom