Goli la Mama: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF

Raisi Samia Suluhu Hassan amesema michezo ya marudio itakayochezwa weekend hii kwa timu ya simba na yanga yeye kila goli litakalo fungwa atatoa milioni tano

Anachezea pesa zetu tu huyu hao wachezaji wanamishahara mikubwa sana huku mtaani wafu hata pesa ya mlo mmoja hawana

Haya ni matumizi ya hovyo ya pesa za walalahoi hizo timu zote pesa wanazo hii ni anasa,je atatumia mshahara wake nani ana hakiki hilo.

Kuna wachezaji pale wanalamba hadi milioni 25 kwa mwezi zaidi ya mishahara ya mawaziri kuna watu hata pesa ya kupanda madaraja hajalipa kuna wazee pensheni hadi leo hakuna kuna hospitali hazina dawa juzi kuna watoto tumeona wanakaa chini shuleni ni matusi na makodi na misururu ya magari kwenye misafara na kutia saini ni malipo ya kila anayehudhuria ,

USSR View attachment 2517115
Nenda chato ukazikwe nae

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Rais wa Tanzania amesema atatoa Tsh 5mil kwa kila goli litalofungwa na hizo timu tajwa, mwishoni mwa wiki hii, watakapokuwa wakicheza michezo yao ya Kimataifa.

Hayo yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali;

=====

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kununua kila goli kwa Sh5 milioni litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa mwishoni mwa wiki hii. Ametibitisha Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Simba itakuwa mwenyeji wa Raja Casablanca Februari 18 mwaka huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikiwaalika TP Mazembe Februari 19, 2023, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: Mwananchi
Safi sana. Kwa hili Mama apewe mataji yake.
 
Rais Samia Suluhu anakuza sekta ya michezo yani huyu Mama haachi gepu kila sehemu anaimarisha
 
Hili wazo ni baya na nitatoa sababu mbili tatu.

Kwanza, linaweza kuharibu mipango ya uchezaji wa timu. Siku hizi timu zinacheza kwa mipango siyo tu kufunga magoli. Tumeona juzi Watunisia baada ya kupata goli mbili wakatulia. Ukiahidi pesa ya magoli kuna timu au wachezaji wanaweza kuwaza kufunga badala ya kucheza kimbinu hasa kama timu tayari inaongoza.

Pili, kwa mazingira ya sasa Rais kuahidi tumilioni 5 kwa shughuli pevu kama ya weekend hii ni kushusha umuhimu wa magoli yenyewe.

Tatu, tuache kutafuta njia za mkato za mafanikio. Simba mwaka 1993 waliahidiwa kupewa basi kila mchezaji na bado wakashindwa kutoboa katika mechi moja tu uwanja wa nyumbani. Nchi iwekeze ipasavyo katika michezo na tuache kurukia pale tunapoona kuna upenyo wa kufaidika kisiasa, hizi njia nyingine tumezijaribu sana hazina mafanikio.
Sasa huo ni uoga ndugu yangu wewe itakuwa ni Yanga unajua hautatoboa lakini sisi Simba tunaona Rais ameongeza hamasa kwa wachezaji pole sana
 
Hamna siyo woga. Mambo hayo hayana tija siku hizi. Juzi Horoya kwenye mechi na Simba waliahidiwa milioni 11 kila mmoja kama sikosei.
 
Rais wa Tanzania amesema atatoa Tsh 5mil kwa kila goli litalofungwa na hizo timu tajwa, mwishoni mwa wiki hii, watakapokuwa wakicheza michezo yao ya Kimataifa.

Hayo yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali;

=====

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kununua kila goli kwa Sh5 milioni litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa mwishoni mwa wiki hii. Ametibitisha Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Simba itakuwa mwenyeji wa Raja Casablanca Februari 18 mwaka huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikiwaalika TP Mazembe Februari 19, 2023, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: Mwananchi
Hapo MILIONI 15 ni za mayele
 
Haya ndio mambo tunayoyapenda safi sana MAMA na Asante.
 
Hapo Watani nawao wanatakiwa wanunue Kila goli watalofunga kwa 2million maana hii biashara mwenye hasara ni Hangaya.
 
Back
Top Bottom