Lile bao hakuna kosa kwa upande wa Simba wala Mwamuzi, ni akili kubwa ya Wachezaji wa Simba kwenye hatua kama zile
Rejea Simba dhidi ya Nkana kwenye Klabu bingwa Afrika, move ya faulo ilikuwa kama ile, Wachezaji wa Nkana walipoteza concentration, Simba wakawahi kuweka (Quick thinking)
Azam au Mtu yoyote ambaye ni Mwanasoka ajue inapotokea faulo yoyote lazima kwanza ukazibe mpira, zibeni mpira huku wengine wanaongea na Mwamuzi
Wenzetu Ulaya ile mali hata akichezewa faulo anawahi kuidaka kwanza ikae eneo lake, wengine kwenye ukuta na wengine wanakaa karibu na mpira
Sasa Azam wengine wapo kwa Mwamuzi na wengine wanajipanga, wakaacha mpira kwa Simba, ni akili ya haraka Simba wakaitumia kufunga lile bao, hizo ndio akili za Wazoefu
Kilichotokea ni kuendelea kujifunza, kukomaa na kujua nini kinahitajika kwa wakati gani
View attachment 1830891